Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Mleta mada uko sahihi, mm natoka moja ya makabila ya mikoa ya mwisho kimaendeleo, my broos wana nafasi kubwa inchi hii nikiwatajia mwaweza shangaa, lkn up to the moment nipo street nahustle kama vile si ndugu yao japo ninavigezo vyote! Nimewaambia kama bac mnamuogopa Magu nipeni capital mm nifanye zangu ujasiliamali nimewaandikia hadi mpango mkakati lkn wapi!

Natamani wangekuwa wachaga, lkn ndo hvo!
Napigika na chaki kwenye kituo kimoja cha tuition hapa mjini, jamaa wanakula viyoyizo. Hawana mda na mm!
Natamani nchii hii ingekuwa ya wachagaa watupu, may be wangekuwa mbali!!
 
"Mikoa ya Kaskazini iliendelezwa kwa juhudi ya Wanakaskazini"

Huo ni Ukweli unaoleta furaha kwa Wanakaskazini na Maumivu kwa wana mikoa mingine.

Nitaelezea kwa Ushahidi ulio wazi kabisaaa!

Kwanza msingi wa maendeleo ni ELIMU NA MAARIFA.

Ni wazi kuwa mikoa/makabila yenye wasomi wengi ni ile iliyowapokea wamissionary mapema na kuwakabidhi Ardhi. Katika hiyo ardhi kila walipojenga Kanisa basi walijenga na shule au hospitali nzuri.

Mikoa hiyo ni Kilimanjaro, Arusha, Kagera na Mbeya. Hiyo ilitokea hasa katika miaka ya 1885 - 1900

SASA TUKIACHA ERA HIYO:

Wananchi binafsi wa Arusha na Kilimanjaro wana spirit na asili ya utafutaji wa elimu na mali na Maendeleo kwa juhudi sana (Hustles indeed)

Mifano ifuatayo inathibitisha hayo:-

1) KUJALI ELIMU

Kufikia uhuru wa Tanzania, tayari Kilimanjaro ilikuwa na shule (Kongwe) zenye sekondari kabisa zaidi ya 38 na vyuo baadhi Shule hizo ni kama lyamungo, Majengo, Kleruu College, MUCCOBS, Marangu TC n.k

Hizo zilijengwa kwa juhudi ya Wazazi na chama kahawa KNCU

Arusha kulikuwa tayari na shule zilizojengwa kwa Juhudi za wazazi kama Moringe Sokoine, Mringa Middle School, Monduli TC (ingawa pia serikali iliweka nguvu), Arusha Sec.school, Ilboru Sec. School iliyojengwa pamoja na kanisa la KKKT mwaka 1904

Kwa kuwajuza zaidi Ilboru sec.school na kanisa la Ilboru zilijengwa na wanawake (wamama wa kimasai) kutoka Kimandolu, Levolosi na Ilboru yenyewe, na ushahidi upo.

Pia Chama cha kahawa ARCU ilichangia sana maendeleo ya Arusha.

- Miji midogo wakati huo kama Monduli, Marangu, Machame, Ilboru na Akheri zilijengwa na juhudi ya wazee wa huko.

* Mfano tu, Monduli iliamuliwa kuwa mji mahali ilipo na Wazee wachache wa monduli akiwepo Sokoine.

Can you imagine mwaka 1970 tayari Sokoine alishaanzisha jengo kubwa kuwa Halmashauri ya Monduli kabla hata serikali haijaamua halmashauri iwe wapi.

Kina Lowassa na wengine walikuja tu kuendeleza zaidi.

* Kwa Upande wa Kilimanjaro, hasa Marangu akina Mareale walikuwa Mbali tu kiasi cha kuweza kujiongoza bila serikali ya JMT.

Mji wa Moshi ulikuwa mbaali kimaendeleo siku nyingi.

