Fundisi Muhapa
JF-Expert Member
- Nov 25, 2013
- 4,422
- 2,115
Umeongea vyema. Kuna haja kuamua kama taifa tunasongaje mbele. Na kwa kuanzia, ni lazima ELIMU isambazwe sana sana sana.Eti kasikazini kuna maendeleo, maendeleo yapi hayo? Hebu nendeni tu hata Rwanda kisha mrudi mseme mmefanya maendeleo!
Mnajidanganya sana, tembea uone namna gani nchi yetu iko nyuma sana kimaendeleo, yawezekana sababu kubwa ni kjendekeza ukabila kama ilivyo mwa wenyeji wa Kilimanjaro.
Huwezi kusimama ukasema kasikazini kumeendelea wakati umasikini bado ni uleule. Huduma zote za kijamii ziko hovyo, miundombinu iko hovyo, uchumi wetu uko chini tunaishia kufanya uchuuzi kwa kimsaidia mchina kuuza bidhaa zake.
Ninyi mnaojiona mmeendelea, wasomi na matajiri mlipaswa basi mzalishe badala ya kufanya uchuuzi. Mikoa mingine mingi wanajitahidi kuzalisha.
Ukabila utakuja kuwafanya mjute, fanyeni kazi acheni ukabila. Mngejua kuwa Tz bado tuko mbali sana kimaendeleo mkiwemo na ninyi, mngeleta maendeleo na msingekaa na ukabila.
Sio kununua ndege badala ya kusambaza madawati na vitabu maktaba za shule.
Kisha afya ziimarike. Za akili na mwili. Na mengineyo muhimu. Ndege zitajileta tu.