Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Huyu jamaa aliwai kuua pia aliwai kumvunja dada kiuno lengo lake ni kukupiga kutoboa macho ili ufe kwa kugonga na gari huyu si mtu wa kawaida ni mastermind sana chunguza nyendo zake hata mahakaman kaingia na nguo zingine very rough akatoka na nguo zingine very smart na cha ajabu mwaka 2012 Alishinda million 20 kwenye dume challenge
 
Huyo alietobolewa macho kwanini hakuenda polisi kureport baada ya tukio,na akasubiri siku kadhaa zimepita ndo akahojiwa na waandishi ndo suala zima likafahamika?,
isijekuwa anamwangushia zali huyo scopion wakati watoboa macho ni vibaka walimtaiti night
 
Huyu jamaa aliwai kuua pia aliwai kumvunja dada kiuno lengo lake ni kukupiga kutoboa macho ili ufe kwa kugonga na gari huyu si mtu wa kawaida ni mastermind sana chunguza nyendo zake hata mahakaman kaingia na nguo zingine very rough akatoka na nguo zingine very smart na cha ajabu mwaka 2012 Alishinda million 20 kwenye dume challenge

Unao ushahidi ndugu?
Au na wewe umesikia story za mtaani ni vyema tukapata mashahidi waliowahi kukabwa au kuumizwa na huyo scop
kuliko kuendeshwa kwa hisi.
Ni mtazamo tu lakini
 
Watz mnajua sana kuunganisha dots! Hv mnataka kusahau mapema hv machungu ya unyama huu na kuanza kumtakasa mtu kwa utafiti wa kufikirika kama huu! Daaa tz yetu jmn! Huyu mtu ameshapoteza duniani watu zaidi ya 4 bado mnatafuta ukweli buguruni? Binadamu tumepewa kipaji cha kusahau haraka!
 
View attachment 415577

Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salum Henjewele 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.

Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.

Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.

Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.

Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...

Tuendelee..

Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.

Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.

Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?

Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.

Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.

Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.

Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.

Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..
Sikuoni mtetezi, ila nashukuru umenisaidia kwenda hatua moja mbele juu ya nilivyomdhania Scorpion mara tu nilipoziona picha zake na kupata picha zake, bado maswali yanazidi kumuhusu huyu jamaa!!!
 
Watz mnajua sana kuunganisha dots! Hv mnataka kusahau mapema hv machungu ya unyama huu na kuanza kumtakasa mtu kwa utafiti wa kufikirika kama huu! Daaa tz yetu jmn! Huyu mtu ameshapoteza duniani watu zaidi ya 4 bado mnatafuta ukweli buguruni? Binadamu tumepewa kipaji cha kusahau haraka!
Kufikirika? Unamaanisha nini? Mkuu mimi siungi mkono unyama huu, nisome vizuri, lakini nilichokikuta ndicho nilichokileta. Huamini? Nenda Buguruni..
 
Unao ushahidi ndugu?
Au na wewe umesikia story za mtaani ni vyema tukapata mashahidi waliowahi kukabwa au kuumizwa na huyo scop
kuliko kuendeshwa kwa hisi.
Ni mtazamo tu lakini
Hayo ndiyo yaliyonifanya nikaenda Buguruni. Kuna maneno mengi sana ya kuokoteza kama hayo ya mkuu hapo juu.
Watanzania, tujisogeze..
 
Huyu jamaa aliwai kuua pia aliwai kumvunja dada kiuno lengo lake ni kukupiga kutoboa macho ili ufe kwa kugonga na gari huyu si mtu wa kawaida ni mastermind sana chunguza nyendo zake hata mahakaman kaingia na nguo zingine very rough akatoka na nguo zingine very smart na cha ajabu mwaka 2012 Alishinda million 20 kwenye dume challenge
Hapana mkuu. Aliwahi kuua na bado awe mtaani tu anafanya shughuli zake? Itendee haki akili yako mkuu.. Usisambaze uongo. Tukemee uovu, ila tusiushetanishe zaidi ili kufurahisha nafsi..
 
