Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Sasa matajiri wa Dar si ni wenye asili ya Oman na India?

Au sio kina Dewji, Bakhresa, Manji n.k ?

Kuna Mzaramo tajiri hasa hapo Dsm?
Haijalishi. Muhimu ni kauli kila mkoa ukitaja matajiri 10 wa4 wa kaska. Sasa taja wa dar
 
Ok, hiyo nikuwa siifahamu. Chuo kimejengwa kwa msaada wa Denmark miaka ya 70. Mwenye jina Dr Klerruu kweli alikuwa mchaga.?
yap kleruu n wachaga wa nwika
jina kamili n Dr Wilbert kleruu alikuwa Mkuu wa mkoa wa iringa miaka ya 70, aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka 1971, na mkulima aitwae mwamwindi kisa mambo ya ujamaa
 
Kama hii ndio sababu kubwa basi sio juhudi za wana wa kaskazini.


hapo kwenye 'juhudi sana' ni zipi hizo ambazo wengine hawatumii? Ila Wachaga nadhani wana culture kama ya western europe kwa maana ya kwamba dependence hawaipi nafasi kabisa. Mfano, kama unahitaji kitu fulani ambacho shangazi yako anacho kwenye biashara yake, kama hauna fedha ya kutosha kukinunua kwa bei aliyoiweka, hupati katu mpaka ukamilishe fedha.



Kwa hiyo ukiwa na faida wanatumia hiyo mipaka?



Kama sababu kubwa ilikuwa ni elimu iliyoletwa na wamissionari iweje Tabora iwe nyuma au wengi wao hawakuichangamkia hiyo elimu? Kuna mzee mmoja wa Tabora niliwahi kumsikia akisema waingereza walivyojenga Tabora Boys walikuwa wanaenda kwenye nyumba za wenyeji kuchukua watoto kwa ajili ya kuwa-enrol lakini cha kushangaza watoto walikuwa wanakimbia!!!
Juhudi nimezielezea kwa mifano kwny mada
 
n kweli pia kuna mwaka wailtaka kwenda umoja wa nataifa kutaka kujutenga yaan kask ijitenge maana makabila mengine yalikuwa nyuma wailona yanawapotezea mda/kuwanyonya
Hujuasoma historia vizuri. Umeongea km mtu wa kijiweni. We mrombo ee?
 
Kama hii ndio sababu kubwa basi sio juhudi za wana wa kaskazini.


hapo kwenye 'juhudi sana' ni zipi hizo ambazo wengine hawatumii? Ila Wachaga nadhani wana culture kama ya western europe kwa maana ya kwamba dependence hawaipi nafasi kabisa. Mfano, kama unahitaji kitu fulani ambacho shangazi yako anacho kwenye biashara yake, kama hauna fedha ya kutosha kukinunua kwa bei aliyoiweka, hupati katu mpaka ukamilishe fedha.



Kwa hiyo ukiwa na faida wanatumia hiyo mipaka?



Kama sababu kubwa ilikuwa ni elimu iliyoletwa na wamissionari iweje Tabora iwe nyuma au wengi wao hawakuichangamkia hiyo elimu? Kuna mzee mmoja wa Tabora niliwahi kumsikia akisema waingereza walivyojenga Tabora Boys walikuwa wanaenda kwenye nyumba za wenyeji kuchukua watoto kwa ajili ya kuwa-enrol lakini cha kushangaza watoto walikuwa wanakimbia!!!
Inawezekana, ndio maana nikasema kuwa watu wa Tabora walikuwa na opportunity kubwa miaka ilee

Kumbuka hata kibiashara wao, wayao na wakamba ndio walishika all major routes za East Africa.

Mimi baba yangu alisoma Tabora boys pia miaka ya 70's
 
yap kleruu n wachaga wa nwika
jina kamili n Dr Wilbert kleruu alikuwa Mkuu wa mkoa wa iringa miaka ya 70, aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka 1971, na mkulima aitwae mwamwindi kisa mambo ya ujamaa
Huyo Kleruu nae alifanya kituko sana kumfuata mtu Xmas kudai shamba?
 
Hayo maendeleo yako wapi??

