Nawezaje kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere?

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
347
462
Kama Taifa, leo ni siku maalum ya kumkumbuka Mwal JK Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanganyika na Tanzania aliyefariki dunia mnamo tarehe 14 Oktoba 1999.

kuna vitu vingi sana vinatufanya tuendelee kumuenzi kutokana na mchango wake katika kulijenga taifa bora.

Haya ni mambo aliyosimamia na ambayo hadi sasa Watanzania na dunia kwa ujumla tunanufaika nayo.

1) Utu: Falsafa hii Mwalimu JK Nyerere aliisimamia vilivyo. Falsafa imewapa watu amani, ukarimu, nidhamu kazini, nk. Falsafa hii pia ilifanya watu wapate ajira, fursa bila kuangalia ni wa kabila gani au katokea upande gani wa nchi au hata dunia.

Pia, kwa sababu ya Falsafa hii ya Utu, Tanzania ilijitoa sana kupigania haki katika nchi zingine za Afrika.

2) Elimu inayofaa: Mwal. JK Nyerere alipambana sana kuondoa ujinga na si kupata vyeti visivyokuwa na tija. Watu wa rika zote walipata fursa ya kusoma ingawaje changamoto zilikuepo.

3) Kujitegemea: Mwalimu JK Nyerere alitaka sana Tanzania na mataifa ya Afrika yajitegemee. Alichukia umaskini.

4). Ni mengi sana

Hakika, Mwalimu JK Nyerere anastahili kuenziwa.
 
Kwa vitendo
e5142e5fa5cd47b7946a8864f48df889.jpg
 
Back
Top Bottom