Watawala hawana mpango na Elimu bora wananchi amkeni

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
1,137
Reaction score
2,702
Viongozi wetu wamekuwa mara kwa mara wanafanya majaribio ya kitaaluma na wakati wote majaribio hayo yameacha simanzi kwa baadhi ya wanafunzi ambao ndio wahanga wakati wote

Humu katikati kuliibuka waziri aliyeunganisha somo la Physics na Chemistry likawa somo moja (Chemistry with Physics),

Akaja mwingine akafuta somo la Book-keeping, commerce, agriculture na michezo mashuleni

Lakini cha ajabu chuo kikuu cha Kilimo - SUA, vyuo vya uhasibu na kozi za biashara vyuoni hakuzifuta sijui alitegemea wataalamu hao watoke wapi

Akaja mwingine na kampeni za BIG RESULTS NOW

Mwingine akaibuka na kutanga kuifuta division ZERO akaweka viwango anavyovijua yeye na matokeo yakawa yanasomeka kwa lugha nyingine nakumbuka neno moja tu "Distinction"

Sasa tunaye Proff. Mkenda amekuja na mtaala mpya (ulioboreshwa) ambao unawaruhusu wanafunzi kujichagulia masomo /combination mara tu wanapoingia kidato cha kwanza tofauti na miaka ya nyuma ambapo walisoma masomo yote hadi kidato cha tatu kabla ya kuchagua michepuo waipendayo

Mtaala huu unawagawa wanafunzi mara tu wanapoingia kidato cha kwanza, wale wanaosoma sayansi si lazima kwao kusoma masomo ya sanaa kama History, na wale wanaosoma masomo ya sanaa sio lazima kwao kusoma masomo ya sayansi kama Biology, Physics wala Chemistry toka kidato cha kwanza huku somo la Commerce likigeuzwa kuwa Bussiness studies na limekuwa la lazima kwa kila mwanafunzi likienda sambamba na Historia ya Tanzania na Maadili linalofundishwa kwa Kiswahili ambalo limekuja kufuta somo la Civics

Maelekezo ya wizara ni kwamba walimu wawashauri wanafunzi wakashauriane na wazazi wao michepuo waipendayo

Ni jambo jema sana lakini lenye angalizo kubwa sana.

Hapa nadhani wamefanya tafiti kwa kuzingatia watoto wanaoishi mazingira wezeshi ya tafakuri hiyo

Kuna watoto wanaishi na wazazi ambao hawajawahi kukanyaga darasani. Hawa wanapata shida sana na walimu wao. Hata hajui ndoto zake ni zipi anaenda kwa kufuata mkumbo. Hata hivyo naamini ikishazoeleka changamoto hii itaondoka yenyewe lakini wakuathirika watakuwa wamekwisha athirika na watanufaika watakaofuata

Katika hili la mtaala mpya limekuja na kitu kinaitwa "AMALI"

Hapa ndo pamenifanya nikumbuke namna elimu yetu inavyochezewa kwa majaribio yanayoacha simanzi kwa wanafunzi

Kwenye maandishi huu mtaala unaotaja amali unavutia sana. Yaani hadi unaona raha na unaweza kushawishika kumpongeza aliyebuni hiki kitu cha mtaala wa amali

Kwamba watoto watajifunza na kupata ujuzi utakaowafanya wamudu stadi za maisha na kujiwezesha baada ya kidato cha nne. Inavutia, inapendeza

Kwa tahadhari serikali imeanzisha mchepuo huu wa amali kwa baadhi ya shule za sekondari (sio zote). Wameteua shule chache kwa kila mkoa/halmashauri na kuzianzishia huu mchepuo wa amali

Hata hivyo tahadhari hiyo bado imekuwa ya kimagumashi kama kawaida yao

Shule nyingi zilizopewa huo mchepuo wa amali hazina miundombinu rafiki ya kuhudumia mchepuo husika

Shule inapelekewa mtaala wa amali kwa fani ambayo haina mwalimu wa fani husika. Kwa mfano, kuna shule zimepelekewa fani za ushonaji bila kuwa na miundombinu wala walimu wa ushonaji, kuna shule zimepelekewa fani ya kilimo bila kuwa na miundombinu ya kilimo na kadhalika

Wanafunzi wamekaa mwaka mzima (mtaala umeanza mwaka jana 2025) bila kufanya kitu cha maana.

Hapa unajiuliza, kati ya kuanzisha mtaala husika mashuleni na kuandaa miundombinu na walimu kipi kilitakiwa kuanza?

