rip faza_nelly
JF-Expert Member
- Feb 19, 2018
- 6,133
- 7,836
umeonesha umasikini na njaa ya hali ya juu sana, gharama alizotumia Ni ndogo sana ambazo ulikuwa na uwezo wa kuzikataa na kujigharamia ww mwenyew. Wewe una njaa huna tofauti na wale wa kunywa bia za watu na kukimbia kwa kujifanya anaenda toilet.Mwaka jana tu nilikuwa naenda mkoa flani sikuwahi kufika kule. Pembeni yangu nilikaa na kaka akaniambia ni mwenyeji kule ninapoenda. Tukawa tunapiga story za hapa na pale tukazoeana. Njia nzima tukawa tukishuka kupata chakula analipia yeye, safari ilikuwa ndefu sana. Basi kufika njiani bus lilipata shida ikasababisha tufike tunakoenda saa4 usiku.
Yule kaka aliniambia ana familia akaenilekeza lodge ili nikalale pale kesho asubuh nielekee ofisi nilokuwa naenda. Akachukua no ya simu. Ila akasema tukifika atapeleka mzigo kwake then atakuja pale lodge ahakikishe kama nimefika salama, nikasema poa. Akanipa hela ya room.
Tukashuka akachukua boda fasta akasepa. Nami nikachukua boda ghafla nkawaza huyu kaka nikikaa vibaya atakuja kunila kimasihara. Basi nkamwambia boda nipeleke lodge nzuri nikalale. Boda akanipeleka lodge nyingine kabisa kufika nikaona jina sio lile alonielekeza yule kaka. Nkasema poa!!!! Nikachukua room.
Baada ya dk 20 yule kaka kapiga simu nipo nje upo room no ngapi? nkamwambia no.... akasema poa nakuja...nikazima simu nikalala. Asubuh kuwasha simu ziliingia text kama 10 za matusi mfululizo, sikumjubu wala!!!!!! daaah wanaume nyie basi tu.
Njaa



