Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
18,266
54,427
Nawasalimu wanaJF.
Leo nimeamua niseme ukweli kuhusu nchi yetu hii ya Tanzania.

Katika miaka 24 ya utawala wa Mwalimu Nyerere, alitangaza maadui wakubwa wa watatu wa watanzania:-
1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI

Mwalimu Nyerere hakuwa visionary leader alikuwa mwanaharakati, badala ya kujenga nchi na kuwapatia elimu watanzania alikuwa na misemo tu, kuongea majukwaani tu bila vitendo.

Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kujenga shule za msingi kila kijiji kwa miaka yote hiyo 24 badala yake akajenga ofsi za chama kila kijiji?

Je, kitu gani Mwalimu Nyerere kilimshinda kwa miaka 24 kujenga vyuo vya ufundi kila wilaya badala yake alijenga viwanja vya mpira wa miguu?

Lowassa aliweza kujenga shule za secondary kila kata. Je, Mwalimu Nyerere kitu gani kilimshinda kwa miaka 24 kujenga Shule hizo?

Tunaweza kutafuta mchawi wa taifa letu. But kusema kweli Nyerere alitukosea sana watanzania.

Nadhani Mwalimu Nyerere alikuwa na mentality za utawala wa kifalme ambao hauna malengo.

Tunaona mataifa mengi yaliyowekeza kwenye elimu alivyopiga hatua.

Yeye Mwalimu Nyerere hakuwa na nia kabisa ya watanzania wengi kupata elimu. Wakati wa Mwalimu Nyerere kusoma ilikuwa ni bahati na siyo haki ya Mtanzania.

Taifa lisilokuwa na elimu haliwezi kujiendesha vizuri, litabaki kuwa ombaomba tu.

Sisi kama Taifa ni lazima tujue tulipoangukia, tukainuke na kusonga mbele. Bado hatujachelewa.

Tanzania tupo na vijiji na mitaa isiyozidi 20,000. Kwani alishindwa nini kuchukua kila kijiji vijana 10 na kuwapeleka kusoma nchi za nje? Vijana 10 kila kijiji maana yake ni watanzania 200,000 tu.

Yaani angechukuwa wanawake 5 na wanaume 5.
But uwezo alikuwa nao wa kufanya hivyo.

Nitaendelea kueleza machungu yangu haya kwenye uzi huu ili tujue wapi tulipoangukia tukainuke na kusonga mbele...
 
Nyerere unamuonea bure.

Nyerere amekuta nchi iko so disorganized, magonjwa, ujinga, umaskini wa kutupwa na ukabila

Nyerere alikua na mlima mrefu sana wa kupanda, kwanza kuhakikisha chembechembe za ukabila zinakufa na kuleta umoja, kupambana na ujinga, kuhakikisha watu wanajua hata kusoma na kuandika. Ulitaka awape elimu gani kama hata kusoma na kuandika hawajui? Ulitaka awape elimu ya uraia wakati hata kusoma hawajui?

Mwalimu kakuta pepopunda, surua, polio, kifua kikuu, kifaduro, kwashakoo na magonjwa mengine yametamalaki kwa watanzania, ulitaka awape alimu ya uraia huku akiwaacha wafe?

Mwalimu kakuta Watanzania ni mafukara wa kutupwa, hawana matumaini ya kesho, akaanzisha vijiji angalau wawe pamoja ili iwe rahisi kuwaletea maendeleo kwa sababu walikua so scattered and disorganized, akaanzisha mashamba ya ushirika ama sustainable farming, akahakikisha anapeleka watu shule wakasome waje wampokee ma kubadilisha nchi kina Chenge na wengine, matokeo yake, wamekua wezi.

Nyerere alipigana kuanzisha viwanda, mashamba ya vijiji, na mambo mengine mengi bila kuuza ardhi hata kipande kimoja kwa waarabu wala wazungu.

