Bulamba
JF-Expert Member
- Sep 17, 2011
- 14,267
- 13,573
Huo uhalifu ulifanyika hadharani.Mashahidi ni kibao.Unataka kujenga hoja gani?Una uhakika gani kuwa ni kweli scorpion ndio aliemtoboa macho???
Huo uhalifu ulifanyika hadharani.Mashahidi ni kibao.Unataka kujenga hoja gani?Una uhakika gani kuwa ni kweli scorpion ndio aliemtoboa macho???
Wakati mwingine kukaa kimya na kutafakari kwa kina ni jibu bora zaidi. Ww hapo juu tayari umeegemea upande mmoja na umeshatuhumu na kuhukumu!!!. Hakika ya ukweli wa jambo hili watu wanaolijua ni Saidi mwenyewe na huyo Scorpion. Stori iliyoenea ni ya uapnde mmoja na watu wengi wanaenda kinyume na Misingi ya utandaji haki ya kiasili kwa kuhukumu kwa stori ya upande mmoja. Binafsi nikikutana na mtu anayekusudia kunidhuru nitapambana naye na nikipata fursa ya kumtoboa macho nitamtoboa depending on kiwango cha madhara anachotaka kunitendea. Kiukweli inatakiwa ipatikane stori ya kwanini Saidi ametobolewa macho ndio nitakuwa kwenye position ya kutuhumu au kuhukumu. Ujumbe ninaotaka kuutoa hapa ni kuwa huenda tukipata upande wa pili wa stori tutagundua kuwa adhabu aliyopata ni ndogo sana au kubwa! Mm bado nasubiri sitaki kuuhukumu upande wowote maana bado kuna maswali mengi ya kujiuliza.Hujasema popote kuwa huyo Scorpion alikuwa na kazi gani rasmi. Unaamini kuwa alikuwa akusaidia ulinzi? Nani amekudhihirishia kuwa aliwahi kukamata wahalifu na kuwafukisha kwenye vyombo vya dola? Kwa maoni yangu Scorpion aliishi kwa kudanganya umma kuwa ni mtu mwema akisaidia kudhibiti wahalifu, shughuli aliyojipa mwenyewe, lakini ni mhalifu aliyejificha katika kivuli cha wema.
Kitendo cha kumvamia mtu na kumdhuru mbele ya kadamnasi bila kuogopa kuwa wananchi wanaweza kunigeuzia kibao kinaonesha jinsi alivyokuwa mbabe wa kutisha! Nani asiyejua hasira ya wananchi inavyokuwa litokeapo tukio la binaadam kufanyiwa vitendo vya kikatili? Polisi wangekuta tayari Scorpion ameuawa na wananchi wenye hasira.
Usijenge mazingira ya kubadili mtazamo wa umma. Scorpion ni mhalifu tena mzoefu maana ilishasemekama mapema kuwa ni hatari watu wa Buguruni wanamuogopa.
Kama mashahidi wapo basi mahakama itamtia hatiani scorpion. Then swali la kwanini alifanya hivyo litapata jibu.Huo uhalifu ulifanyika hadharani.Mashahidi ni kibao.Unataka kujenga hoja gani?
Kisasi pia ni mkono wa mtu. Unatetesi kidogo kuhusiana na ulipwaji wa kisasi mkuu?Hata mimi nimekuwa najiuliza kwanini alimtoboa? Why???
Lazima kuna sababu, na kama sio ya kisasi, basi kuna (mkono wa mtu)
Unakumbuka babu wa loliondo, popobawa na vibwengo? Itoshe tu kukuelezea kuwa reporters wengi bongo ni failures wa normal schooling system ndo wanaenda kuutaarifu umma. Ukanjanja at it's best.Ndugu mwandishi:
Taarifa yako inazua sintofaham baada ya kueleza tofauti na mlengo wa kwanza wa taarifa kutoka kwa muhusika,na vyombo vya habari!! Na mahojiano baadhi yanavosema!!
Kwa taarifa ya mwanzo: mahojiano,
Alikua ni kibaka au mharifu ambaye ashafanya matukio ya hivo kadhaa na mhanga wa kutolewa macho alikua n victim no3 wa matukio ya hivo
Aidha imeonesha hakukuwa na hatua yyte iliyoweza chukuliwa juu yake na wanainchi wala polisi ingawa karibu kunaonekana kulikua na kijituo ya polisi( kulingana na maelezo)
..............................................................
