Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Mpemba yupo Pemba, Dar, na Unguja.
Mkinga yupo Njombe, Iringa, na Dar.

Mchagga yupo Moshi, Arusha, Manyara, Dar, Morogoro na kila mahali.

Wachagga si maskini.
Eti mchaga yuko kila mahali nitajie mchaga yoyote mwenye hats 50 mtaji mkoa Wa Mara au Simiyu hakuna Manka wala Masawe
 
Sasa utalinganisha wilaya za shy na wilaya za Arusha. Yani ulinganishe Monduli na Kahama hahaha
Hebu mbali na kahama nitajie mji mwingine unajivunia

Kahama yenyewe wamejaa wachaga ndio wanachangamsha kwa biashara.
 
Hebu mbali na kahama nitajie mji mwingine unajivunia

Kahama yenyewe wamejaa wachaga ndio wanachangamsha kwa biashara.
Wasukuma unaowadharau kwa miaka 15 tu wameweza kundeleza mkoa Wa Shy mpaka serikali ikaugawa. Leo Sukuma land ina jiji Moja Mwanza. Ina manispaa 4. Shy, Kahama, Bariadi na Geita. Ina miji 9 Ushirombo, Sengerema, Maswa, Ramadi, Mhunze, Misungwi, Magu, Ngudu na Kakola.

Nitajie Manispaa na miji ya kaskazini haha out of Arusha, Moshi na Babati basi tens kwingine vumbi tu.


Haha twanga photoeee


Afu unaijua vyema wilaya ya Msalala iliyoko mkoa Wa Shinyanga. Nakwambia hakuna wilaya Mkoa Arusha ya kuigusa Msalala.
 
Huu uzi naupenda watu wanashindana kwa maendeleo na si kutukanana,wotee nawapa 100!
 
Ukiona sehemu mchaga hayupo ujue hapo mahali hapafai kibiashara.
Haha unawajua wasukuma na wanaitwa Wanyatuzu hao ndo kikwazo cha wachaga huko Simiyu ukienda Mara kunawakurya Mchaga akifika anakunja mkia
 
Wahaya wana spirit nzuri sana ya kutafuta elimu na maisha bora.
Wa Kaskazini (Kilimanjaro + Arusha) kwa gharama yeyote wanasomesha na kupambania maisha.

Mwaka huu 25-12-2016 kumekuwa na watu wengi waliorudi nyumbani mpaka nchi nzima imeshangaa,foleni ilianzia njia panda Himo mpaka round-about ya YMCA na askari wa traffick walizidiwa kuongoza mpaka wakaja field force kuongoza magari.
Arusha foleni ilianZia Kikatiti mpaka Mianzini,hamna namna,Ndege zote zinazotoka Dar-Arusha,MA-Arsha zimejaa mpaka mwakani tarehe 4,Daladala karibu zote za Dar hasa "eicher" za Ubungo -Mbagala,Gongo la Mboto-Simu 2000 zote zimepewa kibali cha kwenda Kilimanjaro na hazijatoshea.

Watu wa kaskaZini kama vile wana asili ya Israel(kukusanyika wote na kujadili maendeleo),na pia WakaskaZini husomesha watoto kwenye mashuke makubwa,Nenda USA,UK,na Australia kote huko utakuta Wachagga wapo,Mapadri wengi Itally utakuta ni wakaskazini,Wengine tuige ,tuache kukusanywa "leaders' na kuitikia 'imoo' bila kujia maana yake,changia maendeleo.

Chukua mtoto mmoja wa ndugu yako alafu msomeshe,hutajutia.

Warombo pekee ndio watu wa kaskazini ambao wamebaki nyuma kielimu,wao ni pombe tuu,wanakuja Marangu kila siku kuomba chakula !

My Take:
Wa kaskazini hata usipowapa ukuu wa wilaya,mkoa na sehem zingine kama ilivyo huwakomoi bali unawapa hasira ya maenedeleo zaidi.
Hapo uliposema Foleni ilianzia Mianzini hadi Kikatiti sio kweli, unadanganya...
 
