Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

father-xmas,
nimefurahi na mada yako. binafsi nimeishi The Netherlands. Ukweli uliopo ni huu. Ughaibuni sio rahisi kujipatia ma-ekari ya ardhi kama hapa bongo. Sio rahisi kujenga. Sio rahisi kuwa na savings za maana labda uwe na vibarua lukuki. Haitakaa uuhisi upendo na kujuliana hali kama bongo. Hautakaa ujifungulie mradi wa kuku 1000 wa nyama/mayai kama kaka zangu pale kipunguni/banana-dar.

Nyumba zako zote ulizojenga bongo si rahisi kumaliza kujenga nyumba moja ya maana western europe, ndio maana ukahamia bongo kujenga!!!!

Pia sio kweli kuwa wanaukata kimaisha eti wote wameanzia ughaibuni. NOOOOOO. Fuatilia familia za kichagga, kinyakyusa, kikurya, wakikuyu, wabaganda na wengi, wanajenga maisha yao kwa HARD WORK na kuamini kuwa mtoaji ni Mungu. Issue ni DISCIPLINE AND FOCUS. Reginald Mengi na Bakhresa na Dialo hawajaishi Scandinavia.

Mimi nina ushahidi wa wenzetu wa nje ambao hata akiambiwa mama kafariki anashindwa ku-board a plane kuja kuzika.

Wewe Mshukuru Mungu kwa ulivyojaliwa kupata. Lakini sio haki kuambatanisha kupata kwako kwa kudhalili maisha ya hapa kwetu.

Ni kweli tulio wengi ni wahanga wa malaria na vifo vya wajawazito, mbona husemi ukweli kuwa pamoja na maisha mazuri tunaoyoona wenzetu wanakaa mbona kwao maradhi makubwa ni DEPRESSION? Kwanini bongo na Africa hatupati DEPRESSION kama jamaa wa SCANDINAVIA NA WESTERN EUROPE?
 
Last edited by a moderator:
ni kweli bongo kuna nafasi kubwa sana mfano huyu jamaa yangu mafanikio aliyopata huko kaja kuyafanya tz kajenga, anafanya biashara ya kuleta used toka denmark etc...tanzania napo ukipapatia maisha mterezo tu....ndomana ukiwaona wazungu wanao fanya kazi geita au barick etc wanakula mishahara ya hatari mpaka hawataki nao kwenda kwao, hata wakina nikola wa sleepway wote mafanikio wameyapata hapa tz....na yule mkurugenzi wa zamanI wa dtv yule mzungu hataki kabisa kurudi kwao, nnachosema hapa mafanikio unaweza pata popote duniani

NI kweli mafanikio popote ila kwa mm nisingeweza kufanikiwa bongo.
 
Wazee wengi humu ndani wanaongea coz hawatoka zaidi ya kwenda Nairobi, Dubai na China/hong kong. mimi nimefanikiwa kutembea nchi za ulaya na marekani (US) nitazungumzia US; safari zangu zilikuwa za kikazi maana wengi wataanza kuniuliza kwa nini sikubaki huko, nilibahatika kutembelea miji ifuatayo nikiwa US: Washingtone DC, Atlanta, Chicago, Seattle na Kansas. kote huko niliwakuta wabongo, wakenya, Wanyarwanda and Burundi. nitazungumzia wabongo wenzangu; watanzania walioko huko wanamaisha mazuri kwaani wameweza kuwasaidia ndg zao walioko hapa bongo. nikiwa US niliona watu wanaoitwa homeless waafrica na wazungu, lkn sikubahatika kuona mtanzania homeless. pia nilipata bahati ya kusafiri na mbongo mmoja kutoka washington DC kuja bongo, alikuwa na mizigo mingi ya business yaani viatu, pafyumu, nguo na nk. huyu bwana asili yake ni mbeya, aliniambia duka lake lipo mikocheni kwa Mwl Nyerere, US alienda kupiga shule alipomaliza akaingia mtaani, tulipofika katika kijiji chetu Dar es salaam, alipata shida sana kutoka kwa watu wa TRA,sidhani km uhamiaji walimsumbua kwaani alikuwa na pass ya Marekeni, alitakiwa kulipia dola 100 kuingia nchini, nilisikitika sana kuona Mtanzania mwenzangu akipanga foleni na wageni kukaguliwa na kulipia kuingia nchi yake ya kuzaliwa, watu hawa wanatafuta maisha tu huko lkn akiri zao ziko huku, angalia analeta biashara nyumbani na analipa kodi. Kwa kifupi wapo wengi walio majuu wapo akina alex kajumlo, Husein Masha, Nteze John na nk. Maisha yanaenda. mfano Alex Kajumlo ni msanii wa maziki na kocha mpira na maisha yanaenda.

