Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Huyu jamaa aliwai kuua pia aliwai kumvunja dada kiuno lengo lake ni kukupiga kutoboa macho ili ufe kwa kugonga na gari huyu si mtu wa kawaida ni mastermind sana chunguza nyendo zake hata mahakaman kaingia na nguo zingine very rough akatoka na nguo zingine very smart na cha ajabu mwaka 2012 Alishinda million 20 kwenye dume challenge
Sipendi kuonekana namtetea, ila naomba kukuuliza kitu, unaushahidi wa mauaji ya huyo dada? Au baada ya kusikia je ulijiaminisha kuwa alimuua huyo dada?
 
Watz mnajua sana kuunganisha dots! Hv mnataka kusahau mapema hv machungu ya unyama huu na kuanza kumtakasa mtu kwa utafiti wa kufikirika kama huu! Daaa tz yetu jmn! Huyu mtu ameshapoteza duniani watu zaidi ya 4 bado mnatafuta ukweli buguruni? Binadamu tumepewa kipaji cha kusahau haraka!
Jaribu kutumia ubongo, walu kidogo. Sasa ukweli kama hautatafutwa sehemu inayodaiwa kutokea tukio utatafutwa wapi? Nani kakuambia ameshapoteza watu zaidi ya 4? Halfu mleta mada hasemi kuwa jamaa hakufanya bali anaelezea alichoambiwa!
 
Huyo alietobolewa macho kwanini hakuenda polisi kureport baada ya tukio,na akasubiri siku kadhaa zimepita ndo akahojiwa na waandishi ndo suala zima likafahamika?,
isijekuwa anamwangushia zali huyo scopion wakati watoboa macho ni vibaka walimtaiti night

Hata mimi imenishangaza kidogo. Kama lilikuwa ni tukio lililofanyika tena eneo la wazi (pia Buguruni Polisi siyo mbali) bila shakalilivuta Watu, na kama taratibu zilivyo angepitishwa Polisi ili kupata PF3 kwa ajili ya matibabu na baadaye kuchukuliwa maelezo.

Lakini unaona ni kama tukio la ghafla lakini taarifa zake zimechelewa kutoka. Kuna nini?
 
Hapana mkuu. Aliwahi kuua na bado awe mtaani tu anafanya shughuli zake? Itendee haki akili yako mkuu.. Usisambaze uongo. Tukemee uovu, ila tusiushetanishe zaidi ili kufurahisha nafsi..
Ni hatari zaidi ya sana, kuwa na kizazi cha sampuli ya huyo [HASHTAG]#onlinenauza[/HASHTAG].
Unaweza kukuta Taifa linaingia kwenye historia ya Rwanda na Burundi kwa sababu ya ndimi za watu wa aina hiyo.
Unao ushahidi ndugu?
Au na wewe umesikia story za mtaani ni vyema tukapata mashahidi waliowahi kukabwa au kuumizwa na huyo scop
kuliko kuendeshwa kwa hisi.
Ni mtazamo tu lakini
 
View attachment 415577

Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salum Henjewele 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.

Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.

Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.

Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.

Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...

Tuendelee..

Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.

Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.

Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?

Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.

Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.

Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.

Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.

Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..
Kwa nini atolewe yeye tu????

Na kwa nini asisaidiwe???

Simtetei mtoboa macho ne tena kama kacheza martial arts......

Lazima alikuwa na adabu ya mchezo....

Aliyetobolewa huenda ana la moyoni
 
Ndugu mwandishi:
Taarifa yako inazua sintofaham baada ya kueleza tofauti na mlengo wa kwanza wa taarifa kutoka kwa muhusika,na vyombo vya habari!! Na mahojiano baadhi yanavosema!!
Kwa taarifa ya mwanzo: mahojiano,
Alikua ni kibaka au mharifu ambaye ashafanya matukio ya hivo kadhaa na mhanga wa kutolewa macho alikua n victim no3 wa matukio ya hivo
Aidha imeonesha hakukuwa na hatua yyte iliyoweza chukuliwa juu yake na wanainchi wala polisi ingawa karibu kunaonekana kulikua na kijituo ya polisi( kulingana na maelezo)
..............................................................
Sa sijajua ww umefanya mahojiano gan ambayo yametoa majibu tofauti na wahojiwa na Millard Ayo na magazeti n hao hao RAIA ulowauliza
Maswali ya kujiuliza
1.Sample uliowauliza ww uliichukuaje kwa kuwachagua au randomly?

