Pole sana Kaka Zito, Allah akuponye haraka!
Namimi nina tatizo kama hilo lako, ilinichukuwa muda sana kujuwa....!
Nimekuwa na tatizo la kupoteza fahamu tangu 1996 nikiwa form I pale Ilboru Secondary, lakini sikuwahi kulihusisha tatizo hilo na ungonjwa huu wa sinusitis, bali nilidhani ni PRESSURE ndivyo nilivyokuwa naambiwa na madaktari wetu hapo Bongo, mpaka hii leo ninapoisoma hii taarifa yako ndo napata mwanga kwamba huenda hata huku kuanguka na kupoteza fahamu kwangu kunatokana na ugonjwa huu sugu wa sinusitis!
Kilichonifanya nijue kama nna ugonjwa huu wa sinusitis, ni baada ya kupoteza uwezo wangu wa kunusa harufu na kuandamwa na flu zisizokwisha...mwaka 2007 nikiwa hapa Sweden, ndio niligundulika kwamba ni SINUSITIS, ambayo tayari ilishakuwa sugu, hizo dawa alizo suggests mdau hapo juu haziwezi kusadia tena ikishafikia stage hio ya usugu, kwa hiyo nilifanyia upasuaji mwaka huo 2007. Lakini hiyo pia si suluhisho la kudumu, sababu hizo polyps zinaota tena, hivyo basi baada ya muda (miaka 2) unatakiwa kurudi kwa checking, kama zitakuwa zimeota tena na ku block njia ya hewa, basi unapasuliwa tena!
Mimi bado sijarudi tena, sababu upasuaji wangu wa kwanza ulikuwa na complication (ulichukuwa masaa 3.30 badala ya 1.45 zilizokusudiwa), sababu nilikuwa nilitoka damu mno, kiasi walishindwa kukata hizo polyps zote, hivyo imenijengea woga wakurudi tena. Inshaallah nikipata ujasiri ntarudi tena. Alienifanyia upasuaji ni daktari bingwa wa ENT hapa Sweden, Dr Morgan!
Mh Zitto, nakutakia matibabu yenye mafanikio, Allah akujaalie uwe mwenye kupona haraka!