Ulimwengu wa mapenzi

Mimi hapa mungwana ninazo hizo tabia
ukweli ninaunena watu wanausikia
kipembeni wanongona maovu kunizulia

Hakika mi habari sina bukheri nimetulia

Uongo wanizulia, walahi sijaunena
tena wanishadidia, wala ukweli hauna
Wacha wako ufisadi, ukweli moyoni huna

Imani yako hupimwa, ovyo hapana ropoka

Tenda wema wende zako, usingoje shukurani,
Yalo mema ya wenzako, yazingatie moyoni,
Usitaje mema yako, kwa fakhari duniani,

Tenda wema usahau, usingoje shukurani.

Muungwana sina shaka nimeswafi yangu nia
Yazidi yangu baraka Mola aniongezea
Yangu yote yanyooka wewe watanga na njia

Wala sito hadhirika kama ulofikiria

Pasta hujanielewa, umekazana na kufoka
sijui umeshalewa, ama kufungwa na Kaka
ubeti (#)3 waongelewa, posti sabini na tatu
sa sema uongo upi, kama si kujifanya fisi!!!!!!!
 
Pasta hujanielewa, umekazana na kufoka
sijui umeshalewa, ama kufungwa na Kaka
ubeti (#)3 waongelewa, posti sabini na tatu
sa sema uongo upi, kama si kujifanya fisi!!!!!!!

Muongo umeniita, adui asiye haya
Betizo ukazikita, muovu tena mbaya
Heshima umeipita, penye uso wa duniya

Kwa kuniita muongo kwa kosa langu ni lipi

Pombe adui wa siha, si matunda ya mwilini
Uso meumbwa na haya, sithubutu asilani
Sihiweki kwenye kaya, madhambi hao ya nini

Matendo mtu mlevi, kinyume na yangu dini

Viumbe kuwaheshimu, tulifundishwa mapema,
Wadogo na wamakamu, wote hupewa heshima,
Twakatazwa kudhulumu, hata porini wanyama,

Adabu tabia njema, pambo langu Islamu.
 
bi dada hongera kwa kuling'amua mapema
maana ungepata presha,ukalazwa hospitali
mwaga lililo moyoni ili upate kupona
songa mbele bi dada,mapenzi yaishi milele!!

umu ndani watu mko juu?ushairi mzuri sana...maana nimecheka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom