Mtoa mada hakua na sababu ya kutonesha mioyo ya watanzania, hivi aliyetobolewa macho angekua kaka yake angeandika haya ambayo dhahili yanaonyesha kutetea vitendo viovu vifanyavyo na watu wachache! Kila mwema ana baya lake na kila mbaya ana jema lake pamoja na Wema woote wa scorpion ubaya wake ni kutuhumiwa kumtoboa macho mwenzieKwanini mtu akiwa na mawazo tofauti, watanzania huwa tunaona ametumwa! Mtoa mada hakuna sehemu alipo-justify alichofanya mhusika lakini huwa ni vizuri kutoa haki ya kusikiliza upande wa pili kabla ya kuamua mihemko na huruma vitoe maamuzi.
Una maana gani unaposema Hastahili? ina maana humuhulumii kijana mwenzio ambaye maisha yake yamebadilishwa kwa muda mfupi sana kutoka kuona nuru kwenda kuona kizaMkuu wa hapahapa, tangu hili sakata limeanza, wewe umeshamsikia mhanga mwingine? Kumtoa mtu macho ni unyama na Scorpion aadhibiwe kwa unyama huo at the same time tusikie kisa cha Said kutolewa macho, isije kuwa tunampa mtu sympathy ilopitiliza ilhali hastaili, mambo mengi huwa yana mambo mengi nyuma ya pazia.
Hakuna yeyote kati yetu mwenye uwezo wa kutoa maamuzi zaidi ya mahakama.
Kama mtoa mada alivyokuwa na mawazo yake tofauti nasi tuna yetu tofauti.
Period
Umeona ee!?Sure
Nimetafakari...nauona ugumu ulipo ktk hii kesi.
"Mtuhumiwa akiwa mita chache...." ina maana mpaka hapo alikuwa anamuona au alihisi (nina uhakika alikuwa haoni tena)Naomba usikilize ile clip aliyokuwa anahojiwa kwani kaeleza yote.Alisema alisaidiwa na raia mwema na ikatokea gari ya polisi na alichukuliwa na hiyo gari ya polisi na mtuhumiwa akiwa mita chache pembeni.Alipelekwa moja kwa moja polisi na kuchukuliwa maelezo na akapewa PF3.
cc Dude (bongo movie)Hii kesi ikisha isha itabidi tutengeneze filamu,hope itauza sana
Una maana gani unaposema Hastahili? ina maana humuhulumii kijana mwenzio ambaye maisha yake yamebadilishwa kwa muda mfupi sana kutoka kuona nuru kwenda kuona kiza
Mkuu wa hapahapa, tangu hili sakata limeanza, wewe umeshamsikia mhanga mwingine? Kumtoa mtu macho ni unyama na Scorpion aadhibiwe kwa unyama huo at the same time tusikie kisa cha Said kutolewa macho, isije kuwa tunampa mtu sympathy ilopitiliza ilhali hastaili, mambo mengi huwa yana mambo mengi nyuma ya pazia.
Hakuna sehemu niliposema Scorpion hajafanya kosa, kabla ya kuandika hayo, niliwa-quote watu wengi, kila mmoja akimshutumu mleta mada ametumwa au kuna kitu kinachomfanya amtetee mtuhumiwa, Kama ulivyokuwa na haki ya kusema mawazo yako bila mwingine kusema umwetumwa na Said, pia mleta mada ana haki ya kueleza mawazo yake bila wengine kusema ametumwa na Scorpion au ana uswahiba naye so long as huna hoja ya kusema ametumwa zaidi ya hisia.
Scorpion hastahili hata kusikilizwa kwa unyama alioutenda akiwa na akili timamu.Mtoa mada hakua na sababu ya kutonesha mioyo ya watanzania, hivi aliyetobolewa macho angekua kaka yake angeandika haya ambayo dhahili yanaonyesha kutetea vitendo viovu vifanyavyo na watu wachache! Kila mwema ana baya lake na kila mbaya ana jema lake pamoja na Wema woote wa scorpion ubaya wake ni kutuhumiwa kumtoboa macho mwenzie
Haijalishi,tukio ameshafanya na kamuaribia mwenzie maisha.
Kila nikiona habari/picha ya yule jamaa (Said) aliyetobolewa macho machozi hunitoka.
Scorpion ni mnyama,hastahili huruma wala msamaha.
Hivi jamani ni nani anayeweza kuvaa viatu vya Said?
Mwanaume aliyekuwa mzima anafanya shughuli zake leo hii ni kipofu.
Ana mke na watoto wanaomtegemea.
Bila kumsahau mama yake...[emoji24] [emoji24] [emoji24]
Kiukweli siwezi kusikiliza utetezi wowote ule juu ya Scorpion kwa unyama alioutenda akiwa na akili timamu.
Anyways...kazi nzuri,lingekuwa tukio tofauti na hili kiasi ungesaidia.
Kwani Said alimtoboa macho Scorpion?tusubiri mahakamani au mahakama wakati wa utetezi wa scorpion ndio tupime, maana leo hii unamtetea au kumuonea huruma Said huku ukiwa hujui au hujapata ukweli wa mtuhumiwa Scorpioni. kwa mfano ikajulikana Said ni mwizi alitaka kumpora scorpion kwa kutumia kisu na scorpion kwa ujasiri akapambana naye utasemaje? hayo ni mawazo tu.. Tusubiri na utetezi wa scorpin...
Kwahiyo ile video ni uongo?Hata yule FRANK MSIGWA kumbe sie, amechafuliwa tu mwalimu wa watu (source: Tanzagiza facebook)
Nimesikitika sana
Kwani Said alimtoboa macho Scorpion?
Na kwanini tuanze kujenga picha ya huenda Said nae ni mbaya?
Maelezo tuliyoyapata na kitendo alichokifanya vinanipa mimi uwezo wa kumtuhumu Scorpion.
Na hata endapo ikija kubainika Said nae alichangia alichofanyiwa itakuwa sawa endapo tu kama amewahi kuua au kumtoboa mtu macho.
Hapo ndipo tutasema aliyeua kwa upanga....
Ila kwa sasa hakuna namna yoyote inayoweza kumtoa Scorpion hatiani.
ni mahakama tu ndio inaweza kumtia hatiani scorpion, vinginevyo ni bwana said kuwahi polisi na kutoa maelezo ambayo yalisababisha scorpion kukamatwa, binafsi siwezi kumuhukumu Scorpion mpaka nione ushahidi wake na utetezi wake ndio nitamuhukumu, kutoboa au kutobolewa macho sio kitu sahihi lakini itategemea na tukio au mazingira, kama nataka kudhuru mtu kwa manufaa yangu halafu huyo mtu akajitetea kwa kutoboa macho atakuwa yuko sahihi, kama scorpion kamtoboa macho Said eti kisa papuchi scorpion atakuwa kakosea na anastahili adhabu.... Tusubiri mahakama, na ushahidi wa Scorpion maana wa Said tumeusikia halafu tutapima...
Hii ripoti imewachanganya wengi. Nimeshangazwa na baadhi ya michango na maoni ya watu humu.
Kuna wanaodhani namtetea scorpion kwa kumtia ubaya Said..
Wapo wanaofikiri ninajaribu kuonyesha kuwa scorpion hakufanya hilo tukio..
Wengine wanahisi niko hapa kufanya propaganda...
Ndugu zangu, sina utetezi wa upande wowote kwa kuwa sina maslahi binafsi. Nimeandika bila kuhariri maelezo yoyote. Hata nikajitahid sana kufafanua kwenye bandiko langu kuwa HAKI ITENDEKE. Sijui ugumu unatoka wapi sasa hapo!
Nasisitiza, sijaweka maoni binafsi. Nimeeleza nilichokikuta ndio maana nikapata ujasiri wa kusema anayehitaji kufahamu aende Buguruni akaulize.
Kwa watu wa Buguruni, Scorpion hakuwahi kuwa muhalifu. Hili tukio la kumtoa mtu macho limemshangaza kila mkazi wa maeneo yale ambae anamfahamu scorpion. Take it from me!
MUHIMU: Tuiachie mahakama ifanye kazi yake, tumuombee ndugu Said apate ahueni na apone maumivu, ikibidi tumuweke hata kwenye maombi, lakini kamwe tusiache kuwajibika kuhoji masuala yenye mkanganyiko ili tuisaidie jamii.
Asante..