Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

View attachment 415577

Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salim Njwete 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.

Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.

Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.

Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.

Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...

Tuendelee..

Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.

Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.

Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?

Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.

Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.

Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.

Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.

Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..
Iko hivii? Wewe mtoa uzi haujatoa authentication ili sisi tukuamini kuwa wewe ndiye huyo na utafiti ulioufanya ni sahihi na wa kweli.
Vita vinapopiganwa, huwa kuna vikundi vya propaganda huundwa ili kupumbaza na kudhoofisha ari ya adui. Huo mfano unakuhusu wewe mwenyewe, kwa sababu waweza kuwa ni propagandist wa kupiga mbiu ili kushusha mihemuko na lawama anazoelekezwa member wako . Na huo ni mfano wa kwanza. Mfano wa pili ulio wazi ni kwamba.
Vibaka,majizi na majambazi wote kwa ujumla wao wana sura mbilimbili. Moja ni ya eneo analoishi na nyingine ya kule anakofanyia matendo yake maovu.
Wana uwezo mkubwa sana wa kutokuonesha uhalifu wao maeneo wanapoishi, wakiwemo ndugu,jamaa na majirani wasiweze kumtambua ukibaka wake. Na siku likibumbumburuka, hutokea ubishi na utetezi mwingi sana kuwa huyu ndugu yetu si mwizi, yeye ni mchungaji na kanisa lake analolihudumia ni lile pale. Wengi wao hutambulika kama wafanya biashara na wajasiliamali wakubwa.
Hadi anakuja kuuawa kwenye tukio watu huendelea kutoamini.
Suala hilo lipo mahakamani na kwakuwa lina sura ya kitaifa, sasa ni lazima ukweli utajulikana tu. Na tukae tusubiri.
 
Watz mnajua sana kuunganisha dots! Hv mnataka kusahau mapema hv machungu ya unyama huu na kuanza kumtakasa mtu kwa utafiti wa kufikirika kama huu! Daaa tz yetu jmn! Huyu mtu ameshapoteza duniani watu zaidi ya 4 bado mnatafuta ukweli buguruni? Binadamu tumepewa kipaji cha kusahau haraka!
Kama keshatoa uhai watu 4 nawe unajua ,kwanini hukutoa taarifa polisi?!
 
Mimi naomba kujua jambo hapa nikuulize jamaa uliyefanya utafiti. Mmiliki wa meza alipokuwa akinunua Said kuku yupo au hayupo? Je, upelelezi wako uliuanzia kwenye meza hiyo? Je, katika ulioongea nao kuna mmoja wapo aliyeshuhudia tukio? Kama alishuhudia tukio, alimwona nani akitenda tukio hilo? Au upelelezi wako ulijikita kujua kama scorpion ni kibaka au la. Sisemi moja kwa moja kuwa scorpion ndiye katenda, hiyo ni kazi ya mahakama lakini anaweza kutenda kwa lengo la visasi cha kwake au kwa niaba ya mtu mwingine. Hii kesi ni ngumu sana zaidi ya watu wanavyofikiria. Said ambaye alichukua PF 3 ama hakuchukua? Kama alichukua PF ni kutoka kituo gani? Kwa maelezo yake ni kwamba alipoteza fahamu, je ni nani aliyempeleka hospitali? Aliyempeleka hospitali alimkuta mazingira gani? Katika maelezo ya Said anasema kuna dogo alimwambia yeye aliona tukio zima, je huyo dogo alimwambia maneno hayo akiwa hospitali ama nyumbani kwake yeye Said? Na huyo dogo wanafahamiana Said tangu zamani au alimfahamu siku ya tukio? Kama alimfahamu siku ya tukio, huyu dogo walionana vipi hadi kumpa taarifa hiyo kuwa aliliona tukio zima? Majibu yatapatikana kwa watu walioshuhudia tukio na si vinginevyo. Polisi Buguruni wanasema kwa nini hawakumkamata Scorpion?
Ungeendelea mbele kidogo kumdadavua, kidogo ukamatishe uongo na upropagandist wake mleta uzi.
 
Hata simu zake hakuchukua mwizi gani aache simu?
Hata kama kuna jambo nyuma ya pazia. Mim na wew hatulijui tunachojua huyu jamaa kamtoa mwenzie macho na kumsababishia ulemavu wa maisha. So angekuwa muungwan au ni mtu mzur angefuata sheria za nchi na angepata haki yake sio kwa kujichukulia maamuz ya bangi kama hayo. Kwa kifup huyo jamaa ni muuwaj
 
Kama sio kibaka mbona kamchukulia cheni zake na pesa? Acheni zenu hizo bana.
Wale walio hojiwa na Gea Habib mbona walikili kumjua na kumuogopa kwa matukio yake.
Labda mtoa mada ni mpambe wa Scopion, maana kama alikua anadhibiti vibaka sasa mbona Saidi alishambulia akiwa kwenye manunuzi na watu hawakusaidia?
 
