Ulimwengu wa mapenzi

Sijalizwa ilikuwa kidogo nilizwe, mpaka nilipompiga marufuku mshori wangu kuimba kwaya.
Dah umeongea kweli,hizi kwaya hizi zinaharibu watu mara nyingi.hasa hawa makwaya masta.Na kwenye kwaya kukuta watu pair si ajabu.Hata Lucifer a.k.a shetani,a.k.a ibilisi naye alikuwa kwayamasta ndio maana ile dhambi inaendelea.
 
Unaonaje tukianzisha kwaya yetu?
 
La nini hilo agano, njoo nikufungulie

Nieleze shida yako, mimi nikutatulie,

Nshafanya mchakato, kwangu mimi utulie,

Ulimwengu wa mapenzi, ni wetu mimi na wewe!

Ya nini yote majonzi, kwangu ndo umefika,
Nitakupa hevi dozi, utaipenda hakika,

Nimehitimu na kozi, ya mapenzi tikatika

Ulimwengu wa mapenzi, ni wetu mimi na wewe!
 
Makubwa,Chrispin nae anataka kuanzisha kwaya nicheke mie

Msindima utakuwa sauti ya kwanza na MJ1, zd na FL1 ya pili, mpwa fidel ya tatu, binamu Nguli ya 4,Mchungaji Masanilo meneja wa kwaya, katekista Geoff mshauri wa kwaya na shemasi mimi ntakuwa kwaya master. Lol! Rose Mhando haoni ndani kwa mauzo ya albam.
 
Ewaa,lakini mimi namudu sauti zote ya kwanza mpaka ya tatu,na hata ukitaka niwe mwalimu wa kwaya niko fit,haya taja jina la kwaya,nani atakuwa mwenyekiti wa kwaya na mtunza pesa je?
 
Ewaa,lakini mimi namudu sauti zote ya kwanza mpaka ya tatu,na hata ukitaka niwe mwalimu wa kwaya niko fit,haya taja jina la kwaya,nani atakuwa mwenyekiti wa kwaya na mtunza pesa je?

NiPM basi tutete zaidi, hapa lazima pana mpango wa Mungu.
 
Wasalaamu salamuni, waungwana nawajia
Mababu wa mizimuni, walokwisha tangulia
Najongea kwa huzuni, najizuia kulia
ulimwengu wa mapenzi, buriani aagia

Ulimwengu wa mapenzi, buriani naagia
naondoka kwa majonzi, mlango najifungia
Si wangu nimemaizi, moyo nafungulia
Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka

Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka
Umeyataka mabawa, meupe yaso na taka
Nimechoka kupagawa, na penzi lenye mashaka
Ulimwengu wa mapenzi, nawaachia wenye bahati.

Now you are talking, bora kulivua pendo kuliko kuteseka kila kukicha..
 
NiPM basi tutete zaidi, hapa lazima pana mpango wa Mungu.

Mchungaji Chrispin umefunuliwa na Bwana kuhusu hii kwaya?halafu wewe uwe kwaya masta? hata sikuamini kama unaweza kulitangaza neno wewe kwa uaminifu. Mpiga Kinanda atakuwa nani?
 
La nini hilo agano, njoo nikufungulie
Nieleze shida yako, mimi nikutatulie,
Nshafanya mchakato, kwangu mimi utulie,
Ulimwengu wa mapenzi, ni wetu mimi na wewe!

Ya nini yote majonzi, kwangu ndo umefika,
Nitakupa hevi dozi, utaipenda hakika,
Nimehitimu na kozi, ya mapenzi tikatika
Ulimwengu wa mapenzi, ni wetu mimi na wewe!

Magehema

Zangu nazitanguliza, shukurani zipokee
Unataka niliwaza, huzuni inipotee
Nimekula nimesaza, wali nyama na matonge
Nimeomba pumzika, naomba nikubalie

Nimeomba pumzika, naomba nikubalie
Nayachelea masika, mbani nende jililie
Nayaogopa majoka, moyo sijejipatie
Nakimbiza zangu mbawa, yatosha yalonifika.
 
Leom utatunga mashairi mpaka utakoma.
 
Mchungaji Chrispin umefunuliwa na Bwana kuhusu hii kwaya?halafu wewe uwe kwaya masta? hata sikuamini kama unaweza kulitangaza neno wewe kwa uaminifu. Mpiga Kinanda atakuwa nani?

Yaani kwa kweli Chriss akiwa kwaya masta sijui itakuwaje?bora umeliona hili la kutangaza neno kwa uaminifu,staki kulisemea sana kwa huyu kwaya masta wetu maana mmmmmhhh.

Usishangae akikwambia mpiga kinanda atakuwa Fidel80,mbona hapo kwaya itakuwa kwaya.
 
Pole dada pole, pole mwana jamii
mapenzi polepole, ndani ya yetu jamii
ulianza hisi polepole, ukadhani huumii
sasa yamegonga kole, watutangazia jamii

nimekusoma kwa kitambo, kwenye forum ya jamii
unalalama kimtindo, ewe mwanajamii
wengi tuliona kombo, kama wana jamii
tukasema mweke kando, akuumizaye mwanajamii

Vera na nyamayao, walikupa zao bidii
wote jinsia yao, walijituma kwa bidii
vidume ni kama zao, wakaanza kwa bidii
wakakaa kimkao, wakusherehe kibidii

lakini hadi sasa, ewe mwana jamii
sipati hata msasa, na kuelewa hii jamii
ni vipi twatakasa, tena kwa zetu bidii
kutoa ndoa takasa, ya Muumba kwa bidii?

MTM

Uamuzi nimetoa, nachelea urejea
wangu moyo nilitoa, yeye akauchezea
kitambo ningelitoa, subira nikarejea
ningeyajua ya moyo, katu singeliumia

Natizama pembe kona, faraja kuitafuta
Ili nipate kunona, mwili upate mafuta
nimekonda kila kona, kama mche wa ufuta
laiti ningeyajua, katu singeliumia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom