Sometimes nasema acha Magufuri ashift the york to lake zoners nao wafaidi mema ya nchi hii baada ya miaka mingi.
Miaka nenda rudi northerners wameinflitrate umafia wao serikalini na kua na nguvu ya ushawishi sehemu muhimu za uchumi wa nchi hivyo kasikazini ikawa inapendelewa katka kila kitu, kuanzia wakati waziri mkuu akiwa msuya akapeleka umeme huko kwao milimani na porini hata hakuna watu, akaja sumaye, Lowassa nk.
Ukija kwa mawaziri wa fedha kina mramba ambao walijaza wakaskazini BOT, TRA, wizara ya fedha kwa kigezo kua wao tu ndio wamesoma mambo ya biashara.
Nimeshangaa watu wanamshambulia Magu kujenga Uwanja wa ndege wa kimataifa chato ila wakasahau ya kina msuya kupelekea nyani umeme miaka hiyo huko milimani, Kwenye rasilimali za nchi hii lake zone ni tajiri kuliko kasikazini.
1.)Hivi kuajiriwa
BOT na TRA ndio kuendeleza ukanda wa ulikotoka? Inawezekana kweli Mtumishi wa BOT au TRA akajenga Barabara, Shule, Hospital, Uwanja wa Ndege, Umeme, Nyumba Bora za kuishi, Usafiri wa Magari binafsi na Huduma ya maji kwao? Atakuwa analipwa shilingi ngapi huyo mtumishi? Mtumishi wa BOT na TRA anaweza akamzidi kipato mtumishi wa
UN, IMF na WB? Hapa kusema ukweli wachaga wanaonewa. Huko BOT na TRA kuna Wapemba, wamakonde, wasukuma, wahaya yaani makabila yote. Kulikoni kwao hakushambuliwi kimaendeleo?
2.) Kiongozi akitoka eneo lako mtapata faida gani wananchi wa huko? Niwarushe roho hadi mbaki na maneno yenu ya Wachaga WEZI na Wanawake wao wanaua!
Maji----Kaskazini hasa Mkoa wa Kilimanjaro wilaya za HAI, SIHA, MOSHI Vijijini na Rombo yapo ya kutosha tena unachagua utumie ya Bomba zilizowekwa na Wamisionary wa Kijerumani wakaipa serikali iangalie- toka Losaa to KIA, BOMA, MERARANI, RUNDUAGAI na kila nyumba kijijini. au ya Mto, au chemchemi au ya Mfereji. Sidhani hapa kama Kaskazini wanahitaji Kiongozi wa kuwaletea Maji. Labda tu mabadiliko ya tabia ya nchi yamechangia kupungua hasa wakati wa Kiangazi. Mchaga hanywi maji ya Visima na Wanyama! Asante Mungu yanatoka huko Mlimani!
Elimu----Shule za kumwaga hadi English Medium za Vidudu, Msingi na Secondary Vijijini!. Refer Modio Islamic English Medium School iko kijijijni lakini Elimu Super. Shule zilizojengwa na Misionnaries, Wananchi, serikali na Masjid. Unachagua shule ya kwenda zenye madawati, madarasa, vitabu na viti. Tena wanafunzi wanapata Lunch na chai shuleni. Waalimu wa kutosha.
Historia: Elimu Kaskazini
Kaskazini ni maeneo ya mwanzo ambayo
Wamisionari wa Ukristo walijenga
MAKANISA na
SHULE. Sababu hii iliwafanya Northernes kuwa wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mikoa wa Kaskazini inaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Shule nyingi za sekondari ziko katika mikoa hii kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamisionari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni
2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Watu wa Kaskazini waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi, wakati wakazi wa mikoa mingine kadhaa walisubiri serikali iwajengee shule.Ni vema pia kusema kuwa shule hizo huvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi tu Northerners.