Sasa kama alikuwa na pass ya marekani, unasemaje unamuonea huruma kupanga foleni kwa wazungu. Huyo sio mtanzania, kwanza ameikana nchi yake akapata uraia wa US unless uniambie hiyo pass ni ya magumashi kitu ambacho kupata pass ya US kimagumashi sidhani. Hatuna uraia wa nchi mbili na hata kusumbuliwa na TRA inawezekana usumbufu huo ni kwa ajili ya mkanganyiko wa uhalali wake wa kufanya shughuli hizo. All tufate sheria iwe mtanzania au mgeni
 
father-xmas,
nimefurahi na mada yako. binafsi nimeishi The Netherlands. Ukweli uliopo ni huu. Ughaibuni sio rahisi kujipatia ma-ekari ya ardhi kama hapa bongo. Sio rahisi kujenga. Sio rahisi kuwa na savings za maana labda uwe na vibarua lukuki. Haitakaa uuhisi upendo na kujuliana hali kama bongo. Hautakaa ujifungulie mradi wa kuku 1000 wa nyama/mayai kama kaka zangu pale kipunguni/banana-dar.

Nyumba zako zote ulizojenga bongo si rahisi kumaliza kujenga nyumba moja ya maana western europe, ndio maana ukahamia bongo kujenga!!!!

Pia sio kweli kuwa wanaukata kimaisha eti wote wameanzia ughaibuni. NOOOOOO. Fuatilia familia za kichagga, kinyakyusa, kikurya, wakikuyu, wabaganda na wengi, wanajenga maisha yao kwa HARD WORK na kuamini kuwa mtoaji ni Mungu. Issue ni DISCIPLINE AND FOCUS. Reginald Mengi na Bakhresa na Dialo hawajaishi Scandinavia.

Mimi nina ushahidi wa wenzetu wa nje ambao hata akiambiwa mama kafariki anashindwa ku-board a plane kuja kuzika.

Wewe Mshukuru Mungu kwa ulivyojaliwa kupata. Lakini sio haki kuambatanisha kupata kwako kwa kudhalili maisha ya hapa kwetu.

Ni kweli tulio wengi ni wahanga wa malaria na vifo vya wajawazito, mbona husemi ukweli kuwa pamoja na maisha mazuri tunaoyoona wenzetu wanakaa mbona kwao maradhi makubwa ni DEPRESSION? Kwanini bongo na Africa hatupati DEPRESSION kama jamaa wa SCANDINAVIA NA WESTERN EUROPE?

Mkuu nakubal wapo wengi wanaofanikiwa kimaisha bila kutoka nje ya bongo.Mm nimeongelea hisyoria yangu,najua wapo watu wengi ambao wana maisha magumu bongo na hadi wamekata tamaa,hao ndio nina walenga mm,nimewaelezea historia yangu na nilichokipata ughaibuni il wakipata nafas wasije wakapuuzia kwenda wakidhan ughaibun ni mateso tu.
Najua wapo watu wanamaisha mazur bongo lkn ni wachache sana,wengi wa watanzania hawana hata elfu hamsini kwa mwez,hawa ndio ninaofanana nao mim.Hao kina mwamvita makamba and alikes hawawez kunielewa sbb Yanzania ninayoijua wao hawaijui.
 
