Jimena
JF-Expert Member
- Jun 10, 2015
- 25,935
- 96,105
Kwa heshima na taadhima... kwenu !! mwana2015 amoneyazan
Nimefuatilia maelezo yenu muruwa yenye utulivu na amani..., So nimeona niongeze elimu kuntu ktk maisha baada ya uhai kuondoka !!
Sasa kuna Maisha ya "barzakh" (ni kipindi cha maisha baada ya kufa hadi kufufuliwa hapo akhera) !!!
Jimena Mpendwa nikujuze kuwa Mwemyeezi Mungu katuumba wanaAdamu katika mfumo ulokuwa na utukufu,ubora na ufufuo... yaani "tulikuwa sii kitu (manii/mbegu) tukaumbika na kuwajibika, na tutafikia mwisho (kufa) na baada ya hapo tutarudishiwa uhai tena !! " Nikupe mfano ktk elimu ya Computer kuna HD "hard disk" humo kuna kila herufi imesajiliwa na kuhifadhika (So waweza kurejesha na kuippambanua time yyte uitakayo) !!
Asante sana Zamiluni Zamiluni kwa maelezo yako ambayo sijayaelewa vizuri.
Umeongelea kuhusu Akhera (kitu ambacho mpaka sasa sijapata uthibitisho wowote wa uwepo wake)
Uhusiano uliopo baina ya Manii na Mungu, maana binadamu hafanyiki kwa manii pekeyake, na kitendo cha yai kurutubishwa na hizo manii mpaka kufanyika mtoto inahusiana nini na maumivu makali sana ambayo yanadaiwa binadamu huyasikia baada ya kufa?
Mwisho tumalizie kuhusu maisha baada ya kifo. Kwenye maisha baada ya kifo ni wazi kuwa kitakachokuwepo pale ni roho na kamwe sio mwili maana baada ya muda mwili huoza kabisa, unless uuchome moto au kuukausha, sasa uhai hurudishwa kivipi? Kwamfano mwili umekaushwa huo uhai wake unarudije? Au mtu amechomwa moto uhai wake unawezaje kurudi? Uhai unarudije kwenye mwili gani labda?
Ntashukuru kama utanijibu swali moja baada ya jingine na hatua kwa hatua ili kuepusha kuzalisha maswali mengi zaidi.
Last edited by a moderator: