Kipaji Halisi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2012
- 2,280
- 1,366
Aseee huu Mjadala unaleta matumaini ya kupata ukweli japo kdg..
cc,Gang Chomba
cc,Gang Chomba
View attachment 415577
Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salim Njwete 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.
Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.
Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.
Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.
Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...
Tuendelee..
Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.
Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.
Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?
Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.
Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.
Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.
Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.
Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..
Tukio ni la juzi lakini aliyetolewa macho alishaenda kulazwa KCMC kama macho yalitobolewa buguruni KCMC alifata nini??kwa nini akwenda MNH?je kule alikuwa na PF 3 yakutoka wapi?je ni siku ngapi zimepita baada ya tukio?je KCMC alikaa siku ngapi? Maswali ni mengi kuliko tatizo lenyewe.
Sasa mimi unajua nipo busy nashugulikia nyumba yangu unajua nina nyumba mpya najenga cha msingi tuonane nikupe nondo zote uende mahakaman ukasimamame shaid wa mlemavu haki lazima itendeke mkuuuUka ripoti polisi kuhusu tukio la uyo dada, na kuhusu mauaji aliofanya. Ili haki itendeke.
ndg za hao watu zaid ya 4 wajitokezee....mbona naona km wako kimyaaa??Watz mnajua sana kuunganisha dots! Hv mnataka kusahau mapema hv machungu ya unyama huu na kuanza kumtakasa mtu kwa utafiti wa kufikirika kama huu! Daaa tz yetu jmn! Huyu mtu ameshapoteza duniani watu zaidi ya 4 bado mnatafuta ukweli buguruni? Binadamu tumepewa kipaji cha kusahau haraka!
wewe kama una nondo zote peleka polisi watashughulikia. Isije kua unaongea sana tu halafu uthubutu huna.Sasa mimi unajua nipo busy nashugulikia nyumba yangu unajua nina nyumba mpya najenga cha msingi tuonane nikupe nondo zote uende mahakaman ukasimamame shaid wa mlemavu haki lazima itendeke mkuuu
Mkuu interest hongera kwa kazi uloifanya katika kufuatilia kiini cha uhalifu uliofanywa na bwana scorpion, lakini naona bado hujamaliza kazi yako maana umetujuza zaidi upande wa mtendaji lakini upande wa mtendewa inaonekana huaufuatilia.View attachment 415577
Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salim Njwete 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.
Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.
Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.
Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.
Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...
Tuendelee..
Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.
Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.
Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?
Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.
Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.
Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.
Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.
Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..
Ni kweli ila tatizo la mjini hakuna ushirikiano, kila mtu anajifanya yupo busy halikua anaona mwenzake anaangamia na kuomba msaada.Mkuu taratibu. Kuna ndg keshakuwa mlemavu wa macho. Mshukuru Mungu kaka, hujafa hujaumbika.
Walishindwa kupiga picha za tukio kwa smartphone zao?..Ni kweli ila tatizo la mjini hakuna ushirikiano, kila mtu anajifanya yupo busy halikua anaona mwenzake anaangamia na kuomba msaada.
Hapa kuna shidaItakuwa kuna kitu nyuma ya pazia.
Kibaka kumtoa mtu macho siyo jambo dogo, wengi tusingekuwa na macho.
hawa wanabebwa na mihemko hawaelewi hata waandikacho mkuu, Ila hili swala sheria inabidi iume hawa hawa Maana nikimwangalia yule ndugu roho inanipasuka kwa hasira sana.Mkuu taratibu. Kuna ndg keshakuwa mlemavu wa macho. Mshukuru Mungu kaka, hujafa hujaumbika.
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza, ila ni vyema wakazi wa maeneo ya mijini kuwa na ushirikiano.Walishindwa kupiga picha za tukio kwa smartphone zao?..
Kwanini mtu akiwa na mawazo tofauti, watanzania huwa tunaona ametumwa! Mtoa mada hakuna sehemu alipo-justify alichofanya mhusika lakini huwa ni vizuri kutoa haki ya kusikiliza upande wa pili kabla ya kuamua mihemko na huruma vitoe maamuzi.
Naam...sasa umenena [emoji4]Mkuu wa hapahapa, tangu hili sakata limeanza, wewe umeshamsikia mhanga mwingine? Kumtoa mtu macho ni unyama na Scorpion aadhibiwe kwa unyama huo at the same time tusikie kisa cha Said kutolewa macho, isije kuwa tunampa mtu sympathy ilopitiliza ilhali hastaili, mambo mengi huwa yana mambo mengi nyuma ya pazia.
Hivi hakuna harufu ya "papuchi"kweli kwenye tukio hili!!??
Anaweza vipi kumtambua akiwa hana macho?Italeta utata sana mahakamani pale hakimu atakapomuamuru Said amtambue Scorpion...hii kesi ipo very tricky!
Kwa maelezo ya Said watu walikuwepo.kwani wakati kitendo hicho kinafanyika ilikuwa muda gani?inamaana hakukuwa hata na mtu mwingine aliyesikia sauti,kelele,kuona tukio lenyewe n.k?