Ukweli kwa walimu

Ukweli kwa walimu

Mtoa mada naomba nikusahihishe hapa kidogo! Unahabari kuwa kuna wahitimu wa 2015 wa kada mbali mbali ikiwemo na ualimu wameshaingia tayari kwenye payroll ya serikali na wanaendelea kufurahia kuhitimu kwao?
Mimi walimu kwangu wa hapa Tanzania kwangu ni takataka tu wengi walifeli sekondari kama sio kufeli walipata grade za mwisho sekondari hasa wa serikali, Siwezi peleka familia yangu kwa walimu wa serikalini hawaelewi wanafundisha kitu gani, vilaza sana. Siku nikiona vijana wa First division wanaenda ualimu wajukuu zangu nikiwa hai watasoma, lugha ya kufundishia walimu hawaelewi hata kuongea
 
Mawazo Haya ya kuchafuana Ndio yanafanya tucheleweshewe MALIPO yetu shame upon you!!! Mleta uzi
 
Unaelewa maana ya Future wewe, Future is uncertain, Maisha yanaanza leo Story za kesho tupa kule, wewe kwa akili zako unategemea ukiwa mwalimu kazini ndio utajua kufundisha, Kama ulishindwa chemistry leo unategemea utaweza Kesho ukiwa mzee, Haya mambo ya kesho wanasiasa wamewadanganya Sana, eti subiri taifa la kesho wakati wao wanakula Leo
 
Ni muhimu kupitia mifumo ya kupata hawa walimu wanazidi kutuharibia Taifa, Mwalimu anashindwa kutofautisha r na L, hao watoto mnaofundisha mnajenga taifa la vituko
jifunze matumizi ya vituo, kituo kikubwa na kidogo.
 
"jifunze "au "Jifunze "unaanza sentensi na herufi ndogo nwanzoni endelea kufikiri kwa kutumia vichwa vya wengine cha kwako umebeba kama mzigo juu ya mabega
kazi ya herufu kubwa na ndogo ni kazi ya kifaa unachotumia kundikia ujumbe wako, ila kuweka vituo ni kazi yako.
 
Ni nani aliyepata À mathematics au À chemistry ni mwalimu, walimu wengi ni watu waliofeli darasani, Mtu akishindwa Maisha anakimbilia kusoma ualimu apate ajira mapema
Haaa haaa unajiuliza swali na kujijibu mwenyewe, wewe jamaaa ni kilaza sana yaani.
Jina lako kamili unaitwa nani tujue ulipata div ipi?
 
Hizo dimension yakupasa uzionyeshe kwenye interview za masomo mtakayopewa, Naunga mkono hoja ya serikali ya kuwachuja kwa interview iwe ya mitihani ya secondary, Ukishindwa sasa ukatafakari hizo strategies Nyumbani kwako
 
Kwa hyo wewe kama ulifundishwa na mwalim kilaza basi utakuwa kilaza tooo infact walim inatakiwa wawe ndo waliofaulu vizur lkn sisi tz no vise versa hahah kichwa cha mwendawazimu alooooh
 
Mnaandika wenyewe kuwa wenye ufaulu nzuri hawaendi ualimu, walimu ni wale walioferi. Sasa unategemea mtu alieferi awe kipanga mbeleni? Nyie wenye div 1 kuweni mainjinia na vilaza wache wawe walimu. Acheni kulalamika
 
Watu wengi ambao hawakusoma ualimu ndio wanaojua vizuri masomo ya hisabati, kemia na biolojia, Tatizo mfumo uliopo ndio uliwafanya wasome kozi zingine, Ukichukua watu waliosoma Engineering au Commerce wapo vizuri kwenye hesabu kuliko walimu waliosomea darasani.

