Ngoja nihadithie kidogo kuhusu yanayonikuta halafu mnipe ushauri
Kabla chuo hakijafungwa last year,Nilikuwa nipo hostel ila nilianza kupiga mishe kitaa ili nijikusanye nianzishe maisha nikiwa kwangu coz hostel kunachosha sana na inaweza kukufanya usiwaze nje ya hostel pekeee........kweli nikapata pesa kiasi ila zilikuwa zinatosha kuanza kupanga
Kuna jamaa yangu sana,wa kishua kweli alinitafuta akaniambia nikaishi nae nyumbani kwao coz anaishi yeye pamoja na Bi'Mkubwa wake na Kuna time uwa hali yake haipo Sawa,so anahitaji msaada wangu kwa hilo pekee (Jamaa ana matatzo ya kupoteza kumbukumbu............Nikakaa nikasema OK poa twende nyumbani,jamaa akanitambulisha kwa Maza ake,mwanzoni yule mama alinikubali na akanichukulia mimi kama mwanae wa kumzaa maana chochote atacho mletea jamaa basi na me lazima angeniletea
Hivi majuzi huyu maza kaanza kubadilika ghafla,nikimsalimia anaitikia kama hataki na kwa dharau sana,anajitungia makosa halafu ananibambikizia mie
Leo nimeamka nikamkuta anaongea na simu,alivyoniona akaongeza Saudi na maneno aliyosema ni haya;
"Kuna mtu kaja kuniharibia budget nyumbani kwangu,anakula tu na wala hajui vinetoka wapi
Muda sio mrefu nahama