Nahisi kuchanganyikiwa. Sometimes nilikua najiuliza inakua vp?
Sipati majibu.
Natamani saaaana kuwa mpelelezi sema MUNGU hapendi niwe

Yeah inachanganya sana. Investigative Journalists ni muhimu sana nchini. Matukio kama haya ni muhimu yakafanyiwa habari za kiuchunguzi, si kama walivyoripoti wale jamaa.
 
Huyu jamaa aliwai kuua pia aliwai kumvunja dada kiuno lengo lake ni kukupiga kutoboa macho ili ufe kwa kugonga na gari huyu si mtu wa kawaida ni mastermind sana chunguza nyendo zake hata mahakaman kaingia na nguo zingine very rough akatoka na nguo zingine very smart na cha ajabu mwaka 2012 Alishinda million 20 kwenye dume challenge
wa hiyo alivyoua hakushtakiwa? Huyo alievunjwa kiuno yuko wapi?
 
Itakuwa kuna kitu nyuma ya pazia.
Kibaka kumtoa mtu macho siyo jambo dogo, wengi tusingekuwa na macho.

Hapo sasa. Wakazi wanasema jamaa hakuwa kibaka. Hili tukio ni zaidi ya tunalivyolifahamu.
Huyo Scorpion abanwe aseme ukweli..
 
Binafsi najiuliza kwanini amtoboe macho.. Na huyu jamaa alietobolewa macho alikua kinyozi.. Hivyo kwa kuangalia tu hakua na Fedha nyingi.. Alikua na maisha ya kawaida.. Na huyu kinyozi inaonyesha anamjua scorpion...
Hapana. Nina interest na ukweli.
Scorpion apewe stahiki yake ila majibu ya maswali tata pia ni muhimu.
Umesoma alivyoandikwa mitandaoni? Kwamba ndio tabia yake blah blah sijui anasukuma watu wagongwe na magari blah blah..

Nenda Buguruni..
 
Kufikirika? Unamaanisha nini? Mkuu mimi siungi mkono unyama huu, nisome vizuri, lakini nilichokikuta ndicho nilichokileta. Huamini? Nenda Buguruni..
Nimekusoma kiongozi but huwezi kujua ukweli ukihitimisha utafiti wako pale buguruni pekeake! Wauwaji huwa wanafanya ishu Mbezi na makazi na Fuji ndogondogo karibu na kwao!
 
View attachment 415577

Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salum Henjewele 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.

Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.

Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.

Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.

Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...

Tuendelee..

Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.

Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.

Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?

Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.

Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.

Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.

Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.

Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..
Mkuu asante sana. Mimi natamani sana JF iwe na memba wengi kama wewe wanajali kuchunguza na si kufuata tu mkumbo! Unakuta mtu anaandika utafikiri alikuwa sehemu ya tukio. Kwa ujumla hili tukio hata mimi nimekuwa na mashaka nalo tangu waanze kuliandika. Kila nikijaribu kujenga kitu fulani kutoka kwenye simulizi ilikuwa inakataa. Maelezo yako naweza kuyakubali kabisa. Huyu jamaa inaonekana hakuwa mwizi. (kumbuka sipingi kama ndie aliyefanya hilo tukio). Lakini bado tunabaki na maswali kadhaa: Ni kwanini (kama ni yeye) alimfanyia jamaa unyama huo? Nadhani wangepatikana watu waliokuwepo wakati wa tukio ndio wanaweza kuelezea zaidi!
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Hapana mkuu. Aliwahi kuua na bado awe mtaani tu anafanya shughuli zake? Itendee haki akili yako mkuu.. Usisambaze uongo. Tukemee uovu, ila tusiushetanishe zaidi ili kufurahisha nafsi..
Ni kwel alishinda M20 za dume condom Mashindano....kuna ishu zinafichika juu ya unyama huu...ukimchek anavyopelekwa Mahakaman anajiamin na anacheka yupo comfortable sana..ni kama anajua analofanya
 
Back
Top Bottom