Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

Mnatuaminisha vipi kama ni kweli hizi mbiu mnazojipigia wakati mnashindwa kusafirisha mwili wa marehemu kwa dola 6000 tu? Tena wa hapo hapo US unapopasemea....

Hivi wewe unajua kusoma na kuelewa kweli?

Wapi ilisemwa kwamba hizo dola 6000 zilikuwa ni za kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Madison kuja Tanzania?

Watu hamsomagi vitu mkavielewa. Matokeo yake mnafikia mahitimisho ya kipumbavu kabisa.

Na kuchanga si lazima. Ni hiari, btw.
 
Kuwa na uraia wa nchi nyingine na kuishi Tanzania kama watanzania wengine wala sio tatizo.
Ingekua ughaibuni ingekua ngumu
ila kwa bongo nafanya kila kitu bila kipingamizi.
Ni kweli kwenye makaratasi mimi sio mtanzania.

Nimekuwa nikishangaa imekuwaje leo hitaji la uraia pacha kuwa suala kubwa hadi kujadiliwa kwenye katiba ilhali bado hatuna mfumo wa kudhihirisha na kudhibiti uraia wa Kitanzania. Sijawahi kusikia Mtanzania awe ndani ya nchi au atokee nje akitakiwa kuthibitisha uraia wake au akinyimwa pasi ya kusafiria au hata akikwazwa kwenye shughuli yoyote nchini kwa sababu hiyo. Nimetokea tu watu wakitangazwa sio raia mara wakitofautiana na wakuu nchini. Ndio maana bado naamini kuwa hiyo hoja inalenga zaidi kuwapa uraia "wawekezaji" wanaotimiza vigezo vya kifisadi. Watu badala ya kuimarisha kwanza mfumo wa udhibiti wa uraia wanakimbilia kwenye kutaka kuidhinisha uraia pacha ili (kwa mtazamo wangu) wacheze dili na mafisadi wa kimataifa.
 
Kuwa na uraia wa nchi nyingine na kuishi Tanzania kama watanzania wengine wala sio tatizo.
Ingekua ughaibuni ingekua ngumu
ila kwa bongo nafanya kila kitu bila kipingamizi.
Ni kweli kwenye makaratasi mimi sio mtanzania.

Nimekuwa nikishangaa imekuwaje leo hitaji la uraia pacha kuwa suala kubwa hadi kujadiliwa kwenye katiba ilhali bado hatuna mfumo wa kudhihirisha na kudhibiti uraia wa Kitanzania. Sijawahi kusikia Mtanzania awe ndani ya nchi au atokee nje akitakiwa kuthibitisha uraia wake au akinyimwa pasi ya kusafiria au hata akikwazwa kwenye shughuli yoyote nchini kwa sababu hiyo. Nimetokea tu watu wakitangazwa sio raia mara wakitofautiana na wakuu nchini. Ndi maana bado naamini kuwa hiyo hoja inalenga zaidi kuwapa uraia "wawekezaji" wanaotimiza vigezo vya kifisadi. Watu baada ya kuimarisha kwanza mfumo wa udhibiti wa uraia wanakimbilia kwenye kutaka kuidhinisha uraia pacha ili (kwa mtazamo wangu) wacheze dili na mafisadi wa kimataifa.
 
Hivi wewe unajua kusoma na kuelewa kweli?

Wapi ilisemwa kwamba hizo dola 6000 zilikuwa ni za kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Madison kuja Tanzania?

Watu hamsomagi vitu mkavielewa. Matokeo yake mnafikia mahitimisho ya kipumbavu kabisa.

Na kuchanga si lazima. Ni hiari, btw.
It doesn't matter zilikuwa za kufanyia nini, but the point is matajiri walishindwa kusaidia wafiwa dola 6000 zikapatikana. Period
 
It doesn't matter zilikuwa za kufanyia nini, but the point is matajiri walishindwa kusaidia wafiwa dola 6000 zikapatikana. Period

Yes it does matter zilikuwa za nini.

Na hakuna aliyeshindwa kusaidia wewe. Dola 6000 nani ashindwe kuzitoa?

Watu hawawezi kutoa tu hela hovyo hovyo pasi na maelezo ya kutosha.

Na kwa vile kutoa ni hiari, kama watu waliamua kutokutoa, that's their prerogative.
 
