Tena kama huna documents utaishia kufanya casual labors tu, kufagia nakuosha vyombo vya hotel. Mi sipendi kuwapa watu taswira tofauti. Ni kweli life standard iko juu kuliko huku nyumbani, hata niliporudi nilipata shida sana kubre-adjust. Miji michafu na dampo hadi kwenye makazi ya watu mambo ambayo nchi niliyokua hayakuwepo. Ila kwenye ukweli si tuseme tuuu
Hebu tufafanulie kilichokua kinakufanya ushindwe kusave pesa.LolNilichojifunza maisha yanaweza kua magumu sehemu zote. Hata mimi mwanzo nilikua siamini mtu anaweza kupigika akiwa nchi za watu. Mi nilikwenda kusoma tena nilikua na scholarship, pia nilifanya vibarua. Nimerudi niko poa ila ni kwasababu scholarship yangu ilikua inanilipia kila kitu. Otherwise saving ni ngumu sana
Kama Ulaya kuzuri mno si muhamie. Mkipata uraia wa huko kuzuri Uraia pacha wa nini.? Na wazungu matajiri waliotoka nchi za kitajiri wanakuja huku kufuata nini? Je wanakuja kuonja ladha ya umaskini? Tatizo nililolibaini tumejifunza kukariri siyo kuchanganua. Ndiyo maana vitu vyetu vyote tunasema kagundua mzungu. Vyakula vyetu vya kishenzi, dawa zetu za kishenzi,utamaduni wetu wa kishenzi.Tunamakaratasi yanaitwa vyeti,tutakapoelimika tutajua thamani yetu na bara letu. Ulaya inaihitaji Afrika kuliko Afrika inavyohitaji Ulaya. Kikwazo ni kizazi cha kunukuu[/QUOTE]
Vijana wengi wanakimbilia huko wanakokuita majuu kwa sababu ya dhiki ya hapa nyumbani; kwanza kama mnakumbuka vijana wengi walianza kuzamia kwa kudandia meli na wengi wao wakatoswa baharini, baadae ndio kumeibuka mtindo wa hawa vijana kugeuzwa punda na kubeba madawa ya kulevya . Adha yote hii vijana wetu wanapata kwasababu ya kukosa njia za kuweza kujikimu maisha yao na ndio maana wanadiriki hata kuwekeza maisha yao rehani kwa kufanya vitendo vinavyohatarisha maisha yao!!
Jakaya Kikwete alisoma UDSM miaka ya sabini na alifundishwa na marehemu Walter Rodney mwandishi wa kitabu HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA; nashawishika kuamini kuwa hakuelewa the gist of what was written in that book!!
Hapo kwenye nyekundu; sio kweli kuwa kikwazo ni kizazi hiki cha kunukuu, kikwazo ni hawa watawala wetu ambao ingawa wanasema wamesoma lakini hawajaelimika kwani vitendo vyao na maamuzi yao sio tofauti na wakina Chief Mangungo wa zamani ambao walibadilisha nchi yetu kwa wakoloni kwa kupewa ushanga!! Hivi leo nchi yetu inasemekana ni maskini lakini sio kweli kwani tungekuwa maskini hawa wachina , wamerekani, na hata wajapani wasingekuwa wanashindana kutubembeleza tuwe marafiki zao. Uzumbukuku wa watawala wetu kwa kukubali kuwapa hawa watawala mamboleo wanaowaita wawekezaji maliasili ya nchi yetu kwa kubadilishana na hizo suti wanazovaa ndio unatufanya tuwe maskini hata vijana wetu wakimbie nchi yao na kwenda kubeba mabox huko ughaibuni!! Hawa watawala wetu hawana tofauti na wakina chief Mngungo wa zamani isipokuwa wakati Mangungo akipewa ushanga wakati huo hawa wa sasa wanapewa suti na 10% na kuwapa hao wageni Dhahabu, Almasi na hata gesi pamoja na ardhi yenyewe!!
Sio sio kweli,binadamu wa aina yeyote awe msomi au sio msomi akishafanikiwa kukanyaga ughaibuni anayo nafasi ya kufanikiwa,cha muhimu kama kwa Scandinavia ni kujua lugha yao then unaenda kusomea kajikoz ka kazi unayotaka kufanya then unaajiriwa,hata wanaosaidia wazee wanasomea,kuuza madukan unasomea,hata kusafisha wanasomea vikoz vya miez mitatu hivi jspo sometimes unaweza kupata bila kusomea hasa usafi na nyingine,ila wazee lazima usomee.
Lucifer our lord
Umeongea ukweli mtupu. Yeyote atakayekubeza au kukukashifu ni ana wivu tu wa maendeleo yako. Hata mimi wakati nasoma kuna mahala nilihisi kama unajivuna hivi au una majigambo lakini hapana ukisoma vizuri you have stated the simple truth according to you. Hongera sana kwa hatua ulizopiga ndugu ni haki yako.
Wengine wameenda huko wakarudi na raba tu. Keep it up. Utafute mke na watoto sasa. Hahahaa!
ww bongo ulipata desapointment nyingi yaelekea ukaenda huko ukatusua ni sawa tu kusema shukurani zako kwa kupata mafanikio huko, kna jamaa yangu mmja naye kakaa sana huko ila yuko bongo yeye anasemaga bila kuja huku asingetusua maisha,
Mkuu kama sikutaka kuwa specific kwenye nchi niliyoishi unafikir ndio nitajibu haya maswali yako?Lol.
Main point ya mada yangu ni uhalisia wa maisha ya wabongo ughaibuni.
Hayo mengine simooo.LOL
I get you very well well lol.father-xmas hongera kwa kurudi, ila mie mwenzio nimeshindwa ku-adjust na loife ya bongo, watu wenyewe wavivu na wezi. Unafanya nae biashara halafu yeye anafikiria jinsi ya kukudhulumu. Kiukweli maisha ya bongo yanahitaji uvumilivu. Maisha ya nje ni mazuri ingawa nyumbani ni nyumbani lakini kuchafu
Kuwa na uraia wa nchi nyingine na kuishi Tanzania kama watanzania wengine wala sio tatizo.
Ingekua ughaibuni ingekua ngumu ila kwa bongo nafanya kila kitu bila kipingamizi.
Ni kweli kwenye makaratasi mimi sio mtanzania.
Aisee, kama ulikuwa kichwani mwangu!Duh kwa uhandishi nahisi unatoka maeneo ya mpakani wa Tanzania na uganda
ni kweli bongo kuna nafasi kubwa sana mfano huyu jamaa yangu mafanikio aliyopata huko kaja kuyafanya tz kajenga, anafanya biashara ya kuleta used toka denmark etc...tanzania napo ukipapatia maisha mterezo tu....ndomana ukiwaona wazungu wanao fanya kazi geita au barick etc wanakula mishahara ya hatari mpaka hawataki nao kwenda kwao, hata wakina nikola wa sleepway wote mafanikio wameyapata hapa tz....na yule mkurugenzi wa zamanI wa dtv yule mzungu hataki kabisa kurudi kwao, nnachosema hapa mafanikio unaweza pata popote dunianikuna stage fulani ya maisha ukifika majuu unaweza usipande tena na hapo ndio ukija bongo utaona opportunities nyingi sana na unapanda sana naamini ndio huyo jamaa yako ndio kilichotokea.
Mkuu wale wabongo wanaosema haya manno utakuta wengi wao wana ndugu tena wala hawajuani, ila kwa hasira utakuta mtu anaandika habari kwa hasira ili tu kuwachamba nduguze walioko huko. majuu tofauti na hapa nyumbani kwani hapa nyumbani mtu akipata mshahara wa milioni moja na hana nyumba yake mwenyewe anaona katajirika. Majuu watanzania wana masters na wanashika hela hata balozi wa Tanzania alieko majuu hapati kwa mwezi. Tanzania ni tanzania tu, huwezi kulinganisha maisha ya wabongo wachache wasiosoma majuu (wabaingazi) na kila mbongo. Huku tanzania watu wakiona party na mikusanyiko ya watanzania majuu basi wao wanafikiri kule ni kujirusha tu, watu wana maisha jamani. Nilipokwenda Marekani mwaka juzi kwa kaka yangu nilishangaa kuona watanzania na maisha ya kifahari, kwa hapa Bongo ukiondoa hawa wazungu wa unga (wafanya biashara ya msimu) sijawahi ona mtu anaishi kivile. majuu si sawa na hapa Bongo, never!
Hata na wewe ni Mtanzania lakini kwa KUJISIFIA umevuka kiwango kwani vitu ambavyo umeviandika haviendani na umri wako kabisa .Envy.
Watanzania nawasifia kwa kuamini kila jambo wanaloambiwa.
Yaani mtu yuko dunia ya tatu lakini anaambiwa mtu aliyeko ughaibuni anateseka basi anaamini afu unasikia kumbe bora mi niliye bongo nina afadhali.
nina nyumba sitaIkatokea zali nikaenda scandinavia,nimesoma,nina masters yangu,nina nyumba sita nimepangisha,nyumba moja ninafanyia biashara zangu na moja ninaishi na wadogo zangu na moja iko mkoani wazee wamejisitiri.Nina viwanja na mashamba.Vyote hivi nisingekuwa navyo leo kama nisingeenda ughaibuni.
Pia Mungu alinisaidia nikakusanya pesa ambazo nilitumia kujiajiri.
Mkuu uhalisia unaotoa uko too general, afterall nchi za Scandinavia ni tofauti sana na nchi zingine za ughaibuni kama UK,Ujerumani au hata Marekani.. wewe ungejiongelea wewe binafsi tu lakini sio kama unavyotaka kuiweka hapa wakati hujui nje ya hizo Scandinavian countries ambako maisha ni mteremko kias[/QUOTE
Ni kweli nimeongelea kilichonitokea mm,ila najua watu wengi mno wenye expirience kama yangu,nina rafiki kibao ktk nchi mbalimbali na wana mafanikio sana.
Sikubishii ila naomba utaje hizo nchi za ughaibuni ambazo mtu huwezi kufanikiwa.
Usije tu ukatutajia uturuki Lol
Sio sio kweli,binadamu wa aina yeyote awe msomi au sio msomi akishafanikiwa kukanyaga ughaibuni anayo nafasi ya kufanikiwa,cha muhimu kama kwa Scandinavia ni kujua lugha yao then unaenda kusomea kajikoz ka kazi unayotaka kufanya then unaajiriwa,hata wanaosaidia wazee wanasomea,kuuza madukan unasomea,hata kusafisha wanasomea vikoz vya miez mitatu hivi jspo sometimes unaweza kupata bila kusomea hasa usafi na nyingine,ila wazee lazima usomee.
Asee wewe sio mtanzania, inabidi uhamiaji, ardhi na TRA wakuchunguze kama hayo mashamba na hizo nyumba ulifata taratibu za foreigner katika kuvipata.