Shukran mkuu kwa uchambuzi mwororo! Ukifuatilia history, Chama cha Kilimanjaro Native Cooperative Union (KNCU) kina mchango mkubwa sana Katika maendeleo ya Kilimanjaro!

Nimefarijika sana kwa huu uchambuzi..
 
"Mikoa ya Kaskazini iliendelezwa kwa juhudi ya Wanakaskazini"

Huo ni Ukweli unaoleta furaha kwa Wanakaskazini na Maumivu kwa wana mikoa mingine.

Nitaelezea kwa Ushahidi ulio wazi kabisaaa!

Kwanza msingi wa maendeleo ni ELIMU NA MAARIFA.

Ni wazi kuwa mikoa/makabila yenye wasomi wengi ni ile iliyowapokea wamissionary mapema na kuwakabidhi Ardhi. Katika hiyo ardhi kila walipojenga Kanisa basi walijenga na shule au hospitali nzuri.

Mikoa hiyo ni Kilimanjaro, Arusha, Kagera na Mbeya. Hiyo ilitokea hasa katika miaka ya 1885 - 1900

SASA TUKIACHA ERA HIYO:

Wananchi binafsi wa Arusha na Kilimanjaro wana spirit na asili ya utafutaji wa elimu na mali na Maendeleo kwa juhudi sana (Hustles indeed)

Mifano ifuatayo inathibitisha hayo:-

1) KUJALI ELIMU

Kufikia uhuru wa Tanzania, tayari Kilimanjaro ilikuwa na shule (Kongwe) zenye sekondari kabisa zaidi ya 38 na vyuo baadhi Shule hizo ni kama lyamungo, Majengo, Kleruu College, MUCCOBS, Marangu TC n.k

Hizo zilijengwa kwa juhudi ya Wazazi na chama kahawa KNCU

Arusha kulikuwa tayari na shule zilizojengwa kwa Juhudi za wazazi kama Moringe Sokoine, Mringa Middle School, Monduli TC (ingawa pia serikali iliweka nguvu), Arusha Sec.school, Ilboru Sec. School iliyojengwa pamoja na kanisa la KKKT mwaka 1904

Kwa kuwajuza zaidi Ilboru sec.school na kanisa la Ilboru zilijengwa na wanawake (wamama wa kimasai) kutoka Kimandolu, Levolosi na Ilboru yenyewe, na ushahidi upo.

Pia Chama cha kahawa ARCU ilichangia sana maendeleo ya Arusha.

- Miji midogo wakati huo kama Monduli, Marangu, Machame, Ilboru na Akheri zilijengwa na juhudi ya wazee wa huko.

* Mfano tu, Monduli iliamuliwa kuwa mji mahali ilipo na Wazee wachache wa monduli akiwepo Sokoine.

Can you imagine mwaka 1970 tayari Sokoine alishaanzisha jengo kubwa kuwa Halmashauri ya Monduli kabla hata serikali haijaamua halmashauri iwe wapi.

Kina Lowassa na wengine walikuja tu kuendeleza zaidi.

* Kwa Upande wa Kilimanjaro, hasa Marangu akina Mareale walikuwa Mbali tu kiasi cha kuweza kujiongoza bila serikali ya JMT.

Mji wa Moshi ulikuwa mbaali kimaendeleo siku nyingi.

2) UHUSIANO WA KARIBU WA WANAKASKAZINI

Kingine kilichoiendeleza Kaskazini ni Interaction ya kuoana watu wa Kilimanjaro na wenyeji wa Arusha mjini, kwani wali utilize ardhi vizuri kuanzia enzi na enzi.

(Hata leo hii ukichunguza utagundua watoto wengi wa familia hizo ndio wamejaa serikalini, kwenye migodi ya madini, biashara n.k)

3) KUTOKUTEKWA NA USHIRIKINA

Wanakaskazini hawana asili ya "Ushirikina" na ukisikia mchaga, mmasai ama mwarusha analoga basi ujue amenunua uchawi.

Hakuna uchawi wa kutumia paka, Jini au Vifuu bila faida yoyote.

