tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,838
- 18,250
Watu mnaopigia debe vifurushi vipya vya NHIF mnapaswa kutafakari kwa umakini sana. Hivi vifurushi vipya ni vya kipuuzi na ovyo kuliko kikotoo na sheria mpya ya mafao kwa wenza wa vigogo.
Kigezo kimoja tu kinachotumiwa kuwapinga AFTHA ni kukosa ubinadam....kwamba walipaswa kutoa notice ya siku 90. Hiki ndicho kichaka ambacho serikali inajificha. Lakini vipi kuhusu NHIF kubadilisha bei ya vifurushi bila kutoa notice kwa watoa huduma au wao hawahitaji kutoa notice? Nafahamu unapoingia mkataba unaingia pia mkataba wa bei za dawa na huduma. Ukibadilisha bei maana yake umevunja mkataba hivyo mnapaswa kukaa mezani na mtoa huduma kubadilisha vipengele vya mkataba au kuingia mkataba mpya.
Nawahakikishia hivi vifurushi vipya ni kandamizi kwa mteja ndio maana waziri Ummy alivisitisha. Kwanini NHIF wanataka kuvipitisha kibabe kwa maslahi yao binafsi badala ya kuzingatia maslahi mapana ya wanachama (wagonjwa)? Huoni kuwa NHIF wanatumia mwanya huu kuwahujumu na kuwakandamiza wanachama wao?
Huu ujinga wanaofanya NHIF ni zaidi ya ule wa kikokotoo kilichopambwa na kupigiwa debe sana na serikali. Mwanzoni kulikuwa na wajinga fulani walioingia mkenge na kukikubali kikokotoo lakini sasa kila mtu analia.
Serikali hii haijawahi kufanya mabadiliko yanayomnufaisha mlalahoi. Mfano halisi ni hii sheria ya kipuuzi ya mafao kwa wake za viongozi. Wanakomba fedha zote za taifa kukipa kikundi cha wachumiatumbo wachache huku wananchi wakiendelea kutopea kwenye umasikini wa kupindukia✍️