2) UHUSIANO WA KARIBU WA WANAKASKAZINI

Kingine kilichoiendeleza Kaskazini ni Interaction ya kuoana watu wa Kilimanjaro na wenyeji wa Arusha mjini, kwani wali utilize ardhi vizuri kuanzia enzi na enzi.

(Hata leo hii ukichunguza utagundua watoto wengi wa familia hizo ndio wamejaa serikalini, kwenye migodi ya madini, biashara n.k)

3) KUTOKUTEKWA NA USHIRIKINA

Wanakaskazini hawana asili ya "Ushirikina" na ukisikia mchaga, mmasai ama mwarusha analoga basi ujue amenunua uchawi.

Hakuna uchawi wa kutumia paka, Jini au Vifuu bila faida yoyote.

Mikoa kama Tabora chini ya machifu wao walipaswa kuwa mbali sana kimaendeleo kama alivyofanya chief fundikira (wajomba wa Samwel Sitta) na matunda yanaonekana hadi kuwasomesha akina Samwel Sitta (Hayati)

Mikoa mingine imekuja kuamshwa na hizi shule za kata, halafu inalialia kuwa Kaskazini inapendelewa. [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Wengine Dini zao ziliwanyima Fursa ya kuishika Elimu dunia leo wanalialia na kuikumbatia elimu dunia.

Kumbukeni...Azimio la Arusha likija Arusha tyr Arusha ilikuwa na majengo makubwa na shule za kuwatosha watoto wa Chuga.

Someni Historia, Fanyeni tafiti kabla ya kuanza kulialia.
Itasaidia nini kwa Tanzania hii tuliyonayo sasa? Umeleta hii mada ili iweje kwa watanzania wa leo, je kuwapa ushawishi nao waendelee au kuwaona wao ni wajinga? Bado elimu haijakusaidia na huijui historia vyema, jamii za mwanzo kuendelea na kupata elimu si za kaskazini, nadhani ni za Pwani, walishaelimika na kuunda taifa lao kushirikiana na waarabu. Hivyo kwa pamoja ukoloni wa mzungu ulikuwa kikwazo kwao. Kwa Tanzania ya leo, wakaskazini wanafanya vyema kiuchumi, hili halina ubishi, zipo njia za wazi pia zisizofaa zilizotumika. Miradi mikubwa kama mabarabara ya lami, umeme na mengineyo hayakutekelezwa na umoja wa akna mama wala ushirika wa kahawa. Inajulikana wazi ilikuwaje, ila huu ni muda muafaka wa kuyahubiri haya? Mi nadhani tuanze xaxa kulijenga taifa letu, bado liko changa na kama yalitokea makosa kamwe yasitumike kama kitu cha kujivunia. Jamii moja kupata elimu mapema kwa msaada wa wamisionari ingekuwa ni faraja kwa taifa lote jipya, tumerithi wataalamu toka kwa wakoloni ingetumika vyema kulijenga taifa lote, kwann ni upande mmoja tu? Kuna eidha walakini wa hizo elimu au kwa waliozipata. Mbeya na Kagera pia zimepitia njia hizo. Kilicho cha msingi sasa, tuisome historia njema ya kaskazini na tuitumie kwa maendeleo ya taifa zima. Nadhani ndicho kifanyikacho kwa sasa, mikoa karibuni yote inakuwa ktk idara zote, nko Simiyu, asilimia zaidi ya 60 ya vijiji vimeshaunganishwa na grid ya taifa, umeme. Shule za kata na za Advance karibia kila tarafa, barabara mitandao inajengwa. Hii ndo Tanzania tuitakayo, ni yetu wote,namaanisha yetu wote. Hakuna sehemu ya wachaga tu au wagogo tu, ni yetu wote. Kuna wachaga hadi uluguluni mgeta, wanaishi kwa kufanya biashara kule, labda uchagani ni kwa Wiki mbili tu kwa mwaka, huduma zote kule, afya, maji, shule, Barbara, umeme nk, je zilizoko kaskazini zinamsaidia nini yeye? Mfano, ucku kipindupindu kimemkamata je atasafirishwa kwenda Rombo kutibiwa? Je kama huduma zote ungezielekeza huko ingekuaje siku hiyo? Ndo mana nilitilia mashaka elimu iliyotolewa au wale waliyoipokea haikuwasaidia kufikiri. Tanzania ni yetu wote.
 