Mikoa kama Tabora chini ya machifu wao walipaswa kuwa mbali sana kimaendeleo kama alivyofanya chief fundikira (wajomba wa Samwel Sitta) na matunda yanaonekana hadi kuwasomesha akina Samwel Sitta (Hayati)

Mikoa mingine imekuja kuamshwa na hizi shule za kata, halafu inalialia kuwa Kaskazini inapendelewa. [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Wengine Dini zao ziliwanyima Fursa ya kuishika Elimu dunia leo wanalialia na kuikumbatia elimu dunia.

Kumbukeni...Azimio la Arusha likija Arusha tyr Arusha ilikuwa na majengo makubwa na shule za kuwatosha watoto wa Chuga.

Someni Historia, Fanyeni tafiti kabla ya kuanza kulialia.



Kweli kabisa
 
Haha unawajua wasukuma na wanaitwa Wanyatuzu hao ndo kikwazo cha wachaga huko Simiyu ukienda Mara kunawakurya Mchaga akifika anakunja mkia
Wanyatuzu sio kikwako kwa wachanga kwa Sumiyu tu bali sehemu zote zenye mishe za biashara huachi kuwakuta miji kama Kahama, Shy, Geita, Mwanza, Igunga, Dar ikitafuta maduka makubwa ya Wasukuma humkosi Mnyantuzu
 
Faida za elimu bure ni kuigeuza Tanzania yote kuwa ni nchi yenye watu wenye kuweza kuhoji.

Siku zote maendeleo huja ikiwa watu wanaanza kuhoji mambo wanayoyaona yakitokea. Na huwezi kuhoji ukaeleweka kama huna elimu.

Tanzania ya miaka 15 ijayo itakuwa na usawa mkubwa sana kimaendeleo, kila ambapo kutafikiwa na elimu, maana yake uwezo wa fikra unakuwa umetajirishwa. Ukishatajirishwa basi kuwepo kwa vitu kama barabara za lami, umeme na maji safi, ni vitu ambavyo upatikanaji wake ni suala la muda tu.
Iwe bure hadi chuo kikuu ndo tujue kuwa hilo ndo lengo lao la kuweza kuhojiwa,mim binafsi sioni umuhimu wake ni bora hata ilivyokuwa kabla ya tamko hilo kwani halijakaa hata kisera na huenda ndo maana hata linachangamotisha watendaji/watekelezaji wake!
 
"Mikoa ya Kaskazini iliendelezwa kwa juhudi ya Wanakaskazini"

Huo ni Ukweli unaoleta furaha kwa Wanakaskazini na Maumivu kwa wana mikoa mingine.

Nitaelezea kwa Ushahidi ulio wazi kabisaaa!

Kwanza msingi wa maendeleo ni ELIMU NA MAARIFA.

Ni wazi kuwa mikoa/makabila yenye wasomi wengi ni ile iliyowapokea wamissionary mapema na kuwakabidhi Ardhi. Katika hiyo ardhi kila walipojenga Kanisa basi walijenga na shule au hospitali nzuri.

Mikoa hiyo ni Kilimanjaro, Arusha, Kagera na Mbeya. Hiyo ilitokea hasa katika miaka ya 1885 - 1900

SASA TUKIACHA ERA HIYO:

Wananchi binafsi wa Arusha na Kilimanjaro wana spirit na asili ya utafutaji wa elimu na mali na Maendeleo kwa juhudi sana (Hustles indeed)

Mifano ifuatayo inathibitisha hayo:-

1) KUJALI ELIMU

Kufikia uhuru wa Tanzania, tayari Kilimanjaro ilikuwa na shule (Kongwe) zenye sekondari kabisa zaidi ya 38 na vyuo baadhi Shule hizo ni kama lyamungo, Majengo, Kleruu College, MUCCOBS, Marangu TC n.k

Hizo zilijengwa kwa juhudi ya Wazazi na chama kahawa KNCU

Arusha kulikuwa tayari na shule zilizojengwa kwa Juhudi za wazazi kama Moringe Sokoine, Mringa Middle School, Monduli TC (ingawa pia serikali iliweka nguvu), Arusha Sec.school, Ilboru Sec. School iliyojengwa pamoja na kanisa la KKKT mwaka 1904

Kwa kuwajuza zaidi Ilboru sec.school na kanisa la Ilboru zilijengwa na wanawake (wamama wa kimasai) kutoka Kimandolu, Levolosi na Ilboru yenyewe, na ushahidi upo.

