Ulimwengu wa mapenzi

Mj1 kweli maji yamefika kwa shingo,mwachie mbawa zote kwangu adondoke,nimpe ya motomoto yako asikumbuke,madoido alokuletea yote yamtoke,ila nakuomba chonde tena usimtake!!!
 
Mj1 kweli maji yamefika kwa shingo,mwachie mbawa zote kwangu adondoke,nimpe ya motomoto yako asikumbuke,madoido alokuletea yote yamtoke,ila nakuomba chonde tena usimtake!!!

Ahahah mchaji umenifanya nicheke katikati ya machungu. Well

Huyu kwako mchukue, chumbani ujiwekee
Na massage umchue, limbwata umuwekee
Yatakuja kufikie, na mie nichekelee
ninakupa wote wote, mimi nishamkinai.

namshukuru muumba, macho kanifunulia
kusahau ameumba, mema kunifunulia
moyo wangu nimefumba, penzile kutolilia
ninakupa wotewote, mimi nishamkinai.


Kila la heri
 
usimtose jamaa, kaeni muongee myamalize huko utakakokwenda utaona afadhali ya kwa zamani. ujasikia watu wanasema kila kukicha afadhali ya jana
 
Shosti unaniangusha, kujiliza hadharani
Chati unampandisha, kakufanya hayawani
Bure unajikondesha, nakujishusha thamani
Amekufanya wa nini, mfanye wa kazi gani.

Mfanye wa kazi gani, amekufanya wa nini
Akipita mtaani, mvalie na miwani
Mmekutana ukubwani, majonzi sasa ya nini
Ulimwengu wa mapenzi, na wewe bado ni memba.

Na wewe bado ni memba, ulimwengu wa mapenzi
Hutakiwi kwenda Pemba, kuyatafuta mapenzi
Wanamuziki waimba, yalianza toka enzi
Aliye na niya hasa, penzi usimbanie.

Penzi usimbanie, aliye na niya hasa
Ila usikimbilie, Fidel Chrispin Masa
Hapana watamkie, usije wapa hamasa
Mbili zero moja mbili, ndoa zao watangaza.

Ndoa zao watangaza, mbili zero moja mbili
Hawajaenda angaza, wameahirisha mara mbili
Hapa nakupa mwangaza, silazimishi ukubali
Ukitala alosoma, jiulize pia why?

Jiulize pia why, ukitaka alosoma
Ningeshauri Bluray, ila kingereza chake noma
Anaongea in a way, tafsiri zinagoma
Pedejee sishauri, unless wahusudu.

Hiki kinaitwa KIPAJI..Safi sana Lizy,Mungu kakujalia kwa kweli!
 
Shosti unaniangusha, kujiliza hadharani
Chati unampandisha, kakufanya hayawani
Bure unajikondesha, nakujishusha thamani
Amekufanya wa nini, mfanye wa kazi gani.
..................
Jiulize pia why, ukitaka alosoma
Ningeshauri Bluray, ila kingereza chake noma
Anaongea in a way, tafsiri zinagoma
Pedejee sishauri, unless wahusudu.

Marhabaa!,

Sinalo la kuongeza, na mimi nakusapoti
kama Pele umecheza, ninayarusha manoti!
Ni mengi umemjuza, nakutolea saluti
Tumebaki navidoti, vichwani tunavijaza!

Vichwani tunavijaza, tulivyoweka vidoti
kwa kina ukaeleza, asije kumpa chati
Apate pia mwangaza, amvalie na koti
Nakutolea Saluti, kama Pele umecheza!

Aendelee kuzoza, asidhanie hapati
Mapenzi anayaweza, na tena ana bahati
Mwanajamii waweza, umeambiwa kwa dhati!
Ni mengi amekujuza, na siyo ya kisaliti!

 
Marhabaa!,

Sinalo la kuongeza, na mimi nakusapoti
kama Pele umecheza, ninayarusha manoti!
Ni mengi umemjuza, nakutolea saluti
Tumebaki navidoti, vichwani tunavijaza!

Vichwani tunavijaza, tulivyoweka vidoti
kwa kina ukaeleza, asije kumpa chati
Apate pia mwangaza, amvalie na koti
Nakutolea Saluti, kama Pele umecheza!

Aendelee kuzoza, asidhanie hapati
Mapenzi anayaweza, na tena ana bahati
Mwanajamii waweza, umeambiwa kwa dhati!
Ni mengi amekujuza, na siyo ya kisaliti!
take 5
 
Hasira inanijia, wangu moyo kuchukia
Ya nini kung'ang'ania, ua lisilochipua
Ni muda nimeusia, safari kujifungia
Ona sasa lilokufika, madonda yasofutika

Mbili alfu nayo tisa, ulishajiamulia
Kumi mwezi katikisa, nikajua watulia
kiberiti kutikisa, njiti tele metulia
Ona sasa lilokufika, madonda yasofutika

Sasa koma mwana koma, sijesikia kilia
Sijipalie ukoma, ukaja kulia lia
Nitakutoa na ngoma, uzomewe mitaani
Tamati utamatie,mapenzi si yako dhima
 
Huyu analipenda limtu lisilo mpenda na kumjali sasa mm nampenda yeye hanipendi umeona sasa ni vice versa mtu umpendae yeye hakupendi na unae mpenda nae hakupendi.


usiombe kukutwa na hiyo hali ya kupenda usipopendwa,
 
NIPASIENI MIE JAMANI MBONA ANATABIKA BURE NA SIE TUPO MJ1 COME BABY UTATULIA
UMEWAHI KULA SUKARI GULU WEYE
cONQUEST-ATM YANGU INATOA 500/-
 
Salamu tumepokea, pole nakusambazia
walokwisha tangulia, ujumbe menitumia
pole wanakutwangia, kwa yaliyokufikia
-wasema-
jambo lisilokuua, nguvu lakuongezea.

Tangu kale tumeona, kupendwa kukataliwa
tulodhani wapendana, mioyo wakavunjiwa
kisha wakaapa sana, bada ya kusalitiwa
keshoye wakapatana, sa waruka kama njiwa.

Sisemi tu kukubeza, nimeyaona jameni
sasa unaona kiza, pendo tena hulioni
safari kaikatiza, machozi tele moyoni
thamani ya pendo skiza, utaipata mbeleni.

Leo unajililia, kisa amekukataa
kesho utafurahia, umpatapo Jambia
sababu mejionea, machungu na raha pia
MJ we tulia, kesho tanihadithia.

Sa Nyutoni alisema, mapenzi ni kama nguvu
wezi vunja ta kwa chuma, ila waweza hamisha
toka Peter kwenda Juma, au Anna kwenda Asha
kamwe usikate tama, bahati haijesha!
 
Wasalaamu salamuni, waungwana nawajia
Mababu wa mizimuni, walokwisha tangulia
Najongea kwa huzuni, najizuia kulia
ulimwengu wa mapenzi, buriani aagia

Ulimwengu wa mapenzi, buriani naagia
naondoka kwa majonzi, mlango najifungia
Si wangu nimemaizi, moyo nafungulia
Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka

Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka
Umeyataka mabawa, meupe yaso na taka
Nimechoka kupagawa, na penzi lenye mashaka
Ulimwengu wa mapenzi, nawaachia wenye bahati.

Mwana jamii sikia, usia nakupatia
mapenzi yana udhia, kweli ninakuambia
Wengi walivumilia, Wakaishia kulia

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia

Utampenda fulani, kwa yako yote nia
kamuweka fuwadini, Na moyoni kamtia
Atakudharau chini, kulia ukaishia

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia

Njoo kwangu nakuasa, penzi nitakupatia
Uje ule sambuasa, na mikate ya sinia
Utasahau kabisa, moyoni nashuhudia

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia

Beti nne kadi tama, mbele sitoendelea
Takuachia mtima, Moyo wangu upokea
Usibaki tena nyuma, hima na hima jongea

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia
 
Mwana jamii sikia, usia nakupatia
mapenzi yana udhia, kweli ninakuambia
Wengi walivumilia, Wakaishia kulia

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia

Utampenda fulani, kwa yako yote nia
kamuweka fuwadini, Na moyoni kamtia
Atakudharau chini, kulia ukaishia

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia

Njoo kwangu nakuasa, penzi nitakupatia
Uje ule sambuasa, na mikate ya sinia
Utasahau kabisa, moyoni nashuhudia

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia


Beti nne kadi tama, mbele sitoendelea
Takuachia mtima, Moyo wangu upokea
Usibaki tena nyuma, hima na hima jongea

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia

Ustaadh , mafunzo ya dini yanaruhusu kutongoza ONLINE?..Bwe hee he he..
 
