Unaanza kujisifu sasa, kilicholeta maendeleo kasikazini ni misisngi iliyojengwa na watangulizi; nakubaliana na wengi kwamba elimu ilipewa kipaumbele zaidi na matokeo yake, ajira za msingi zikaenda huko. Lakini sio siri kuna na ujasiri fulani ambao sio wa kawaida kwa baadhi yenu, hasa wanapokabidhiwa mali za umma. Wakasikazini wanafanyakazi zaidi, sio siri, lakini nionyeshe viwanda ambavyo unawezasema vimebuniwa na wakazi wa huko na kuwaletea maendeleo watu wengine. Nitajie wagunduzi bora kabisa ambao wameiletea nchi sifa na heshima taifa hili. Maendeleo ya kweli yanaambukiza, wa kasikazini wameambukiza wapi? Dodoma ni majirani zenu, Singida, Tanga, Mara mbona hawa kuaambukiza watu wengine? Kasikazini imendelezwa na mali ya watanzania wote.
Nihitimishe kwa kusema kasikazini imeendelezwa na msingi bora wa elimu na ujasiri wa kupita kiasi kwa wale wanaokabidhiwa mali za umma.
..una mchango mzuri tu. Na mimi nakubaliana na 50% ya ulichoandika.
..Kilimanjaro imebahatika kuwa na hali ya hewa nzuri, mazao ya biashara, na kupakana na Kenya ambayo ina uchumi mkubwa hapa Afrika Mashariki.
..Eneo lingine lenye mazingira kama ya Kilimanjaro ni mkoa wa Mbeya. Hali ya hewa ni nzuri. Wana mazao ya Kahawa na Mpunga. Wanapakana na Zambia na Malawi.
..Hakuna tofauti ya kimaendeleo kati ya mikoa hiyo miwili.
..Ukiangalia uhalisia wa miradi ya maendeleo baada ya UHURU serikali
imepeleka miradi mikubwa maeneo mengine ya Tz kuliko ilivyopeleka Kilimanjaro.
..ukiuliza wachangiaji humu ndani serikali imepeleka mradi gani wa maendeleo Kilimanjaro tangu tupate uhuru wachache wataweza kuitaja.
..lakini zaidi ukiuliza ni mradi gani umepelekwa Kilimanjaro na haukustahili kupelekwa huko hakuna mradi hata mmoja.
..Sasa ndiyo hapo ninapotofautiana na hicho unachoita " ujasiri " wa watendaji toka Kilimanjaro waliopewa dhamana ktk serikali zetu tangu tupate uhuru.
..Kama ni " ujasiri" hebu nionyeshe mwenyeji wa Kilimanjaro aliyeuza nyumba za serikali nchi nzima. I mean the whole country, mtu anachukua uamuzi wa kuuza nyumba za serikali tena kwa bei ya hasara.
..mwaka 1971 tuliamua kuhamia Dodoma. Taifa halikuwa na uwezo wa kiuchumi kuchukua uamuzi kama ule. Wala hilo halikuwa hitaji la wananchi wa Dodoma wala Taifa.
..Fedha zilizofujwa Dodoma zingeweza kusaidia miradi ambayo ni sustainable maeneo mengi ya nchi yetu na hata Dodoma kwenyewe.
..Kuhusu kutaja watu wa Kilimanjaro ambao wamekuwa +ve influence mahali pengine Tz sidhani kama ni sahihi. Sidhani kama ni vizuri kutaja majina ya watu, unless mhusika amekutuma.
..Lakini kama unapenda kujisomea matukio makubwa ya nchi hii kama harakati za uhuru, vita vya kagera, etc etc huwezi kukosa michango ya wananchi wa Kilimanjaro au kanda ya kaskazini.
..Umetumia neno "ujasiri" ktk mada yako. Sasa kuna "ujasiri" ulioenea hapa nchini wa kushambulia integrity ya wananchi wa Kilimanjaro.
..imekuwa ni kitu cha kawaida kulaumu, kutuhumu, na kuzusha, dhidi ya wananchi wa Kilimanjaro na sasa kanda ya kaskazini.
..Tumefika mahali people are not held to the same standards. Kwa mfano, mwanasiasa mwenyeji wa Kilimanjaro au kaskazini anatakiwa achunge kauli na matendo yake, huku wale wa maeneo mengine wakiachwa wadhalilishe na kubeza wananchi.
..Hebu rejea kauli ya "kila mtu abebe msalaba wake." Sasa linganisha ilivyopokelewa ilipotolewa na mwanasiasa toka Kilimanjaro vs ilipotolewa na mwanasiasa toka Geita.
..Hii nchi ni yetu sote.
cc
Nguruvi3