Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Ukweli ni upi kuhusu tukio la Scorpion wa Buguruni?

Jinsi anavyoua ni kutoboa macho kisha anakutupa barabaran ili gar likugonge na yeye hana kesi hapo kesi ya mauaji ya dereva...ushaid mimi ni mkazi wa mnyamani huyu ana genge lake la wacheza karet akifika kibandani kwako kula chips halipi ni ubabe tu

cc: Interest
 
Wala si ndugu yangu. Sijawahi hata kumuona. Nilichoandika nimekifahamu jana.

Sitetei, sihukumu.

Nataka haki itendeke. Kila mtu apate stahiki yake.
Mbona sijasikia utetezi wa upande wa scopion?
 
Hata kama kuna kitu nyuma ya pazia hiyo haiwezi kujustfy kumtoa mtu macho. Kuna mtu juzi kafungwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumlawiti mwanaume aliyemfumania gest na mke wake.
Kama kunasheria za kumhukumu alietembea na mke wa mtu, alielawitiwa nae ana kesi ya kujibu.
 
kwani wakati kitendo hicho kinafanyika ilikuwa muda gani?inamaana hakukuwa hata na mtu mwingine aliyesikia sauti,kelele,kuona tukio lenyewe n.k?
Kwani mkuu hujapata kuskia audio said akielezea tukio zima?
 
Itakuwa kuna kitu nyuma ya pazia.

Kibaka kumtoa mtu macho siyo jambo dogo, wengi tusingekuwa na macho.
Huyu sio kibaka ni jambazi lilokubuhu. Kesi yake inaitwa "armed robbery". Kibaka anafanya unyag'anyi wa kutumia silaha? Akifanya hivyo si kibaka ni jambazi.
 
Huyu jamaa aliwai kuua pia aliwai kumvunja dada kiuno lengo lake ni kukupiga kutoboa macho ili ufe kwa kugonga na gari huyu si mtu wa kawaida ni mastermind sana chunguza nyendo zake hata mahakaman kaingia na nguo zingine very rough akatoka na nguo zingine very smart na cha ajabu mwaka 2012 Alishinda million 20 kwenye dume challenge
Uka ripoti polisi kuhusu tukio la uyo dada, na kuhusu mauaji aliofanya. Ili haki itendeke.
 
Kwa watanzania iko hivi, ukitangulia kufikisha malalamiko basi wewe ndio umeonewa...


huyo skopion kujichukulia sheria mkononi kumemponza...

na kwa nn huyo said amtaje huyo skopion na sio mtu mwingine...

Hata kama kuna kitu nyuma ya pazia hiyo haiwezi kujustfy kumtoa mtu macho. Kuna mtu juzi kafungwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumlawiti mwanaume aliyemfumania gest na mke wake.
 
Jinsi anavyoua ni kutoboa macho kisha anakutupa barabaran ili gar likugonge na yeye hana kesi hapo kesi ya mauaji ya dereva...ushaid mimi ni mkazi wa mnyamani huyu ana genge lake la wacheza karet akifika kibandani kwako kula chips halipi ni ubabe tu
Hao waliouawa hawana ndugu? Yaani muuaji anajulikana watu wako kimya tu hachukuliwi hatua zozote? Ukiambiwa uende mahakamani ukatoe ushahidi wa hayo mauaji uko tayari?
 
View attachment 415577

Kama ambavyo raia wengine walivyoshtushwa na tukio zima la kusisimua kuhusu bwana Salim Njwete 'Scorpion', kumnyofoa macho ndugu Said, nami ndivyo nilivyopata mshangao na butwaa juu.

Sitaki kurejea tena sakata hilo kwa kuwa kila mtu analifahamu. Badala yake nitajikita zaidi kwenye kile nilichokifahamu baada ya tukio. Sitaongeza wala kupunguza neno.

Usiku wa tarehe 9/10/2016, siku chache baada ya tukio hili kutokea, nilifika eneo la tukio kuokoteza mawili matatu kuhusu ishu nzima.

Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii ilinilisha taarifa za kutosha, lakini ziliniacha na maswali ambayo nisingeweza kupata majibu isipokuwa kwa kufika mwenyewe eneo la tukio na kuuliza. Hivyo nikaenda.

Shauku ilinipa sababu za kuhoji. Nikahoji kuanzia barabarani kwa wafanyabiashara ninaofahamiana nao pale. Nikaenda kuhoji mtaani kwetu nilipokuwa nikiishi zamani (niliwahi kuishi Buguruni miaka ya 2010 kurudi nyuma), mwisho nikamalizia kuhoji kwa waendesha bajaj na bodaboda ninaowafahamu. Hawa wote wapo katika kitovu cha eneo ambako tukio hili lilitokea, nikaonyeshwa mpaka meza ya nyama ambako ndiko tukio hili ulifanyika...

