Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Mleta mada uko sahihi, mm natoka moja ya makabila ya mikoa ya mwisho kimaendeleo, my broos wana nafasi kubwa inchi hii nikiwatajia mwaweza shangaa, lkn up to the moment nipo street nahustle kama vile si ndugu yao japo ninavigezo vyote! Nimewaambia kama bac mnamuogopa Magu nipeni capital mm nifanye zangu ujasiliamali nimewaandikia hadi mpango mkakati lkn wapi!

Natamani wangekuwa wachaga, lkn ndo hvo!
Napigika na chaki kwenye kituo kimoja cha tuition hapa mjini, jamaa wanakula viyoyizo. Hawana mda na mm!
Natamani nchii hii ingekuwa ya wachagaa watupu, may be wangekuwa mbali!!
We sio mtu mzuri
 
Mkuu uyo poyoyo hajui chochote kuhusu Northern Zone, achana nae..
Huyu haeleweki, yupo Mwanza iliyopata umeme wa vijijini juzi analinganisha na Moshi hii na Arusha.
 
Lakini nitoe angalizo kwa ukuaji wa miji ya wilayani naona kanda ya kasikazini imesimama/imedumaa sana.
Kwa miaka 20 ya sasa yaani tangu 1995 tumeshuhudia miji mingi ikikua sehemu mbali mbali kuliko miji ya kasikazini mfano Tunduma, Kahama, Ifakara, Tarime, Bariadi, Mpanda, Geita, na nk lakini mji ya kasikazini in duni na imedumaa.

Kuhusu Shule miaka Ishirini ya sasa tumeshuhudia shule za Kasikazini zikidiwa na kutupiliwa mbali na shule za Mwanza, Mbeya Na Kagera. Check matokeo ya Form four na darasa la saba. Leo hakuna mtu anauchu wa kupeleka mwanae akasome Moshi kama ilivyokua zamani.

Katika vyuo vikuu hakuna dominance ya kanda yoyote mwenye mawazo hayo amesoma chuo miaka ya 90.

Zaidi watu wa Arusha wamevalishwa lemba la ukoka na watu wa Moshi. Kilimanjaro kuna social services Arusha hakuna. Wasisifie gari za jirani.

Jamani Wasonjo nao waseme wako juu haha...
hapa umeropoka masta
 
Hayo maeneoni ya Ukanda wa Kaskazini au ni ya MOSHI.

Hii post inachanganya. Inaongelea maendeleo kanda ya kaskazini ilhali mifano yote ni moshi na kwa mbali Arusha mjini.

Hivi mikoa ya Tanga na Manyara ipo ukanda gani?

Wamabg'ati Watindiga na Wairak wapo kanda ipi na vipi maendeleo yao yakoje.

Tukiongelea ukanda tuongelee maeneo yote na si wilaya moja.

Hivi kipato cha wilaya za same na mwanga kwa pamoja kinaifikia wilaya ya kahama au hata ya mahenge.

Huu uzi ubadilike uwe specific. Badala ya maneno UKANDA WA KASKAZINI iandikwe HIMAYA YA WACHAGGA ambako mgeni haruhusiwi kumiliki ardhi kama ilivyo Pemba.
Hivi we waIraqw unawachukulia kirahisi ee? Ndo waliomtoa Dr. Slaa, Sumaye n.k.

Achana na siasa. Umeshaona jamii yao kjjn wanavyoishi vzr? Wanalimia matrekta na wanavunia combine harvesters. Unadhani wa kawaida hao?

Miji yao (homesteads) ni ya kudumu na ni kwa tofali za kuchoma na bati. Imetengwa vzr sehemu za mifugo bustani n.k.

Btw......... waIraqw ndo wamefundisha wachagga kula mbogamboga. Na nchi nzima pia. Ni kwa kupenda kwao kulima mbogamboga tumeneemeka kama taifa. Na ndio kilichowapa akili kubwa. Tena ukiziona bustani ziivyopangiliwa....... we mtu wewe.

Haishii hapo. WaIraqw na waFiomi ndo kabila la zamani zaidi hapa Tz. Huenda ndo maana fuvu la mtu wa kale sana lilipatikana Ngorongoro. Next to their homelands.

Soma historia na jifunze
 
Wewe sijui wa wapi?

Wasonjo wapo manyara sio Arusha.

Arusha ina waarusha,/wamasai wachaga na wameru

Nenda kaangalie maisha yao, kaangalie nyumba zao, kaangalie miundo mbinu halafu ulinganishe na huko kwenu.
Lakini ni jamii ya kaskazini.

Kuhusu waSonjo. Ndio jamii yenye mifumo ya umwagiliaji ya kale sana. Nenda soma kuhusu "Engaruka basin and the lost tribe". Google tu pia utapata more info.

Leo hii tunapohangaika kuhusu kilimo cha umwagiliaji, wao walishajenga "jiji" kupitia hiyo. Wasonjo hao. Sehemu ya kaskazini
 
Mkuu ni kweli lile lilikuwa taifa tayari likiwa na kila kitu, hata ukigogle utakuta bendera yenye nembo ya mlima Kilimanjaro ikiwa na maneno " Lukuwawie na Ruwa" yakiwa na maana ambayo ni tujikumbatie na Mungu
Hivi ilikua mlima klm au Chui na mgomba?
 
Nadhani ukilinganisha kanda hizi mbili utaona ni ipi inaendelea kwa kasi. Pia utaona mabadiliko makubwa hasa kwenye sekta ya elimu umeme na makazi.

Pia ukiongelea hizi kanda uwe specific unaongelea mji au eneo gani.

Ki mkoa hakuna mkoa wa kaskazini unaoikaribia Mwanza kama mkoa kwa kila kitu. Labda barabara.

Kwa ufupi. Ukiondoa MOSHI ambayo wana lami hadi milimani huko machame. Hakuna maendeleo ya zaidi yaliyopo kanda ya kaskazini ambayo kanda ya ziwa hawana KWA UJUMLA WAKE.

Iwe ni elimu maji ujenzi wa nyumba za kuishi na za biashara. kipato yaani utajiri wa mmoja mmoja au hata umeme na afya.

Tukubali kwamba wasukuma wanajenga kwao kwa kasi ya ajabu na miji ya usukumani inakua kwa kasi sana.
Na sasa ni zamu ya wasukuma kucement nguvu yao kimaendeleo. Hata vyuoni kwa sasa ni wengi sana na wanafanya vizuri.

Nawapenda maana wameona kilichowalet down ni ELIMU ELIMU ELIMU. Mwanza inakua kwa kasi ya ajabu na in 20yrs Dar itaiskia mwz
 
... Kuna mzee mmoja wa Tabora niliwahi kumsikia akisema waingereza walivyojenga Tabora Boys walikuwa wanaenda kwenye nyumba za wenyeji kuchukua watoto kwa ajili ya kuwa-enrol lakini cha kushangaza watoto walikuwa wanakimbia!!!

Umang'atini waliwah pelekewa shule ya watu wazima. Wakiwa darasani dikidiki akapita. Mwalimu hakuamini jamaa wiki nzima hawajarudi class. Hadi leo
 
Huyo ni mlinzi wako lakini ana kaka yake yupo mererani ana mgodi au ana mabucha ya nyama

Wasukuma waliopo Arusha wanalisha ng'ombe hawa wa sedentary halafu kaka zao wapo wanalima na kupalilia majaruba ya mpunga.
Hao wasukuma watasomesha watoto. ELIMU ELIMU ELIMU. Kisha watakuza mitaji na kufungua biashara. Before you know it, mshapitwa.

Msilewe sifa za kale. Focus on building more wealth and opportunities.
 
Haha Mlinzi wangu toka Arusha Siku moja aliniambia anadawa ya kukuza dudu nikamjibu langu linanitosha haha.

Ila nawapongenza watu wa Arusha kitu kimoja ni vigumu kupata house gal toka Arusha.
We jamaa balaa....... hadi dudu umehusisha?
 
Kama hii ndio sababu kubwa basi sio juhudi za wana wa kaskazini.


hapo kwenye 'juhudi sana' ni zipi hizo ambazo wengine hawatumii? Ila Wachaga nadhani wana culture kama ya western europe kwa maana ya kwamba dependence hawaipi nafasi kabisa. Mfano, kama unahitaji kitu fulani ambacho shangazi yako anacho kwenye biashara yake, kama hauna fedha ya kutosha kukinunua kwa bei aliyoiweka, hupati katu mpaka ukamilishe fedha.



Kwa hiyo ukiwa na faida wanatumia hiyo mipaka?



Kama sababu kubwa ilikuwa ni elimu iliyoletwa na wamissionari iweje Tabora iwe nyuma au wengi wao hawakuichangamkia hiyo elimu? Kuna mzee mmoja wa Tabora niliwahi kumsikia akisema waingereza walivyojenga Tabora Boys walikuwa wanaenda kwenye nyumba za wenyeji kuchukua watoto kwa ajili ya kuwa-enrol lakini cha kushangaza watoto walikuwa wanakimbia!!!
Hapana sijaelezea kuwa umisionary pekee ndio sababu ya maendeleo huko
 
Back
Top Bottom