Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ni wazi kuwa mikoa/makabila yenye wasomi wengi ni ile iliyowapokea wamissionary mapema na kuwakabidhi Ardhi. Katika hiyo ardhi kila walipojenga Kanisa basi walijenga na shule au hospitali nzuri.

Kama hii ndio sababu kubwa basi sio juhudi za wana wa kaskazini.

Wananchi binafsi wa Arusha na Kilimanjaro wana spirit na asili ya utafutaji wa elimu na mali na Maendeleo kwa juhudi sana (Hustles indeed)
hapo kwenye 'juhudi sana' ni zipi hizo ambazo wengine hawatumii? Ila Wachaga nadhani wana culture kama ya western europe kwa maana ya kwamba dependence hawaipi nafasi kabisa. Mfano, kama unahitaji kitu fulani ambacho shangazi yako anacho kwenye biashara yake, kama hauna fedha ya kutosha kukinunua kwa bei aliyoiweka, hupati katu mpaka ukamilishe fedha.

Hakuna uchawi wa kutumia paka, Jini au Vifuu bila faida yoyote.

Kwa hiyo ukiwa na faida wanatumia hiyo mipaka?

Mikoa kama Tabora chini ya machifu wao walipaswa kuwa mbali sana kimaendeleo kama alivyofanya chief fundikira (wajomba wa Samwel Sitta) na matunda yanaonekana hadi kuwasomesha akina Samwel Sitta (Hayati)

Kama sababu kubwa ilikuwa ni elimu iliyoletwa na wamissionari iweje Tabora iwe nyuma au wengi wao hawakuichangamkia hiyo elimu? Kuna mzee mmoja wa Tabora niliwahi kumsikia akisema waingereza walivyojenga Tabora Boys walikuwa wanaenda kwenye nyumba za wenyeji kuchukua watoto kwa ajili ya kuwa-enrol lakini cha kushangaza watoto walikuwa wanakimbia!!!
 
Hivyo unalinganisha Mwanza na Arusha au Moshi. Hahaha kwa taarifa yako in jiji la Arusha tu ndo kunanyumba za miti na matope. Nenda kata ya ungalimited
Kwenye comment yangu kuna sehemu nimetaja Arusha? Acha kukurupuka
 
mada ya kikabila hii, ku class watanzania kulingana na makabila ndio root ya chuki na ubaguzi wa kikabila
On the contrary, mwenye kuwaza vema mada hii ni chachu ya kufanya vyema. Muige alietangulia mazuri yake. Mkosoe anapokosea na jifunze kupaboresha.
 
Kwenye comment yangu kuna sehemu nimetaja Arusha? Acha kukurupuka
Hivyo unakubali Mwanza is better than Arusha. Na unapinga Mwanza haizidi Moshi.

OK nakuunga mukono in context of proportions. Asilimia ya watu wengi wa mkoa wa Kilimanjaro wanapata social services kuliko Mwanza lakini ukisema Arusha ntakataa.
 
Nadhani ukilinganisha kanda hizi mbili utaona ni ipi inaendelea kwa kasi. Pia utaona mabadiliko makubwa hasa kwenye sekta ya elimu umeme na makazi.

Pia ukiongelea hizi kanda uwe specific unaongelea mji au eneo gani.

Ki mkoa hakuna mkoa wa kaskazini unaoikaribia Mwanza kama mkoa kwa kila kitu. Labda barabara.

Kwa ufupi. Ukiondoa MOSHI ambayo wana lami hadi milimani huko machame. Hakuna maendeleo ya zaidi yaliyopo kanda ya kaskazini ambayo kanda ya ziwa hawana KWA UJUMLA WAKE.

Iwe ni elimu maji ujenzi wa nyumba za kuishi na za biashara. kipato yaani utajiri wa mmoja mmoja au hata umeme na afya.

Tukubali kwamba wasukuma wanajenga kwao kwa kasi ya ajabu na miji ya usukumani inakua kwa kasi sana.
Acha mzaha wewe, huwezi linganisha vijiji vya uchagani na vya kisukuma vilivyoanza kupata umeme wa REA
 
Hii nchi ni maskini. Hayo maendeleo mnayaongelea siyaoni hata Dar sembuse Kaskazini! Tembeni dunia mgundue jinsi mnavyojitambia ujinga.
Hata kwenye wajinga kabisa kuna mjanja wao. Nadhani ndo mawazo ya humu. Wajinga tunasaidiana ilikuaje mwenzetu akapata 10 ya 100?
 