That man died poor, had nothing kwa kuwapigania Watanzania

Na alivyokua mwema yule bwana, alipotoka madarakani aliangalia nyuma, akaona failures zake na success zake, akakiri kwamba kweli kuna mahala alifeli, na sababu kubwa za failure za mwalimu zilikua nje ya uwezo wake, kumbuka oil crisis and financial crisis za 70s and 80's.

Yule jamaa alipoona he can continue failing, akajipumzikia yeye mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yeyote. Angeweza kufia madarakani.

Tukubaliane kwamba CCM ndio ya kulaumiwa, ila kumpa Nyerere zigo la lawama ni kumuonea. Yule bwana aliachia hii nchi miaka zaidi ya 35 iliyopita, hao wengine waliofuata walifanya nini?
 
Kuhusu katiba.
Mwalimu Nyerere alikuwa na nafasi kubwa mno ya kutengeneza nchi yenye katiba nzuri na yenye kujali wananchi.

Kwa miaka yote hiyo 24. Mwalimu Nyerere aliamua kuishi na katiba iliyokuwa inamlinda yeye. Alijiwekea madara yote bila kutenga.
Rais ndiye:-
1. Mkuu wa nchi
2. Mkuu wa serikali
3. Amiri jeshi mkuu.

Halafu Rais huyo anakuwa nguvu kubwa kwenye chama. Inakuwa ngumu kuweza kumdhibiti kwenye matumizi mabaya ya cheo.

Alishindwa nini kuweka kuwa Waziri Mkuu kuwa Mkuu wa serikali na raisi akabaki kuwa Mkuu wa nchi na Amiri jeshi mkuu? Uwezo huo alikuwa nao lakini kwanini hakufanya hivyo?
 
Mwl alifeli pia kwa kukitukuza kiswahili na kukipromote kuwa lugha ya taifa .
Tunetengeneza taifa ambalo lipo isolated sana na dunia. Watu wanahitaji akina mkandara kutafsiriwa cnn english news.
 
Nyerere unamuonea bure.

Nyerere amekuta nchi iko so disorganized, magonjwa, ujinga, umaskini wa kutupwa na ukabila

Nyerere alikua na mlima mrefu sana wa kupanda, kwanza kuhakikisha chembechembe za ukabila zinakufa na kuleta umoja, kupambana na ujinga, kuhakikisha watu wanajua hata kusoma na kuandika. Ulitaka awape elimu gani kama hata a lawama ni kumuonea. Yule bwana aliachia hii nchi miaka zaidi ya 35 iliyopita, hao wengine waliofuata walifanya nini?
Alikaa ikulu kwa zaidi ya miaka 20 ! Bado alishindwa ku organise hata katiba tu?
 
Nyerere unamuonea bure.

Nyerere amekuta nchi iko so disorganized, magonjwa, ujinga, umaskini wa kutupwa na ukabila

Nyerere alikua na mlima mrefu sana wa kupanda, kwanza kuhakikisha chembechembe za ukabila zinakufa na kuleta umoja, kupambana na ujinga, kuhakikisha watu wanajua hata kusoma na kuandika. Ulitaka awape elimu gani kama hata kusoma na kuandika hawajui? Ulitaka awape elimu ya uraia wakati hata kusoma hawajui?

Mwalimu kakuta peppunda, surua, polio, kifua kikuu, kifaduro, kwashakoo na magonjwa mengine yametamalaki kwa watanzania, ulitaka awape alimu ya uraia huku akiwaacha wafe?

Mwalimu kakuta Watanzania ninfukara wa kutupwa, hawana matumaini ya kesho, akaanzisha vijiji angalau wawe pamoja ili iwe rahisi kuwaletea maendeleo kwa sababu walikua so scattered and disorganized, akaanzisha mashamba ya ushirika ama sustainable farming, akahakikisha anapeleka watu shule wakasome waje wampokee ma kubadilisha nchi kina chenge na wengine, matokeo yake, wamekua wezi.

Nyerere alipigana kuanzisha viwanda, mashamba ya vijiji, na mambo mengine mengi bila kuuza ardhi hata kipande kimoja kwa waarabu wala wazungu.

