Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Nyie watu mbona hamuelewi?

Kleruu ilianzia Moshi mjini tena ikiwa ndogo ndio miaka ya 70 serikali ikaipeleka Iringa ili kubalance maendeleo ya miji midogo.
We jamaa mbona Jana saa 6:52 ulinielewsha jinsi chuo kilivyoanza, nashangaa leo unavyosema sielewi. Pia mimi ni mchaga wa Marangu Samanga sina ukabila na sijawahi kujivunia kuwa Mchaga au ukaskazini kama nyie, zaidi ya Utanzania wangu.
 
Mm nina rafiki yangu mpaka leo anaogopa kwenda kwao,na akienda hatoi taarifa wala haendi na gari lake kwa sababu ya mambo Haya ya kishirikina,sehemu Kama Kilosa huko ohho ni noma
Ni balaa tu yaani bora kutafuta eneo ukawahamisha wazee maana hakuna sababu yakua na maisha mazuti
 
Hivi Siku hizi neno "Watanzania" limeanza kufifia na watu wanaanza kujiita wakaskazini. Ebu tuache kitu hicho jamani kitatugawa Watanzania!
 
Huenda wakadai tena kadri democrasia inavyofifia nchini. Ila machief nadhani walikuwa madikteta. Kwa mfano makngi Sina wa Kibosho.
 
Kaskazini watu wameendelea kwa Kilimo na Biashara. Ninamfahamu mzee fulani hakuwahi kuwa kiongozi wala mtumishi wa Umma. Ukifika kwake kwa Standard za kwetu utadhani umekwenda kwa tajiri wa kizungu.

Hawa watu wa aina hii wako wengi kila mahali japo ni wachache, labda kama haujatembea; mimi baba yangu ni mfano mdogo, aliishia darasa la 2, hakuwahi kuajiriwa, pamoja na msaada wa sera ya elimu nzuri za wakati huo, ni mtu aliyewezesha watoto wake 5 kati ya wanane kuipata elimu ya chuo kikuu. Ange kuwa hai ( Mungu amlaze mahali pema) leo angekuwa anaishi kama mtu aliyefanikiwa sana. Aina ya uwekezaji ni moja ya jambo muhimu katika kumuinua binadamu au kumkumdidimiza katika umasikini. Tukubaliane, na hapa hatuchambani, tunaelimishana; kuna wakati tulikuwa na university moja- UDSM, na vyuo mashuhuri kama 5( Mzumbe,IFM,Maji,Ushirika, Dar tech) vyuo vyote hivi vilikuwa vya umma na elimu yake ilikuwa bure. Ndugu zangu wa kasikazini walichokifanya ni kusomesha watoto wao sekondari( miaka minne) baada ya hapo watoto wengi waliochaguliwa walisomeshwa na umma ( raslimali za umma). Mfano; katika mkoa wa Kagera, miaka ya sabini ilikuwa na sekondari 6 tu, wakati huo huo Mkoa wa Kilimajaro walikuwa na sekondari 80. Kwa vyovyote vile, wasomi wa mkoa huo ( Kilimanjaro) watakuwa wengi ukilinganisha na wa mkoa wa Kagera. Angalia Kagera :45 x 6= 270; Kilimanjaro, 45 X 80= 3600. Hata tukisema wanafunzi wote wa mkoa wakagera wamefanya vizuri waende chuo kikuu na wa mkoa wa Kilimanjaro waende robo; mkoa wa Kilimajaro utapeleka watu 900. Na baada ya kuhitimu( 270 +900=1170); tukiajiri watu 800, hii ina maana zaidi 530 watakuwa wametoka kasikazini. Na kama waajiriwa wote, watakuwa na moyo safi wa kukumbuka nyumbani na kila mtu akapeleka Tshs. 1,000,000 kwa mwaka kwa sababu mbalimbali, kasikazini zitaenda Tshs 530,000,000 wakati Kagera zitaenda 270,000,000.

Kimsingi mkakati ( strategy) ulikuwa nzuri ambao ulisaidia kuchota raslimali za taifa kuwendeleza nchi. Na wala hakuna anayelalamikia hili. Ninapoenda hospitali siulizi kabila la watoa huduma, na kwa mantiki ya maelezo hayo hapo juu ndio ( wakasikazini) wanaotoa huduma wakiwa wengi na kila mahali. Ndio maana wapo kila mahali.

Ninancho kataa ni majingambo yenye misingi potofu. Hii ndio inayosababbisha chuki miongoni wa wananchi wa taifa moja.
 
20161227_180630.jpg
na bado tupo tunamalizia mbuzi, wakaskazini hasa wachagga wanaelewa hapa wapi
 
mimi sio wa kaskazini,lakini sio siri napenda spirit ya watu wa kaskazini mwa Tz ktk kutafuta maendeleo.pia nakuwa inspired na spirit ya wahaya ktk kutafuta elimu.

huu ni mtizamo wangu,simlazimishi mtu yoyote asiye wa kaskazini kukubaliana nami.
uko sahihi na mtizamo wako,mimi nawasifu sana wafipa.kurogana wao kwa wao na mtu anayepata mafanikio.hata akiwa msomi vipi bado anakua na karoho ka kwa nini????
 
uko sahihi na mtizamo wako,mimi nawasifu sana wafipa.kurogana wao kwa wao na mtu anayepata mafanikio.hata akiwa msomi vipi bado anakua na karoho ka kwa nini????
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hiyo misaada kwann isifike huko kwenu.....?K'njaro imeendelea kupitia watu wake acha pirojo
Ndyo imeendelea kupitia watu wake kupewa misaada mingi na serikali,mfano nyumba,makanisa,maskuli na akili,pia walipewa elimu ya kufanya biashara buree,serikali nyie mungu anawaoneni!!!!
 
Hawa watu wa aina hii wako wengi kila mahali japo ni wachache, labda kama haujatembea; mimi baba yangu ni mfano mdogo, aliishia darasa la 2, hakuwahi kuajiriwa, pamoja na msaada wa sera ya elimu nzuri za wakati huo, ni mtu aliyewezesha watoto wake 5 kati ya wanane kuipata elimu ya chuo kikuu. Ange kuwa hai ( Mungu amlaze mahali pema) leo angekuwa anaishi kama mtu aliyefanikiwa sana. Aina ya uwekezaji ni moja ya jambo muhimu katika kumuinua binadamu au kumkumdidimiza katika umasikini. Tukubaliane, na hapa hatuchambani, tunaelimishana; kuna wakati tulikuwa na university moja- UDSM, na vyuo mashuhuri kama 5( Mzumbe,IFM,Maji,Ushirika, Dar tech) vyuo vyote hivi vilikuwa vya umma na elimu yake ilikuwa bure. Ndugu zangu wa kasikazini walichokifanya ni kusomesha watoto wao sekondari( miaka minne) baada ya hapo watoto wengi waliochaguliwa walisomeshwa na umma ( raslimali za umma). Mfano; katika mkoa wa Kagera, miaka ya sabini ilikuwa na sekondari 6 tu, wakati huo huo Mkoa wa Kilimajaro walikuwa na sekondari 80. Kwa vyovyote vile, wasomi wa mkoa huo ( Kilimanjaro) watakuwa wengi ukilinganisha na wa mkoa wa Kagera. Angalia Kagera :45 x 6= 270; Kilimanjaro, 45 X 80= 3600. Hata tukisema wanafunzi wote wa mkoa wakagera wamefanya vizuri waende chuo kikuu na wa mkoa wa Kilimanjaro waende robo; mkoa wa Kilimajaro utapeleka watu 900. Na baada ya kuhitimu( 270 +900=1170); tukiajiri watu 800, hii ina maana zaidi 530 watakuwa wametoka kasikazini. Na kama waajiriwa wote, watakuwa na moyo safi wa kukumbuka nyumbani na kila mtu akapeleka Tshs. 1,000,000 kwa mwaka kwa sababu mbalimbali, kasikazini zitaenda Tshs 530,000,000 wakati Kagera zitaenda 270,000,000.

Kimsingi mkakati ( strategy) ulikuwa nzuri ambao ulisaidia kuchota raslimali za taifa kuwendeleza nchi. Na wala hakuna anayelalamikia hili. Ninapoenda hospitali siulizi kabila la watoa huduma, na kwa mantiki ya maelezo hayo hapo juu ndio ( wakasikazini) wanaotoa huduma wakiwa wengi na kila mahali. Ndio maana wapo kila mahali.