Acha mzaha wewe, huwezi linganisha vijiji vya uchagani na vya kisukuma vilivyoanza kupata umeme wa REA
Umenikumbusha ule usemi wa Mchungaji Peter Msigwa aliwahi kusema mgeni akienda mahali kwa mara ya kwanza lile eneo anatakalo shukia kwKwa mwonekano wake ni kielelezo tosha cha ile jamii inayozunguka pale kuonyesha wale wenyeji wape ni jamii ya aina.gani nachekaga sana nikisikiliza haya maneno jamaa ni Genius sana .
 
Ukitafuta tu sehemu chache zenye mapungufu haitaleta maana kwasababu hata USA kuna mahali tu kuna gheto za ajabu

Hara Mwanza na kuendelea kote kuna sehemu tu yenye nyumba za hovyo.

Umeenda meru na uarushani huko migombani?
Taja kijiji cha usukumani chenye nyumba kama za wamasai.

Mmasai ni miongoni mwa jamii ambazo badi zinatakiwa kupewa elimu waachane na ujima. Vijiji vya wamasai na vya wasukuma tunafahamu tofauti iliyopo kwenye miundombinu yake hasa nyumba.

Huko mjini unakoongelea nadhani kanda ya ziwa inaongoza kuwa na miji mingi mikubwa kuliko kanda yoyote.
 
Kwahiyo hayo ni magari ya shoe shiners wanaenda marangu kupeleka hesabu ya kifungia mwaka

..hayo ni magari ya shoe shiners, washona viatu, wachoma mishikaki, mafundi welding, wa miaka ya 70 na 80.

..watu wa kwanza kuja Dsm kufanya umachinga na biashara ndogo ndogo ni Wachaga.

..baadaye walikuza mitaji na wengine wakafanikiwa kuwa wabiashara wakubwa.
 
naona wakazkazini wamejaa mikoa mengine kama kazkazini kuna maendeleo na maisha mazuri mbona wanapakimbia .
Wahindi walivyojaa Bongo kwani matajiri kuliko India? Huo ndo upambanaji bro. Mtoto hakui kwao
 
hawa watu wa kaskazini wana ubinafsi sana. ni wachapakazi na wanapenda sana kuendeleza kwao. wanapenda kujenga kwao na hata mtu akipewa uwaziri anahakikisha kila mradi wa maana anapeleka kwao. hii ndio sababu kwao kumeendelea tofauti na kwa wagogo au wafipa nk.. mimi naamini siku mchaga akipewa urais.. atahamishia ikulu kaskazini..

kama mwl nyerere angekuwa na roho ya namna hii, mara kungekuwa ni heaven ya Tanzania.
Na sasa kuna mataa ya kuongozea magari Chattle
 
My father alikua graduate wa Ilboru in 1952; and my mother Marangu TC, in late 60's, ni kweli mkuu, kaskazini hua elimu ya mtoto ni kila kitu, na hua maendeleo ni mashindano kwa kila familia.

Ingawa naamini kwamba Tanzania ili iendelee, tunahitaji elimu na Afya kwa viwango vya juu sana!
Na sio kununua midege isiyo na maana
 
Unataka kufananisha Kilimanjaro na Mpanda au Liwale?

Umepoteza dira kifikra. Hakuna mfanano na hautakuja kuwepo! Panatofauti za kijiografia, kihali ya hewa, uoto, utajiri wa asili kila eneo kwa namna yake na hivyo mpishano huo hufanya tofauti hata ktk mambo nengine! Kwanini tu masikini kifikra kiasi hiki!
 
Taja kijiji cha usukumani chenye nyumba kama za wamasai.

Mmasai ni miongoni mwa jamii ambazo badi zinatakiwa kupewa elimu waachane na ujima. Vijiji vya wamasai na vya wasukuma tunafahamu tofauti iliyopo kwenye miundombinu yake hasa nyumba.

Huko mjini unakoongelea nadhani kanda ya ziwa inaongoza kuwa na miji mingi mikubwa kuliko kanda yoyote.
Haha mi walinzi wangu ni Wamasai nawalipa 80000/ kwa mwezi haha na walinzi wawili from Arusha so cheap. Msukuma hawezi kubali this kind of cheap labour.
 
Hivyo unakubali Mwanza is better than Arusha. Na unapinga Mwanza haizidi Moshi.

OK nakuunga mukono in context of proportions. Asilimia ya watu wengi wa mkoa wa Kilimanjaro wanapata social services kuliko Mwanza lakini ukisema Arusha ntakataa.
Mkuu unajua Arusha ina wilaya ngapi na unechunguza maendeleo yake?

Ni Arumeru magharibi, Arumeru mashariki, Monduli-Mto wa mbu na Longido.

Kote huko hakuna tatizo la maji, ardhi wala umeme kasoro Longido kidogo.

Inawezekana wewe unazungumzia Manyara.

Kuhusu Maendeleo Mwanza hilo lipo wazi.
 
Back
Top Bottom