Mbona mwanza imepata hadhi ya kuwa jijji mwaka 2000 lakini Kilimanjaro mpaka leo ni manispaa??
Pamoja na ujiji Mwanza inashika nafasi ya 5 kwa utajiri wkt K'njaro ambapo Moshi ni makao Makuu na ni manisipa inashika nafasi ya 2 takwimu 2016/17 katika bunge la bajeti,vgezo ni kipato cha MTU mmoja mmoja,kuingiza pato kwenda serikali kuu,miundombinu yani mahospitali,mashule na barabara,me sitoki K'njaro ila K'njaro iko kuu pamoja na watu wake apo hamna ubishi.
 
Nimewaelewa na tunapaswa kujifunza jema kama linafanywa na wenzio,ukikataa wewe mjinga,na uzuri toka jamii ilipogundua kua elimu ni muhimu hakuna hata jamii moja imekataa elimu kwa makusudi,Kwa hiyo mi sioni sababu ya watu wa moshi na Arushs kuwananga wenzenu kwa kukosa elimu,ni fursa mlizikuta kutoka kwa wamisionary mkaendelea nazo not otherwise,sasa kule kusoma soma ndio kukatengeneza tabaka la watu mnaojali elimu,hao mnaowasema kuwa walikataa elimu ya duniani ni kwa kua mmeamua kutumia propaganda hiyo kuwapaka matope wenzenu,mnajua jitihada walizozifanya kujikwamua kielimu kuanzia enzi za ukoloni hadi sasa? Lindi na Mtwara ndio mikoa pekee ambayo ienasemekana kwa elimu iko chini kabisa,lakini pia ni watu waliojitahidi sana kufanya mikoa yao iendelee kuwa juu kielimu licha ya jitihada zao kugomga ukuta.Kwa bahati mbaya mikoa yetu toka ilivyoachwa na wamisionari mpaka leo hii imeendelea kubakia kama ilivyoachwa,barabara nyingi ni zile zile nk,sisi tumeboresha tu vichache,ila Muda unakuja jamii haitakua na matabaka tena wala ukanda kwa kutumia propagnda za kielimu,mikoa ya mkoloni ni ileile mpaka leo mbeya,bukoba nk,na hata mnavyosema kaskazini bado ni kauli za kibaguzi,kaskazini gani yenye maendeleo? kaskazini inabebwa na mikoa mitatu tuu arusha,bukoba na moshi tuu? hivi moshi na Tanga kuna umbali gani mtu akashindwe kupata elimu moshi au arusha,yaani moshi iwe juu kimaendeleo Tanga jirani iwe masikini?
 
Eti kasikazini kuna maendeleo, maendeleo yapi hayo? Hebu nendeni tu hata Rwanda kisha mrudi mseme mmefanya maendeleo!
Mnajidanganya sana, tembea uone namna gani nchi yetu iko nyuma sana kimaendeleo, yawezekana sababu kubwa ni kjendekeza ukabila kama ilivyo mwa wenyeji wa Kilimanjaro.
Huwezi kusimama ukasema kasikazini kumeendelea wakati umasikini bado ni uleule. Huduma zote za kijamii ziko hovyo, miundombinu iko hovyo, uchumi wetu uko chini tunaishia kufanya uchuuzi kwa kimsaidia mchina kuuza bidhaa zake.
Ninyi mnaojiona mmeendelea, wasomi na matajiri mlipaswa basi mzalishe badala ya kufanya uchuuzi. Mikoa mingine mingi wanajitahidi kuzalisha.
Ukabila utakuja kuwafanya mjute, fanyeni kazi acheni ukabila. Mngejua kuwa Tz bado tuko mbali sana kimaendeleo mkiwemo na ninyi, mngeleta maendeleo na msingekaa na ukabila.
 
HAWA WATU WA KASKAZ NI WAJIVUNI TU MAENDELEO WALIYOPATA SIO YA KUJIVUNIA SANA KWANI BADO KUNA KUNDI KUBWA LA WASIOSOMA NA MASIKINI WALIONDELEA NI WACHACHE YAPO MAKABILA WATU WANA PESA LAKINI KIMYA KAMA WAPEMBA NA WAKINGA.HUKO HUKO KASKAZ NDO KUNA WATU WANAVAA NGOZI NA WANALALA NYUMBA MOJA NA NGOMBE
kwanza Arusha na Moshi kuna maendeleo gani ya kutisha mi huwa sioni tofauti ya mikoa hyo na mingine,propaganda na ubaguzi ndio vinavyowasumbua
 
hapo
Eti kasikazini kuna maendeleo, maendeleo yapi hayo? Hebu nendeni tu hata Rwanda kisha mrudi mseme mmefanya maendeleo!
Mnajidanganya sana, tembea uone namna gani nchi yetu iko nyuma sana kimaendeleo, yawezekana sababu kubwa ni kjendekeza ukabila kama ilivyo mwa wenyeji wa Kilimanjaro.
Huwezi kusimama ukasema kasikazini kumeendelea wakati umasikini bado ni uleule. Huduma zote za kijamii ziko hovyo, miundombinu iko hovyo, uchumi wetu uko chini tunaishia kufanya uchuuzi kwa kimsaidia mchina kuuza bidhaa zake.
Ninyi mnaojiona mmeendelea, wasomi na matajiri mlipaswa basi mzalishe badala ya kufanya uchuuzi. Mikoa mingine mingi wanajitahidi kuzalisha.
Ukabila utakuja kuwafanya mjute, fanyeni kazi acheni ukabila. Mngejua kuwa Tz bado tuko mbali sana kimaendeleo mkiwemo na ninyi, mngeleta maendeleo na msingekaa na ukabila.
ndio huwa pananishangaza hata mimi
 
HAWA WATU WA KASKAZ NI WAJIVUNI TU MAENDELEO WALIYOPATA SIO YA KUJIVUNIA SANA KWANI BADO KUNA KUNDI KUBWA LA WASIOSOMA NA MASIKINI WALIONDELEA NI WACHACHE YAPO MAKABILA WATU WANA PESA LAKINI KIMYA KAMA WAPEMBA NA WAKINGA.HUKO HUKO KASKAZ NDO KUNA WATU WANAVAA NGOZI NA WANALALA NYUMBA MOJA NA NGOMBE
Wewe acha kujidanganya nenda kaskazn ujionee.....!
 
Hakuna Mkaskazi aliefanya biashara na akawa Prominent in the Precolonial period! Centre of trade were at the central line! Hujui historia ww
Nilisema hivyo kumaanisha kuwa Kaska walianza kuparangana kabla ya ukoloni. Kwamba hawakua prominent ni jambo jema zaidi.

Kumbe hata alie chini leo kuna mambo akifanya leo kesho atakua juu kuzidi alie juu leo. Ndo uzuri wa uzi kama huu.

Turudi duniani. Taifa la China liliwahi kuwa na nguvu kuzidi ya ulaya. Walidominate Asia yote. Kumbuka silk road na opium wars. Then akaja mjamaa Mao se Tung na watawala wengine kabla yake (mfano yule aliechoma vitabu vyote na maandishi yote).

Hao watawala waliwarudisha nyuma sana kiasi mataifa ya ulaya na sasa marekani yakatamalaki. Juzi kati wameamua kukumbatia ELIMU ubepari na ujasiariamali wanafunguka.

Wakiachia na demokrasia China hawatashikika. Ila hilo ndo kilema chao. Miaka zaidi ya 5000 hawajui demokrasia ikoje. Ni ufalme au ujamaa. Kwisha!!

So madhali bado tuu "wachanga", tujifunze ndani kwa ndani na huko duniani.
 