Wengi wakiwa majuu wanakuwa wabinafsi wengi wenu mkija mnalalamika sana kuhusu ilo jirekebisheni undugu kufaana sio kufanana
 
Envy.
Watanzania nawasifia kwa kuamini kila jambo wanaloambiwa.
Yaani mtu yuko dunia ya tatu lakini anaambiwa mtu aliyeko ughaibuni anateseka basi anaamini afu unasikia kumbe bora mi niliye bongo nina afadhali.

huwa nikija bongo nawasikitia sana wenzangu niliowaacha..watu wamezeeka utadhani haturingani umri..achilia mbali kuridhika na umaskin walionao wakati ni graduates tena wengine wana masters....
Kweli bora uoshe wazee ughaibuni for five yrs ukusanye hio hela urudi bongo kuliko kupokea laki tisa kwa mwezi bongo...hii ni kwa wanaume wanaopokea laki tisa kwa mwezi.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Wickama , ndugu ni kweli wapo wenye kufanikiwa na wasiofanikiwa Bongo hata Ughaibuni pia.
Mada kama nilivomuelewa father-xmas ni kujibu au kuondoa dhana potofu iloandikwa hapa jf na mtoto wa waziri mkuu mstaafu wa tanzania John S. Malecela aitwaye william j Malecela Le Mutuz .

Kufanikiwa ni jitahada zako, lakini ni ukweli ulio wazi kwa mtoto wa maskini na usiye na connection (godfathers) kwa Bongo inahitaji nguvu za ziada kufanikiwa iwe kupata mtaji au kupata elimu nzuri , ila kwa nchi tajiri kama Scandinavia kwa father-xmas ni rahisi. Mfano kwa kupata mshahara wa Tsh milion 2-4 kwa Ulaya sio mpaka ufanye kazi fulani special wakati Bongo mshahara huo lazima uwe na kazi fulani. Kufagia Ulaya unapata mshahara mzuri tu, ni kweli gharama ya maisha Ulaya ipo juu japo ni maisha quality lakini kwa mtu mwenye malengo anayefanya savings/kutunza fedha ya Ulaya akibadilisha kwa fedha ya Bongo ni hela nyingi tu.

Mfano unafanya kazi ya kufagia unalipwa milion nne unasave/tunza milion 1.5 kwa mwaka unakua na milion 18 Tsh. unaweza kununu anyumba ya kawaida/mkoani .??? na ukifanya kazi kwa muda mrefu na mshahara unaongezeka pia na labda savings inaongezeka pia.
Siku zote ni malengo na determination.
william j Malecela Le Mutuz na wengine wa caliber yake walikuwa hawana malengo wanataka nini na wafanye nini, walitaka kuishi maisha ya wenyeji ilihali wao sio wenyeji, wakaangukia pua na kubaki kusema uongo badala ya kujihoji udhaifu wao nini. Le Mutuz ni mtoto wa kigogo mwenye fursa nyingi ukilinganisha na mtoto wa Mtz mlalahoi lakini alishindwa kuzitumia. Ajiulize ni Watz wangapi wana uwezo wa kwenda Marekani kama yeye?? Mbona baadhi wamekwenda Ulaya wamekuja Bongo na maisha mazuri?? mbona mzee Mengi alikwenda Ulaya akarudi Bongo na elimu nzuri kazi nzuri na mipango mizuri ya kibiashara??

Nafahamu baadhi ya familia ambazo maisha yao yamekua bora baada ya kuwa na ndugu zao huko Ulaya na Marekani, hawakua wasomi na wengine wameondoka kimazabe mazabe, lakini sasa hivi ndugu zao wana maisha bomba.
william j Malecela Le Mutuz don't look the success look the personality
Salute
 
Last edited by a moderator:
mambo ya watoto wa kishua ilikua zamani now days ngoma drooo kwanza watoto wengi wa vigogo washasanda........baadhi ya watoto wa vigogo waliokuwa wanaenda nje wengi wao sijui kama walikuwa wanapiga mzigo....ila watoto wa uswahilinI wakienda huko lazima wajitume tu.....ona vijana wa kino na ilala baadhi yao wamenda nje na wamerudi huku wamefanya mambo makubwa sana......kufanikiwa ni kujituma tu na mafanikio unaweza pata popote

Salute Mkuu
 
It doesn't matter zilikuwa za kufanyia nini, but the point is matajiri walishindwa kusaidia wafiwa dola 6000 zikapatikana. Period

Kinachokusumbua wewe ni ''kufikiria kibongo bongo''. Wewe unafikiri kwasababu uko Ulaya au Marekani basi utaitisha mchango tu na upewe! Kusaidia hakua uhusiano wowote na utajiri....
 
kilio changu,

nashukuru kwa maelezo yako, nadhani ni vyema ikajulikana kuwa kuyatafuta maisha ni kokote, ila hiyo kokote sio lazima ifuatane na hisia mbaya za kule ulikoanzia. wachina wengi walifika marekani kama wasotaji wa mtaani, lakini leo walio wengi wana milki biashara lukuki katika nchi ile. Sio rahisi kuwasikia wakiambatanisha mafanikio yao na udhalili wa maisha huko kwao.

