Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Haijalishi,tukio ameshafanya na kamuaribia mwenzie maisha.
Kila nikiona habari/picha ya yule jamaa (Said) aliyetobolewa macho machozi hunitoka.
Scorpion ni mnyama,hastahili huruma wala msamaha.

Hivi jamani ni nani anayeweza kuvaa viatu vya Said?
Mwanaume aliyekuwa mzima anafanya shughuli zake leo hii ni kipofu.
Ana mke na watoto wanaomtegemea.
Bila kumsahau mama yake...[emoji24] [emoji24] [emoji24]

Kiukweli siwezi kusikiliza utetezi wowote ule juu ya Scorpion kwa unyama alioutenda akiwa na akili timamu.


Anyways...kazi nzuri,lingekuwa tukio tofauti na hili kiasi ungesaidia.

Utaishia kulialia tu mikamasi uso mzima...
Sheria haiko hivyo unavyotaka wewe na wakurupukaji wenzio...
 
Kwa maelezo ya Said watu walikuwepo.
Hata kwa akili ya kawaida tu buguruni inaweza kukosa watu saa 3 usiku?

Pia alisema alipokuwa akiomba msaada hakuna aliyejitokeza kumsaidia.
Ndipo Scorpion akamuambia "hapa hakuna atakayekusaidia"
Hii ina maana gani?

Kuna mtu ameuliza hapa "Hivi jamani kuna jambo jingine mimi linanishangaza, huyu aliyetobolewa macho kachukua muda gani kupona makovu?"

Sasa tafakari hilo, usitumie kichwa kubebea mashkio hayo
 
Mtoa mada hakua na sababu ya kutonesha mioyo ya watanzania, hivi aliyetobolewa macho angekua kaka yake angeandika haya ambayo dhahili yanaonyesha kutetea vitendo viovu vifanyavyo na watu wachache! Kila mwema ana baya lake na kila mbaya ana jema lake pamoja na Wema woote wa scorpion ubaya wake ni kutuhumiwa kumtoboa macho mwenzie

Sio mioyo ya watanzania...andika baadhi ya mioyo ya wakurupukaji wasio juwa Sheria.

Scorpion hastahili hata kusikilizwa kwa unyama alioutenda akiwa na akili timamu.
Hata kama angekuwa mtu mwema kiasi gani...
Ingekuwa alimuibia mali zake akamuachia macho yake huenda tungesema ni hali ngumu ya maisha (japo halina uzito kihivyo ila afadhali kuliko alichokifanya)

Kama hujui Sheria usiandike uharo hapa.
Kila mshtakiwa anayo haki ya kusikilizwa kwa mujibu wa Sheria. Sasa unavyokuja kutujazia server kwa kuandika vitu visivyo na mashiko next time tutabofya kitufe na ndio utakuwa mwisho wako hapa JF.
Kama huna la maana la kuandika piga kimya.

Kwahiyo ile video ni uongo?

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala amesema kwa taarifa iliomfikia toka kwa timu ya Serikali ilioagizwa kufika na kufuatilia sakata la Dogo kufunzwa adabu amesema ripoti inasema mitoto ya shule ya Mbeya Sec ni mijeuri na mikaidi ilio mithirikia.
 
Taarifa ya mkewe si itakuwa ya kuhadithiwa na mumewe? Sishangai ikitofautiana maana hakuwa eneo la tukio.
Tena kwa 100% Mkuu. Mbona hiyo ' Kesi ' ipo wazi tu na ' nyepesi ' mno. Hamna ' Kesi ' hapo Mkuu hasa kwa mazingira halisi ya jambo lenyewe.
Abanwe said pia

Mume anasema alitoka kazini akapitia kununua kitoweo...
Mke anasema Mume alitoka kazini na kisha akafika nyumbani na kuacha funguo kisha akatoka kwenda anakojuwa mwenyewe na yakamkuta ya kumkuta.

Na Saidi hawezi kueleza ukweli, atabaki na porojo hizohizo, maana anajuwa ukweli ukifika kwa mkewe basi atabeba begi lake kama alivyo na kusepa...

Shtukeni, sio mnaburuzwa kama kia la Kenge...
 
Hata kama Scorpion atashinda kesi mahakamani,atakuja kuhukumiwa kitaani labda ahame kwa Mnyamani.

Binafsi niliyafuatilia haya mahojiano kutoka Clouds na nitaendelea kukiamini kile nilichokisikia kule kuliko hizi hekaya za online strangers wa JF.

Kama Scorpion angekuwa kweli ni mtu innocent ni lazima jamii yake ingesha-react kwenye media siku nyingi sababu hili tukio limepata coverage kubwa mno.

Kwa nini watetezi wake wawe online strangers pekee? Nendeni hata EFM mkajitambulishe kwa majina yenu then mfanye hiki mnachokifanya.
 