Logic:kama uliwachagua ,labda ulienda kuuliza marafiki au ndugu wa Muuaji/Mshitakiwa

2 je ni kweli kwamba hakukua na Vyombo vya habar ambavyo vilivyoshindwa kuchimba au kuona upande uliouona

3. Kama ni kweli kwamba mtuhumiwa anahistoria ya sifa nzuri kama hyo ni nn mass media znajaribu kufcha au kufumbia macho?

4.Unadai mtuhumiwa hakushikwa alijisalimisha( maelezo yako)
Na maelezo yamwanzo yanaonesha mtuhumiwa alikua akifanya ukatili au uhalifu huo hadharan bila kushkwa wala kutiwa nguvuni!!..Naunganisha doti....nini kipo nyuma ya pazia hapa (Uhusiano wa mhalifu na serikali n UPI?)
...................Sijajua sana kuhusu ukusanyaji wako wa taarifa ingekua official zaidi tungeweza pata majibu sahihi lakin nahis wapo watu wanaweza kutusaidia kuchimba.............
 
Jaribu kutumia ubongo, walu kidogo. Sasa ukweli kama hautatafutwa sehemu inayodaiwa kutokea tukio utatafutwa wapi? Nani kakuambia ameshapoteza watu zaidi ya 4? Halfu mleta mada hasemi kuwa jamaa hakufanya bali anaelezea alichoambiwa!
Haya ntatumia ubongo kdg! But fatilia comment zangu kwa makini! Ukweli unaanza kuutafuta mahali tukio limetokea ni sawa! Huo tunauita preliminary investigation! Ndio maana hata mahakamani wamekwambia upelelezi haujakamilika! Kinachofuata baada ya hapo nitakwambia cku nyingine! Lzm na ww ujue ukweli wa kipolisi unatofautiana pakubwa na ukweli wa kitaaluma!
 
Bado mkuu... una nafasi ya kutumia ubongo zaidi. Upelelezi wa polisi HAUWEZI kutofautiana na upelelezi wa kitaalam kama unavyodai, kwani upelelezi wa polisi (kama utafanyika kwa weledi) basi ni wa kitaalam! Halafu FYI jamaa mwanzisha mada hakufikia hitimishio ila amejaribu kufanya upelelezi na aka-share hapa. Sasa wewe kama unajua polisi bado wanafanya upelelezi kwanini usiwe open kwa maelezo kutoka kwa watu tofauti tofauti?
 
Kwanini mtu akiwa na mawazo tofauti, watanzania huwa tunaona ametumwa! Mtoa mada hakuna sehemu alipo-justify alichofanya mhusika lakini huwa ni vizuri kutoa haki ya kusikiliza upande wa pili kabla ya kuamua mihemko na huruma vitoe maamuzi.
Eti haki! Vipi kuhusu haki ya macho ya Saidi yaliyong'olewa, we unaona haina maana!?
 
View attachment 415577

Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salum Henjewele 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.

Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.

Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.

Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.

Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...

Tuendelee..

Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.

Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.

Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?

Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.

Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.

Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.

Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.

Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..

Sioni maelezo yako yanasadia vipi jamii ikiwa hukuyawasilisha poilisi, ili wakushauri lipi la kufanya. Unachoita upelelezi unaweza kutafsiriwa kwamba ni kuingilia kazi isiyo yako au una lengo la kuingilia upelelezi wa poilisi kwa sababu unazozijua mwenyewe. Mhusika ni mtu mzima na ana akili timamu naamini hivyo, yeye ndiye anajua alikuwa wapi siku ya tukio; wewe ni nani wa kumsemea? Pamoja na hayo sheria za nchi zinampa haki kusikilizwa kabla ya hukumu. You are presumed innocent until the court proves you guilty beyond reasonable doubt.
 