Kwamba hili nalo halikufahamika? Kwamba wasomi wetu hawakulijua? Unaweza kuhamia kwenye nyumba ambayo haujajenga?

Kusema kwamba wasomi wetu na viongozi wetu hawakulijua si sawa. Ila ni kwasababu wanazozijua wao wenyewe ndiomaana wameanzisha mtaala bila kuandaa wataalamu wala miundombinu

Na kingine cha msingi kabisa hapa wahanga si watoto wao. Naamini hivyo

Swala fikirishi katika mtaala huu wa amali ni hili la vyuo vyetu vya VETA

Ukiangalia kwa undani hili swala la kuanzisha mafunzo ya amali linafanana kwa asilimia 100% na mafunzo yanayotolewa na vyuo vya VETA. Kwa lugha rahisi hakuna kitu kipya kilichoanzishwa

Kwa mtazamo huo, unaweza kujiuliza kwanini serikali isingeboresha hivi vyuo vya VETA vikawa na uwezo wa kuwapokea na kuwahudumia wanafunzi wote wanaopenda na waliochagua kusoma mchepuo wa amali?

Huku sekondari walipowapeleka hakuna karakana, hakuna walimu wa amali wala mazingira yanayoonekana ya kutoa ujuzi

Hawa watoto wanaosoma mchepuo wa amali wanaruhusiwa kusoma masomo machache tu ya sekondari ambayo wangeweza kuyasoma huko huko VETA.

Kwanini serikali yetu inapenda kujipa mzigo isioweza kuubeba? Kwanini wataalamu wetu hawalioni hili?

Tuseme somo la amali litashamiri na kuvutia wanafunzi wengi na wakati huo huo kuna taasisi ya VETA inatoa mafunzo hayo hayo tena kwa ufanisi mkubwa. Kwanini wasiiongezee nguvu taasisi hiyo hawa vijana wakaenda kupata ujuzi huko na maboresho yakafanywa kwa kuwapa certificate zinazolingana na ujuzi wao na nyongeza ya NECTA kama hofu ni hicho cheti cha form four?

Swala lingine lililonifanya niseme viongozi wanachezea elimu yetu ni hili la kubadilika badilika kwa viwango vya ufaulu na alama za ufaulu

Miaka ya nyuma kidogo daraja "A" lilisoma mwanafunzi akipata alama 85+ lakini siku hizi ni alama 75+ kwa sekondari

Wastani wa serikali hasa kuvuka kidato cha Pili kwenda cha tatu ulikuwa wastani wa 30 kwa masomo saba ya msingi, lakini siku hizi ni ufaulu wa masomo mawili tu kwa alama 30 (yaani upate 30 masomo mawili au 45 kwa somo moja). Hii maana yake ni Division four na hata mwanafunzi wa kidato cha nne naye anapimwa hivyo hivyo

Hapa ni maandishi yanayosomeka kwenye makaratasi / miongozo yao lakini ukiongea na walimu wanaofundisha na yale wanayoyashuhudia kwenye usahihishaji wa kitaifa na matokeo yanapotangazwa vinakuwa vitu viwili tofauti

Wenyewe (Walimu) wanasema kunakuwa na maelekezo mengi ya kuhakikisha wanasahihisha kwa umakini lakini kwa kuangalia "mwelekeo" wa alichoandika mwanafunzi kama kinaelekeana na jibu sahihi basi apewe alama hata kama hakufikia kwenye jibu lenyewe.

Hata hivyo, pamoja na kufuata maelekezo hayo bado matokeo yanapotangazwa wanabaki kuduwaa kwa kuona ufaulu mkubwa tofauti na uhalisia waliouona wanaposahihisha.

Hili limebaki kuwa siri ya NECTA. Wanachokifanya wanakijua wao wenyewe kwasababu wanaoingiza alama za wanafunzi ni walimu lakini hata wao hubaki na butwaa matokeo yanapotangazwa

Hali hii imepelekea vyuo vya kati na vyuo vikuu kupokea wanafunzi wenye uwezo mdogo wa kumudu masomo kwa ngazi husika

Hali hii inazalisha watumishi wasio na uwezo katika fani zao na matokeo yake ni Taifa kushindwa kusonga mbele
 
Screenshot_20260415-144632~2.png
 
Lengo la fisiemu ni kuzalisha wajingawajinga kama Mwashamba. Can you imagine, leo karne ya 21 zama za nano-technology and IA mtoto wa Kitanzania anafundishwa kufinyanga vyungu darasani vitu vya zama za mawe za kati. Hivi vitamsaidia nini hali huko majumbani kila mtu anatumia sahana za udongo na mfupa toka China.
 
