Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Kwa taarifa ni kuwa scorpion anajulikana sana hapo kimboka na pia anafahamika na polisi kwa aina ya ukatili anao ufanya. Hata baada ya kufanya tukio hilo aliendelea kudunda barabarani kana kwamba hakuna kosa lolote alilo lifanya.
 
Ngoja mahakama ifanye kazi yake...pale pia si kuna madada poa?isije ikawa jamaa kala mzigo akagoma kulipa,mdada akaenda kumchongea kwa bauncer....ndo maana wanamtetea...maana anawasaidia kwa hilo labda!jambo baya ni kumtoa mtu macho huo ni uuaji tayari.
 
Mengi yamejificha tukianza sikia na upande wa Pili upepo utabadilika..

Hii inanikumbusha tukio la juzi tu huko Singida yule jamaa alietolewa ulimi upepo ulivyombadilikia kesi IPO kwake sasa kama mbakaji..

Tuiache mahakama ifanye Nazi yake.
 
Ujue mimi ninacho hoji nakunitia shaka ni kwamba
Mlalamikaji anasema alivamiwa akachomwa visu na nilimsikiliza akasema na kisu kingine alichomwa tumbo mbona hayo majeraha ya visu siyaoni????

Pili walimtoa macho tukio liliripotiwa na clouds na moja ya sheria za hospital na hadi uende na PF3 sasa vip hapa na mbona ile hali ya kutolewa macho inaoneka kama ni siku zimepita??? Mbona yule said hana majeraha?

Mlalamikaji tumemsikiliza lakini katika maelezo yake kuna kitu anajichanganya inamaana yeye hakufanya jitihadi zozote za kujiokoa?

Hapa kuna kitu hakiko sawa na hawa cloud FM wanaangalia upande mmoja tu wa shilingi kwa nini wasingempata na scorpion wamhoji?

Maana hainiingii akili mtu from nowhere aje akutoe macho inamaana hakukuwa na wanunuaji wengine hapo na iweje said afike tu wamtende, kama ni unyang'anyi kwa mujibu wa said anasema ilikuwa mida ya saa nne kama alikuwa anatafuta hela ya kula kwa nini hakwenda kuteka wengine??

Kibaka huwa kila siku usiku ni kazi yake haya basi ni watu wangapi wameripotiwa kutolewa macho na kwanini cloud FM hawakuwafikia kuwathibitishia wananchi kwamba ni tabia yake??
 
Huu Uzi umenifikirisha sana
Kesi itatajwa lini?

Watu wameuliza maswali dadisi japo wamepewa majibu ya kimuhemuhe flani hivi.

Ngoja nisubirie. Hadi sasa sina Upande wowote.
 
Pia ilikuaje said akubali kupelekwa buguruni na dereva wa bajaj aliyekutana nae juu kwa juu tena ucku mnene?
Hili swali hata mimi nimejiuliza sana. Yaan daladala tu ijaribu kupita njia za mkato huwaga ni shughuli sembuse bajaji ambayo umeikodi mwenyewe. Ukodi bajaji ya kwenda ubungo external Hlf ikupeleke buguruni?????? Ukubali kwenda buguruni hlf ulipe na uchukue tena Usafiri mwingine wa kukupeleka ulipotaka kwenda. Duh kweli Siku yako ikifika shida. Scorpion itakua alipanga njama na Serena bajaji. Hivyo yule dereva naye akamatwe alete ushahidi
 
Point ni, huyo jamaa hakuwa mhalifu kwa mujibu wa wakazi wa maeneo yale. Wao wenyewe wameshangaa iweje amtoe mtu macho?
Kila kitu kina first time, kama hakuwa mhalifu basi ndio hivyo kaanza sasa kwa kumng'oa mtu macho...
 
Kwanini mtu akiwa na mawazo tofauti, watanzania huwa tunaona ametumwa! Mtoa mada hakuna sehemu alipo-justify alichofanya mhusika lakini huwa ni vizuri kutoa haki ya kusikiliza upande wa pili kabla ya kuamua mihemko na huruma vitoe maamuzi.
Hawahawa ikijaonekana Scopion kasingiziwa wataanza kuwalaumu jeshi la polisi na viongozi wa serikali. Kuendeshwa na mihemko na hisia kunasababisha maamuzi mabovu au yasiyozingatia haki pande zote, mfano tukio la waalimu Mbeya day na kumtesa mwanafunzi ghafla viongozi wetu walisukumwa na hisia za huruma wakawafukuza chuo waalimu watarajiwa lakini naona wamepata habari halisi upande wa pili wamewasamehe wale waalimu. Hili ni janga jipya katika jamii yetu ukiachana na maadui wetu aliowataja Nyerere yaani Maradhi,Ujinga na Umaskini basi na mihemko na hisia vimeongeza maadui wetu wa maendeleo.
 