Nina uhakika hata Nairobi hujawahi fika Lol.
Hebu quote sehemu niliyodhalilisha Tanzania?
Inshort point zako zinatokana na story zakusikia huko vijiwen mmakoshinda bila kazi.
Afu watu wanaoukana utanzania na kujipa ukimbizi ili wapate maisha mazuri mim nawaita Mashujaa.Lol
 
Last edited by a moderator:
Mbona nje kuna baraka nyingi sana !! tafakari usemi huu:- teembeeni kwenye mgongo wa ardhi hii mupate kunufaika!
 
Kinachokusumbua wewe ni ''kufikiria kibongo bongo''. Wewe unafikiri kwasababu uko Ulaya au Marekani basi utaitisha mchango tu na upewe! Kusaidia hakua uhusiano wowote na utajiri....
Sasa utajiri wenu una maana gani kama mnashindwa kusaidiana ugenini na nyie ni watanzania wote? Mbona mnatuaminisha kupitia vibirthday vyenu kuwa mnaishi kwa umoja? Au ni umoja wa kwenye goodtimes tu, kwenye matatizo No? Acheni vijisababu bana.....hela hazijifichi!
 
Nimebahatika kufika Dubai, India na China huko sijui tuipe uswazi maana mateso yanafanana, hata huko marekani Marland bado watu ni mlo mmoja lakini kuna nchi zimebarikiwa katika bara la Africa ziko kama ulaya, nchi kama Kenya kuna watu wanaishi kama mbinguni lakini ukizama tu pembeni ya mji kuna mtu kutwa kula uchafu tu. Ingawaje ukiweza kupiga mbwa mswaki, kuogesha wazee unaweza kumzidi nesi anayebeba vima hivyo hivyo pesa upatayo hiko pale pale kwa sababu wewe unaziona nyingi kwa idadi lakini ukikatwa kodi, ukaripia umeme na maji unabaki kama mbongo, imefikia mtu anakufa huko mnamchoma kutokana na maisha magumu. Hivi huko uliko ukiishiwa nguvu unafanyaje kama wewe kazi yako ni kutumia nguvu? mnajibakiziaga pension za uzeeni au mnasubiri mkifa mchomwe moto. Umetusaidia kutotaka uraia pacha maana umekwepa upopo, basi taja nchi uliyopo kama ni kwema nasi tuende kuzisaka na kurudi kujenga nchi yetu kama wewe unavyoijenga sasa remotely

HAhaaaa
 
Kinachokusumbua wewe ni ''kufikiria kibongo bongo''. Wewe unafikiri kwasababu uko Ulaya au Marekani basi utaitisha mchango tu na upewe! Kusaidia hakua uhusiano wowote na utajiri....


Nakuona kamanda
 
Mkuu nipatie namba yako PM unipe mchongo wa kwenda huko kupiga BOX.
 
Sasa utajiri wenu una maana gani kama mnashindwa kusaidiana ugenini na nyie ni watanzania wote? Mbona mnatuaminisha kupitia vibirthday vyenu kuwa mnaishi kwa umoja? Au ni umoja wa kwenye goodtimes tu, kwenye matatizo No? Acheni vijisababu bana.....hela hazijifichi!

Ni kweli ughaibuni hakuna deal.
Happy now?
LoL
 
Mnatuaminisha vipi kama ni kweli hizi mbiu mnazojipigia wakati mnashindwa kusafirisha mwili wa marehemu kwa dola 6000 tu? Tena wa hapo hapo US unapopasemea....


Kule Marekani kuwa watanzania wanaishi kule kinyume na sheria (hawana makaratasi), pia kuna wabangaizaji, na watu wa kuparty tu, utakuta mtu kama huyu hana issue yeyote ya maendeleo na hata hayo mambo ya kujiwekea akiba bank hana yeye anawaza kujirusha tu. Nimeshuhudia mwenyewe mwaka juzi, Marekani kuna watu wana maisha bwana, asikudanganye mtu.
 
Sasa utajiri wenu una maana gani kama mnashindwa kusaidiana ugenini na nyie ni watanzania wote? Mbona mnatuaminisha kupitia vibirthday vyenu kuwa mnaishi kwa umoja? Au ni umoja wa kwenye goodtimes tu, kwenye matatizo No? Acheni vijisababu bana.....hela hazijifichi!

Kwani kusaidia ni lazima? We vipi wewe...
 
Back
Top Bottom