Last edited by a moderator:
Hata na wewe ni Mtanzania lakini kwa KUJISIFIA umevuka kiwango kwani vitu ambavyo umeviandika haviendani na umri wako kabisa .
  • umepata zali,
  • ukaenda chukua Master
  • hapohapo ukapata muda wa kutengeneza magari (Kuunganisha nuts assembly) sijui ni kuunda Volvo
  • ukaanza biashara
  • nina nyumba sita Ndugu yangu nyumba za Bongo sio km zamani ukasimamishe tembe Kijijini uiite nyumba, siku hiti kuna kulipia ardhi ya Tanzania kwa sq meter na kiwanja ni zaidi ya 4,90,000.00 hapa Dodoma sasa wewe una viwanja 6 bado nyumba ya chini ni 36M
    • nyumba 6 za 36M ni sawa na 216,000,000.00
    • Na kwa jinsi unavyohadithia Hadithi za Shigongo umeweza kukaa nyumba 4 mbili umeacha Sadaka
Kajipange tena kuwa Mwandishi wa UDAKU kazi Rudini tu Tanzania km Le Mutuz tupo naye hapa Dodoma na Dar huyu Diaspora mwenye uhakika, Blog na mashamba na nyumba Dodoma na Mvumi tunajua ni zake sasa hizo 6 hiyo abaru sikuimalizia

nina nyumba sita
Hahaa
LOL
 
Pengine kwakua mimi nilienda kusoma nikiwa na ajira yangu nyumbani ndio maana sielewi unachoeleza. Kweli mi kubaki kule kufagia na kuosha wazee hali nyumbani ofisi imenipa gari na dereva niliona ni kijinyanyasa
Hongera sana
 
Hata na wewe ni Mtanzania lakini kwa KUJISIFIA umevuka kiwango kwani vitu ambavyo umeviandika haviendani na umri wako kabisa .
  • umepata zali,
  • ukaenda chukua Master
  • hapohapo ukapata muda wa kutengeneza magari (Kuunganisha nuts assembly) sijui ni kuunda Volvo
  • ukaanza biashara
  • nina nyumba sita Ndugu yangu nyumba za Bongo sio km zamani ukasimamishe tembe Kijijini uiite nyumba, siku hiti kuna kulipia ardhi ya Tanzania kwa sq meter na kiwanja ni zaidi ya 4,90,000.00 hapa Dodoma sasa wewe una viwanja 6 bado nyumba ya chini ni 36M
    • nyumba 6 za 36M ni sawa na 216,000,000.00
    • Na kwa jinsi unavyohadithia Hadithi za Shigongo umeweza kukaa nyumba 4 mbili umeacha Sadaka
Kajipange tena kuwa Mwandishi wa UDAKU kazi Rudini tu Tanzania km Le Mutuz tupo naye hapa Dodoma na Dar huyu Diaspora mwenye uhakika, Blog na mashamba na nyumba Dodoma na Mvumi tunajua ni zake sasa hizo 6 hiyo abaru sikuimalizia

nina nyumba sita

Umemshtukia eeh! Wanadhani hakuna alieishi huko
 
Naona kumekua na maneno meengi kuhusu watanzania waishio ughaibuni.
Mimi nimeishi Scandnavia kwa muda mrefu ila baada ya kutimiza malengo yangu nilirudi nyumbani for good.Kwa sasa huwa ninakwenda mara kwa mara kwa sababu ya kibiashara kisha ninarudi nyumbani.

Kusema ule ukweli wa Mungu,kwa watoto wa maskini kama mimi ulaya ni bora kuliko bongo.Hapa nitaiongelea ulaya kama ninavyoifahamu mimi.Mimi mzee wangu hakua tajiri kama mzee wa Le mutuz,Tanzania niliyozaliwa mimi na kukulia ni tofauti sana na Tanzania aliyozaliwa na kukulia kaka yangu Le Mutuz.Mim Mungu alinijalia sana akili za darasani lakini kutokana na umaskini wa wazee nilishindwa kuendelea na chuo.

Ikatokea zali nikaenda scandinavia,nilienda kule nikiwa na malengo mawili,kusoma na kutafuta mtaji wa maana wa kijiajiri.Mungu alinisaidia,nimesoma,nina masters yangu,nina nyumba sita nimepangisha,nyumba moja ninafanyia biashara zangu na moja ninaishi na wadogo zangu na moja iko mkoani wazee wamejisitiri.Nina viwanja na mashamba.Vyote hivi nisingekuwa navyo leo kama nisingeenda ughaibuni.

Pia Mungu alinisaidia nikakusanya pesa ambazo nilitumia kujiajiri.

Mimi niliajiriwa kwenye kampuni ya kutengeneza magari.Huko nilikua na waafrika wengine wengi tu.

Sio kweli kwamba sehemu pekee wabongo waliyo nayo ni kwenye birthday za sebuleni tu LOL.Ulaya kuna viwanja vya maana bana za kula bata bongo itasubiri sana tu.Kitu kinachofanya wabongo wakusanyike kwenye hivyo vipati hadi nadhani ni ile hali ya kufurahia kukutana na wabongo wengine.Pia sio kila mtu anapenda kuwa kwenye hiyo mikusanyiko ya wabongo,mimi ni mmoja wa watu ambao nilikua sipendi kujimix na wabongo wenzangu.

Suala la kwamba wabongo walioko ughaibuni wana maisha magumu sikubaliani nalo.Kwanza kabisa idadi ya watanzania walioko tanzania wenye access ya internet inayowawezesha kusema wabongo wa ughaibuni wanateseka ni ndogo sana ukilinganisha na watanzania walioko bongo wasiojua hata internet ni nini.

Mimi kwa sasa ninaishi Tanzania na ninafurahia maisha ya hapa sababu ughaibuni imenisaidia leo hii sihitaji kwenda kujambiana kwenye madaladala,leo hii nikipata ugonjwa usio na tiba ya kueleweka bongo naenda zangu kutibiwa Scandinavia,mm nina uraia wa scandinavia tayari.

Hakuna binadamu yeyote awe muafrika au mzungu au muarabu hata awe amechoka vipi financialy aliyeko scandinavia anayelala njaa eti kisa hana hela ya chakula.Kwa Tanzania kila jua linapokuchwa kuna mamilioni ya watoto na watu wazima wanalala njaa.

Scndinavia inaongoza kwa uchache wa vifo vya watoto na wazazi,kwa Tanzania hebu tuchukue sekunde tano kuwaombea R.I.P dada na mama zetu watakaokufa wakati wakijifungua usiku wa leo.Tanzania mama zetu wanajifungua huku wakitzabwa makofi na manesi.Dada zetu waliko ughaibuni wanajifungualia katika mazingira kama mtu yuko hotelini,hata wanaojifungulia Aghakhan watasubiri sana compare na wanaojifungulia hospitali za serikalini ughaibuni.

Tokea nimeishi ughaibuni sijawahi shuhudia umeme ukikatika wala maji.Huwa wanayafunga tu kwa masaa au kuukata umeme kwa masaa na hapo mnapewa taarifa kuwa saa fulani mpaka saa fulani maji au umeme utazimwa.Sijawahi kuona watoto wanaotembea peku na kaptura zimechanika kwenye masaburi.Sijawahi ona mtoto akishindwa kusoma kwa sababu mzazi hana pesa,sijawahi ona mtu anakufa kwa kukosa elfu mbili ya kununua dawa,sijawahi ona watoto wenye utapiamlo,sijawahi ona watu wakitembea pekupeku,sijawahi ona ambulance za vibajaji LOL,sijawahi ona wakulima masikini kama hawa wa Tanzania.

Scandinavia maji huchemshi,unafungua bombani unakunywa,ukitaka ya baridi au ya moto kila wakati yapo.

Wkati naishi ughaibuni nilikua sina gari binafsi,japo magari ni bei chee sana kila mtu anaweza kuwa nalo cha muhimu tu uwe na vibali vya kukuwezesha kupata driving licence.Sikuhitaji gari binafsi kwa sababu usafiri wa public ni wa starehe.Baada ya kurudi bongo imenibidi tu niwe na usafiri sababu daladala kusema ukweli ni hiyo shida tu lakini ni mateso.

Wabongo walioko ughaibuni wanabezwa kwa kazi wanazofanywa,fine,hata mimi huko kwenye kampuni ya magari sikuwa nafanya kazi niliyosomea,ila ukweli ni kwamba nilikuwa nalipwa vizuri,wakati naanza nilikua nalipwa kama milioni sita za madafu kwa mwezi.Baadae waliniongeza,sasa kwa mtoto wa maskini kama mimi ukiniambia nilivokua ughaibuni nilikua nateseka nakuona unaongea kichini maana mdingi wangu angekua nazo hizo nisingeshindwa kwenda chuo bongo wakati kichwani kuko vizuri.

Hata wanaosafisha wazee hakuna anayepokea chini ya milioni nne za madafu kwa mwezi.Hapo nimetaja kima cha chini.

Kitu ambacho ambacho kwangu kilikua kinanipa stress enzi naishi ughaibuni ni kwamba sijawahi kufeel at home.Hii hali ndiyo ilinifanya kusave na kufanya kazi kwa bidii hadi nikatimiza malengo yangu nikarudi home.Kwa kifupi social life ya ughaibuni sucks(,huu ni mtizamo wangu).

Inshort kwa upande wangu mimi hata wale watanzania wanaoishi ughaibuni bila vibali mateso yao hayafikii hata theluthi ya mateso ya watanzania masikini walioko Tanzania.

Ughaibuni ni kweli kuna maisha ya ghali,ila ukiishi kwa malengo yako hakuna asiyefanikiwa.Pia ukiamua kuwa mtu wa bata ughaibuni utakula bata za maana kuliko wala bata wa bongo.

Ni kweli wahamiaji wengi(sio wabongo tu) wanafanya kazi za wazee,kusafisha na nyingine kama hizo ila ni ukweli pia kuwa wapo wapo wengi tu wenye kazi zao za maana.
Pia wewe secretary au mfanyakazi kwenye kampuni ya simu bongo na nyingine kama hizo hebu jiulize unapata shilingi ngapi kwa mwezi hadi umcheke mwenzio anayesafisha wazee na kupata milioni zake nne kwa mwezi?

Kitu ambacho wabongo wamewazidi walioko ughaibuni ni good social life tu.

Mkuu umeandika nini?
 
kuna wengine naona wanataka kufanya mashindano sasa kuishi nje.....mleta uzi ashasema yeye mafanikio yake kayapata huko scandinavia....na nyinyi semeni mafanikio yenu basi
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kusemaa ukweli mkuu mimi hata sina habari na hayo mambo ya dual citizenship.
Mim nina uraia wa huko nilikokua.
Uraia wa Tanzania una faida gani hasa kwa mfano?

Kilichonifanya nirudi Tanzania ni hivi,nyumbani ni pale moyo wako unapojisikia uko nyumbani,hata kama ni pangoni.
Ulaya kweli kuna maisha mazuri ila sikua na feel at home kutokana na social life ya kule.
Pamoja na kuwa sikua nafeel at home ila nisingerudi bongo iwapo sikua na uhakika wa kuishi maisha ninayoishi leo,yaani ningebaki nifie huko huko kuliko kurudi bongo nikiwa siko vizuri.
Tanzania ukiwa masikini ni masikini kweli kweli,hayo mateso yake kama hujawahi kuishi kama masikini huwezi kuyaelewa.
Acheni kina Le Mutuz wapakashifu ulaya maana sidhani kama yule jamaa hata anajua maana ya kuamkia uji,kushindia uji na kulala njaa.

kweli hauna faida kwako......hihihihihi!!!
 
father-xmas,
nimefurahi na mada yako. binafsi nimeishi The Netherlands. Ukweli uliopo ni huu. Ughaibuni sio rahisi kujipatia ma-ekari ya ardhi kama hapa bongo. Sio rahisi kujenga. Sio rahisi kuwa na savings za maana labda uwe na vibarua lukuki. Haitakaa uuhisi upendo na kujuliana hali kama bongo. Hautakaa ujifungulie mradi wa kuku 1000 wa nyama/mayai kama kaka zangu pale kipunguni/banana-dar.

Nyumba zako zote ulizojenga bongo si rahisi kumaliza kujenga nyumba moja ya maana western europe, ndio maana ukahamia bongo kujenga!!!!

Pia sio kweli kuwa wanaukata kimaisha eti wote wameanzia ughaibuni. NOOOOOO. Fuatilia familia za kichagga, kinyakyusa, kikurya, wakikuyu, wabaganda na wengi, wanajenga maisha yao kwa HARD WORK na kuamini kuwa mtoaji ni Mungu. Issue ni DISCIPLINE AND FOCUS. Reginald Mengi na Bakhresa na Dialo hawajaishi Scandinavia.

Mimi nina ushahidi wa wenzetu wa nje ambao hata akiambiwa mama kafariki anashindwa ku-board a plane kuja kuzika.

Wewe Mshukuru Mungu kwa ulivyojaliwa kupata. Lakini sio haki kuambatanisha kupata kwako kwa kudhalili maisha ya hapa kwetu.

Ni kweli tulio wengi ni wahanga wa malaria na vifo vya wajawazito, mbona husemi ukweli kuwa pamoja na maisha mazuri tunaoyoona wenzetu wanakaa mbona kwao maradhi makubwa ni DEPRESSION? Kwanini bongo na Africa hatupati DEPRESSION kama jamaa wa SCANDINAVIA NA WESTERN EUROPE?
Wickama , ndugu ni kweli wapo wenye kufanikiwa na wasiofanikiwa Bongo hata Ughaibuni pia.
Mada kama nilivomuelewa father-xmas ni kujibu au kuondoa dhana potofu iloandikwa hapa jf na mtoto wa waziri mkuu mstaafu wa tanzania John S. Malecela aitwaye william j Malecela Le Mutuz .

Kufanikiwa ni jitahada zako, lakini ni ukweli ulio wazi kwa mtoto wa maskini na usiye na connection (godfathers) kwa Bongo inahitaji nguvu za ziada kufanikiwa iwe kupata mtaji au kupata elimu nzuri , ila kwa nchi tajiri kama Scandinavia kwa father-xmas ni rahisi. Mfano kwa kupata mshahara wa Tsh milion 2-4 kwa Ulaya sio mpaka ufanye kazi fulani special wakati Bongo mshahara huo lazima uwe na kazi fulani. Kufagia Ulaya unapata mshahara mzuri tu, ni kweli gharama ya maisha Ulaya ipo juu japo ni maisha quality lakini kwa mtu mwenye malengo anayefanya savings/kutunza fedha ya Ulaya akibadilisha kwa fedha ya Bongo ni hela nyingi tu.

Mfano unafanya kazi ya kufagia unalipwa milion nne unasave/tunza milion 1.5 kwa mwaka unakua na milion 18 Tsh. unaweza kununu anyumba ya kawaida/mkoani .??? na ukifanya kazi kwa muda mrefu na mshahara unaongezeka pia na labda savings inaongezeka pia.
Siku zote ni malengo na determination.
william j Malecela Le Mutuz na wengine wa caliber yake walikuwa hawana malengo wanataka nini na wafanye nini, walitaka kuishi maisha ya wenyeji ilihali wao sio wenyeji, wakaangukia pua na kubaki kusema uongo badala ya kujihoji udhaifu wao nini. Le Mutuz ni mtoto wa kigogo mwenye fursa nyingi ukilinganisha na mtoto wa Mtz mlalahoi lakini alishindwa kuzitumia. Ajiulize ni Watz wangapi wana uwezo wa kwenda Marekani kama yeye?? Mbona baadhi wamekwenda Ulaya wamekuja Bongo na maisha mazuri?? mbona mzee Mengi alikwenda Ulaya akarudi Bongo na elimu nzuri kazi nzuri na mipango mizuri ya kibiashara??

Nafahamu baadhi ya familia ambazo maisha yao yamekua bora baada ya kuwa na ndugu zao huko Ulaya na Marekani, hawakua wasomi na wengine wameondoka kimazabe mazabe, lakini sasa hivi ndugu zao wana maisha bomba.
william j Malecela Le Mutuz don't look the success look the personality
 
mambo ya watoto wa kishua ilikua zamani now days ngoma drooo kwanza watoto wengi wa vigogo washasanda........baadhi ya watoto wa vigogo waliokuwa wanaenda nje wengi wao sijui kama walikuwa wanapiga mzigo....ila watoto wa uswahilinI wakienda huko lazima wajitume tu.....ona vijana wa kino na ilala baadhi yao wamenda nje na wamerudi huku wamefanya mambo makubwa sana......kufanikiwa ni kujituma tu na mafanikio unaweza pata popote
 
Last edited by a moderator:
Umemshtukia eeh! Wanadhani hakuna alieishi huko

binafsi ilinichekesha kukuta wabongo nao wapo viwanjani na mbwa ili mbwa wapate mazoezi. Wengine wamedanganya kuwa ni wakimbizi toka Burundi hali ya kuwa ni vijana wa hapa Ngamiani tanga. ukimuaga aisee wiki ijayo ndiyo tunarudi tanga, basi hata euro 200 za 'PELEKEA' mama hamna ila maneno kibaooo. na pia maarufu kwa kutoa makosa kila cha bongo (hii pscho ploy ya kuji-defend kwa vile wengi wao hawana uwezo wa kuyamudu maisha ya bongo). Akija kutembea, ukoo mzima unasubiri atafanya vitu kama nabii Musa, wanashangaa jamaa anajikata kisha anasepa bila hata kuuliza viwanja vya Pongwe city vinapatikana wapi!!!!

Ukweli unabaki kuwa ulaya hutakaa upate ekari 3 za kulima kama pale Morogoro, hutakaa uuze mazagazaga (terminolgy ya Tarime), hutafungua kioski kando ya stendi ya magari kama pale bunda na hutafungua mama ntilie kama pale kigamboni. Ukiwa mzee ndio balaa, jiandae kulundikwa kwenye kambi za wazee wenzio sio uwalete kelele wajukuu! Jiandae kusema "i dont care" pale mwanao wa kiume anapoolewa na dume mwenziwe kwa ndoa "halali" (town hall-sawa na bomani), jiandae kutathmini kuwa hili jibu alilonipa huyu jamaa ni sawa? au kwa sababu mimi ni mweusi?'

Mwenyezi Mungu tumshukuru kutujaalia hili bara. yaani KWETU.
 
kilio changu,

nashukuru kwa maelezo yako, nadhani ni vyema ikajulikana kuwa kuyatafuta maisha ni kokote, ila hiyo kokote sio lazima ifuatane na hisia mbaya za kule ulikoanzia. wachina wengi walifika marekani kama wasotaji wa mtaani, lakini leo walio wengi wana milki biashara lukuki katika nchi ile. Sio rahisi kuwasikia wakiambatanisha mafanikio yao na udhalili wa maisha huko kwao.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom