Nikimpigia simu jioni anasema ametoka kazini amechoka nijaribu (sio nimpigie na uhakika) asubuhi, nikimpigia asubuhi hapokei nikipiga mchana ananiambia alikuwa kwenye foleni asubuhi asingeweza kuongea na muda huu yupo kazini na boss wake yupo hivyo niwe mpole atapiga. Hapigi mpaka jioni, nikimtafuta ananiambia nisubiri afike home. Kwahiyo siku mbili nzima mzunguko ulikuwa huo nikaona huu ni ufala. Nikamlamba pini moja nzito mpaka kwenye social network kisha nikafuta namba zake zote na call history.
Nilikaa kama wiki tatu nikaingia kusoma spam messages nikakuta meseji zake nyingi akilalamika na ya mwisho akaandika asante. Makisudi nikampigia nikamuuliza "wewe nani, nimekuta meseji zako kwenye simu yangu." Akauliza kama nimeshafuta namba yake nikamwambia ajitambulishe sikumbuki. Akataja jina nikamwambia endelea na kazi za boss wako kisha nikakata.
Kalinifanya nikawa na moyo mgumu kwa mwanamke. Sasahv hata nikiamka asubuhi nikaambiwa naondoka najibu poa fanya chap.