Hivyo hawa walimu tulionao wa Science wengi ni vilaza sana, Fuatilia masomo ya kidato cha tano wengi hufundishwa na watu ambao hawana mpango wa ualimu na wapo vizuri, Naunga mkono serikali ikague vyeti vyao walipata nini huko sekondari, utawezaje fundisha hesabu kidato cha sita wakati ulipata herufi za mwisho darasani.
Nadhani unamaanisha ulifundishwa na vilaza kwa vile ulifundishwa na vilaza na we we ni kilaza
 
Facilitator wakati huelewi unafacilitate nini, Wewe ulipata E mathematics A level umekaa chuo miaka 3 unarudi A level kuzidi kufacilitate E au, Ndio maana tunasema serikali iwa kague upya na wale walimu wa dot Com wafanyishwe interview ili tuanze upya, Ni muhimu nyie walimu mufanyishwe mitihani ya secondary kabla ya kuajiriwa tupime uwezo wenu
Engineer awe Engineer
Mwalimu awe Mwalimu
By the way unafikiri nani wana uwezo mkubwa wa Hisabati na Sayansi hapa TZ?
 
Wakati mwingine kunahoja nyingine ukiziangalia na kuzisoma na zinaweza kukuhadaa kuwa za kweli vile na mtu akajitutumua kuuaminisha umma jambo kana kwamba anauhakika nalo kiutafiti kwa asilimia mia.

Haiwezekani mtu akaja na vihoja vyake hapa bila utafiti na kuuaminisha umma huo ndiyo ukweli.

1.Mtoa hoja anaweza kutueleza ni utafiti gani alifanya kujua watu wa mitaani ndiyo ni wanafundisha vizuri kuliko darasani?

2.Ni wanafunzi wangapi walifundishwa mtaani na wakafanya vizuri kuliko wale waliofundishwa na walimu darasani?

3.Ufaulu wao ulikuwaje?

4.Alipataje sampuli yake kufikia hitimisho hilo?

5.Ni walimu wangapi aliopitia vyeti vyao nakujirisha kuwa hakuna walimu wenye A za masomo tajwa?

6.Alitumia vigezo gani kujua kama walimu ni matokeo ya kushindwa maisha?

7.Anathibitishaje kuwa mwalimu kuto deliver vya kutosha darasani kunatokana na mwalimu kuwa anaufaulu hafifu?

8.Inawezekanaje kuwe na watu wengi mtaani wenye A+ za sayansi pasipo kupita kwa walimu?Hao wanazalishwa na nani?

9.Nafasi za visababishi vingine kama,utayari,ukosefu wa maabara,madawa, maslahi duni ,nk aliweka wapi?

10.Katika kila shule ni wanafunzi wangapi hupita mikononi mwa non-professional teachers na wangapi hupita kwa professional teachers na mpishano ni asilimia ngapi?na mwaka gani?

11.Ni mtaalamu gani au chombo gani kilithibitisha ubora wa hao wanaojiita walimu wa mitaani?

12.Kwaasilimia ngapi ya hao wanaojiita walimu wa mitaani ipo kwa kila somo?

Haya ni maswali machache tu naweza mwuliza mtoa hoja,yapo zaidi ya hayo,nikijibiwa vema naweza kukubali hoja za mtoa mada,zaidi ya hapo alikuwa afurahisha umma.

Mwalimu Nyerere naye! Jee vipi mwalimu maghufuri wote walikuwa viraza. Ngoja niwambie kitu ufaulu wa masomo sio kigezo tosha cha kumfanya mtu awe mwalimu bora! Mwalimu anaweza akapata hata hizo dvns za mwisho kama msemavyo lakini akaandaliwa vya kutosha na akawa mwalimu bora kuliko hata hao waliofanya vizuri katika masomo yao. Kitu kingine Tanzania ni nchi inayotumia mtaala mmoja kitu ambacho kwa shule za vijijini ni changamoto kwa sababu utamkuta mtoto kule kijijini anao uwezo mkubwa kuliko wa mjini anajituma kadiri ya uwezo wake mwisho wa siku anapata dvn III kutokana na changamoto za kijijini lakini yule wa mjini anapata dvns II ukiwachukua hawa wote wawili na ukawaweka ktk darasa moja na kuwandisha utabaini utofauti wao ambaye yule wa shule za kayumba tena za vijijini yuko vzr kuliko wa mjini. So I would like to conclude that, having division 1 or 2 doesn't mean of being a good teacher. Good teacher iz created no matter what divions she/he has......ni hayo tu. Think big....!!!
 
Watu wengi ambao hawakusoma ualimu ndio wanaojua vizuri masomo ya hisabati, kemia na biolojia, Tatizo mfumo uliopo ndio uliwafanya wasome kozi zingine, Ukichukua watu waliosoma Engineering au Commerce wapo vizuri kwenye hesabu kuliko walimu waliosomea darasani.