Tuendelee..

Nilielezwa kuwa, huyu scorpion amekuwa ni mwenyeji wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani kwa kipindi kirefu kidogo. Hupatikana zaidi maeneo ya Hotel ya Popex iliyopo mkabala na mataa ya Barabara ya Mandela, pembeni kidogo ya Bar maarufu ya Kimboka. Anafahamika kama mlinzi wa eneo lile hasa nyakati za jioni. Si mgeni, kila mtu anamjua.

Pale Kimboka kwa machangudoa, pamekuwa pakilalamikiwa uwepo wa vibaka na vijana wahuni ambao hukaba na kupora watu wanaofika kufanya manunuzi. Vibaka hawa huwapora abiria mikoba yao wanaopita na pikipiki pamoja na mali nyingine kama simu na kadhalika.

Sasa wakazi wote nilobahatika kuzungumza nao, wamekiri kuwa Scorpion amekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa pale hasa nyakati za jioni na usiku, kwa kuweza kutokomeza tatizo la wizi na uporaji. Hapa nilishtuka na kushangaa sana! Scorpion huyu huyu?

Si hivyo tu, wapo walioeleza kuwa licha ya kuonekana ni mtu mwenye manguvu, Scorpion hakuwahi kufanya tukio lolote baya la kuiba, kupora wala uvamizi, zaidi ya kujishughulisha na masuala ya usalama wa maeneo hayo, hivyo tukio hili la kumtoa macho kijana Said limemwacha kila mtu mdomo wazi na kubakisha maswali mengi mpaka hivi sasa.

Mshangao mwingine, huu unatoka kwa dereva wa Bajaj aliyenirudisha kwenye makazi yangu, alisema anashangazwa kuwa baada ya tukio, ilipita wiki nzima na Scorpion aliendelea kuwepo mtaani akiendelea na mishe zake kama kawaida bila kukamatwa mpaka alipoamua kwenda kujisalimisha.

Lingine, wapo wanaodhani tukio hili ni la kisasi kati ya Said na Scorpion, ama inawezekana Scopion 'alitumwa' kumshughulikia Said. Hata hivyo, zote hizi ni dhana tu ambazo hazina budi kufanyiwa kazi.

Kwa ufupi, tunaweza kukubaliana kuwa unyama aliofanyiwa ndugu Saidi ni wa kukemewa kwa nguvu zote na sheria ifuate mkondo wake ipasavyo, lakini tusiache kutafuta majibu ya maswali ya msingi kuhusu tukio zima.

Unaniona mtetezi? Nenda Buguruni kaulize..
Alikuwa mlinzi volunteer, akilipwa na Nani?yangu niliyosikia ni kuwa anajeshi LA vibaka, linapofanya kazi yeye huwa pembeni akisimamia, endelea kuleta utetezi wako
 
Binafsi najiuliza kwanini amtoboe macho.. Na huyu jamaa alietobolewa macho alikua kinyozi.. Hivyo kwa kuangalia tu hakua na Fedha nyingi.. Alikua na maisha ya kawaida.. Na huyu kinyozi inaonyesha anamjua scorpion...
Hujafuatilia story ili ujue mhanga alinyanganya nini, acha uongo
 
Alikuwa mlinzi volunteer, akilipwa na Nani?yangu niliyosikia ni kuwa anajeshi LA vibaka, linapofanya kazi yeye huwa pembeni akisimamia, endelea kuleta utetezi wako
Mi nilivyosikia vibaka wate walihama mtaa kwa kumuogopa na alikuwa analipwa na wafanyabiashara hapo mtaani kwa kuwalindia biashara na wateja wao!
 
Tukio ni la juzi lakini aliyetolewa macho alishaenda kulazwa KCMC kama macho yalitobolewa buguruni KCMC alifata nini??kwa nini akwenda MNH?je kule alikuwa na PF 3 yakutoka wapi?je ni siku ngapi zimepita baada ya tukio?je KCMC alikaa siku ngapi? Maswali ni mengi kuliko tatizo lenyewe.
Cc Gang Chomba
 
Binafsi najiuliza kwanini amtoboe macho.. Na huyu jamaa alietobolewa macho alikua kinyozi.. Hivyo kwa kuangalia tu hakua na Fedha nyingi.. Alikua na maisha ya kawaida.. Na huyu kinyozi inaonyesha anamjua scorpion...
imeonesha wapi ya kuwa kinyoozi alikua anamfaham scorpion? ??
 
Back
Top Bottom