Unapoona wanandoa wanarudi nyumban NA kkukisiana siokwamba awana mchepuko.sikuwakifumaniwa ma watu ndio unajua hee hatayule
Usemalo ni kweli kabisa lakini yote yanawezekana inaweza kuwa sio Scorpion aliyemtoboa macho na kumpiga visu au ni kweli lakini chanzo sio wizi labda ugoni/usaliti wa mapenzi au kudhurumiana vitu n.k. tunachotaka police wafanye uchunguzi wa kina bila kuharakisha kesi ili kuwafurahisha viongozi au jamii iliyohuzunishwa na hali ya ndugu Saidi.
 
Nlmi mwenyewe siamini kama alihusika inawezekana wapo waliotumia jina lake vibaya baada ya kuona anawadhibiti sana
 
Nimepata hamu kubwa yakujua kilichopo nyuma ya pazia... Naomba Kwa yeyote aliye Na historia fupi ya hili tukio atuelezee,,, nikimaanisha
Tukio lilitokea lini?
Wapi Na akitokea au akielekea wapi Na kama alikotoka aliongozana Na yeyote
Nani alimpeleka kituo cha polisi kuchukua PF3 Na nikituo gani hicho??
Baada ya hapo alipelekwa Hosp. Gani Na alikaa Kwa muda gani??
Ni Hosp. Ngapi alizotembelea Na Kwa muda gani??
Aliyeibua hili Jambo ni Nani Na ni baada ya muda gani??
Aliyemuokota (msamalia mwema huyo) yupo wapi??
Jamaa (said) amepona tayri au bado... Na imechukua muda gani kupona,,, ikumbukwe ni majeraha mbalimbali Na hususani Na macho kutolea bila utaalam wakitabibu Nadhani ingelichukua muda).. Nategemea kuna madaktari watatusaidia katika hili,,,
Alimtambuaje kuwa mhusika ni nge??
Scorpion alikamatwaje??
Ni chombo kipi kingine cha habari kilichofanya uchunguzi au kuripoti Kwa karibu ukiachilia mawingu??
Nini kinaendelea mpka sasa (kesi ni lini au uchunguzi bado unaendelea)...
Ni hayo tu... Naomba tuendelee kujadili Kwa ajili yakupata taarifa zaidi
 
Ndugu mwandishi:
Taarifa yako inazua sintofaham baada ya kueleza tofauti na mlengo wa kwanza wa taarifa kutoka kwa muhusika,na vyombo vya habari!! Na mahojiano baadhi yanavosema!!
Kwa taarifa ya mwanzo: mahojiano,
Alikua ni kibaka au mharifu ambaye ashafanya matukio ya hivo kadhaa na mhanga wa kutolewa macho alikua n victim no3 wa matukio ya hivo
Aidha imeonesha hakukuwa na hatua yyte iliyoweza chukuliwa juu yake na wanainchi wala polisi ingawa karibu kunaonekana kulikua na kijituo ya polisi( kulingana na maelezo)
..............................................................
Sa sijajua ww umefanya mahojiano gan ambayo yametoa majibu tofauti na wahojiwa na Millard Ayo na magazeti n hao hao RAIA ulowauliza
Maswali ya kujiuliza
1.Sample uliowauliza ww uliichukuaje kwa kuwachagua au randomly?

Logic:kama uliwachagua ,labda ulienda kuuliza marafiki au ndugu wa Muuaji/Mshitakiwa

2 je ni kweli kwamba hakukua na Vyombo vya habar ambavyo vilivyoshindwa kuchimba au kuona upande uliouona

3. Kama ni kweli kwamba mtuhumiwa anahistoria ya sifa nzuri kama hyo ni nn mass media znajaribu kufcha au kufumbia macho?

4.Unadai mtuhumiwa hakushikwa alijisalimisha( maelezo yako)
Na maelezo yamwanzo yanaonesha mtuhumiwa alikua akifanya ukatili au uhalifu huo hadharan bila kushkwa wala kutiwa nguvuni!!..Naunganisha doti....nini kipo nyuma ya pazia hapa (Uhusiano wa mhalifu na serikali n UPI?)
...................Sijajua sana kuhusu ukusanyaji wako wa taarifa ingekua official zaidi tungeweza pata majibu sahihi lakin nahis wapo watu wanaweza kutusaidia kuchimba.............
Uyo Miladi Ayo ndo mungu wenu nini? Kumbe na yeye mavi tu kama hao clouds ...fanya uchunguzi kabla ya kuropoka.
Hili tukio ni zaidi ya uhalifu...kuna chanzo na ndo tunachoka kujua..na kutu-feed na news zenye maslahi kwao..
 