Vya kuandika ni vingi mnooo. Nenda pahala popote hapa Tz utakutana na mtu wa kaskazini anafanya biashara fulani hivi. Nenda university yoyote hapa Tz utakuwa wakufunzi wengi ni hao hao[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Na nyie mmezidi kujisifu!
Watu mnaacha wake zenu wanagongwa na wazee kule kisa mmeenda kutafuta hela Dar. Hata huko Dar mnagongewa maana shughuli ile mnaipotezea mnasaka hela kama vile mtazikwa nazo. Ndio maana watani zenu Wazaramo wanawazidi kwa kula maisha.
 
Haya ndo madhara ya kutokujua vitu ! hivi unazungumzia jiji la mwanza au mkoa mwanza ? Maana there's contradiction. ILA tukizungumzia social services you can't make any comparative analysis between Kilimanjaro and Mwanza. Northerners Wako 100 miles ahead, take it from me.
Hayo maendeleo yako wapi??

Mbona mwanza imepata hadhi ya kuwa jijji mwaka 2000 lakini Kilimanjaro mpaka leo ni manispaa??

Shame on you
 
sisi yakwetu imwishia sehemu flani ivi ukiwa unapanda kibosho panaitwa kirima- mkoring'a. Kiongozi aliyepo sasa tunataka tumbane wamalize nipande kilichobaki kuunganisha ikutane na ya kibosho umbwe inayotoka kibosho road. Dah kwa kweli ni lami mpaka vijijini[emoji12] [emoji23]
Hayo maeneoni ya Ukanda wa Kaskazini au ni ya MOSHI.

Hii post inachanganya. Inaongelea maendeleo kanda ya kaskazini ilhali mifano yote ni moshi na kwa mbali Arusha mjini.

Hivi mikoa ya Tanga na Manyara ipo ukanda gani?

Wamabg'ati Watindiga na Wairak wapo kanda ipi na vipi maendeleo yao yakoje.

Tukiongelea ukanda tuongelee maeneo yote na si wilaya moja.

Hivi kipato cha wilaya za same na mwanga kwa pamoja kinaifikia wilaya ya kahama au hata ya mahenge.

Huu uzi ubadilike uwe specific. Badala ya maneno UKANDA WA KASKAZINI iandikwe HIMAYA YA WACHAGGA ambako mgeni haruhusiwi kumiliki ardhi kama ilivyo Pemba.
 
Napafahamu sana tu, Ushuke huko japo uishie Tengeru uone ujenzi wa barabara..
Hili Barbara la King'or limenialibia tairi ahaha Mawe tupu afu MTU anaandika hapa JF eti Kaskazin ohh kumbe anamaanisha Moshi.

Afu wewe jamaa kwa hiyo huku Ngarenanyuki so Arusha. Afu mbona uku poa ukilinganisha na Ngorongoro na Monduli uwii no nmesahu kule Hanang haha Kasikazini moja
 
Sifa za Kijinga vitu vimejengwa na Wakoloni and then mtu anasema kimejengwa na kina mama wa Kimasai au Kimachame n.k Hizo Shule ukienda zitizama zina majengo ya kale ya tawala za Wajerumani Nenda Kolila Old Moshi n.k Shule Nyingi zilikuwa za Dini
Kwanini hawakujenga kwenu huko ugogoni?
 
Lakini nitoe angalizo kwa ukuaji wa miji ya wilayani naona kanda ya kasikazini imesimama/imedumaa sana.
Kwa miaka 20 ya sasa yaani tangu 1995 tumeshuhudia miji mingi ikikua sehemu mbali mbali kuliko miji ya kasikazini mfano Tunduma, Kahama, Ifakara, Tarime, Bariadi, Mpanda, Geita, na nk lakini mji ya kasikazini in duni na imedumaa.

Kuhusu Shule miaka Ishirini ya sasa tumeshuhudia shule za Kasikazini zikidiwa na kutupiliwa mbali na shule za Mwanza, Mbeya Na Kagera. Check matokeo ya Form four na darasa la saba. Leo hakuna mtu anauchu wa kupeleka mwanae akasome Moshi kama ilivyokua zamani.

Katika vyuo vikuu hakuna dominance ya kanda yoyote mwenye mawazo hayo amesoma chuo miaka ya 90.

Zaidi watu wa Arusha wamevalishwa lemba la ukoka na watu wa Moshi. Kilimanjaro kuna social services Arusha hakuna. Wasisifie gari za jirani.

Jamani Wasonjo nao waseme wako juu haha...
Wewe sijui wa wapi?

Wasonjo wapo manyara sio Arusha.

Arusha ina waarusha,/wamasai wachaga na wameru

Nenda kaangalie maisha yao, kaangalie nyumba zao, kaangalie miundo mbinu halafu ulinganishe na huko kwenu.
 
Wewe sijui wa wapi?

Wasonjo wapo manyara sio Arusha.

Arusha ina waarusha,/wamasai wachaga na wameru

Nenda kaangalie maisha yao, kaangalie nyumba zao, kaangalie miundo mbinu halafu ulinganishe na huko kwenu.
Mmeanza kukataana. Kwa hiyo Manyara si kasikazini haha Mshale umekuingia
 
Ktk post yote umenifurahisha hapo uliposema marangu(wachaga)waliweza kujiongoza bila JMT.Niliwahi kusikia wachaga walikuwa na Rais wao na serikali yao je hii ni kweli?Nijibu ili niendelee kudadisi
Mkuu ni kweli lile lilikuwa taifa tayari likiwa na kila kitu, hata ukigogle utakuta bendera yenye nembo ya mlima Kilimanjaro ikiwa na maneno " Lukuwawie na Ruwa" yakiwa na maana ambayo ni tujikumbatie na Mungu
 
Mleta mada uko sahihi, mm natoka moja ya makabila ya mikoa ya mwisho kimaendeleo, my broos wana nafasi kubwa inchi hii nikiwatajia mwaweza shangaa, lkn up to the moment nipo street nahustle kama vile si ndugu yao japo ninavigezo vyote! Nimewaambia kama bac mnamuogopa Magu nipeni capital mm nifanye zangu ujasiliamali nimewaandikia hadi mpango mkakati lkn wapi!

Natamani wangekuwa wachaga, lkn ndo hvo!
Napigika na chaki kwenye kituo kimoja cha tuition hapa mjini, jamaa wanakula viyoyizo. Hawana mda na mm!
Natamani nchii hii ingekuwa ya wachagaa watupu, may be wangekuwa mbali!!
Pole sana mkuu
 
Na nyie mmezidi kujisifu!
Watu mnaacha wake zenu wanagongwa na wazee kule kisa mmeenda kutafuta hela Dar. Hata huko Dar mnagongewa maana shughuli ile mnaipotezea mnasaka hela kama vile mtazikwa nazo. Ndio maana watani zenu Wazaramo wanawazidi kwa kula maisha.
Anzisha mada yako mkuu

K A S K A Z I N I HOYEEE !!!
 
Haha hata sasa hivi Niko Ngarenanyuki unapafahamu?
Kumbe umetoka huko kwenu ukaishia ngarenanyuki meru?

[emoji23] [emoji23] [emoji23] basi huijui Arusha wewe.
 
Ukiona mtu anajivunia ukanda ujue huyo ni MBUMBUMBU hata kama kasoma hadi kukuta kibao chenye maandishi NO MORE SCHOOLS AHEAD
 
Back
Top Bottom