Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Kufikirika? Unamaanisha nini? Mkuu mimi siungi mkono unyama huu, nisome vizuri, lakini nilichokikuta ndicho nilichokileta. Huamini? Nenda Buguruni..
Kwenye kutoa macho HAUJAKANA na kwa maandishi yako inaelekea umeambiwa kweli amemtoa ndio ukashangaaa.... Sasa tuambie ulipohoji WALISEMAJE ALIMPIGA HAKUMPIGA!!!! ALIMTOA MACHO AU HAKUMTOA!!!
 
Ukienda Buguruni ukauliza Scop alikuwa kibaka? 10/10 watakujibu HAPANA.
Waliohojiwa na millardayo na gea habibu ni wakazi wa mkuranga au kibamba eti!!!!...na pale alipoenda Makonda kuongea na wananchi wa eneo LA tukio palikuwa ni chanika ati mkuu!!!!!
 
mkuu binafsi sipingani na wewe, ila kidogo uchunguzi wako naona kama haujakamilika hivi....,,,,

Mahojiano yako yalifika nyumbani kwa kina Scorpion ( i mean mtaani kwa scorpion na nduguze)..
Mahojiano kwenye meza lilipotokea tukio, na meza nyingine mbili tatu za tukio.
Mahala pa kazi pa Scorpion, na marafikize kwa maana ya mabaunsa wenzie.
Said Mwenyewe, mkewe, na nduguze wawili watatu.
Ofisini kwa Said, mahala pake pa kazi...
Unaweza kumalizia sehemu ambayo unaona imepelea!
 
Kuhukumiwa na kufungwa law Scorpion kutategemea na aina ya mashitaka aliyofunguliwa pamoja na ushahidi unaojitosheleza kumtia hatiani, vinginevyo jamaa atarudi mtaani.
 
alietolewa macho ni muongo ndio maana maswali ni mengi taarifa zake na za mke wake zimetofautiana!

Taarifa ya mkewe si itakuwa ya kuhadithiwa na mumewe? Sishangai ikitofautiana maana hakuwa eneo la tukio.
 
na mbona aliyetobolewa macho anaonekana kama mlemavu wa muda mrefu ukimtazama

Mawazo ya Watanzania sasa yanawaza nini juu ya kitu gani nyeti na ambacho kinaweza kusumbua mamlaka kisha ni chombo gani cha Habari ambacho kina infulence kubwa masikioni na kitakachosaidia kufanya spin doctoring kisha patatafutwa strategy maalum kwa msaada wa kitu kiitwacho Media Agenda Setting na likikamilika hilo anajitokeza Mtu mmoja mwenye kujua kutaka Sifa kisha analibeba lote huku Watu muhimu wakiwa tayari wameshaandaliwa kutekeleza mambo fulani ili jambo lifanikiwe. Naomba niishie hapa tafadhalini ila nilichogundua Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo. Hata hivyo nawapongeza Wote waliokuwa nyuma ya ' kituko ' hiki ila tunaojua ' kujiongeza ' mchezo wote tumeshauangalia kwa jicho la tatu. Pole sana ' Mtobolewaji ' na Pole mno ' Nge ' japo yawezekana sasa salio ' linasoma ' vizuri.
 
Huyu jamaa aliwai kuua pia aliwai kumvunja dada kiuno lengo lake ni kukupiga kutoboa macho ili ufe kwa kugonga na gari huyu si mtu wa kawaida ni mastermind sana chunguza nyendo zake hata mahakaman kaingia na nguo zingine very rough akatoka na nguo zingine very smart na cha ajabu mwaka 2012 Alishinda million 20 kwenye dume challenge

Noted
 
Yaani kabisa unawaamini mashuhuda wanao letwa na Gea?
The thing is huyo Said ni mwongo.
Alidai alitoka Kazini akapitia kununua Kuku kisha aende Nyumbani...wakati Mkewe anasema alirudi Nyumbani akaacha funguo za Ofisi kisha akatoka na kwenda alikokwenda ambapo siku si nyingi mtapajuwa tu na ndipo mtagundua kuwa huyo Saidi hakuwa na kheri.

Hio taarifa ya kutobolewa kwake Macho imechelewa kutolewa kwa kuwa ukweli wanaujuwa, na hata waliokurupuka kuipika habari na kuipeleka hewani iko siku yatawarudia tu...maana walisema wahenga Malipo ni hapahapa Duniani.

Mkuu nikija huko Tanzania mwezi November tarehe 18. 2016 kutoka huku kwetu nchini Rwanda nilipo sasa naomba tukutane ili nikupe zawadi yako nzuri ya kuthamini ' madini ' haya ya maana na uhakika uliyoyaweka hapa kwani ulichoandika ni kwamba umemaliza kila kitu. Nakuunga mkono 100% ulichokiandika.
 
Kua makini na kauli zako... Dunia ina mengi sana na nchi hii kwa kupakaziana ndiyo yetu tabia...
Leo imekua kwa scorpion na usishangae kesho ukabebeshwa ww zaid ya la scorpion

Mtu kajisalimisha mwenyewe

Kweli unachekesha
 
Ndiyo maana nikasema kesi ipo very tricky! Kama Scorpion akipata lawyer mzuri, basi possibility ya kushinda ni kubwa sana.

Tena kwa 100% Mkuu. Mbona hiyo ' Kesi ' ipo wazi tu na ' nyepesi ' mno. Hamna ' Kesi ' hapo Mkuu hasa kwa mazingira halisi ya jambo lenyewe.
 
Video ni ya kweli. Na yule aliempiga mwanafunzi pia anaitwa Mwl Frank lakini sio Mwl Frank Msigwa
Aiseeee.... !!! Kwahiyo itakuwaje maana anatajwa kuwa nae kafukuzwa chuo na mkopo umesitishwa?
 
Ni kweli Scorpion amemtoboa mtu macho.
Swali ni nini kilichomfanya afanye uhalifu huo tena hadharani?
Wehu?
Bangi?
Kisasi?
Alitumwa?
 
Hivi hakuna harufu ya "papuchi"kweli kwenye tukio hili!!??

Shaka ondoa.
Soon itafahamika tu, na wale viongozi wanaokimbilia matukio ili kujitangaza, sijui sura zao wataziweka wapi?

Maana kuna kiongozi mmoja wa kuteuliwa na Raisi amelisimamia suala hili na wapo wakurupukaji wanaosikilizaga taarifa ya kwanza na ndio hio wanaiamini, basi weeeh wanamfagiliaje?
 
Back
Top Bottom