Sioni maelezo yako yanasadia vipi jamii ikiwa hukuyawasilisha poilisi, ili wakushauri lipi la kufanya. Unachoita upelelezi unaweza kutafsiriwa kwamba ni kuingilia kazi isiyo yako au una lengo la kuingilia upelelezi wa poilisi kwa sababu unazozijua mwenyewe. Mhusika ni mtu mzima na ana akili timamu naamini hivyo, yeye ndiye anajua alikuwa wapi siku ya tukio; wewe ni nani wa kumsemea? Pamoja na hayo sheria za nchi zinampa haki kusikilizwa kabla ya hukumu. You are presumed innocent until the court proves you guilty beyond reasonable doubt.
Kwa hapa inakuaga Guilty until proven innocent jombaa.
 
Nimepata hamu kubwa yakujua kilichopo nyuma ya pazia... Naomba Kwa yeyote aliye Na historia fupi ya hili tukio atuelezee,,, nikimaanisha
Tukio lilitokea lini?
Wapi Na akitokea au akielekea wapi Na kama alikotoka aliongozana Na yeyote
Nani alimpeleka kituo cha polisi kuchukua PF3 Na nikituo gani hicho??
Baada ya hapo alipelekwa Hosp. Gani Na alikaa Kwa muda gani??
Ni Hosp. Ngapi alizotembelea Na Kwa muda gani??
Aliyeibua hili Jambo ni Nani Na ni baada ya muda gani??
Aliyemuokota (msamalia mwema huyo) yupo wapi??
Jamaa (said) amepona tayri au bado... Na imechukua muda gani kupona,,, ikumbukwe ni majeraha mbalimbali Na hususani Na macho kutolea bila utaalam wakitabibu Nadhani ingelichukua muda).. Nategemea kuna madaktari watatusaidia katika hili,,,
Alimtambuaje kuwa mhusika ni nge??
Scorpion alikamatwaje??
Ni chombo kipi kingine cha habari kilichofanya uchunguzi au kuripoti Kwa karibu ukiachilia mawingu??
Nini kinaendelea mpka sasa (kesi ni lini au uchunguzi bado unaendelea)...
Ni hayo tu... Naomba tuendelee kujadili Kwa ajili yakupata taarifa zaidi

Tafuta interview aliyoifanya na Clouds utapata majibu yako.

Au mtafute Gea Habibu.
 
Characteristic moja ya vinyozi ni wanyoaji wazuri maeneo hata yasiyo wahusu.... Rejea wimbo wa spea tairi maneno aliyo yazungumza mpoki wakati anampiga mkwara mzito matonya.
Huyo jamaa kafanya kitu na mhanga ka retaliate kwa ku hire assassin. Sema nafikiri aliemtuma skopioni alitoa maelekezo ya kumyofoa gogozi kifaa ambacho kilianzisha tamaa ya mhanga ili asiendelee kutamani mali ya mtu mwingine.
Mambo ambayo yanaweza kusababisha ukang'olewa macho, ukaliwa 0714, ukatolewa roho etc
1-Usingizi wa mwanaume mwenzio, pumziko la moyo wake
2-Dhuluma na utapeli.
NB :Hii nimeifikiria kwa sauti tu na haina tofauti na hoja za Darwin.
Au sio kwa hyo kwa mfano we usingizi wako umezinguliwa utafanyaje
 
Kikubwa...
Uchunguzi wa kina ufanyike ilikubaini ukweli juu ya jambo hili cz kuna utata mkubwa na tusiwe wafwata upepo tu na kudhania kirahisi ivo
 
Kama sio kibaka mbona kamchukulia cheni zake na pesa? Acheni zenu hizo bana.
Wale walio hojiwa na Gea Habib mbona walikili kumjua na kumuogopa kwa matukio yake.
Labda mtoa mada ni mpambe wa Scopion, maana kama alikua anadhibiti vibaka sasa mbona Saidi alishambulia akiwa kwenye manunuzi na watu hawakusaidia?
Unajuaje kama huyo gea alichagua wa kuwahoji?
 
Back
Top Bottom