Nimewaelewa na tunapaswa kujifunza jema kama linafanywa na wenzio,ukikataa wewe mjinga,na uzuri toka jamii ilipogundua kua elimu ni muhimu hakuna hata jamii moja imekataa elimu kwa makusudi,Kwa hiyo mi sioni sababu ya watu wa moshi na Arushs kuwananga wenzenu kwa kukosa elimu,ni fursa mlizikuta kutoka kwa wamisionary mkaendelea nazo not otherwise,sasa kule kusoma soma ndio kukatengeneza tabaka la watu mnaojali elimu,hao mnaowasema kuwa walikataa elimu ya duniani ni kwa kua mmeamua kutumia propaganda hiyo kuwapaka matope wenzenu,mnajua jitihada walizozifanya kujikwamua kielimu kuanzia enzi za ukoloni hadi sasa? Lindi na Mtwara ndio mikoa pekee ambayo ienasemekana kwa elimu iko chini kabisa,lakini pia ni watu waliojitahidi sana kufanya mikoa yao iendelee kuwa juu kielimu licha ya jitihada zao kugomga ukuta.Kwa bahati mbaya mikoa yetu toka ilivyoachwa na wamisionari mpaka leo hii imeendelea kubakia kama ilivyoachwa,barabara nyingi ni zile zile nk,sisi tumeboresha tu vichache,ila Muda unakuja jamii haitakua na matabaka tena wala ukanda kwa kutumia propagnda za kielimu,mikoa ya mkoloni ni ileile mpaka leo mbeya,bukoba nk,na hata mnavyosema kaskazini bado ni kauli za kibaguzi,kaskazini gani yenye maendeleo? kaskazini inabebwa na mikoa mitatu tuu arusha,bukoba na moshi tuu? hivi moshi na Tanga kuna umbali gani mtu akashindwe kupata elimu moshi au arusha,yaani moshi iwe juu kimaendeleo Tanga jirani iwe masikini?
Punguza hasira bro
 
"Mikoa ya Kaskazini iliendelezwa kwa juhudi ya Wanakaskazini"

Huo ni Ukweli unaoleta furaha kwa Wanakaskazini na Maumivu kwa wana mikoa mingine.

Nitaelezea kwa Ushahidi ulio wazi kabisaaa!

Kwanza msingi wa maendeleo ni ELIMU NA MAARIFA.

Ni wazi kuwa mikoa/makabila yenye wasomi wengi ni ile iliyowapokea wamissionary mapema na kuwakabidhi Ardhi. Katika hiyo ardhi kila walipojenga Kanisa basi walijenga na shule au hospitali nzuri.

Mikoa hiyo ni Kilimanjaro, Arusha, Kagera na Mbeya. Hiyo ilitokea hasa katika miaka ya 1885 - 1900

SASA TUKIACHA ERA HIYO:

Wananchi binafsi wa Arusha na Kilimanjaro wana spirit na asili ya utafutaji wa elimu na mali na Maendeleo kwa juhudi sana (Hustles indeed)

Mifano ifuatayo inathibitisha hayo:-

1) KUJALI ELIMU

Kufikia uhuru wa Tanzania, tayari Kilimanjaro ilikuwa na shule (Kongwe) zenye sekondari kabisa zaidi ya 38 na vyuo baadhi Shule hizo ni kama lyamungo, Majengo, Kleruu College, MUCCOBS, Marangu TC n.k

Hizo zilijengwa kwa juhudi ya Wazazi na chama kahawa KNCU

Arusha kulikuwa tayari na shule zilizojengwa kwa Juhudi za wazazi kama Moringe Sokoine, Mringa Middle School, Monduli TC (ingawa pia serikali iliweka nguvu), Arusha Sec.school, Ilboru Sec. School iliyojengwa pamoja na kanisa la KKKT mwaka 1904

Kwa kuwajuza zaidi Ilboru sec.school na kanisa la Ilboru zilijengwa na wanawake (wamama wa kimasai) kutoka Kimandolu, Levolosi na Ilboru yenyewe, na ushahidi upo.

Pia Chama cha kahawa ARCU ilichangia sana maendeleo ya Arusha.

- Miji midogo wakati huo kama Monduli, Marangu, Machame, Ilboru na Akheri zilijengwa na juhudi ya wazee wa huko.

* Mfano tu, Monduli iliamuliwa kuwa mji mahali ilipo na Wazee wachache wa monduli akiwepo Sokoine.

Can you imagine mwaka 1970 tayari Sokoine alishaanzisha jengo kubwa kuwa Halmashauri ya Monduli kabla hata serikali haijaamua halmashauri iwe wapi.

Kina Lowassa na wengine walikuja tu kuendeleza zaidi.

* Kwa Upande wa Kilimanjaro, hasa Marangu akina Mareale walikuwa Mbali tu kiasi cha kuweza kujiongoza bila serikali ya JMT.

Mji wa Moshi ulikuwa mbaali kimaendeleo siku nyingi.

2) UHUSIANO WA KARIBU WA WANAKASKAZINI

Kingine kilichoiendeleza Kaskazini ni Interaction ya kuoana watu wa Kilimanjaro na wenyeji wa Arusha mjini, kwani wali utilize ardhi vizuri kuanzia enzi na enzi.