Ninancho kataa ni majingambo yenye misingi potofu. Hii ndio inayosababbisha chuki miongoni wa wananchi wa taifa moja.
Hivi Siku hizi neno "Watanzania" limeanza kufifia na watu wanaanza kujiita wakaskazini. Ebu tuache kitu hicho jamani kitatugawa Watanzania!
Mgawanyo huu Uliasisiwa Na Wabunge wa CCM!! Mmojawapo akiwa Mudhihir Mudhihir akipinga kujengwa barabara ya Rombo - Nairobi, akaja John Cheyo akipinga Mrema kuchaguliwa Rais 1995,. Mgawanyo huu ukatiwa Petrol baada ya kuona watu wa Kaskazini wanaunga mkono Upinzani. Ccm ili kuwafanya Watz wasiwachague wakawaaminisha kuwa hawa watu ni wezi, wamemaliza raslimali za taifa. Eti wengi wameajiriwa Mgodini Tra, Bot Na TPA. Taasisi ambazo Serikali imeachia watumishi wake kujipangia mshahara na Posho. As a result kila mtawala anahakikisha hafanyi kazi Na bosi wa taasisi Mchaga. Refer to Mrema wa Tanroads!
 
U
Ugogoni ilikuwa ni pathway tu so even wewe ungekuwa kama unafanya biashara zako Kibaha na Kariakoo for sure utajenga Kibaha na Kariakoo tu huwezi jenga Mbezi au kongowe... tumia akili ndogo tu kujadili hoja nyepesi usifanye kama tunashindana... tuepuke kuonekana wajinga... Maeneo ambayo wakoloni walikaza ni Kwenye mazo na malighafi walizozifuata na sehemu haswa zilizoboreshwa ni zile biashara ilipofanyikia maana ilikusanya wafanya biashara wendi zaidi Historia zipo wazi hii sio ligi ndogo Elimu ya historia tu
Mzungu hakupendi maeneo ya nusu Jangwa kama Ugogoni. Alipendelea Highlands penye baridi.
 
Kwanza elimu bure ni kushusha kiwango cha elimu na upo mpango wa kufundisha kwa kutumia kiswahili kuanzia msingi mpaka chuo hii nayo ni hatari nyingine sijui watu huwa wanawaza nini apo mikataba mnaandikiwa kingereza sehemu nyingi ili kupata kazi kuna kigezo cha kuongea kingereza na kingereza ni lugha ya kimataifa sisi tutakuwa na wasomi wasioweza kuongea kingereza ukienda popote ili uweze kueleweka inabidi uongee kingereza na utaweza kuchangamana na watu wa aina zote, south afrika waligoma kufundishwa africans kwa sababu haina maslai kwa sababu ili upate kazi unabidi ujue kuongea kingereza sasa sijui kwetu vipi kuhusu kiswahili.me naona hii ni akili ya kazi kwa utawala
Mkuu kingereza ni lugha kubwa lakini kiswahili ndio utambulisho wetu. Huwezi kuukwepa utambulisho wako.
 
Usisahau na kwetu Ngara, sema tu genocide ilituhalibia vibaya wallahi
 
Pomoja na kupata Elimu watu wa Kaskazini walipoingia madarakani hawakuwa Waadirifu ktk kugawa vipaumbele vya Serikali kwa kuangalia sehemu nyingine za nchi,,

Wengi miradi mingi ya maendeleo waliikimbizia kwao kaskazini huku wakiacha mikoa ya kusini ikidirora,,
Utaona wakina Msuya walisambaza Umeme kwao Mwanga hadi vijijini lakini mikoa Kama Lindi na Ruvuma ikiwa haina Umeme wa uhakika.
Kwa kuwa sasa mnajivunia mafanikio yenu ya kuliibia taifa hili basi hatutegemei kusikia mkilalamika pale miradi ya maendeleo ikipelekwa katika kanda zingine,,

Maana tayari mmesha anza kulalama kwa ujenzi wa Chato International Airport.
Sasa mtulie tuendeleze kanda mnazozimea sasa ili zifanane na nyie.
 
Back
Top Bottom