Hata me nimeshangazwa sana Kwa jinsi alivo na muonekano wake,ningekuwa na uwezo ningemwajiri Kazi ya kupambana na wezi
 
Ndugu mwandishi:
Taarifa yako inazua sintofaham baada ya kueleza tofauti na mlengo wa kwanza wa taarifa kutoka kwa muhusika,na vyombo vya habari!! Na mahojiano baadhi yanavosema!

Kwa taarifa ya mwanzo: mahojiano,
Alikua ni kibaka au mharifu ambaye ashafanya matukio ya hivo kadhaa na mhanga wa kutolewa macho alikua n victim no3 wa matukio ya hivo.

Aidha imeonesha hakukuwa na hatua yyte iliyoweza chukuliwa juu yake na wanainchi wala polisi ingawa karibu kunaonekana kulikua na kijituo ya polisi( kulingana na maelezo).

Sa sijajua ww umefanya mahojiano gan ambayo yametoa majibu tofauti na wahojiwa na Millard Ayo na magazeti n hao hao RAIA ulowauliza.

Maswali ya kujiuliza;
1. Sample uliowauliza ww uliichukuaje kwa kuwachagua au randomly?

Logic: Kama uliwachagua ,labda ulienda kuuliza marafiki au ndugu wa Muuaji/Mshitakiwa

2. Je, ni kweli kwamba hakukua na Vyombo vya habar ambavyo vilivyoshindwa kuchimba au kuona upande uliouona

3. Kama ni kweli kwamba mtuhumiwa anahistoria ya sifa nzuri kama hyo ni nn mass media znajaribu kufcha au kufumbia macho?

4. Unadai mtuhumiwa hakushikwa alijisalimisha( maelezo yako)

Na maelezo ya mwanzo yanaonesha mtuhumiwa alikua akifanya ukatili au uhalifu huo hadharan bila kushkwa wala kutiwa nguvuni!!.. Naunganisha doti....nini kipo nyuma ya pazia hapa (Uhusiano wa mhalifu na serikali n UPI?)

...................Sijajua sana kuhusu ukusanyaji wako wa taarifa ingekua official zaidi tungeweza pata majibu sahihi lakin nahis wapo watu wanaweza kutusaidia kuchimba.............

Asante sana mkuu kwa maswali mazuri. Kwa kuwa sina maslahi na tukio hili, hivyo nitakujibu kwa uhuru tu.

1. Sijaelewa unaposema kuchagua au randomly unamaanisha nini hasa. Ila cha msingi nilifika eneo la tukio. Niliowauliza ni wenyeji wa pale. Wengi wao tunafahamiana kwa kuwa niliishi sana kule (nilieleza kwa kirefu).

2. Vyombo vya habari vipo. Vimeripoti tukio kama vilivyoripoti. Sina nafasi ya kuvisemea authenticity ya taarifa zao lakini naamini wamefanya kazi yao kwa kiasi walichoona kinatosha.

3. Bado sitosemea mass media, ila kimsingi nilichokileta ndicho kilichopo. Uzuri Buguruni kunafikika kirahisi kwa wakazi wa Dar. Ajitolee anayeweza kufika akajiridhishe.

4. Si maelezo yangu. Hayo niliyapata kwa kuuliza. Bahati mbaya hili swali nililiuliza kwa mtu mmoja tu wa mwisho (kuhusu arrest) kwa kuwa nililisahau hivyo siwezi kuliwekea hakika kwamba alijisalimisha au alikamatwa kwa msako. Ila point ya msingi hapo ni kuwa tukio lilijiri na wiki moja baadae ndio mhalifu akawa mikononi mwa polisi.

Hayo maelezo ya awali kuhusu uhalifu wa mtuhumiwa hayapo uraiani. Yaani hakuna rekodi yoyote ya uhalifu ambayo nilitajiwa. Wanaoishi pale wanasema jamaa hakuwa mhalifu kabisa. Go ask.

Taarifa hizi nimeeleza namna nilivyozikusanya. Wala haikuwa official task or anything like that. Nimeenda tu kama raia mwenye shauku ya kupata majibu ya maswali yaliyonitatiza.

Asante.
 
