Ukweli mchungu kwanini Congo haiwezi kupata amani milele

Ukweli mchungu kwanini Congo haiwezi kupata amani milele

Hao mabeberu ndo hupendwa na CHADEMA. Hii nchi bila CCM imara itakuwa kama DRC au Zambia. Hiyo UN ilikuwa inaweza zuia mauaji ya Lumumba na Rwanda genocide ila haikufanya kitu kwa makusudi kabisa. Cha kushangaza chama cha siasa nchini kwetu ndo kimbelembele kudhani kwamba hao mabeberu wataisaidia nchi hii na demokrasia yao ya kihuni.
Mabeberu ndio wafadhali wakubwa wa bajeti ya Serikali zote za Ccm toka tupate Uhuru.

Makampuni mengi ya mabeberu yaliyopo Tanzania yaliingia mikataba na serikali za Ccm.
 
Hii Dunia Ina sehemu zimejaa mali za thamani kubwa kuliko huko Congo DR lakini zipo katika hali ya amani. Sababu kubwa ya umwagikaji wa damu DRC ni malipizi ya karma juu ya damu za mbilikimo waliouwawa na wabantu during Bantu Great Migration. Kwenye ardhi ya DRC pamoja na utajiri wa madini, Kuna damu za mbilikimo zinazolilia kisasi cha damu. Auwae kwa upanga naye hufa kwa upanga.
Hii Dunia unyama dhidi ya jamii nyingi umefanyika hata historia ya Marekani inaonyesha namna wahindi wekundu walivyofanyiwa ukatili....Kuna siku mabeberu na wao watajutia hilo.
 
Tuanze na kesi ya Sudan
Inatakiwa Blue Nile state iwe nchi
Inatakiwa Darful iwe nchi.
Hii itapunguza vita za kuimpose Islamic culture na religion.

Kongo imara ni tishio
Kwa nchi za afrika mashariki
Inatakiwa ivunjike kwenye nchi Tano au zaidi.
Hii ni kwa maslahi mapana ya afrika mashariki
Hata uivunje mara million watu wataendelea kuuana
Na hio islam culture ni sababu mfu kwani congo nao wanapigania islamic culture?
 
Tuanze na kesi ya Sudan
Inatakiwa Blue Nile state iwe nchi
Inatakiwa Darful iwe nchi.
Hii itapunguza vita za kuimpose Islamic culture na religion.

Kongo imara ni tishio
Kwa nchi za afrika mashariki
Inatakiwa ivunjike kwenye nchi Tano au zaidi.
Hii ni kwa maslahi mapana ya afrika mashariki
Maslahi mapana ya Africa Mashariki ni yapi ?...

Tishio la Drc Imara kwa Africa Mashariki ni lipi?....mbona Drc Imara ndio faida kubwa zaidi kwa Africa Mashariki?..
 
Nakubaliana na hoja yako ila ni kweli matatizo ya kukosekana amani huko Drc (hasa maeneo ya Kivu) ni mabeberu pekee na makampuni yao ndio wakulaumiwa?..

zitto junior Tresor Mandala JokaKuu
Afrika tunapenda kutafuta scape goat ya kulaumu mabeberu tu kwa kila failure yetu.

Tatizo kubwa la Afrika ni ubinafsi (individualism) tofauti na nchi zilizoendelea kama China ambako kila uamuzi wa kiongozi unaangalia jamii nzima (Collectivism) ya leo na miaka ijayo. Hii ndio inazaa ufisadi, rushwa n.k

Kingine kukosa uvumilivu wa kisiasa (political tolerance). Hapa Afrika kila mtu anataka kujiona ni bora kuliko mwenzake. Hakuna aliye tayari kuzidiwa umaarufu na mtu, hata mpinzani akishinda anakua yale yale. Ni tatizo la kijamii zaidi kuliko shinikizo la mabeberu.

Hapo DRC wazungu tayari wana mikataba mikubwa ya kuvuna gesi, dhahabu, cobalt n.k sioni sababu ya wao kuanzisha vita ili kuvuna rasilimali.
 
Hapo DRC wazungu tayari wana mikataba mikubwa ya kuvuna gesi, dhahabu, cobalt n.k sioni sababu ya wao kuanzisha vita ili kuvuna rasilimali.
Sahihi kabisa na hili ni kwa nchi nyingi za Africa.

Lawama nyingi hutupiwa mabeberu (hasa nchi inapochafuka) rejea ya October,29 eti 'njama za mabeberu kuiba rasilimali', wakati hizo rasilimali tumewapa sisi wenyewe tena kwa bei sawa na bure tu.
 
Ukiona hivyo ujue kilichotokea Congo kilikuwa kikubwa kuliko America. Sometimes wazungu wana utu sana, angalia walivyochukuwa watu weusi Africa na ku retain vizazi vyao hadi sasa. Hata hao Red Indiana hawakuuwawa kikatili. Wengi wao walikufa kutokana na magonjwa yaliyoletwa na wazungu na hata sasa kizazi chao bado kipo.
Wali retain? Unajua 80% ya total population ya Red Indians walifanyiwa genocide?? Au hujui hata wabelgiji walihusika na vifo vya 50% ya Zaire yote kwa starvation, magonjwa na mauaji!! Hapo sijaongelea genocide ya Herero na Nama ambapo zaidi ya 60% ya waNamibia waliuwawa kwa sumu kumwagwa kwenye vyanzo vya maji.

So wazungu ni heartless tu
 
Hii Dunia Ina sehemu zimejaa mali za thamani kubwa kuliko huko Congo DR lakini zipo katika hali ya amani. Sababu kubwa ya umwagikaji wa damu DRC ni malipizi ya karma juu ya damu za mbilikimo waliouwawa na wabantu during Bantu Great Migration. Kwenye ardhi ya DRC pamoja na utajiri wa madini, Kuna damu za mbilikimo zinazolilia kisasi cha damu. Auwae kwa upanga naye hufa kwa upanga.
Kwamba karma hizo zinaipata tu congo?
Kwamba karma ni kwa waafrika tu?
Wakoloni walinyonga waliua watu mbona hiyo karma haiwapati ndo kwanza mataifa yao yanaendelea tu.
Rwanda je? Mauaji ya rwanda yenyewe hayana karma?
 
Wali retain? Unajua 80% ya total population ya Red Indians walifanyiwa genocide?? Au hujui hata wabelgiji walihusika na vifo vya 50% ya Zaire yote kwa starvation, magonjwa na mauaji!! Hapo sijaongelea genocide ya Herero na Nama ambapo zaidi ya 60% ya waNamibia waliuwawa kwa sumu kumwagwa kwenye vyanzo vya maji.

So wazungu ni heartless tu
Kama wazungu ni heartless waarabu utasemaje?
 
Simu, tablet, au laptop unayotumia kusoma ujumbe huu hivi sasa. Betri yake inayowaka hapo ndani haingeweza kufanya kazi bila madini mawili ya ajabu: Cobalt na Coltan.

Zaidi ya 70% ya madini yote ya Cobalt duniani yanatoka sehemu moja tu: Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Bila madini haya kutoka Congo, makampuni makubwa zaidi ya teknolojia na magari ya umeme duniani (kama Apple, Tesla, Samsung, na Google) yatasimama kufanya kazi ndani ya masaa 24.

Lakini jiulize swali hili la msingi: Kwa nini nchi yenye utajiri wa madini yenye thamani ya zaidi ya Dola Trillion 24 chini ya ardhi, inabaki kuwa nchi yenye umaskini wa kutisha na vita visivyomalizika kwa zaidi ya miaka 30?

Vyombo vya habari vya kimataifa vitakuambia ni "chuki za makabila" au "udhaifu wa serikali." HUU NI UONGO WA KUSANIFU.

Ukweli uliojificha nyuma ya pazia ni huu hapa: AMANI NCHINI CONGO NI ADUI WA BIASHARA YA MABILIONI YA DOLA!

1. MBINU CHAFU ZINAZOTUMIKA KUIPIGISHA CONGO MAGOTI:
Amani Inaleta Kodi na Sheria: Siku Congo ikipata amani na utulivu, serikali itaweka sheria kali za kuzuia unyonyaji, kodi za haki, na usimamizi wa kimataifa kwenye migodi. Hii ina maana makampuni ya Magharibi na Mashariki yatalazimika kulipa mara 10 ya bei wanayolipa sasa hivi kupata Cobalt.

2. Kutengeneza Waasi: Ili kupata madini kwa bei ya "kutupa," makundi ya kibiashara ya kimataifa na madalali wa silaha wanagharamia zaidi ya makundi 100 ya waasi mipakani. Vita vikilipuka, wananchi wanakimbia, na madini yanavunjwa na kutoroshwa usiku wa manane kupitia njia za panya bila kodi wala ukaguzi wowote.

Watoto wadogo na kina mama wanachimba madini hayo kwa mikono wakiwa chini ya mitutu ya bunduki, wakilipwa chini ya dola 2 kwa siku moja. Madini hayo hayo yakifikishwa Ulaya, Marekani, au Asia, yanazalisha mabilioni ya dola ya faida.

Dunia nzima sasa hivi inapigia kelele teknolojia ya "Green Energy" na magari ya umeme ili kuokoa mazingira... Lakini ukweli mchungu ni kwamba, teknolojia hiyo mpya "safi" inatengenezwa kwa kutumia damu, machozi, na maisha ya mamilioni ya wananchi wa Congo waliotengwa na dunia.

Congo haikosI amani kwa sababu haina uwezo... inakosa amani kwa sababu ulimwengu unahitaji iwe kwenye ghasia ili uendelee kupata teknolojia ya bei nafuu!

Unadhani siku viongozi wa Afrika watakapoungana na kupiga marufuku usafirishaji wa madini ghafi kwenda nje, ndio utakuwa mwanzo wa amani ya Congo? Au mabeberu watatafuta mbinu mpya ya kumpindua kila kiongozi atakayejaribu kuweka amani?
Kama alivyouawa Patrice Lumumba....!?
Sio DRC peke yake, nchi zote za Afrika, tatizo UJINGA.
 
Umeanzia mbali, sema tu wazi unawapenda kutokana na imani yako

Na kama ulivyoelezwa hapo juu, unyama waliofanya wazungu afrika, mwarabu akasome
Nasubiri ubishe , nianze kushusha evidence
154798.jpg

😁😁 wewe ni matako
 
Back
Top Bottom