Pole sana mkuu,
The bold,
Nenda/ wasiliana na Mhariri wa gazeti hilo, inawezekana Mhariri hajui chochote ila mwandishi kajifanya amefanya uchambuzi kisha kaipeleka gazetini (na kulipwa haki asiyostahiki). Mimi ilinitokea mwaka 2011, nilikuwa nafanya uchambuzi kutokana na makala za kitafiti kuhusu sekta ya filamu, na mwandishi mmoja (mwanadada nimemsahau jina) alikuwa na tabia ya kunakiri makala zangu za uchambuzi na kuzitoa kwenye gazeti la Tanzania Daima, nilimfuata Mhariri (wakati huo alikuwa Ansbert Ngurumo) nikaripoti jambo hilo, na sheria zikafuata mkondo ingawa niliwaomba wasimfukuze kazi yule binti...