That man died poor, had nothing kwa kuwapigania Watanzania

Na alivyokua mwema yule bwana, alipotoka madarakani aliangalia nyuma, akaona failures zake na success zake, akakiri kwamba kweli kuna mahala alifeli, na sababu kubwa za failure za mwalimu zilikua nje ya uwezo wake, kumbuka oil crisis and financial crisis za 70s and 80's.

Yule jamaa alipoona he can continue failing, akajipumzikia yeye mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yeyote. Angeweza kufia madarakani.

Tukubaliane kwamba CCM ndio ya kulaumiwa, ila kumpa Nyerere zigo la lawama ni kumuonea. Yule bwana aliachia hii nchi miaka zaidi ya 35 iliyopita, hao wengine waliofuata walifanya nini?
Mwalimu Nyerere alitawala miaka 24. Niambie kwanini aliweza kujenga viwanja vya mpira kila mkoa? Kwanini aliweza kujenga ofsi za chama kila kijiji?

Alishindwa nini kuweka sera hata ya miaka 5 kujenga shule za sekondari kila kata kama alivyofanya Lowassa?

Yaani yapo mataifa mengi tu tulikuwa sawa nayo wakati tunapata uhuru lakini waliwekeza kwenye elimu. Nchi za Malaysia, Thailand nk.

Waliwekeza kwenye elimu. Alishindwa nini kujenga shule za msingi kila kijiji?
 
Kuhusu katiba.
Mwalimu Nyerere alikuwa na nafasi kubwa mno ya kutengeneza nchi yenye katiba nzuri na yenye kujali wananchi.

Kwa miaka yote hiyo 24. Mwalimu Nyerere aliamua kuishi na katiba iliyokuwa inamlinda yeye. Alijiwekea madara yote bila kutenga.
Rais ndiye:-
1. Mkuu wa nchi
2. Mkuu wa serikali
3. Amiri jeshi mkuu.

Halafu Rais huyo anakuwa nguvu kubwa kwenye chama. Inakuwa ngumu kuweza kumdhibiti kwenye matumizi mabaya ya cheo.

Alishindwa nini kuweka kuwa Waziri Mkuu kuwa Mkuu wa serikali na raisi akabaki kuwa Mkuu wa nchi na Amiri jeshi mkuu? Uwezo huo alikuwa nao lakini kwanini hakufanya hivyo?
Upande wa katiba tunaweza kumlaumu.

But anamambo yake mazuri ambayo tukiyapima hakuna mwingine aliefuata ana weza mfikia

Nayo ni uadilifu kama kiongozi, uzalendo, Uchapa kazi, nk

Imagine alikataa watu wasichimbe madini kisa tu hatuna watz wenye elimu ya kutosha kutusaidia kusimamia hili zoezi. Akaendesha nchi kwa kilimo cha pamba na karafuu

Jamaa alikua mtu wa style yake
 
Yule jamaa alipoona he can continue failing, akajipumzikia yeye mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yeyote. Angeweza kufia madarakani.
Acha kutuongopea wewe Mwalimu aling'atuka kutokana na mabadiliko ya falsafa za mabepari kuanza kuzidi nguvu ujamaa.
Mwl alikuwa mjamaa hivyo isingekuwa rahisi kufuata sera za kibepari wakati alikuwa akiziponda.

Suala la kuunganisha vijiji mnalipa ukubwa tu Wala halikuwa kubwa.

Miaka 24 ni mingi ilitosha kabisa kutuachia taifa lisilo na Uchawa.
 
Wakati tunapata uhuru 1961 population ya Watanzania ilikuww 10.3m.

Miaka 24 ya utawala wa mwalimu Nyerere hakuweka kipaumbele kwenye elimu. Utaratibu ulibaki uleule mpaka leo. Eti kiongozi wa kisiasa sifa yake ni kujua kusoma na kuandika tu!!!

