Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Kuna yule mwingine wa big brother 500mil sijui siliishia wapi
Ni kweli mkuu
Yule Mwisho Mwampamba wa Big brother,nae zilimpeleka kisha akapotea kabisaa,mwisho ikawa bla blaaa

Sasa huyu mpaka kufikia mlinzi tena wa Bar za vichochoroni,basi mjue alikuwa tayari ameishavugwa na tension za Maisha.Na siku yoyote angefanya tukio,na ndio hilo

Wakimpima tu akili,watapata jibu kwamba jamaa amedata kitambo,ila siku hiyo alifanya tu hitma ya ku mskopion mwenzie regardless ametumwa au la

Acheni kurembaremba,mara ohhh alikwa mwema saana,alikuwa anasaidia sana watu,hizo kiki wanafanya wanafunzi wake wa ngumi na kundi lake ambalo linatafutwa na polisi.
 
Mimi nina rekodi nzima ya kipindi cha Dida kuhusiana na hilo tukio. Idadi ya mashahidi imepelea, labda kwasababu siyo serious radio program!
Uyo dida ndo nani.? Ama yule kipa wa zamani wa Brazil?
Kwan Idadi gani ya mashahidi ni tosheleza?
 
Mawili:
1) Wewe BOYA

Au

2) Unapenda sana wake za
watu...

kwahiyo una wasiwasi ukifumaniwa utafanywaje, hivyo unajaribu kuhamasisha ujinga jamii isiwahukumu watu wa aina yako.
Sawa si mtazamo wako nikuulize tu swali anaemilik nyapu ni nani ???
 
Mengi yamejificha tukianza sikia na upande wa Pili upepo utabadilika..

Hii inanikumbusha tukio la juzi tu huko Singida yule jamaa alietolewa ulimi upepo ulivyombadilikia kesi IPO kwake sasa kama mbakaji..

Tuiache mahakama ifanye Nazi yake.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Kweli mkuu...!
 
Haya umetueleza ila mazuri yote aliyofanya haimaanishi alikuwa hana mabaya ambayo hakuyaonyesha wazi.

Asubiri hukumu tu.
Mkuu umenena vizuri,mtoa maada ana lake jambo mbona alishindwa kuwauliza hao wanaomjua "kwa nini wanamwita Nge?"nadhani angeanzia hapo,vitabu vya mungu husema majina huumba.
 
Kama unaamin alikua anafanya uharifu kwakujificha ili wananchi wamwone mwema kwanin hilo tukio alilifanya mbele yakadamnasi.....fikilia tena
Nadhani umejibu swali langu kuwa alikuwa mbabe, hivyo wananchi walimuogopa. Ndio maana hawakumgusa. Huvi unatetea nini? Angetolewa macho ndugu yako au mwanao ungesimama kumjadili huyu mhalifu Scorpion? Umenielewa vibaya, alikuwa anafanya uhalifu kwa kuwazuga wananchi kuwa alikuwa anapambana na vibaka wa Buguruni.
 
Ni kweli mkuu
Yule Mwisho Mwampamba wa Big brother,nae zilimpeleka kisha akapotea kabisaa,mwisho ikawa bla blaaa

Sasa huyu mpaka kufikia mlinzi tena wa Bar za vichochoroni,basi mjue alikuwa tayari ameishavugwa na tension za Maisha.Na siku yoyote angefanya tukio,na ndio hilo

Wakimpima tu akili,watapata jibu kwamba jamaa amedata kitambo,ila siku hiyo alifanya tu hitma ya ku mskopion mwenzie regardless ametumwa au la

Acheni kurembaremba,mara ohhh alikwa mwema saana,alikuwa anasaidia sana watu,hizo kiki wanafanya wanafunzi wake wa ngumi na kundi lake ambalo linatafutwa na polisi.
Acha kututoa katika mada. Tofauti kubwa kati ya hao unaiwataja ni kuwa mmoja absushi kivyake na Scorpion ni mkatili ba anastahili adhabu kali bila kujali umaarufu wake
 
wachangiaji weeengi, lakini hakuna mwenye sababu ya said kutumbuliwa macho!!!! sasa mkioko dar si mfuatilie mjue sababu mtuambie na cc
 
Naona unakurupuka. Ishu hapa sio jamaa kutobolewa macho. Macho yametobolewa na ni kosa kisheria ilo, Aliyetoboa atapata adhabu stahili. Hatupingi hilo.

Ishu hapa ni nini chanzo cha yote hayo? Mana hao wapumbavu wana-feed jamii news imuone jamaa kama ndo muhanga wa taifa, ni kama yule demu aliyeparalize yani walimpromote watu wamuonee huruma kama ndo muhanga wa nchii hii vile. Wakati kuna watu kibao wana matatzo.

Ili TUMUONEE HURUMA NA KUMCHANGIA kama wanavotaka, basi na tujue chanzo cha tukio ni nn, na sio kutuaminisha kua ni tukio la kihalifu, wakati kuna kila dalili kua ni zaid ya uhalifu.

Vibaka wanaiba na wanajeruhi watu sana lakini hawatoi watu macho...
Tumia akili kufikiri na sio makalio

Naunga mkono hoja yako. Hapa kuna watu wanalialia ili jamaa aonewe huruma tu...ila wenye akili tunataka kujuwa chanzo.

Ukweli unatafutiwa Jf?

Wewe usiye mvivu nenda Buguruni ndiyo Kuna ukweli siyo kuleta ngonjera humu.

Na bila Ruge hii habari wewe wala usingeisikia.

Huyohuyo Ruge alikuletea porojo za Babu wa Loriondo, wapuuzi ndio wanaoburuzwa na Ruge na Shigongo, hio habari ya Said kitumbuliwa macho huwezi kuikuta kwenye redio na magazeti yenye akili...puuzi huburuzwa na puuzi wenzao

scorpion alitumwa atekeleze hyo kaz kwa said na sio kuwa jmaaa n kibka....said inasemekana alikuwa anatembea na mke wa mtu.

Hii ndio habari iliopo Buguruni.
Alipotoka kazini akarudi nyumbani na kuacha funguo na kisha akatoka na kwenda kwenye uasherati...we have to speak it out and loud huyo dogo alitegwa na akanasa, na alishaambiwa siku nyingi sana ila akawa bado anaendelea na huo uasherati kwa mke wa mtu.

Na siku mkisikia mkewe kambalasa msije sema ooh wanawake wa siku hizi wanakupenda ukiwa na macho...huyo jamaa ni mzinzi na ishu hii inafunikwa mambo mengi sana, ila watu wa kale walisema uongo hauwezi kuuzika ukweli...

Ipo siku mtajuwa ukweli kama ambavyo mliujuwa ukweli wa kuwa yule Babu na kikombe chake cha Samunge ni kanjanja tu na ni fiksi
 
View attachment 415577

Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salim Njwete 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.

Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.

Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.

Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.

Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...

Tuendelee..

Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.

Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.

Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?

Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.

Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.

Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.

Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.

Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..
Umenisumbua kusoma upuuzi
 
Anyongwe kabisa ikiwezekana,, ikishindikana atobolewe macho basi
 
Mkuu umeongea Kitu...
Sasa Hivi Kama Kila Anaetembea Na Mke wa Mtu Akitolewa Macho Ni Sahihi kisheria?
Acha Sheria Ichukue Mkondo wake kosa la Kujeruhi Miaka 30/40.
Eti umetumwa...kuvunja Sheria....
Ulipofanyiwa Kosa alichukua Uamuzi Gani Kisheria....Eti ndo alimtuma Scorpion...Sasa jela Inamuhusu...
 
Asante...
Haya ndio majibu mujarab ya JF...
Safi sana

Mkuu Scorpion ataozea Jela Sheria Inamhusu...Eti alitumwa Kwa Kuwa Eti jamaa anatembea Na MKE wa Mtu...
Mvua ya Miaka Inamhusu...
Sheria Mkononi...
 
Hapo sasa. Wakazi wanasema jamaa hakuwa kibaka. Hili tukio ni zaidi ya tunalivyolifahamu.
Huyo Scorpion abanwe aseme ukweli..
Nahisi hata huyo askari mtesaji atakuwa na woga kumtesa huyo scorpion,maana anajua siku atakapobahatika kutoka atamtafuta hata home kwake akamnyofoe macho na yeye.
 
Back
Top Bottom