Mbaya sana kuingiza siasa zao kwenye elimu
Nimejaribu kupitia somo la physics (kama wanvyoita wao mtaala mpya) aisee ni mauaji kwa watoto wa kidato cha kwanza na cha pili, ile physics niliyoisoma advance ndio imewekwa mtoto wa form 2 aisome.
 
Kuna sehemu ngozi nyeusi tulimkosea Mungu
Sio kwa uduni huu
 
Mkuu umeandika yalioko kwenye fikra zangu. 100% nakuunga mkono.
Mfano kwenye mtaala mpya waliacha walimu wa uchimi wakaajiri watu wa accountancy ambao hawajui chochote kuhusu teaching methodology eti wakafundishe business study.
Binafasi nachukia sana kiongozi anapoingiza mambo ya msingi kuwa mtaji wa kiasa.
mfano.Hili la matokeo kuwa siri ya NECTA. Wanachokifanya wanakijua wao wenyewe kwasababu wanaoingiza alama za wanafunzi ni walimu lakini hata wao hubaki na butwaa matokeo yanapotangazwa
 
Wizara ya elimu inabidi iongozwe na wataalamu wa elimu, tunao wengi sana vyuoni, hii ni wizara iliyobeba hatma ya kizazi chetu. Kuanzia Waziri, Naibu Waziri, KM, NKM na wasaidizi wao wote ni lazima wawe wabobevu wa elimu.
 
Viongozi wetu wamekuwa mara kwa mara wanafanya majaribio ya kitaaluma na wakati wote majaribio hayo yameacha simanzi kwa baadhi ya wanafunzi ambao ndio wahanga wakati wote

Humu katikati kuliibuka waziri aliyeunganisha somo la Physics na Chemistry likawa somo moja (Chemistry with Physics),

Akaja mwingine akafuta somo la Book-keeping, commerce, agriculture na michezo mashuleni

Lakini cha ajabu chuo kikuu cha Kilimo - SUA, vyuo vya uhasibu na kozi za biashara vyuoni hakuzifuta sijui alitegemea wataalamu hao watoke wapi

Akaja mwingine na kampeni za BIG RESULTS NOW

Mwingine akaibuka na kutanga kuifuta division ZERO akaweka viwango anavyovijua yeye na matokeo yakawa yanasomeka kwa lugha nyingine nakumbuka neno moja tu "Distinction"

Sasa tunaye Proff. Mkenda amekuja na mtaala mpya (ulioboreshwa) ambao unawaruhusu wanafunzi kujichagulia masomo /combination mara tu wanapoingia kidato cha kwanza tofauti na miaka ya nyuma ambapo walisoma masomo yote hadi kidato cha tatu kabla ya kuchagua michepuo waipendayo

Mtaala huu unawagawa wanafunzi mara tu wanapoingia kidato cha kwanza, wale wanaosoma sayansi si lazima kwao kusoma masomo ya sanaa kama History, na wale wanaosoma masomo ya sanaa sio lazima kwao kusoma masomo ya sayansi kama Biology, Physics wala Chemistry toka kidato cha kwanza huku somo la Commerce likigeuzwa kuwa Bussiness studies na limekuwa la lazima kwa kila mwanafunzi likienda sambamba na Historia ya Tanzania na Maadili linalofundishwa kwa Kiswahili ambalo limekuja kufuta somo la Civics

Maelekezo ya wizara ni kwamba walimu wawashauri wanafunzi wakashauriane na wazazi wao michepuo waipendayo

Ni jambo jema sana lakini lenye angalizo kubwa sana.

Hapa nadhani wamefanya tafiti kwa kuzingatia watoto wanaoishi mazingira wezeshi ya tafakuri hiyo

Kuna watoto wanaishi na wazazi ambao hawajawahi kukanyaga darasani. Hawa wanapata shida sana na walimu wao. Hata hajui ndoto zake ni zipi anaenda kwa kufuata mkumbo. Hata hivyo naamini ikishazoeleka changamoto hii itaondoka yenyewe lakini wakuathirika watakuwa wamekwisha athirika na watanufaika watakaofuata

Katika hili la mtaala mpya limekuja na kitu kinaitwa "AMALI"

Hapa ndo pamenifanya nikumbuke namna elimu yetu inavyochezewa kwa majaribio yanayoacha simanzi kwa wanafunzi