Yaani kwa Maelezo ya yule aliyetobolewa macho it means alimvamia straight akaanza kumchoma visu Bila sababu. MI nahisi kuna mengi yamejicha nyuma ya pazia. Kuna haja ya kudadisi Zaidi mengi yatafichuka. Na watanzania wengi wameshamhukumu scorpion.
 
Kama sio kibaka mbona kamchukulia cheni zake na pesa? Acheni zenu hizo bana.
Wale walio hojiwa na Gea Habib mbona walikili kumjua na kumuogopa kwa matukio yake.
Labda mtoa mada ni mpambe wa Scopion, maana kama alikua anadhibiti vibaka sasa mbona Saidi alishambulia akiwa kwenye manunuzi na watu hawakusaidia?

Yaani kabisa unawaamini mashuhuda wanao letwa na Gea?
The thing is huyo Said ni mwongo.
Alidai alitoka Kazini akapitia kununua Kuku kisha aende Nyumbani...wakati Mkewe anasema alirudi Nyumbani akaacha funguo za Ofisi kisha akatoka na kwenda alikokwenda ambapo siku si nyingi mtapajuwa tu na ndipo mtagundua kuwa huyo Saidi hakuwa na kheri.

Hio taarifa ya kutobolewa kwake Macho imechelewa kutolewa kwa kuwa ukweli wanaujuwa, na hata waliokurupuka kuipika habari na kuipeleka hewani iko siku yatawarudia tu...maana walisema wahenga Malipo ni hapahapa Duniani.
 
Yaani kwa Maelezo ya yule aliyetobolewa macho it means alimvamia straight akaanza kumchoma visu Bila sababu. MI nahisi kuna mengi yamejicha nyuma ya pazia. Kuna haja ya kudadisi Zaidi mengi yatafichuka. Na watanzania wengi wameshamhukumu scorpion.

Kwa watanzania iko hivi, ukitangulia kufikisha malalamiko basi wewe ndio umeonewa...
 
Tukio linasisimua, linasononesha na linaumiza kila mtu anatueleza anayo yaona yeye na wengine wanachangia kulingana na mihemko yako ambapo wachangiaji wanazidi kutuchanganya!, kilichofanyika Buguruni sio siri wana Buguruni wanajua kilichotokea siku ya tukio ila najua hawajui maisha halisi ya nyuma waliokuwa wakiishi Scorpion na aliyetobolewa macho watu wanao wafahamu fika na wataalam watusaidie hilo kwanza. Hayo mengine tuiachie mahakama itende kazi yake.
 
Kwanini mtu akiwa na mawazo tofauti, watanzania huwa tunaona ametumwa! Mtoa mada hakuna sehemu alipo-justify alichofanya mhusika lakini huwa ni vizuri kutoa haki ya kusikiliza upande wa pili kabla ya kuamua mihemko na huruma vitoe maamuzi.
Kwakweli huyu jamaa kafanya utafiti kitu ambacho media haijakifanya. Nilijiuliza sana kwann kibaka akutoe macho na shida ya kibaka inajulikana. Hapa kuna story ndefu tamu na mtolewa macho huenda anaijua vyema. Nafkir vibaka wamesherekea watarudi maeneo hayo kwa mwendo kasi.
 
Aliyeng'olewa atamtambuaje kwa kuwa yeye sasa ni kipofu? Utasema sauti, wewe unaweza kukariri sauti ya mtu ambaye hukuwahi kumfahamu?
Nyie endeleeni na uhalifu wenu, ila kumbuka damu za watu zitawafuata, na hamtabaki salama.
 
Kama sio kibaka mbona kamchukulia cheni zake na pesa? Acheni zenu hizo bana.
Wale walio hojiwa na Gea Habib mbona walikili kumjua na kumuogopa kwa matukio yake.
Labda mtoa mada ni mpambe wa Scopion, maana kama alikua anadhibiti vibaka sasa mbona Saidi alishambulia akiwa kwenye manunuzi na watu hawakusaidia?
Huo bado sio ushahidi inawezekana alietolewa macho ni muongo....
 
Tukio ni la juzi lakini aliyetolewa macho alishaenda kulazwa KCMC kama macho yalitobolewa buguruni KCMC alifata nini??kwa nini akwenda MNH?je kule alikuwa na PF 3 yakutoka wapi?je ni siku ngapi zimepita baada ya tukio?je KCMC alikaa siku ngapi? Maswali ni mengi kuliko tatizo lenyewe.
 
Hata kama kuna kitu nyuma ya pazia hiyo haiwezi kujustfy kumtoa mtu macho. Kuna mtu juzi kafungwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumlawiti mwanaume aliyemfumania gest na mke wake.
 
Back
Top Bottom