Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

father-xmas

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2010
Posts
982
Reaction score
1,127
Naona kumekua na maneno meengi kuhusu watanzania waishio ughaibuni.
Mimi nimeishi Scandnavia kwa muda mrefu ila baada ya kutimiza malengo yangu nilirudi nyumbani for good.Kwa sasa huwa ninakwenda mara kwa mara kwa sababu ya kibiashara kisha ninarudi nyumbani.

Kusema ule ukweli wa Mungu,kwa watoto wa maskini kama mimi ulaya ni bora kuliko bongo.Hapa nitaiongelea ulaya kama ninavyoifahamu mimi.Mimi mzee wangu hakua tajiri kama mzee wa Le mutuz,Tanzania niliyozaliwa mimi na kukulia ni tofauti sana na Tanzania aliyozaliwa na kukulia kaka yangu Le Mutuz.Mim Mungu alinijalia sana akili za darasani lakini kutokana na umaskini wa wazee nilishindwa kuendelea na chuo.

Ikatokea zali nikaenda scandinavia,nilienda kule nikiwa na malengo mawili,kusoma na kutafuta mtaji wa maana wa kijiajiri.Mungu alinisaidia,nimesoma,nina masters yangu,nina nyumba sita nimepangisha,nyumba moja ninafanyia biashara zangu na moja ninaishi na wadogo zangu na moja iko mkoani wazee wamejisitiri.Nina viwanja na mashamba.Vyote hivi nisingekuwa navyo leo kama nisingeenda ughaibuni.

Pia Mungu alinisaidia nikakusanya pesa ambazo nilitumia kujiajiri.

Mimi niliajiriwa kwenye kampuni ya kutengeneza magari.Huko nilikua na waafrika wengine wengi tu.

Sio kweli kwamba sehemu pekee wabongo waliyo nayo ni kwenye birthday za sebuleni tu LOL.Ulaya kuna viwanja vya maana bana za kula bata bongo itasubiri sana tu.Kitu kinachofanya wabongo wakusanyike kwenye hivyo vipati hadi nadhani ni ile hali ya kufurahia kukutana na wabongo wengine.Pia sio kila mtu anapenda kuwa kwenye hiyo mikusanyiko ya wabongo,mimi ni mmoja wa watu ambao nilikua sipendi kujimix na wabongo wenzangu.

Suala la kwamba wabongo walioko ughaibuni wana maisha magumu sikubaliani nalo.Kwanza kabisa idadi ya watanzania walioko tanzania wenye access ya internet inayowawezesha kusema wabongo wa ughaibuni wanateseka ni ndogo sana ukilinganisha na watanzania walioko bongo wasiojua hata internet ni nini.

Mimi kwa sasa ninaishi Tanzania na ninafurahia maisha ya hapa sababu ughaibuni imenisaidia leo hii sihitaji kwenda kujambiana kwenye madaladala,leo hii nikipata ugonjwa usio na tiba ya kueleweka bongo naenda zangu kutibiwa Scandinavia,mm nina uraia wa scandinavia tayari.

Hakuna binadamu yeyote awe muafrika au mzungu au muarabu hata awe amechoka vipi financialy aliyeko scandinavia anayelala njaa eti kisa hana hela ya chakula.Kwa Tanzania kila jua linapokuchwa kuna mamilioni ya watoto na watu wazima wanalala njaa.

Scndinavia inaongoza kwa uchache wa vifo vya watoto na wazazi,kwa Tanzania hebu tuchukue sekunde tano kuwaombea R.I.P dada na mama zetu watakaokufa wakati wakijifungua usiku wa leo.Tanzania mama zetu wanajifungua huku wakitzabwa makofi na manesi.Dada zetu waliko ughaibuni wanajifungualia katika mazingira kama mtu yuko hotelini,hata wanaojifungulia Aghakhan watasubiri sana compare na wanaojifungulia hospitali za serikalini ughaibuni.