Kwenye maandishi huu mtaala unaotaja amali unavutia sana. Yaani hadi unaona raha na unaweza kushawishika kumpongeza aliyebuni hiki kitu cha mtaala wa amali

Kwamba watoto watajifunza na kupata ujuzi utakaowafanya wamudu stadi za maisha na kujiwezesha baada ya kidato cha nne. Inavutia, inapendeza

Kwa tahadhari serikali imeanzisha mchepuo huu wa amali kwa baadhi ya shule za sekondari (sio zote). Wameteua shule chache kwa kila mkoa/halmashauri na kuzianzishia huu mchepuo wa amali

Hata hivyo tahadhari hiyo bado imekuwa ya kimagumashi kama kawaida yao

Shule nyingi zilizopewa huo mchepuo wa amali hazina miundombinu rafiki ya kuhudumia mchepuo husika

Shule inapelekewa mtaala wa amali kwa fani ambayo haina mwalimu wa fani husika. Kwa mfano, kuna shule zimepelekewa fani za ushonaji bila kuwa na miundombinu wala walimu wa ushonaji, kuna shule zimepelekewa fani ya kilimo bila kuwa na miundombinu ya kilimo na kadhalika

Wanafunzi wamekaa mwaka mzima (mtaala umeanza mwaka jana 2025) bila kufanya kitu cha maana.

Hapa unajiuliza, kati ya kuanzisha mtaala husika mashuleni na kuandaa miundombinu na walimu kipi kilitakiwa kuanza?

Kwamba hili nalo halikufahamika? Kwamba wasomi wetu hawakulijua? Unaweza kuhamia kwenye nyumba ambayo haujajenga?

Kusema kwamba wasomi wetu na viongozi wetu hawakulijua si sawa. Ila ni kwasababu wanazozijua wao wenyewe ndiomaana wameanzisha mtaala bila kuandaa wataalamu wala miundombinu

Na kingine cha msingi kabisa hapa wahanga si watoto wao. Naamini hivyo

Swala fikirishi katika mtaala huu wa amali ni hili la vyuo vyetu vya VETA

Ukiangalia kwa undani hili swala la kuanzisha mafunzo ya amali linafanana kwa asilimia 100% na mafunzo yanayotolewa na vyuo vya VETA. Kwa lugha rahisi hakuna kitu kipya kilichoanzishwa

Kwa mtazamo huo, unaweza kujiuliza kwanini serikali isingeboresha hivi vyuo vya VETA vikawa na uwezo wa kuwapokea na kuwahudumia wanafunzi wote wanaopenda na waliochagua kusoma mchepuo wa amali?

Huku sekondari walipowapeleka hakuna karakana, hakuna walimu wa amali wala mazingira yanayoonekana ya kutoa ujuzi

Hawa watoto wanaosoma mchepuo wa amali wanaruhusiwa kusoma masomo machache tu ya sekondari ambayo wangeweza kuyasoma huko huko VETA.

Kwanini serikali yetu inapenda kujipa mzigo isioweza kuubeba? Kwanini wataalamu wetu hawalioni hili?

Tuseme somo la amali litashamiri na kuvutia wanafunzi wengi na wakati huo huo kuna taasisi ya VETA inatoa mafunzo hayo hayo tena kwa ufanisi mkubwa. Kwanini wasiiongezee nguvu taasisi hiyo hawa vijana wakaenda kupata ujuzi huko na maboresho yakafanywa kwa kuwapa certificate zinazolingana na ujuzi wao na nyongeza ya NECTA kama hofu ni hicho cheti cha form four?

Swala lingine lililonifanya niseme viongozi wanachezea elimu yetu ni hili la kubadilika badilika kwa viwango vya ufaulu na alama za ufaulu

Miaka ya nyuma kidogo daraja "A" lilisoma mwanafunzi akipata alama 85+ lakini siku hizi ni alama 75+ kwa sekondari

Wastani wa serikali hasa kuvuka kidato cha Pili kwenda cha tatu ulikuwa wastani wa 30 kwa masomo saba ya msingi, lakini siku hizi ni ufaulu wa masomo mawili tu kwa alama 30 (yaani upate 30 masomo mawili au 45 kwa somo moja). Hii maana yake ni Division four na hata mwanafunzi wa kidato cha nne naye anapimwa hivyo hivyo

Hapa ni maandishi yanayosomeka kwenye makaratasi / miongozo yao lakini ukiongea na walimu wanaofundisha na yale wanayoyashuhudia kwenye usahihishaji wa kitaifa na matokeo yanapotangazwa vinakuwa vitu viwili tofauti

Wenyewe (Walimu) wanasema kunakuwa na maelekezo mengi ya kuhakikisha wanasahihisha kwa umakini lakini kwa kuangalia "mwelekeo" wa alichoandika mwanafunzi kama kinaelekeana na jibu sahihi basi apewe alama hata kama hakufikia kwenye jibu lenyewe.