Ndugu mwandishi:
Taarifa yako inazua sintofaham baada ya kueleza tofauti na mlengo wa kwanza wa taarifa kutoka kwa muhusika,na vyombo vya habari!! Na mahojiano baadhi yanavosema!!
Kwa taarifa ya mwanzo: mahojiano,
Alikua ni kibaka au mharifu ambaye ashafanya matukio ya hivo kadhaa na mhanga wa kutolewa macho alikua n victim no3 wa matukio ya hivo
Aidha imeonesha hakukuwa na hatua yyte iliyoweza chukuliwa juu yake na wanainchi wala polisi ingawa karibu kunaonekana kulikua na kijituo ya polisi( kulingana na maelezo)
..............................................................
Sa sijajua ww umefanya mahojiano gan ambayo yametoa majibu tofauti na wahojiwa na Millard Ayo na magazeti n hao hao RAIA ulowauliza
Maswali ya kujiuliza
1.Sample uliowauliza ww uliichukuaje kwa kuwachagua au randomly?

Logic:kama uliwachagua ,labda ulienda kuuliza marafiki au ndugu wa Muuaji/Mshitakiwa

2 je ni kweli kwamba hakukua na Vyombo vya habar ambavyo vilivyoshindwa kuchimba au kuona upande uliouona

3. Kama ni kweli kwamba mtuhumiwa anahistoria ya sifa nzuri kama hyo ni nn mass media znajaribu kufcha au kufumbia macho?

4.Unadai mtuhumiwa hakushikwa alijisalimisha( maelezo yako)
Na maelezo yamwanzo yanaonesha mtuhumiwa alikua akifanya ukatili au uhalifu huo hadharan bila kushkwa wala kutiwa nguvuni!!..Naunganisha doti....nini kipo nyuma ya pazia hapa (Uhusiano wa mhalifu na serikali n UPI?)
...................Sijajua sana kuhusu ukusanyaji wako wa taarifa ingekua official zaidi tungeweza pata majibu sahihi lakin nahis wapo watu wanaweza kutusaidia kuchimba.............
hao victim wengine wako wapi? Wewe unawajua? Hao walioporwa kwa nini hawakuripoti polisi?
 
Sioni maelezo yako yanasadia vipi jamii ikiwa hukuyawasilisha poilisi, ili wakushauri lipi la kufanya. Unachoita upelelezi unaweza kutafsiriwa kwamba ni kuingilia kazi isiyo yako au una lengo la kuingilia upelelezi wa poilisi kwa sababu unazozijua mwenyewe. Mhusika ni mtu mzima na ana akili timamu naamini hivyo, yeye ndiye anajua alikuwa wapi siku ya tukio; wewe ni nani wa kumsemea? Pamoja na hayo sheria za nchi zinampa haki kusikilizwa kabla ya hukumu. You are presumed innocent until the court proves you guilty beyond reasonable doubt.
Mbona unanihukumu? Mimi nimesema nilichokikuta na wala huu sijauita upelelezi. Kuyaweka hapa JF ni kusaidia polisi pia. Sie wengine kukaa karibu na zile khaki hatuwezi hivyo tunasaidia kwa njia hii..
 
Hapo sasa. Wakazi wanasema jamaa hakuwa kibaka. Hili tukio ni zaidi ya tunalivyolifahamu.
Huyo Scorpion abanwe aseme ukweli..

Kwa maelezo ya watangazaji wa clouds, watu walio hojiwa na mwenyewe wanasema scop alikua ni kibaka mzoefu katika eneo hilo
Napata ukakasi sana kuwaamini sana hawa watu waliohojiwa mana kabla yake sidhani kama kuna tukio liliripotiwa kumuhusu scop. Isije kuwa ni kazi maalum mana maelezo yanakinzana na na majirani na scop.
Muda na mahakama utakua jibu zuri kwetu.
 
Ukienda Buguruni ukauliza Scop alikuwa kibaka? 10/10 watakujibu HAPANA.
 
Ni kwel alishinda M20 za dume condom Mashindano....kuna ishu zinafichika juu ya unyama huu...ukimchek anavyopelekwa Mahakaman anajiamin na anacheka yupo comfortable sana..ni kama anajua analofanya
Hilo nalo..
 
Back
Top Bottom