Barabara---- Kwa Interest za Wakoloni ilikuwa lazima wajenge barabara ya kuunganisha mikoa ya kaskazini na Kenya. Hivyo ni rahisi kutoka Moshi, Arusha kwenda Kenya kwa barabara ya lami. Kihistoria Arusha in Makao makuu ya East Afrika tangu 1967 haikuwa busara kujenga barabara hapo? Arusha kuna vivutio vya Kimataifa vya Kitalii from wanyama, Rift Valley, Crater, Oldvai, Wamasai na Culture yao. Mkoa unaingiza pesa tena ya Dolars, EURO na Pound. Tukirudi Moshi mnapopaonea Wivu: Kwa juhudi za wananchi kupaza sauti zao na kudai zimepatikana. Marangu to Moshi iliwekwa na wakoloni,
Machame to Moshi, Siha to Moshi, Moshi to Uru, Kibosho to
Moshi hawa watu hawawezi kumsahau Mrema aliwapigania ikapatikana.
Moshi to Holili - hii lazima inaenda mpakani na Kenya. Moshi to Tarakea Lazima iwepo kuunganisha nchi na Kenya. Huko Upareni sijastudy sana za huko. Kijijini wananchi wana siku zao maalum ya kufanya kazi za jamii kwa pamoja bila kushuritishwa: kujenga barabara za ndani, kujenga shule. Kule watu wamejitune wanawajibika.
Hospital----Za kutosha hadi ya Rufaa nyingi zilijengwa na Missionaries. Ila ile ya TB ya Kibong’oto iliyokuwa inachukua wagonjwa wote wa TB Tanzania sina hakika nani walijenga.
Usafiri wa Ndege, Treni---- Asante Serikali, Asante Wazungu. Unachagua unataka kusafiri kwa njia ipi( Ndege, barabara au Treni).
Umeme---------- hadi mabanda ya kuku na nguruwe pesa yako tu ya kuvuta ndani. Hata huko katikati ya Kahawa na Migomba.
Baada ya kupata hizi huduma za jamii Wananchi wa Kaskazini wakatumia fursa hizi kusomesha watoto wao kwa hali na mali,
wakajihusisha na kilimo na Ufugaji - Kilichopatikana wakajenga nyumba nzuri za matofali na bati katikati ya migomba yao na kahawa ikawa rahisi kwao kupatiwa umeme vijijini haraka kabla ya REA. Kumbuka umeme unahitaji nyumba bora siyo ya nyasi na tope. Waliotoka wakaendeleza ndugu zao kielimu na kibiashara huku wakiwafundisha kurudi kwao kwenda kujenga nyumba ya tofali ili siku matatizo ya kifo au furaha kama harusi wasipate aibu. Natamani kama nyie Chaga Haters mngeweza kusafiri muende eneo linaitwa Nronga' ni kwenye mwinuko lakini kuna nyumba nzuri utadhani umetua Ulaya'. Huko hakuna Mtumishi wa BOT wala TRA ni kwa wakulima wachakarikaji. Kuna hadi Kiwanda cha Kusindika Product za Maziwa- Juhudi za kina mama wajasiriamali na wafugaji. Hata Northerners wasipokuwa na mtetezi serikalini kwao kutazidi kuendelea. Mpika Chips wa Dar es salaam Mnorthener akikupeleka kwao December utashangaa maendeleo aliyopeleka kwao. hata wale washona viatu, makondakta na madereva wanaojitambua from Northern wanawazidi kimaendeleo wana Mentality ya maendeleo siyo Kubebwa.
Hata hivyo mkumbuke Raslimali za watanzania ni zetu wote. Kama nyie mlishindwa Kuendeleza kwenu kwa Juhudi zenu msinyime watu wengine eti walipendelewa. Nyerere hakuwa Northerner, alitoa fursa kwa watu wote, Northerner- Ingekuwa hivyo Leo Mara na Mwanza kusingekuwa na nyumba za nyasi kungekuwa kama New York.