Hii biashara nilikua nafuata mwenyewe songea na baada ya kuzoeana sana na wauzaji walikuwa wananipa kwa mali kauli nije kuuza DSM halafu nikiuza natuma hela aisee kwa mara ya kwanza nilishika 1M kupitia hii biashara.
Sema utoto ulikua mkubwa kupiga pumbu halafu baadae nikawa naendekeza kulemba chumba tu bila kuwekeza kwingine jambo ambalo niliwekeza nalo halikunilipa nilinunua boda boda(biashara kichaa). Baadae nikahama Dar niende mkoa kusoma(huu ndo usenge mkubwa nilifanya) kwani nilipoteza wateja na connection maana nilikua nimemuachia mtu akawa ana devela mwisho ikawa chali.
Niliporudi DSM nikataka kuirudia nikafeli nikapotezea kwani masoko yale yalikua yashachukuliwa na watu wengine. Mimi nilikua nachukua mzigo songea labda wa laki 3 naleta DSM kisha nasambaza kwenye magenge makubwa wanauza mzigo ukiisha ndani ya siku 5-7 nafuata mpunga nilikua na soko la uhakika sana na faidi ilikua nusu kwa nusu.
Mafanikio niliyofanya kupitia Dagaa nyasa 2017-2018

Kununua boda boda 1

Vitu vya ndani vya kisasa

Kufungua akaunti ya bank ilifika hadi 3M.

Kujitegemea kula,kuvaa na kodi

Exposure ya kusafiri sana na kuyajua maisha.