Sa sijajua ww umefanya mahojiano gan ambayo yametoa majibu tofauti na wahojiwa na Millard Ayo na magazeti n hao hao RAIA ulowauliza
Maswali ya kujiuliza
1.Sample uliowauliza ww uliichukuaje kwa kuwachagua au randomly?
Logic:kama uliwachagua ,labda ulienda kuuliza marafiki au ndugu wa Muuaji/Mshitakiwa
2 je ni kweli kwamba hakukua na Vyombo vya habar ambavyo vilivyoshindwa kuchimba au kuona upande uliouona
3. Kama ni kweli kwamba mtuhumiwa anahistoria ya sifa nzuri kama hyo ni nn mass media znajaribu kufcha au kufumbia macho?
4.Unadai mtuhumiwa hakushikwa alijisalimisha( maelezo yako)
Na maelezo yamwanzo yanaonesha mtuhumiwa alikua akifanya ukatili au uhalifu huo hadharan bila kushkwa wala kutiwa nguvuni!!..Naunganisha doti....nini kipo nyuma ya pazia hapa (Uhusiano wa mhalifu na serikali n UPI?)
...................Sijajua sana kuhusu ukusanyaji wako wa taarifa ingekua official zaidi tungeweza pata majibu sahihi lakin nahis wapo watu wanaweza kutusaidia kuchimba.............
Jr kama alikia kipofu tangu zamani? Maana mbona tangu atolewe macho hadi apone ninmuda mfupi sana? Chini ya mwezi nadhani.Eti haki! Vipi kuhusu haki ya macho ya Saidi yaliyong'olewa, we unaona haina maana!?
Ndugu unaweza nitajia majina ya waliopotezwa au ndugu zao wanapokaa hapa dar?Watz mnajua sana kuunganisha dots! Hv mnataka kusahau mapema hv machungu ya unyama huu na kuanza kumtakasa mtu kwa utafiti wa kufikirika kama huu! Daaa tz yetu jmn! Huyu mtu ameshapoteza duniani watu zaidi ya 4 bado mnatafuta ukweli buguruni? Binadamu tumepewa kipaji cha kusahau haraka!
Only learned counsels will understand what you mean. Lay people will burst into insultsAtobolewe macho na nani? Serikali au wananchi na kama serikali hauoni kwamba serikali itakuwa inafanya kitu ambacho inakikataza?
Namkumbuka Jaji Mwalusanya aliwahi kupinga adhabu ya kifo kwani haiwezekani serikali izuie kifo kwa kuua, je anayebakwa adhabu yake itakuwa kubakwa?, anayeiba naye aibiwe?
Alafu wewe chomba usitake kujifanya kibatala humu ndani, eti mioyo ya Watanzania Wakurupukaji [emoji9] [emoji9] [emoji9] hovyo huoni hata haya! Sheria ipi inayokataza jamii kusikitika na kutoa kidogo walicho nacho? Hakuna kingine kinachokusumbua zaidi ya wivu tu, tobolewa na wewe ili tukusikitikie kwa sheria mwehu wewe, hujalazimishwa lakini nakushangaa unataka kulazimisha wengine walibaliane na utumbo wako! Haya ameshapewa mwenzio Nyumba ya GSM, boda boda 5 na bajaji 2 [emoji108] we una nini cha maana au ndo kati ya masalia ya walalahoi wa TanzaniaSio mioyo ya watanzania...andika baadhi ya mioyo ya wakurupukaji wasio juwa Sheria.
Kama hujui Sheria usiandike uharo hapa.
Kila mshtakiwa anayo haki ya kusikilizwa kwa mujibu wa Sheria. Sasa unavyokuja kutujazia server kwa kuandika vitu visivyo na mashiko next time tutabofya kitufe na ndio utakuwa mwisho wako hapa JF.
Kama huna la maana la kuandika piga kimya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala amesema kwa taarifa iliomfikia toka kwa timu ya Serikali ilioagizwa kufika na kufuatilia sakata la Dogo kufunzwa adabu amesema ripoti inasema mitoto ya shule ya Mbeya Sec ni mijeuri na mikaidi ilio mithirikia.