(Hata leo hii ukichunguza utagundua watoto wengi wa familia hizo ndio wamejaa serikalini, kwenye migodi ya madini, biashara n.k)

3) KUTOKUTEKWA NA USHIRIKINA

Wanakaskazini hawana asili ya "Ushirikina" na ukisikia mchaga, mmasai ama mwarusha analoga basi ujue amenunua uchawi.

Hakuna uchawi wa kutumia paka, Jini au Vifuu bila faida yoyote.

Mikoa kama Tabora chini ya machifu wao walipaswa kuwa mbali sana kimaendeleo kama alivyofanya chief fundikira (wajomba wa Samwel Sitta) na matunda yanaonekana hadi kuwasomesha akina Samwel Sitta (Hayati)

Mikoa mingine imekuja kuamshwa na hizi shule za kata, halafu inalialia kuwa Kaskazini inapendelewa. [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Wengine Dini zao ziliwanyima Fursa ya kuishika Elimu dunia leo wanalialia na kuikumbatia elimu dunia.

Kumbukeni...Azimio la Arusha likija Arusha tyr Arusha ilikuwa na majengo makubwa na shule za kuwatosha watoto wa Chuga.

Someni Historia, Fanyeni tafiti kabla ya kuanza kulialia.
acha kupotosha mkuu,historia tunaijua,usiseme mikoa ya Arusha na moshi tena usiseme kaskazini maana utakua unatuongopea,mlibebwa na wamisionari kielimu mkafanikiwa kuingia serikalini na kutumia rasilimali za nchi kuitengeneza mikoa ya hiyo miwili,bukoba sijafika ila moshi na arusha mna maendeleo ya kawaida sana,mliowengi shule yenyewe hamjaenda,jamii za kawaida tu kama watanzania wengine,mmejaaliwa sana ubaguzi kujiona nyie mko juu lakini tukifuata tathmini za kisayansi hata nyie kimaendeleo bado mko taabani tu
 
Eti kasikazini kuna maendeleo, maendeleo yapi hayo? Hebu nendeni tu hata Rwanda kisha mrudi mseme mmefanya maendeleo!
Mnajidanganya sana, tembea uone namna gani nchi yetu iko nyuma sana kimaendeleo, yawezekana sababu kubwa ni kjendekeza ukabila kama ilivyo mwa wenyeji wa Kilimanjaro.
Huwezi kusimama ukasema kasikazini kumeendelea wakati umasikini bado ni uleule. Huduma zote za kijamii ziko hovyo, miundombinu iko hovyo, uchumi wetu uko chini tunaishia kufanya uchuuzi kwa kimsaidia mchina kuuza bidhaa zake.
Ninyi mnaojiona mmeendelea, wasomi na matajiri mlipaswa basi mzalishe badala ya kufanya uchuuzi. Mikoa mingine mingi wanajitahidi kuzalisha.
Ukabila utakuja kuwafanya mjute, fanyeni kazi acheni ukabila. Mngejua kuwa Tz bado tuko mbali sana kimaendeleo mkiwemo na ninyi, mngeleta maendeleo na msingekaa na ukabila.
Punguza hasira
 
Nimewaelewa na tunapaswa kujifunza jema kama linafanywa na wenzio,ukikataa wewe mjinga,na uzuri toka jamii ilipogundua kua elimu ni muhimu hakuna hata jamii moja imekataa elimu kwa makusudi, ...

Zipo jamii za hivyo. Wachina ni mojawapo. Aliwahi tokea mtawala maelfu ya miaka huko kale akachoma vitabu na maandiko yao yote.

Alichoua sio elimu tu. Bali kumbukumbu zote, kanuni zote, teknolojia na kila walichokua wameshafanikisha kilipotea. Pia aliua wasomi wote waliopingana nae au kuwafumba midomo na kuwafungia magerezani.

Nini kilitokea baada ya UJINGA huo?

Wachina waliowahi kutawala Japan na Asia yote wakapoteza teknolojia ya bunduki. Japan wakaiboresha hiyo teknolojia hadi kuja kuitawala China (kumbuka Manchuria).

So kuna jamii huwa wanakataa ELIMU na matokeo yake huwa mara zote ni hasi kwao.
 
Back
Top Bottom