Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Binafsi najiuliza kwanini amtoboe macho.. Na huyu jamaa alietobolewa macho alikua kinyozi.. Hivyo kwa kuangalia tu hakua na Fedha nyingi.. Alikua na maisha ya kawaida.. Na huyu kinyozi inaonyesha anamjua scorpion... Huyu scorpion anafaa kua mlinzi wa viongozi wa CHADEMA
ni kweli scopion hakuwa kibaka na wafanyabiashara ndogondogo za usiku walikuwa wakimpa pesa kwa ajili ya usalama maana vibaka walikuwa wakiwapora sana pesa zao! ila hilo kumtoa mtu macho hata mim linanishangaza.....sheria ichukue mkondo wake na wajue kuna nin nyuma ya pazia
 
Kwanini mtu akiwa na mawazo tofauti, watanzania huwa tunaona ametumwa! Mtoa mada hakuna sehemu alipo-justify alichofanya mhusika lakini huwa ni vizuri kutoa haki ya kusikiliza upande wa pili kabla ya kuamua mihemko na huruma vitoe maamuzi.


ktk hao mtoa mada alio wahoji angekuwepo mhanga naye anamtetea skopion ningeona mtoa mada sio mnafiki...
 
Kuna maswali mengi mno kuhusu tukio la kutobolewa macho ndugu Said. naamini jeshi la Polisi halitaendeshwa na mitazamo ya mob justice, watapeleleza vizuri tukio zima na haki itatendeka. Ila kuna maswali mengi sana kuhusu tukio zima na mtuhumiwa.
 
Kuna mengi sana nyuma ya pazia juu la ya tukio... lakini ukweli ni kwamba ni Scopion hajawahi kuwa kibaka wakazi wakazi wote wa buguruni wanalijua hili
Naamini ata Polisi wanatambua pia hilo,
 
ktk hao mtoa mada alio wahoji angekuwepo mhanga naye anamtetea skopion ningeona mtoa mada sio mnafiki...

Mkuu wa hapahapa, tangu hili sakata limeanza, wewe umeshamsikia mhanga mwingine? Kumtoa mtu macho ni unyama na Scorpion aadhibiwe kwa unyama huo at the same time tusikie kisa cha Said kutolewa macho, isije kuwa tunampa mtu sympathy ilopitiliza ilhali hastaili, mambo mengi huwa yana mambo mengi nyuma ya pazia.
 
taarifa za daktari zinasema aliyetobolewa macho hawezi kuona tena.

hayo maneno ya vijiweni tuachane nayo. tusubiri upelelez wa polisi na hukumu ya mahakama.
Upelelezi wa kipolisi utafanyika wapi sini hapohapo mtaani ama
 
kwani wakati kitendo hicho kinafanyika ilikuwa muda gani?inamaana hakukuwa hata na mtu mwingine aliyesikia sauti,kelele,kuona tukio lenyewe n.k?
 
Uhmmm,makubwa tusubiri mahakama itatupa majibu yote!!
 
View attachment 415577

Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salum Henjewele 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.

Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.

Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.

Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.

Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...

Tuendelee..

Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.

Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.

Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?

Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.

Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.

Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.

Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.

Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..
Unapoona wanandoa wanarudi nyumban NA kkukisiana siokwamba awana mchepuko.sikuwakifumaniwa ma watu ndio unajua hee hatayule
 
Back
Top Bottom