Hata hivyo, pamoja na kufuata maelekezo hayo bado matokeo yanapotangazwa wanabaki kuduwaa kwa kuona ufaulu mkubwa tofauti na uhalisia waliouona wanaposahihisha.

Hili limebaki kuwa siri ya NECTA. Wanachokifanya wanakijua wao wenyewe kwasababu wanaoingiza alama za wanafunzi ni walimu lakini hata wao hubaki na butwaa matokeo yanapotangazwa

Hali hii imepelekea vyuo vya kati na vyuo vikuu kupokea wanafunzi wenye uwezo mdogo wa kumudu masomo kwa ngazi husika

Hali hii inazalisha watumishi wasio na uwezo katika fani zao na matokeo yake ni Taifa kushindwa kusonga mbele
Pitia huu Uzi uone uhalisia wa kuchezewa kwa elimu yetu.
 
Lengo la fisiemu ni kuzalisha wajingawajinga kama Mwashamba. Can you imagine, leo karne ya 21 zama za nano-technology and IA mtoto wa Kitanzania anafundishwa kufinyanga vyungu darasani vitu vya zama za mawe za kati. Hivi vitamsaidia nini hali huko majumbani kila mtu anatumia sahana za udongo na mfupa toka China.
Nacheka kama mazuri
 
Mtu anachaguaje mchepuo ilhali bado hajaexperience juu ya hicho anachokichagua?

Sanasana hapa wengi wataangukia kutokana na hearsays tu kwamba mchepuo fulani huwa ni mgumu au rahisi..

Kama sivyo, basi atachaguliwa na watu ambao yeye anawaamini kwenye kile wanachomwambia.

Changamoto kiukweli
 
Hoja Yako ya VETA ni Nzuri sana, ✅.

VETA ilitakiwa iwe naunafu pingine iwe na mikopo kwa vile helsb.
 
Kwakweli majaribio kwenye maisha y a watu hayafai. Kuna mtoto mmoja aliacha masomo ya sayansi mwanzoni tu akiwa form one ila ilipofika mwezi wa kumi akataka kusoma hayo masomo. Ikabidi tumshauri tu aendekee na arts. So Kwa mwaka huu kama shule tumewambia form one wote wasome masomo yote,watachagua wakifika f2
Kuhusu swala LA NECTA tuliombee taifa letu kwakweli!
 
Baadhi ya shule kwa kuzingatia kuwa wanafunzi wengi wanakuwa hawana uelewa mzuri wa hizi combinataion, wameamua kuwagawa katika mikondo hiyo (sayansi, arts, nk) kwa kuzingatia ufaulu wao wa darasa la saba kitu ambacho sio maelekezo ha wizara wala matakwa ya wanafunzi

Katika hili, nani wa kufuatilia? Mwanafunzi wa form one ataweza kubishana na Mwalimu kama ametoka familia ambayo nayo haina uelewa?

Hapa wametengeneza tatizo lingine badala ya kutatua tatizo
 
Wameweka business studies lazima shule zote na walimu hawapo kinachotokea lina fundishwa na yeyote
 
Wakati huo huo kuna wahitimu wengi tu mtaani wa ualimu waliosomea Economics, Commerce wako mtaani hawajaajiliwa

Halafu kwasasa wamekuja na mpango wa kupelekea "walimu wa kujitolea" ambao hawakusomea ualimu (baadhi wamesoma Bussiness administration) wakafundishe kwa mwaka mmoja mashuleni

Hapa unajiuliza, kipi kilitakiwa kuanza kati ya kusomesha walimu kwanza kisha somo lianzishwe au somo linaanza halafu ndo walimu wanatafutwa?
 
Mbaya sana kuingiza siasa zao kwenye elimu
Nimejaribu kupitia somo la physics (kama wanvyoita wao mtaala mpya) aisee ni mauaji kwa watoto wa kidato cha kwanza na cha pili, ile physics niliyoisoma advance ndio imewekwa mtoto wa form 2 aisome.
Na hapo ukiuliza wanakwambia mbona mtot anaweza kukariri lugha za catoon...imgn mtu analinganisha cartoon na formula za calculus
 
Back
Top Bottom