Mwana jamii sikia, usia nakupatia
mapenzi yana udhia, kweli ninakuambia
Wengi walivumilia, Wakaishia kulia

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia

Utampenda fulani, kwa yako yote nia
kamuweka fuwadini, Na moyoni kamtia
Atakudharau chini, kulia ukaishia

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia

Njoo kwangu nakuasa, penzi nitakupatia
Uje ule sambuasa, na mikate ya sinia
Utasahau kabisa, moyoni nashuhudia

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia

Beti nne kadi tama, mbele sitoendelea
Takuachia mtima, Moyo wangu upokea
Usibaki tena nyuma, hima na hima jongea

Mapenzi yataka moyo, kweli ninakuapia

Mkuu....kumbe nawe huvumi lakini umo.......Safi sana aisee
 
Mkuu tupo tuna jaribu jaribu tu...!
Pasta acha uongo, Mola anakuona
wewe umo ka kigongo, bahati sijaiona
umeiva kama gongo, mashairi yalotuna

ila acha uongo, kujipigia pasi!


acha kujipiga pasi, subiri akukubali
usilazimishe nafsi, kupenda sipokubali
moyowe huna nafasi, kupenda kusipojali

ashaumizwa jamani, subiri we ahueni.


Kizuri kinajiuza, wahenga walishasema
kibaya chajitembeza, hilo alisema mama
iweje leo kupaza, pendo wataka kufuma

kupenda ye hatoweza, moyowe unamuuma!


Mvumilivu hula mbivu, tena walituambia
kama wazitaka mbivu, mawe hutazitupia
tena uwe msikivu, wa nyakati na hisia

usimtolee uvivu, sababu ameumia!

<usisubiri kuwa fisi kufuata vilojeruhiwa>
 
Pasta acha uongo, Mola anakuona
wewe umo ka kigongo, bahati sijaiona
umeiva kama gongo, mashairi yalotuna

ila acha uongo, kujipigia pasi!


acha kujipiga pasi, subiri akukubali
usilazimishe nafsi, kupenda sipokubali
moyowe huna nafasi, kupenda kusipojali

ashaumizwa jamani, subiri we ahueni.


Kizuri kinajiuza, wahenga walishasema
kibaya chajitembeza, hilo alisema mama
iweje leo kupaza, pendo wataka kufuma

kupenda ye hatoweza, moyowe unamuuma!


Mvumilivu hula mbivu, tena walituambia
kama wazitaka mbivu, mawe hutazitupia
tena uwe msikivu, wa nyakati na hisia

usimtolee uvivu, sababu ameumia!

<usisubiri kuwa fisi kufuata vilojeruhiwa>

Mimi hapa mungwana ninazo hizo tabia
ukweli ninaunena watu wanausikia
kipembeni wanongona maovu kunizulia

Hakika mi habari sina bukheri nimetulia

Uongo wanizulia, walahi sijaunena
tena wanishadidia, wala ukweli hauna
Wacha wako ufisadi, ukweli moyoni huna

Imani yako hupimwa, ovyo hapana ropoka

Tenda wema wende zako, usingoje shukurani,
Yalo mema ya wenzako, yazingatie moyoni,
Usitaje mema yako, kwa fakhari duniani,

Tenda wema usahau, usingoje shukurani.

Muungwana sina shaka nimeswafi yangu nia
Yazidi yangu baraka Mola aniongezea
Yangu yote yanyooka wewe watanga na njia

Wala sito hadhirika kama ulofikiria
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom