Ukweli mchungu: Dhana ya kusoma uwe upate kazi na uwe na maisha mazuri inapotea na kufutika kabisa

Ghayo El Yehudi

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2024
Posts
880
Reaction score
1,822
Mzuka Wana jamvi....

Mika ya nyuma na kipindi nipo mdogo kulikuwa na wimbi kubwa la Wazazi na Jamii kwa ujumla wakihamasisha watoto wasome ili waukimbie umasikini wapate kazi na wawe na maisha mazuri , na ilikuwa unatishwa kweli kweli kuwa ukizingua tu maisha yatakushikisha adabu.

Baada ya miaka kupita sasa wote tunaongea lugha Moja watu wengi wamegundua kuwa dhana hiyo inafanya kazi kwa asilimia ndogo sana haswa ukizingatia ushahidi upo wazi Wasomi MaJobless ni wengi nchini wengine wanaacha walivyosomea na wanafanya poor paying Jobs wakati mwingine unakuta Msomi fundi simu ,Dalali , pamoja na biashara nyingine ndogondogo amabazo kimsingi hazimtoshelezi kukidhi haja zake za msingi.

Wazazi na Jamii sasa wamekosa nguvu kabisa na husikii wakiwaambia watoto kuwa wasome wapate kazi na maisha Bora na kinachosikitisha zaidi hata wasio soma kutwa wanawadharau na kiwasimanga Wasomi kuwa wamepoteza mda wo Bure kabisa ....

Je, suluhisho ni lipi kukabiliana na lundo la Wasomi mtaani wasio na ajira ?
images (38).jpeg
 
Elimu ni muhimu sana katika Dunia yetu ya Leo...lakini naona wasomi wetu wajiongeze baada ya chuo au vyovyote wawe na lugha za ziada Kama kifaransa , kichina , kituruki , kiarabu.
Nina genge langu nilifungua kigezo ilikua nipate mtu anejua lugha zote hizo aisee!!! Sikupata, niliajiri mwenye elimu ya mtaani tu though mwenyewe nahusika huku nikimfundisha huyu la nne c mwenzangu.
 
Umeongea point ya msingi sana
 
Mzuka Wana jamvi....

Mika ya nyuma na kipindi nipo mdogo kulikuwa na wimbi kubwa la Wazazi na Jamii kwa ujumla wakihamasisha watoto wasome ili waukimbie umasikini wapate kazi na wawe na maisha mazuri , na ilikuwa unatishwa kweli kweli kuwa ukizingua tu maisha yatakushikisha adabu.

Baada ya miaka kupita sasa wote tunaongea lugha Moja watu wengi wamegundua kuwa dhana hiyo inafanya kazi kwa asilimia ndogo sana haswa ukizingatia ushahidi upo wazi Wasomi MaJobless ni wengi nchini wengine wanaacha walivyosomea na wanafanya poor paying Jobs wakati mwingine unakuta Msomi fundi simu ,Dalali , pamoja na biashara nyingine ndogondogo amabazo kimsingi hazimtoshelezi kukidhi haja zake za msingi.

Wazazi na Jamii sasa wamekosa nguvu kabisa na husikii wakiwaambia watoto kuwa wasome wapate kazi na maisha Bora na kinachosikitisha zaidi hata wasio soma kutwa wanawadharau na kiwasimanga Wasomi kuwa wamepoteza mda wo Bure kabisa ....

Je, suluhisho ni lipi kukabiliana na lundo la Wasomi mtaani wasio na ajira ?View attachment 3250371

Dhima ya elimu ni mtu asome na kuelimika. Ajitambue na awe na uwezo wa kutafuta majawabu kwenye changamoto zinazomzunguka

Sisi tulisoma ili tuajiriwe na kupata kazi. Baada tulisoma ili tuibie waajiri. Lakini haya yote yanaenda yakiisha. Hayawezi kuwa sustainable.

Leo nimesikia CAG na watu wa Takukuru wakieleza yanayoendelea kwenye baadhi ya taasisi za umma. Yanatia aibu na kinyaa. Kwa matendo yao hayo,wengi wamepoteza kabisa sifa za kuendelea kupewa dhamana.

Lakini wapi bwana...wanatuchezea cheusi chekundu wakifikiria watafanya hivyo milele
 
Na hata ukifanikiwa kupata kazi bado sio kigezo cha kufanikiwa kuteseka kupo pale pale otherwise uwe taasisi zenye maslahi
 
Back
Top Bottom