Kuna mtu ameuliza hapa "Hivi jamani kuna jambo jingine mimi linanishangaza, huyu aliyetobolewa macho kachukua muda gani kupona makovu?"

Sasa tafakari hilo, usitumie kichwa kubebea mashkio hayo
Scorpion alipopelekwa mahakamani alikua mtu mwenye tabasam la bashasha tofaauti kabisa na tension iliyokuwepo katika jamii na media. "body language".
 
Sasa Uchunguzi wako umegundua Ni Nani Aliemtoa macho?
 
Kupata taarifa na kuelewa taarifa ni mambo mawili tofauti. Wabongo ni mabigwa wa mihemko.
Scorpion huyu wa dume condom yawezekana tukio hili kafanya ila ukiangalia kwa undani c kama tunavyolidhani; sio mazingira ya ukibaka zaidi!! Basi wajitokeze na wahanga wengine wapaze sauti zao!! Kuna kitu nyuma ya hili tukio c bure! Ukikutana na anaemjua vzr ana mtetea na vibaka wanaofanya uharifu buguruni wana mwogopa mbaya
Justification ya kutoa macho ipo??

Hilo ndio kubwa madam na linamshangaza kila mmoja.

Ila kwa mujibu wa maelezo ya wengi, jamaa hakuwa kibaka wala mhalifu, sasa huku kutoboana macho vipi?
 
Mume anasema alitoka kazini akapitia kununua kitoweo...
Mke anasema Mume alitoka kazini na kisha akafika nyumbani na kuacha funguo kisha akatoka kwenda anakojuwa mwenyewe na yakamkuta ya kumkuta.

Na Saidi hawezi kueleza ukweli, atabaki na porojo hizohizo, maana anajuwa ukweli ukifika kwa mkewe basi atabeba begi lake kama alivyo na kusepa...

Shtukeni, sio mnaburuzwa kama kia la Kenge...
hiyo clip au sauti ambayo mke wa Said alisema Said alipitia nyumbani kwanza....tuwekee humu tuisikilizeee
 
Yeah inachanganya sana. Investigative Journalists ni muhimu sana nchini. Matukio kama haya ni muhimu yakafanyiwa habari za kiuchunguzi, si kama walivyoripoti wale jamaa.
Mkuu hapa hatuna na hatuwezi kupata investigate journalists maana wote wanaishi kwa kutegemea bahasha za khaki. Hawana independent minds
 
Maswali.
1.Said alitobolewa macho lini?
2.Vidonda na Macho mbona linaonyesha kama tukio la mda?
3.Said alisema mtu aliyemtoboa macho ni mweupe ila scorpion mweusi,hapo vipi?
4.Kwanini samjet alijipeleka mwenyewe kituoni na hata alivyopelekwa mahakamani alikuwa mtu wa furaha,spinning escrow ?
 
Tukio ni la juzi lakini aliyetolewa macho alishaenda kulazwa KCMC kama macho yalitobolewa buguruni KCMC alifata nini??kwa nini akwenda MNH?je kule alikuwa na PF 3 yakutoka wapi?je ni siku ngapi zimepita baada ya tukio?je KCMC alikaa siku ngapi? Maswali ni mengi kuliko tatizo lenyewe.
Umesahau na CCBRT alisema ameenda
 
View attachment 415577

Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salim Njwete 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.

Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.

Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.

Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.

Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...

Tuendelee..

Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.

Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.

Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?

Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.

Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.

Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.

Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.

Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..
Hujasema popote kuwa huyo Scorpion alikuwa na kazi gani rasmi. Unaamini kuwa alikuwa akusaidia ulinzi? Nani amekudhihirishia kuwa aliwahi kukamata wahalifu na kuwafukisha kwenye vyombo vya dola? Kwa maoni yangu Scorpion aliishi kwa kudanganya umma kuwa ni mtu mwema akisaidia kudhibiti wahalifu, shughuli aliyojipa mwenyewe, lakini ni mhalifu aliyejificha katika kivuli cha wema.

Kitendo cha kumvamia mtu na kumdhuru mbele ya kadamnasi bila kuogopa kuwa wananchi wanaweza kunigeuzia kibao kinaonesha jinsi alivyokuwa mbabe wa kutisha! Nani asiyejua hasira ya wananchi inavyokuwa litokeapo tukio la binaadam kufanyiwa vitendo vya kikatili? Polisi wangekuta tayari Scorpion ameuawa na wananchi wenye hasira.

Usijenge mazingira ya kubadili mtazamo wa umma. Scorpion ni mhalifu tena mzoefu maana ilishasemekama mapema kuwa ni hatari watu wa Buguruni wanamuogopa.
 
Ni kweli Scorpion amemtoboa mtu macho.
Swali ni nini kilichomfanya afanye uhalifu huo tena hadharani?
Wehu?
Bangi?
Kisasi?
Alitumwa?
Una uhakika gani kuwa ni kweli scorpion ndio aliemtoboa macho???
 
Back
Top Bottom