Tokea nimeishi ughaibuni sijawahi shuhudia umeme ukikatika wala maji.Huwa wanayafunga tu kwa masaa au kuukata umeme kwa masaa na hapo mnapewa taarifa kuwa saa fulani mpaka saa fulani maji au umeme utazimwa.Sijawahi kuona watoto wanaotembea peku na kaptura zimechanika kwenye masaburi.Sijawahi ona mtoto akishindwa kusoma kwa sababu mzazi hana pesa,sijawahi ona mtu anakufa kwa kukosa elfu mbili ya kununua dawa,sijawahi ona watoto wenye utapiamlo,sijawahi ona watu wakitembea pekupeku,sijawahi ona ambulance za vibajaji LOL,sijawahi ona wakulima masikini kama hawa wa Tanzania.

Scandinavia maji huchemshi,unafungua bombani unakunywa,ukitaka ya baridi au ya moto kila wakati yapo.

Wkati naishi ughaibuni nilikua sina gari binafsi,japo magari ni bei chee sana kila mtu anaweza kuwa nalo cha muhimu tu uwe na vibali vya kukuwezesha kupata driving licence.Sikuhitaji gari binafsi kwa sababu usafiri wa public ni wa starehe.Baada ya kurudi bongo imenibidi tu niwe na usafiri sababu daladala kusema ukweli ni hiyo shida tu lakini ni mateso.

Wabongo walioko ughaibuni wanabezwa kwa kazi wanazofanywa,fine,hata mimi huko kwenye kampuni ya magari sikuwa nafanya kazi niliyosomea,ila ukweli ni kwamba nilikuwa nalipwa vizuri,wakati naanza nilikua nalipwa kama milioni sita za madafu kwa mwezi.Baadae waliniongeza,sasa kwa mtoto wa maskini kama mimi ukiniambia nilivokua ughaibuni nilikua nateseka nakuona unaongea kichini maana mdingi wangu angekua nazo hizo nisingeshindwa kwenda chuo bongo wakati kichwani kuko vizuri.

Hata wanaosafisha wazee hakuna anayepokea chini ya milioni nne za madafu kwa mwezi.Hapo nimetaja kima cha chini.

Kitu ambacho ambacho kwangu kilikua kinanipa stress enzi naishi ughaibuni ni kwamba sijawahi kufeel at home.Hii hali ndiyo ilinifanya kusave na kufanya kazi kwa bidii hadi nikatimiza malengo yangu nikarudi home.Kwa kifupi social life ya ughaibuni sucks(,huu ni mtizamo wangu).

Inshort kwa upande wangu mimi hata wale watanzania wanaoishi ughaibuni bila vibali mateso yao hayafikii hata theluthi ya mateso ya watanzania masikini walioko Tanzania.

Ughaibuni ni kweli kuna maisha ya ghali,ila ukiishi kwa malengo yako hakuna asiyefanikiwa.Pia ukiamua kuwa mtu wa bata ughaibuni utakula bata za maana kuliko wala bata wa bongo.

Ni kweli wahamiaji wengi(sio wabongo tu) wanafanya kazi za wazee,kusafisha na nyingine kama hizo ila ni ukweli pia kuwa wapo wapo wengi tu wenye kazi zao za maana.
Pia wewe secretary au mfanyakazi kwenye kampuni ya simu bongo na nyingine kama hizo hebu jiulize unapata shilingi ngapi kwa mwezi hadi umcheke mwenzio anayesafisha wazee na kupata milioni zake nne kwa mwezi?

Kitu ambacho wabongo wamewazidi walioko ughaibuni ni good social life tu.
 
Umesema ukweli kuna watu watakukasirikia kama umefanya kitu kibaya wakati wewe umesema ukweli tu. Wewe ni mfano mzuri wa mtu wa kutoka familia ya kawaida kupata nafasi kufanikiwa na kurudi nyumbani kuwekeza sasa kama mtu asikotaka maisha kama hayo wangetaka wewe ufanye nini? ungebaki bongo bila elimu, na umasikini kwa sababu eti ukiondoka wewe si mzalendo! sasa unaajiri watu badala ya kuajiriwa, wewe sio masikini tena ume break mzunguko wa umasikini kwenye familia na una upeo wa kuona mengi!. Kama tungechukua muda kupeana mbinu badala ya kupigana madongo tungekuwa mbali
 
Ah mi niko poa tu ingawa sielewi hii obsession na wabongo waishio ughaibuni inatoka wapi hasa.....

Kutwa kucha wabeba maboksi hivi...wabongo waishio ughaibuni vile....

Kunani?

Envy.
Watanzania nawasifia kwa kuamini kila jambo wanaloambiwa.
Yaani mtu yuko dunia ya tatu lakini anaambiwa mtu aliyeko ughaibuni anateseka basi anaamini afu unasikia kumbe bora mi niliye bongo nina afadhali.
 
Envy.
Watanzania nawasifia kwa kuamini kila jambo wanaloambiwa.
Yaani mtu yuko dunia ya tatu lakini anaambiwa mtu aliyeko ughaibuni anateseka basi anaamini afu unasikia kumbe bora mi niliye bongo nina afadhali.

Oh well....acha tu wajifariji.
 
ada ya kibali chetu cha kuishi nchini unatulipa uhamiaji??
 
Mleta hoja, je unalizungumziaje swala la uraia wa zaidi wa nchi moja?
Na kitu gani haswa kimekushawishi kurudi tena hapa bongo wakati maisha yako ni mazuri tu huko ulaya?


Sent from my iPad using JamiiForums

Kusemaa ukweli mkuu mimi hata sina habari na hayo mambo ya dual citizenship.
Mim nina uraia wa huko nilikokua.
Uraia wa Tanzania una faida gani hasa kwa mfano?

Kilichonifanya nirudi Tanzania ni hivi,nyumbani ni pale moyo wako unapojisikia uko nyumbani,hata kama ni pangoni.
Ulaya kweli kuna maisha mazuri ila sikua na feel at home kutokana na social life ya kule.
Pamoja na kuwa sikua nafeel at home ila nisingerudi bongo iwapo sikua na uhakika wa kuishi maisha ninayoishi leo,yaani ningebaki nifie huko huko kuliko kurudi bongo nikiwa siko vizuri.Tanzania ukiwa masikini ni masikini kweli kweli,hayo mateso yake kama hujawahi kuishi kama masikini huwezi kuyaelewa.
Acheni kina Le Mutuz wapakashifu ulaya maana sidhani kama yule jamaa hata anajua maana ya kuamkia uji,kushindia uji na kulala njaa.
 
Mimi kwa sasa ninaishi Tanzania na ninafurahia maisha ya hapa sababu ughaibuni imenisaidia leo hii sihitaji kwenda kujambiana kwenye madaladala, leo hii nikipata ugonjwa usio na tiba ya kueleweka bongo naenda zangu kutibiwa Scandinavia, mm nina uraia wa scandinavia tayari.

Hivi kuna uraia wa Scandinavia? Nilidhani Scandinavia ni eneo lililopo kaskazini mwa Ulaya linalojumuisha nchi za Denmark, Norway na Sweden?

Let's assume kuwa Scandinavia ni nchi, kwa hiyo unaishi Tanzania kama Mscandinavia au pia una uraia wa Tanzania?

Najaribu ku-figure out wale wanaodai kuwa Tanzania ina uraia wa nchi mmoja na wanapinga uraia pacha wakati in practice kuna Watanzania wenye uraia wa nchi nyingine na wanaishi Tanzania.
 
Hivi kuna uraia wa Scandinavia? Nilidhani Scandinavia ni eneo lililopo kaskazini mwa Ulaya linalojumuisha nchi za Denmark, Norway na Sweden?

Let's assume kuwa Scandinavia ni nchi, kwa hiyo unaishi Tanzania kama Mscandinavia au pia una uraia wa Tanzania?

Najaribu ku-figure out wale wanaodai kuwa Tanzania ina uraia wa nchi mmoja na wanapinga uraia pacha wakati in practice kuna Watanzania wenyewe uraia wa nchi nyingine na wanaishi Tanzania.

Nimesema Scandinavia sababu sijataka kutaja nchi hasa niliyokuwepo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi kuna uraia wa Scandinavia? Nilidhani Scandinavia ni eneo lililopo kaskazini mwa Ulaya linalojumuisha nchi za Denmark, Norway na Sweden?

Let's assume kuwa Scandinavia ni nchi, kwa hiyo unaishi Tanzania kama Mscandinavia au pia una uraia wa Tanzania?

Najaribu ku-figure out wale wanaodai kuwa Tanzania ina uraia wa nchi mmoja na wanapinga uraia pacha wakati in practice kuna Watanzania wenyewe uraia wa nchi nyingine na wanaishi Tanzania.

Kuwa na uraia wa nchi nyingine na kuishi Tanzania kama watanzania wengine wala sio tatizo.
Ingekua ughaibuni ingekua ngumu ila kwa bongo nafanya kila kitu bila kipingamizi.
Ni kweli kwenye makaratasi mimi sio mtanzania.
 
Kuna jamaa yangu aliamua kurudi nchini miaka ya karibuni. Yeye tayari alikuwa na uraia wa huko alikokuwa anaishi. Kurudi kwake nchini ilikuwa ni kuanzisha biashara ambayo wageni hawaruhusiwi kuifanya bali Watanzania tu. Sasa alikuwa na mikakati mbali mbali ya kuhakikisha anaingia nchini kama mbongo. Na mikakati hiyo ilikuwemo pia kusaidiwa na kingunge mmoja mkubwa kuja kumpokea JKNIA na kumsaidia kuingia nchni kama "mbongo" na mikakati mingine pia. Kupata passport ya Tanzania alisema haikuwa tatizo. Na aliingia nchini salama salmini kama mbongo.

Wapo wabongo wengi wenye uraia wa nchi za nje ambao wanaishi nchini. Kama hupigipigi kelele kuhusu uraia uliokuwa nao wa nje basi hakuna atakayekufahamu ila ukipiga piga mayowe kila siku kuhusu uraia wako wa nje basi unaweza kuchomewa na ukapewa 24 hours kuondoka nchini.

Hivi kuna uraia wa Scandinavia? Nilidhani Scandinavia ni eneo lililopo kaskazini mwa Ulaya linalojumuisha nchi za Denmark, Norway na Sweden?

Let's assume kuwa Scandinavia ni nchi, kwa hiyo unaishi Tanzania kama Mscandinavia au pia una uraia wa Tanzania?

Najaribu ku-figure out wale wanaodai kuwa Tanzania ina uraia wa nchi mmoja na wanapinga uraia pacha wakati in practice kuna Watanzania wenyewe uraia wa nchi nyingine na wanaishi Tanzania.
 
Mkuu wale wabongo wanaosema haya manno utakuta wengi wao wana ndugu tena wala hawajuani, ila kwa hasira utakuta mtu anaandika habari kwa hasira ili tu kuwachamba nduguze walioko huko. majuu tofauti na hapa nyumbani kwani hapa nyumbani mtu akipata mshahara wa milioni moja na hana nyumba yake mwenyewe anaona katajirika. Majuu watanzania wana masters na wanashika hela hata balozi wa Tanzania alieko majuu hapati kwa mwezi. Tanzania ni tanzania tu, huwezi kulinganisha maisha ya wabongo wachache wasiosoma majuu (wabaingazi) na kila mbongo. Huku tanzania watu wakiona party na mikusanyiko ya watanzania majuu basi wao wanafikiri kule ni kujirusha tu, watu wana maisha jamani. Nilipokwenda Marekani mwaka juzi kwa kaka yangu nilishangaa kuona watanzania na maisha ya kifahari, kwa hapa Bongo ukiondoa hawa wazungu wa unga (wafanya biashara ya msimu) sijawahi ona mtu anaishi kivile. majuu si sawa na hapa Bongo, never!
 
Kama Ulaya kuzuri mno si muhamie. Mkipata uraia wa huko kuzuri Uraia pacha wa nini.? Na wazungu matajiri waliotoka nchi za kitajiri wanakuja huku kufuata nini? Je wanakuja kuonja ladha ya umaskini? Tatizo nililolibaini tumejifunza kukariri siyo kuchanganua. Ndiyo maana vitu vyetu vyote tunasema kagundua mzungu. Vyakula vyetu vya kishenzi, dawa zetu za kishenzi,utamaduni wetu wa kishenzi.Tunamakaratasi yanaitwa vyeti,tutakapoelimika tutajua thamani yetu na bara letu. Ulaya inaihitaji Afrika kuliko Afrika inavyohitaji Ulaya. Kikwazo ni kizazi cha kunukuu
 
Back
Top Bottom