Ukweli mchungu: Zanzibar tunaishi kwa kudra za Tanganyika!

Nakwambia hivi, Tanganyika kwa sasa ndio inatusitiri sisi wazanzibar. Bila Tanganyika hatuna ulinzi, usalama wala umeme.

Karafuu iliyokuwa inatupa jeuri ilishakufa kitambo sana, na kwa uvivu wetu tumeshindwa kuifufua, na sasa tunasikia huko Tanganyika mlishaanza kuotesha na kuvuna karafuu yenu kwa fujo.....

Bandari ya Zanzibar iko mahututi maana kila jirani yetu (Beira, Mombasa, Comoro, Eritrea, Djibout, Dar, Mtwara, Tanga) alisha imarisha bandari yake, Zanzibar hatuna tena upekee wa kibandari....

Zanzibar tumebakia na Utalii pekee yake (ambao ni wa msimu, na watalii wenyewe wengi huanzia bara au kumalizia bara maana huko wako huru kuvaa chochote, kula mwaka mzima (huku kula hadharani kipindi cha Ramandan ni mwiko!), kula chochote (hata kitimoto), kunywa chochote(pombe), hapa Zanzibar watalii wanapita kwa siku zisizozidi tatu (kushangaa mchanga mweupe wa beach ambao umegundulika umejaa vilivyo kule Tanganyika (Kigamboni), kutafuna machoko wakizenji na kubwia unga kwa uhuru kisha kusepa zao). Bahati mbaya sana na huo utalii pekee hautoshi kuendesha maisha ya wazanzibar zaidi ya 1.5milioni kwa siku zaidi ya 90.

Yote kwa yote, mmasai ameshaingia Zanzibar na sasa anataka kutawala utaliii wote.

Nasema hivi, Zanzibar bila Tanganyika twafaa!
Mtanganyika anatujali mnooo.
NIMEFURAHI UMEKUWA MKWELI NA MUWAZI HASA!
-POSSIBLY ENDAPO TUTATENGANA ZANZIBAR WAKAVURUGANA IKAWA DHAHMA KUBWA!, MANAKE KILA MTU MJUAJI.
 
Potential gani hiyo?
Itaje tuone.
Usitaje bandari,hakuna ataeshushia mzigo huko kwani hatakuwa na mahali pa kuupitisha.
Karafuu,mwani&nazi hazitawafanya wakidhi mahitaji.
Watalii hawawezi kwenda kuona bahari tu.
Vivutio vipo huku Tanganyika...kule huenda kupumzika tu.
Option yao ni moja tu....kuwa colony la mtu.
Kwani wakiwa koloni la mtu wewe unapata shida gani? Mbona kisiwa kimoja cha Ngazija cha Mayotte walikataa uhuru wakataka kuwa chini ya France mpaka leo mbona wanaishi tena vizuri kuliko sie
 
Japokuwa huu muungano ni kichefu chefu tu kwa wazanzibar lakini ukweli mchungu ni kuwa, bila huruma na upendo wa Tanganyika basi huenda Zanzibar tusiweze kutoboa hata miezi mitatu.

Kuanzia Ulinzi, Usalama mpaka umeme tunapewa bureee na watanganyika. Kodi na rasimali za watanganyika ndio zinatupa maisha wazanzibar.

Rasimali na mapato yetu ya ndani ya Zanzibar hayawezi kutosha kugharamia ulinzi, usalama, umeme na huduma zingine muhimu za kijamii kwa zaidi ya miezi mitatu, tutaangamia!
Mkuu huo ndoyo ukweli wenyewe, lakini hao "chogo bapa" hawapendi kabisa kuusikia.
 
Ni sawa na kusema Tanzania bila ya misaada ya Ulaya isinge toboa.

Hivi kuna kisiwa duniani hakiwezi jiendesha wenyewe?.
Kisiwa hakijiendeshi, ni watu huendesha maisha yao wenyewe.
Hata hivyo, kwa Afrika, fikra za kutoweza kujiendesha binafsi ndiyo changamoto.
Kuanzia viongozi hadi raia hawaamini kuweza zaidi ya kutegemea watu wa nje (msingi wa utumwa na umasikini).
Fikra na vitendo vya ukombozi (Uhuru) zipo kwa wachache na wanazidiwa na wengi wasiojielewa.
 
Kwani wakiwa koloni la mtu wewe unapata shida gani? Mbona kisiwa kimoja cha Ngazija cha Mayotte walikataa uhuru wakataka kuwa chini ya France mpaka leo mbona wanaishi tena vizuri kuliko sie
Kwani kuku, ng,ombe, mbuzi, nguruwe,.... wanapofugwa na mwishowe wakachinjwa kuna shida kwao?
 
Na Wazanzibari wakumbuke nje ya Muungano hakuna Uzanzibari;Kuna taifa la Unguja na Pemba!
 
Japokuwa huu muungano ni kichefu chefu tu kwa wazanzibar lakini ukweli mchungu ni kuwa, bila huruma na upendo wa Tanganyika basi huenda Zanzibar tusiweze kutoboa hata miezi mitatu.

Kuanzia Ulinzi, Usalama mpaka umeme tunapewa bureee na watanganyika. Kodi na rasimali za watanganyika ndio zinatupa maisha wazanzibar.

Rasimali na mapato yetu ya ndani ya Zanzibar hayawezi kutosha kugharamia ulinzi, usalama, umeme na huduma zingine muhimu za kijamii kwa zaidi ya miezi mitatu, tutaangamia!
Huijui Zanzibar. Ungetulia tu.
 
Nakwambia hivi, Tanganyika kwa sasa ndio inatusitiri sisi wazanzibar. Bila Tanganyika hatuna ulinzi, usalama wala umeme.

Karafuu iliyokuwa inatupa jeuri ilishakufa kitambo sana, na kwa uvivu wetu tumeshindwa kuifufua, na sasa tunasikia huko Tanganyika mlishaanza kuotesha na kuvuna karafuu yenu kwa fujo.....

Bandari ya Zanzibar iko mahututi maana kila jirani yetu (Beira, Mombasa, Comoro, Eritrea, Djibout, Dar, Mtwara, Tanga) alisha imarisha bandari yake, Zanzibar hatuna tena upekee wa kibandari....

Zanzibar tumebakia na Utalii pekee yake (ambao ni wa msimu, na watalii wenyewe wengi huanzia bara au kumalizia bara maana huko wako huru kuvaa chochote, kula mwaka mzima (huku kula hadharani kipindi cha Ramandan ni mwiko!), kula chochote (hata kitimoto), kunywa chochote(pombe), hapa Zanzibar watalii wanapita kwa siku zisizozidi tatu (kushangaa mchanga mweupe wa beach ambao umegundulika umejaa vilivyo kule Tanganyika (Kigamboni), kutafuna machoko wakizenji na kubwia unga kwa uhuru kisha kusepa zao). Bahati mbaya sana na huo utalii pekee hautoshi kuendesha maisha ya wazanzibar zaidi ya 1.5milioni kwa siku zaidi ya 90.

Yote kwa yote, mmasai ameshaingia Zanzibar na sasa anataka kutawala utaliii wote.

Nasema hivi, Zanzibar bila Tanganyika twafaa!
Mtanganyika anatujali mnooo.
Sasa mbona mzanzibar hawaleti Dipi wedi kuboresha bandari huko?
 
Japokuwa huu muungano ni kichefu chefu tu kwa wazanzibar lakini ukweli mchungu ni kuwa, bila huruma na upendo wa Tanganyika basi huenda Zanzibar tusiweze kutoboa hata miezi mitatu.

Kuanzia Ulinzi, Usalama mpaka umeme tunapewa bureee na watanganyika. Kodi na rasimali za watanganyika ndio zinatupa maisha wazanzibar.

Rasimali na mapato yetu ya ndani ya Zanzibar hayawezi kutosha kugharamia ulinzi, usalama, umeme na huduma zingine muhimu za kijamii kwa zaidi ya miezi mitatu, tutaangamia!
Wewe mchaga kutoka machame upo Zanzibar kuuza vinyago toka lini umekua Mzanzibari ?
 
Mwarabu anatamani leo au kesho arudi Zanzibar, na wanaamini sehemu kubwa ya Zanzibar ni mali yao... Na wanamiliki ardhi kubwa Zanzibar... Kazi kwenu, nchi inaweza pata viongozi wehu na wakaamua kuuvunja huu muungano, ndugu zetu watateseka sana tena sana...
 
Back
Top Bottom