Mtu hajui hata sera za nchi, hajui hata international politics, hajui hata Historia ya taifa lake, hajui hata jiografia anakuwa Kiongozi. Alishindwa kuwapa kipaumbele viongozi wa kisiasa ili kwamba yeye aendelee kutawala tu.

For 24 years alishindwa kuweka utaratibu mzuri wa upatikanaji wa viongozi. Mpaka leo hii zimwi hili linatumaliza. Unakuta mtu anachaguliwa kuwa mbunge hajui chochote kuhusu nchi hii.

Ni hatari mno.
 
Nawasalimu wanaJF.
Leo nimeamua niseme ukweli kuhusu nchi yetu hii ya Tanzania.

K
Huyu huyu Nyerere alilea Dini yake ya ukatoliki kwa kukandamiza madhehebu mengine ya kikristu, mpaka wakatoliki wanajiona wana steki kubwa kufanya uamuzi zaidi ya dini zingine kuhusu serikali, kimya kimya alikua ana promote ukatoliki serikalini kwa kuwapa vyeo mbali mbali na huku nje anaonyesha iko sawa kwa wote, Nyerere alikua Mdini wa chini chini.
 
Mwl alifeli pia kwa kukitukuza kiswahili na kukipromote kuwa lugha ya taifa .
Tunetengeneza taifa ambalo lipo isolated sana na dunia. Watu wanahitaji akina mkandara kutafsiriwa cnn english news.
Hoja ya kipumbavu kabisa.

Hivi karne hii lugha nayo ni shida?

Watanzania wameshindwa kufanya nini kwa sababu ya kutokujua kingereza?

What an idiot.
 
Upande wa katiba tunaweza kumlaumu.

But anamambo yake mazuri ambayo tukiyapima hakuna mwingine aliefuata ana weza mfikia

Nayo ni uadilifu kama kiongozi, uzalendo, Uchapa kazi, nk

Imagine alikataa watu wasichimbe madini kisa tu hatuna watz wenye elimu ya kutosha kutusaidia kusimamia hili zoezi. Akaendesha nchi kwa kilimo cha pamba na karafuu

Jamaa alikua mtu wa style yake
Sasa kwa miaka hiyo 24 aliyokaa alifanya nini kutengeneza watanzania wenye elimu ya kuchimba hayo madini? Je alijenga shule ngapi za sekondari zinazofundisha mambo ya madini? Kumbuka alikaa 24yrs kwenye uongozi.

Alifanya nini sasa kuhusu watanzania kupata elimu ya madini? Ilimshinda nini kila wilaya kuchukua watu watano wakasomee madini kwenye nchi zilizokuwa zimeendelea.

Watu 5 kila wilaya kama upo na wilaya 100 maana yake ni wasomi 500 wa madini baada ya miaka sita. Alishindwa nini?
 
Wakati tunapata uhuru 1961 population ya Watanzania ilikuww 10.3m.

Miaka 24 ya utawala wa mwalimu Nyerere hakuweka kipaumbele kwenye elimu. Utaratibu ulibaki uleule mpaka leo. Eti kiongozi wa kisiasa sifa yake ni kujua kusoma na kuandika tu!!!

Mtu hajui hata sera za nchi, hajui hata international politics, hajui hata Historia ya taifa lake, hajui hata jiografia anakuwa Kiongozi. Alishindwa kuwapa kipaumbele viongozi wa kisiasa ili kwamba yeye aendelee kutawala tu.

For 24 years alishindwa kuweka utaratibu mzuri wa upatikanaji wa viongozi. Mpaka leo hii zimwi hili linatumaliza. Unakuta mtu anachaguliwa kuwa mbunge hajui chochote kuhusu nchi hii.

Ni hatari mno.
Sasa huyo mbunge aliechaguliwa na hajui chochote kuhusu nchi si kachaguliwa na watu kama wewe mnaoijua nchi ama alijichagua mwenyewe?

Yani watu hamtaki ku accept failures zenu, mnafanya blame shifting.
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom