Ukweli kuhusu kuzomewa kwa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu kuzomewa kwa Kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Giddy Mangi, Oct 21, 2011.

 1. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  WanaJF naomba kujua kama kweli jana Umma uliweza kumfikishia ujumbe Kikwete kuwa hatumtaki na tumemchoka huku nchi ikiwa imemshinda.
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Wewe unategemea Mangi atakuwa na mawazo gani zaidi ya Uchagga na CDM
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jamaa amepewa Phd ya 5 jana na ndio anakuwa Rais wa kwanza Tanzania na Afrika kwa ujumla kupata Phd 5 kwa muda mfupi. Watanzania wanamtaka na hawajamchoka , labda wewe ambae uko ughaibuni na ni raia wa burundi . Jamaa ni kichwa !
   
 4. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wee jibu swali kama hujui nyamaza kama mimi
   
 5. S

  Sgaga Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kichwa kwa mama yako
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Unataka jibu gani tena wakati kaishajibiwa au na wewe Mangi CDM...mimi siwezi kunyamazishwa na wewe pumba tupu
   
 7. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145  hahahahaaaa ntarudi
   
 8. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Arooo acheni hizo bwana
   
 9. M

  Marytina JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  jk jana alidhania anaenda ofisi za bakwata akaipatapata
   
 10. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mambo vyp ndugu Ritz?
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sasa Mkuu Chuo ambacho wanajumiya yake WAMEKUZOMEA halafu wanakupa PhD si DHIHAKA hiyo
   
 12. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Zinaitwa kupiga kona na kuwahi kufunga.
   
 13. M

  Marytina JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  kabakisha mbili tu amfikie Mugabe
  atakuwa akifikiri kwa uwezo wa juu kama MUGABE
   
 14. Bambanza jr.

  Bambanza jr. JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kha! Kali sana.
   
 15. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Stori nzima ilikuwa hivi kwa ufupi....

  Awali wanafunzi hao walionekana wakiwa wameshika mabango hayo lakini walizuiwa na polisi na kuelezwa kuwa kama ni ujumbe tayari ulishafika hivyo waendelee na shughuli nyingine.
  Hata hivyo, wanafunzi hao ambao hawakutaka kutaja majina yao walizunguka nyuma ya Ukumbi wa Nkrumah na kuyaficha mabango hayo, huku wengine wakijipanga tayari kwa kumpokea Rais Kikwete ambaye alikuwa bado hajafika eneo hilo.

  Mara baada ya Rais Kikwete kufika chuoni hapo alikwenda kusaini katika kitabu cha wageni na wakati akielekea katika ukumbi huo huku akipunga mkono, wanafunzi hao walikuwa kimya.
  Rais Kikwete wakati akiendelea kuwapungia mkono wanafunzi hao, walianza kumzomea na kutoa mabango yao waliyokuwa wameyaficha huku wakiimba, "Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi".
  source gonga hapa
   
 16. i

  ipod Member

  #16
  Oct 21, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Sio vizuri kuchukua chakula cha watoto na kuwapa mbwa lakini hata mbwa wanakula makombo yanayoanguka chini ya meza ya bwana wake..Mkandara mnafiki tu
   
 17. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nina hamu na wewe sana
   
 18. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Labda wewe na wenzio wenye akili kama zako ndio hamjamchoka na hizo Phd za kupewa zisizo na maana.
   
 19. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Wanafunzi UDSM wachafua hali ya hewa ujio wa JK

  Thursday, 20 October 2011 20:46

  Fidelis Butahe

  WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) jana walichafua hali ya hewa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho baada ya kumzomea Rais Jakaya Kikwete.

  Rais Kikwete ambaye alikuwa ameambatana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa pamoja na viongozi wengine wa Serikali alikutwa na zomeazomea hiyo saa 6:23 mchana wakati akiingia katika Ukumbi wa Nkrumah ambapo yalifanyika maadhimisho hayo. Wanafunzi hao mbali na kumzomea Rais huyo wa awamu ya nne pia walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakiimba, "Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi, hatukutaki ondoka,".

  Baadhi ya mabango hayo yalikuwa yameandikwa, ''Wao walisoma bure sisi tunalala nje, Miaka 50 ya uhuru mikopo hatupati, Tusiilipe Dowans, Wanafundisha UDSM makazi Bagamoyo je ni haki?, Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi.

  Awali wanafunzi hao walionekana wakiwa wameshika mabango hayo lakini walizuiwa na polisi na kuelezwa kuwa kama ni ujumbe tayari ulishafika hivyo waendelee na shughuli nyingine.

  Hata hivyo, wanafunzi hao ambao hawakutaka kutaja majina yao walizunguka nyuma ya Ukumbi wa Nkrumah na kuyaficha mabango hayo, huku wengine wakijipanga tayari kwa kumpokea Rais Kikwete ambaye alikuwa bado hajafika eneo hilo.

  Mara baada ya Rais Kikwete kufika chuoni hapo alikwenda kusaini katika kitabu cha wageni na wakati akielekea katika ukumbi huo huku akipunga mkono, wanafunzi hao walikuwa kimya.

  Rais Kikwete wakati akiendelea kuwapungia mkono wanafunzi hao, walianza kumzomea na kutoa mabango yao waliyokuwa wameyaficha huku wakiimba, "Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi".
  Polisi waliokuwa eneo hilo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana walilazimika kutumia busara kuwanyamazisha wanafunzi hao ambao waliendelea kuzomea na kuimba licha ya kuwa Rais Kikwete alikuwa ameshaingia katika ukumbi huo.
  Wakati shughuli za maadhimisho hayo zikiwa zinaendelea wanafunzi hao walikuwa bado wakiimba nyimbo hizo na kuzomea, mpaka walipoombwa kutoendelea kuimba na baadhi ya polisi ambao waliwaeleza kuwa kuzomea hakuwezi kuwaletea mikopo vyuoni, bali wajenge hoja za msingi na kuziwasilisha sehemu husika.

  Hata wakati Rais Kikwete akisoma hotuba yake na kugusia maendeleo ya chuo hicho pamoja na uboreshwaji wa utoaji mikopo vyuoni, wanafunzi hao waliokuwa wakifuatilia hotuba hiyo kupitia Televisheni kubwa walikuwa wakizomea.

  "Hivi Rais anajua jinsi tunavyopigika hapa chuoni, wengine inaonekana tumepewa mikopo, lakini mpaka leo hatujapata, hivi anajua tunaishi vipi huyu, anajua tunalala wapi," walisikika wakisema baadhi ya wanafunzi.
  Katika hatua nyingine, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika alisema kuwa kilichofanywa na wanafunzi hao kinatakiwa kutazamwa kwa macho mawili.
  Mnyika alisema kuwa ahadi zilizotolewa na Rais Kikwete kuhusu maendeleo ya chuo hicho zinatakiwa kutekelezwa na kufafanua kuwa hata katika utawala wa Mwalimu Nyerere matatizo vyuoni yalikuwapo na kwamba dawa ni kuyatatua.

  Akizungumzia kitendo cha wanafunzi hao kumzomea Rais Kikwete mbele ya Rais Museveni, Mnyika alisema kuwa hilo ni jambo la kawaida kwa kuwa Museveni amewahi kusoma katika chuo hicho na anajua harakati za wanafunzi.
  "Wakati Museveni akisoma alikuwa na kikundi chake ambacho kilikuwa na msimamo mkali na kutoa kauli za kimapinduzi kwa viongozi mbalimbali wa Afrika, Museveni anakijua hiki chuo,"
  chanzo:gazeti la mwanachi
   
 20. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Wanafunzi UDSM wachafua hali ya hewa ujio wa JK

  Thursday, 20 October 2011 20:46

  Fidelis Butahe

  WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) jana walichafua hali ya hewa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho baada ya kumzomea Rais Jakaya Kikwete.

  Rais Kikwete ambaye alikuwa ameambatana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa pamoja na viongozi wengine wa Serikali alikutwa na zomeazomea hiyo saa 6:23 mchana wakati akiingia katika Ukumbi wa Nkrumah ambapo yalifanyika maadhimisho hayo. Wanafunzi hao mbali na kumzomea Rais huyo wa awamu ya nne pia walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakiimba, “Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi, hatukutaki ondoka,”.

  Baadhi ya mabango hayo yalikuwa yameandikwa, ‘’Wao walisoma bure sisi tunalala nje, Miaka 50 ya uhuru mikopo hatupati, Tusiilipe Dowans, Wanafundisha UDSM makazi Bagamoyo je ni haki?, Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi.

  Awali wanafunzi hao walionekana wakiwa wameshika mabango hayo lakini walizuiwa na polisi na kuelezwa kuwa kama ni ujumbe tayari ulishafika hivyo waendelee na shughuli nyingine.

  Hata hivyo, wanafunzi hao ambao hawakutaka kutaja majina yao walizunguka nyuma ya Ukumbi wa Nkrumah na kuyaficha mabango hayo, huku wengine wakijipanga tayari kwa kumpokea Rais Kikwete ambaye alikuwa bado hajafika eneo hilo.

  Mara baada ya Rais Kikwete kufika chuoni hapo alikwenda kusaini katika kitabu cha wageni na wakati akielekea katika ukumbi huo huku akipunga mkono, wanafunzi hao walikuwa kimya.

  Rais Kikwete wakati akiendelea kuwapungia mkono wanafunzi hao, walianza kumzomea na kutoa mabango yao waliyokuwa wameyaficha huku wakiimba, “Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi”.
  Polisi waliokuwa eneo hilo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana walilazimika kutumia busara kuwanyamazisha wanafunzi hao ambao waliendelea kuzomea na kuimba licha ya kuwa Rais Kikwete alikuwa ameshaingia katika ukumbi huo.
  Wakati shughuli za maadhimisho hayo zikiwa zinaendelea wanafunzi hao walikuwa bado wakiimba nyimbo hizo na kuzomea, mpaka walipoombwa kutoendelea kuimba na baadhi ya polisi ambao waliwaeleza kuwa kuzomea hakuwezi kuwaletea mikopo vyuoni, bali wajenge hoja za msingi na kuziwasilisha sehemu husika.

  Hata wakati Rais Kikwete akisoma hotuba yake na kugusia maendeleo ya chuo hicho pamoja na uboreshwaji wa utoaji mikopo vyuoni, wanafunzi hao waliokuwa wakifuatilia hotuba hiyo kupitia Televisheni kubwa walikuwa wakizomea.

  “Hivi Rais anajua jinsi tunavyopigika hapa chuoni, wengine inaonekana tumepewa mikopo, lakini mpaka leo hatujapata, hivi anajua tunaishi vipi huyu, anajua tunalala wapi,” walisikika wakisema baadhi ya wanafunzi.
  Katika hatua nyingine, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika alisema kuwa kilichofanywa na wanafunzi hao kinatakiwa kutazamwa kwa macho mawili.
  Mnyika alisema kuwa ahadi zilizotolewa na Rais Kikwete kuhusu maendeleo ya chuo hicho zinatakiwa kutekelezwa na kufafanua kuwa hata katika utawala wa Mwalimu Nyerere matatizo vyuoni yalikuwapo na kwamba dawa ni kuyatatua.

  Akizungumzia kitendo cha wanafunzi hao kumzomea Rais Kikwete mbele ya Rais Museveni, Mnyika alisema kuwa hilo ni jambo la kawaida kwa kuwa Museveni amewahi kusoma katika chuo hicho na anajua harakati za wanafunzi.
  “Wakati Museveni akisoma alikuwa na kikundi chake ambacho kilikuwa na msimamo mkali na kutoa kauli za kimapinduzi kwa viongozi mbalimbali wa Afrika, Museveni anakijua hiki chuo,”
  chanzo:gazeti la mwanachi
   
Loading...