Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

View attachment 415577

Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salum Henjewele 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.

Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.

Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.

Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.

Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...

Tuendelee..

Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.

Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.

Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?

Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.

Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.

Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.

Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.

Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..
Mkuu, haujaandika chochote cha msaada kwa Scorpion mwenyewe, Said, Police wala wananchi.

Kwa ushauri siku nyingine ukitaka kuandika habari kama hii kumbuka huu msemo, " Two wrongs do not make a right"!
 
Nani amezuia polisi wasifanye kazi yao? Nenda Buguruni kaulize..

Tatizo kila mtu anazungumza lake huko buguruni ila nilichosikia huyu kila mtu anazungumza lake kuna kijana pale chama muuza supu alikuwa anasema huyo kijana na scopioni walipishana kauli tuu
 
Screenshot_2016-10-10-20-55-58.png
Hii ndio account ya lihalifu
 
Jinsi anavyoua ni kutoboa macho kisha anakutupa barabaran ili gar likugonge na yeye hana kesi hapo kesi ya mauaji ya dereva...ushaid mimi ni mkazi wa mnyamani huyu ana genge lake la wacheza karet akifika kibandani kwako kula chips halipi ni ubabe tu
Ww unafaa kusaidia Polisi. Ni wangapi umewashuhudia kutobolewa macho na scopion kisha kurushwa barabarani na kugongwa na gari?? Ikiwa ww ni raia mwema ulichukua hatua gani??
 
Haya umetueleza ila mazuri yote aliyofanya haimaanishi alikuwa hana mabaya ambayo hakuyaonyesha wazi.

Asubiri hukumu tu.
Kua makini na kauli zako... Dunia ina mengi sana na nchi hii kwa kupakaziana ndiyo yetu tabia...
Leo imekua kwa scorpion na usishangae kesho ukabebeshwa ww zaid ya la scorpion
 
Hilo ndio kubwa madam na linamshangaza kila mmoja.

Ila kwa mujibu wa maelezo ya wengi, jamaa hakuwa kibaka wala mhalifu, sasa huku kutoboana macho vipi?
Sio rahisi kwa mtu ambae sio kibaka au hafanyi uharifu wowote halafu from nowhere akamtoe macho binadamu mwenzake lazima atakuwa alishapotia uhalifu mdogo mdogo kumtia mtu kilema cha milele na mahakamani unacheka sio jambo la kitoto
 
Mimi naomba kujua jambo hapa nikuulize jamaa uliyefanya utafiti. Mmiliki wa meza alipokuwa akinunua Said kuku yupo au hayupo? Je, upelelezi wako uliuanzia kwenye meza hiyo? Je, katika ulioongea nao kuna mmoja wapo aliyeshuhudia tukio? Kama alishuhudia tukio, alimwona nani akitenda tukio hilo? Au upelelezi wako ulijikita kujua kama scorpion ni kibaka au la. Sisemi moja kwa moja kuwa scorpion ndiye katenda, hiyo ni kazi ya mahakama lakini anaweza kutenda kwa lengo la visasi cha kwake au kwa niaba ya mtu mwingine. Hii kesi ni ngumu sana zaidi ya watu wanavyofikiria. Said ambaye alichukua PF 3 ama hakuchukua? Kama alichukua PF ni kutoka kituo gani? Kwa maelezo yake ni kwamba alipoteza fahamu, je ni nani aliyempeleka hospitali? Aliyempeleka hospitali alimkuta mazingira gani? Katika maelezo ya Said anasema kuna dogo alimwambia yeye aliona tukio zima, je huyo dogo alimwambia maneno hayo akiwa hospitali ama nyumbani kwake yeye Said? Na huyo dogo wanafahamiana Said tangu zamani au alimfahamu siku ya tukio? Kama alimfahamu siku ya tukio, huyu dogo walionana vipi hadi kumpa taarifa hiyo kuwa aliliona tukio zima? Majibu yatapatikana kwa watu walioshuhudia tukio na si vinginevyo. Polisi Buguruni wanasema kwa nini hawakumkamata Scorpion?
 
Wanaume wa dar walikua wapi mwenzao akishambuliwa mpaka kutolewa macho?
 
kwani wakati kitendo hicho kinafanyika ilikuwa muda gani?inamaana hakukuwa hata na mtu mwingine aliyesikia sauti,kelele,kuona tukio lenyewe n.k?
Watu eneo la tukio walikuwa wengi kama unavyojua kwa mida inayotajwa Buguruni ndio kuna kuwa kumekucha!. Yaliyo nyuma ya pazia wataalam watusaidie kuyaweka wazi, nasema haiwezekani katika mazingira ya kawaida raia mwema aumizwe mbele za mamia ya watu wanaangalia, na kwa nini jeshi letu la polisi likae kimya kwa muda wakati taarifa za uharifu huo wanazo maana eneo hilo hilo ndipo gari la Doria linapo paki kila siku usiku, mtu anayetajwa kuwa hatari kama Scorpion anaamkia, anashinda na mida ya usiku anakuwa eneo hilo hilo, ila tuache Sheria ichukue mkondo wake ili haki itendeke na mara mahakama itakapo mtia hatiani Scorpion apokee adhabu anayo stahili.
 
Mimi naomba kujua jambo hapa nikuulize jamaa uliyefanya utafiti. Mmiliki wa meza alipokuwa akinunua Said kuku yupo au hayupo? Je, upelelezi wako uliuanzia kwenye meza hiyo? Je, katika ulioongea nao kuna mmoja wapo aliyeshuhudia tukio? Kama alishuhudia tukio, alimwona nani akitenda tukio hilo? Au upelelezi wako ulijikita kujua kama scorpion ni kibaka au la. Sisemi moja kwa moja kuwa scorpion ndiye katenda, hiyo ni kazi ya mahakama lakini anaweza kutenda kwa lengo la visasi cha kwake au kwa niaba ya mtu mwingine. Hii kesi ni ngumu sana zaidi ya watu wanavyofikiria. Said ambaye alichukua PF 3 ama hakuchukua? Kama alichukua PF ni kutoka kituo gani? Kwa maelezo yake ni kwamba alipoteza fahamu, je ni nani aliyempeleka hospitali? Aliyempeleka hospitali alimkuta mazingira gani? Katika maelezo ya Said anasema kuna dogo alimwambia yeye aliona tukio zima, je huyo dogo alimwambia maneno hayo akiwa hospitali ama nyumbani kwake yeye Said? Na huyo dogo wanafahamiana Said tangu zamani au alimfahamu siku ya tukio? Kama alimfahamu siku ya tukio, huyu dogo walionana vipi hadi kumpa taarifa hiyo kuwa aliliona tukio zima? Majibu yatapatikana kwa watu walioshuhudia tukio na si vinginevyo. Polisi Buguruni wanasema kwa nini hawakumkamata Scorpion?
Kiukweli hili shauri likimpata wakili "fundi" jamaa lazima achomoke, maana tukio zima limejaa baadhi ya chembe za shaka
Hi kesi mwenye asilimia nyingi ya kushinda ni Scorpion..ngoja tusubiri siku..
 
Back
Top Bottom