Hivyo hawa walimu tulionao wa Science wengi ni vilaza sana, Fuatilia masomo ya kidato cha tano wengi hufundishwa na watu ambao hawana mpango wa ualimu na wapo vizuri, Naunga mkono serikali ikague vyeti vyao walipata nini huko sekondari, utawezaje fundisha hesabu kidato cha sita wakati ulipata herufi za mwisho darasani.
Hizi ni hasira za kufeli tu! Resit kijana....
 
Mimi walimu kwangu wa hapa Tanzania kwangu ni takataka tu wengi walifeli sekondari kama sio kufeli walipata grade za mwisho sekondari hasa wa serikali, Siwezi peleka familia yangu kwa walimu wa serikalini hawaelewi wanafundisha kitu gani, vilaza sana. Siku nikiona vijana wa First division wanaenda ualimu wajukuu zangu nikiwa hai watasoma, lugha ya kufundishia walimu hawaelewi hata kuongea
iko siku baba yako kama hakukununulia shati la sikukuu kwajili ya kiburi chako utasema ni kama takataka tu,kwa walimu ni hivyo pia kama ulikuwa unajivutia bangi ukiwa shule na misele sana badala ya kusoma lazima upate zero na uwaone walimu wako ndiyo chanzo,karudie mtihani dogo,kamasi zinakutoka bure hapa
 
Mimi walimu kwangu wa hapa Tanzania kwangu ni takataka tu wengi walifeli sekondari kama sio kufeli walipata grade za mwisho sekondari hasa wa serikali, Siwezi peleka familia yangu kwa walimu wa serikalini hawaelewi wanafundisha kitu gani, vilaza sana. Siku nikiona vijana wa First division wanaenda ualimu wajukuu zangu nikiwa hai watasoma, lugha ya kufundishia walimu hawaelewi hata kuongea
Kwa majibu haya unaonekana dhahiri kabisa mishe zako zimekwama hivyo uko frustrated na ulipokuwa unapaona unaweza kutokea napo umepakuta pana pini hivyo ukaamua kupunguzia hasira kwa kuponda career ya ualimu. Jipe moyo utayashinda hata hawa walimu unaowaponda sio wao waliokusababishia matatizo yako ila matatizo yako yanatokana na ushauri mbovu ulioupata kutoka kwa mshauri wako hivyo ulichokuwa unakitegemea hakijaja kivile ulivyodhhania itakuwa! Lakini bado unayo nafasi ya kurekebisha ulipokosea! Karibu jamvini!
 
Mimi walimu kwangu wa hapa Tanzania kwangu ni takataka tu wengi walifeli sekondari kama sio kufeli walipata grade za mwisho sekondari hasa wa serikali, Siwezi peleka familia yangu kwa walimu wa serikalini hawaelewi wanafundisha kitu gani, vilaza sana. Siku nikiona vijana wa First division wanaenda ualimu wajukuu zangu nikiwa hai watasoma, lugha ya kufundishia walimu hawaelewi hata kuongea
Kitendo cha kuongea bila utafiti ni kufeli pia
 
Watu wengi ambao hawakusoma ualimu ndio wanaojua vizuri masomo ya hisabati, kemia na biolojia, Tatizo mfumo uliopo ndio uliwafanya wasome kozi zingine, Ukichukua watu waliosoma Engineering au Commerce wapo vizuri kwenye hesabu kuliko walimu waliosomea darasani.

Hivyo hawa walimu tulionao wa Science wengi ni vilaza sana, Fuatilia masomo ya kidato cha tano wengi hufundishwa na watu ambao hawana mpango wa ualimu na wapo vizuri, Naunga mkono serikali ikague vyeti vyao walipata nini huko sekondari, utawezaje fundisha hesabu kidato cha sita wakati ulipata herufi za mwisho darasani.
Huu hauwezi kuwa ukweli kwababu hauna ushahidi wa kisayansi ambao ulifanyiwa utafiti,hivyo sema huu ni mtazamo wangu kuhusu ualimu na siyo huu ni ukweli kuhus ualimu
 
Back
Top Bottom