Pia Chama cha kahawa ARCU ilichangia sana maendeleo ya Arusha.

- Miji midogo wakati huo kama Monduli, Marangu, Machame, Ilboru na Akheri zilijengwa na juhudi ya wazee wa huko.

* Mfano tu, Monduli iliamuliwa kuwa mji mahali ilipo na Wazee wachache wa monduli akiwepo Sokoine.

Can you imagine mwaka 1970 tayari Sokoine alishaanzisha jengo kubwa kuwa Halmashauri ya Monduli kabla hata serikali haijaamua halmashauri iwe wapi.

Kina Lowassa na wengine walikuja tu kuendeleza zaidi.

* Kwa Upande wa Kilimanjaro, hasa Marangu akina Mareale walikuwa Mbali tu kiasi cha kuweza kujiongoza bila serikali ya JMT.

Mji wa Moshi ulikuwa mbaali kimaendeleo siku nyingi.

2) UHUSIANO WA KARIBU WA WANAKASKAZINI

Kingine kilichoiendeleza Kaskazini ni Interaction ya kuoana watu wa Kilimanjaro na wenyeji wa Arusha mjini, kwani wali utilize ardhi vizuri kuanzia enzi na enzi.

(Hata leo hii ukichunguza utagundua watoto wengi wa familia hizo ndio wamejaa serikalini, kwenye migodi ya madini, biashara n.k)

3) KUTOKUTEKWA NA USHIRIKINA

Wanakaskazini hawana asili ya "Ushirikina" na ukisikia mchaga, mmasai ama mwarusha analoga basi ujue amenunua uchawi.

Hakuna uchawi wa kutumia paka, Jini au Vifuu bila faida yoyote.

Mikoa kama Tabora chini ya machifu wao walipaswa kuwa mbali sana kimaendeleo kama alivyofanya chief fundikira (wajomba wa Samwel Sitta) na matunda yanaonekana hadi kuwasomesha akina Samwel Sitta (Hayati)

Mikoa mingine imekuja kuamshwa na hizi shule za kata, halafu inalialia kuwa Kaskazini inapendelewa. [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Wengine Dini zao ziliwanyima Fursa ya kuishika Elimu dunia leo wanalialia na kuikumbatia elimu dunia.

Kumbukeni...Azimio la Arusha likija Arusha tyr Arusha ilikuwa na majengo makubwa na shule za kuwatosha watoto wa Chuga.

Someni Historia, Fanyeni tafiti kabla ya kuanza kulialia.


Mimi naamini kuwa si dini ndizo zinazopelekea kutokuwa na maendeleo bali asili ya watu wa mahali husika...

KAMA ingekuwa dini inapelekea kutokuwa na maendeleo hiyo unayosema kuhusu elimu Dunia...basi Wachaga wa MODIO, MACHAME, MASAMA wengi wangekuwa hawana maendeleo...kwani walio wengi ni wale wenye dini kama ni Muslim ni muslim kweli, kama ni christian ni christian kweli..
Watu tuu na asili zao...Mchaga awe Muslim awe Christian ni mtu wa hapa kazi tuu...
 
Na sasa kibosho ipo pia mkuu njoo uone,mimi nkipanda gari ubungo nakanyaga lami mpaka mgombani kwetu kule kibosho,nikiingia msikitini napiga rakaaa ktk zulia na huo pia upo mgombani huko kibosho
Mbona hata mimi nimeenda bariadi kwetu lami imepita hadi mbele ya nyumba ya bibi na babu? Ujivuni mwingine wa kijinga, hizo lami mmejenga nyie au serikali?
 
Mbona hata mimi nimeenda bariadi kwetu lami imepita hadi mbele ya nyumba ya bibi na babu? Ujivuni mwingine wa kijinga, hizo lami mmejenga nyie au serikali?
bariadi unataka kuifananisha na KILIMANAJRO AU ARUSHA sasa??
 
Back
Top Bottom