Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Jana tukiwa safarini kutoka Dar kuja Kilimanjaro tukiwa angani kuna hali ya sitofahamu ikitokea kwa muda nadhani dakika 5. Inawezekana hizi ndege zina matatizo tumeingizwa mjini sasa kama aliyenunua anasema yeye msema kweli mpenzi wa Mungu anashindwa nini kuchukua dhidi hao waliomdanganya kuhusu hizi ndege? Mengi yamesemwe sana kuhusu ndege kama hujawahi kusafiri nayo huwezi kuamini hicho ambacho kinasemwa .Serikali hizi ndege nimeingizwa chaka!
huu ni uongo nimesafiri na bombardier zaidi ya Mara kumi mpaka sasa hilo la hali ya Hewa kuzingua Ndege itatikisika tu. Mnyonge mnyongeni Haki yake mpeni
 
KWA TAARIFA YAKO UNAPOTEZA MUDA NA KUDANGANYA UMMA, NDEGE INAYOTENGENEZWA UNAJUA HATA INJINI YAKE SERIKALI BADO HAIJACHAGUA? LAKINI PIA UNAKARIBISHWA KIPINDI NWATAALAM WATAKAPOTEMBELEA KUJUA HATUA ZA UJENZI WA NDEGE HIYO ZIKIENDELEA. ! NAONA UNATOKA POVU TU NA KUSIKITISHA! UNAWAPOTEZEA WATU MUDA WAO BURE NA KWA TAARIFA TU, HAYO YOTE YALIONEKANA HATA KABLA YA KUSAINI MKATABA KWA KUWA KULIKUWA NA USHINDANI WA KIJINGA KATI YA BOEING NA AIRBUS. NA NDEGE UNAYOITAJA ILIONYESHWA IKIWA HAIJANUNULIWA NA IPO PARKING NA SI SEHEMU YA NDEGE MPYA YA TANZANIA. POLE SANA UNASIKITISHA!
kwa nini umetumia nguvu nyingi sana kuwaamisha wana jamvi?? mbona hujaweka "clues" zozote?? mleta uzi kaweka na links hapo sidhani kama umetembelea hizo kurasa??
wewe ndio naona kabisa umeshupaza shingo na povu jingi mnoo!!
 
Rafiki yangu Areafiftyone, jana nilieleza kitaalamu wasiwasi wangu kuhusu uvumi kuwa tumeuziwa moja wapo ya terrible teens. Mojawapo ya hoja zilizoletwa ni kupata line number na serial number ya hiyo ndege mpya ili tuone kama iko tofauti na hii ninayodai ni fake. Mh Waziri kajibu hilo Serial number ni 64249 tofauti na ile ya terrible teens na Line number ni 719 na siyo 19.

Areafiftyone, ninajaribu tu kukieleza kile ninachokiamini kwa uelewa wangu na sijawa mtetezi wa wezi hata siku moja. Kama ningejilidhisha kuwa kuna ufisadi, ningesema pia. Sijaliangalia hili swala kwa mihenuko ya kisiasa bali kwa kitaaluma. Sina upande wa sasa tumewapata na kuishi kwa kuviziana ili upate mtaji wa kisiasa badala ya kutetea maslahi ya nchi yangu bila kuangalia au kuongozwa na itikadi. nafikiri ni vizuri mikataba ikawa wazi huenda hili ninalolitetea lingeeleweka kwa urahisi hata kama huna uelewa wa maswala ya ndege.
 
Rafiki yangu Areafiftyone, jana nilieleza kitaalamu wasiwasi wangu kuhusu uvumi kuwa tumeuziwa moja wapo ya terrible teens. Mojawapo ya hoja zilizoletwa ni kupata line number na serial number ya hiyo ndege mpya ili tuone kama iko tofauti na hii ninayodai ni fake. Mh Waziri kajibu hilo Serial number ni 64249 tofauti na ile ya terrible teens na Line number ni 719 na siyo 19.
Hivi nyie huko shuleni mlikuwa mnaelewa nini?? Au ndo mkimaliza shule mnabakiza akili zote kule kule chuoni...!! Mbona mleta uzi kaeleza kila kitu, ambacho hamuelewi ni nini?
 
Rafiki yangu Areafiftyone, jana nilieleza kitaalamu wasiwasi wangu kuhusu uvumi kuwa tumeuziwa moja wapo ya terrible teens. Mojawapo ya hoja zilizoletwa ni kupata line number na serial number ya hiyo ndege mpya ili tuone kama iko tofauti na hii ninayodai ni fake. Mh Waziri kajibu hilo Serial number ni 64249 tofauti na ile ya terrible teens na Line number ni 719 na siyo 19.
Hivi nyie huko shuleni mlikuwa mnaelewa nini?? Au ndo mkimaliza shule mnabakiza akili zote kule kule chuoni...!! Mbona mleta uzi kaeleza kila kitu, ambacho hamuelewi ni nini?
 
Guys mbona ndege zinajengwa na si kwamba zilishajengwa zamani. Yaan tunavyoongea hivi ndege zinajengwa. Na zilizododa zilishajengwa long time ago.
 
huu ni uongo nimesafiri na bombardier zaidi ya Mara kumi mpaka sasa hilo la hali ya Hewa kuzingua Ndege itatikisika tu. Mnyonge mnyongeni Haki yake mpeni
Ndege ya aina yeyote inatingisha angani kwa Sababu ya Aero-dynamics... yaani flowing ya hela/upepo angani! Any frequent flier understand this very well!
 
Guys mbona ndege zinajengwa na si kwamba zilishajengwa zamani. Yaan tunavyoongea hivi ndege zinajengwa. Na zilizododa zilishajengwa long time ago.
Waziri amemaliza huu uongo kwa sentensi ambazo hazidi mbili ... serial no. na laini namba yenye maelezo marefu ya huu uzi... ni tofauti na serial no. na laini namba ya ndege iliyonunuliwa na TGFA ... in short kulinda heshima ya jukwaa delete the whole story!
 
tunanunua sukari 2800 kwa kununua ndege mtumba!!!!!!!!!!!!
Mungu yupo
evidence hiyo hapo aje mtu abishe
dege liko onorder
 
Huna lolote badala ya kuangalia uchumi wa MTU mmoja mmoja unajaji uchumi wa miaka 30 ijayo ndege huwezi kuzinunua zote kwa miaka miwili haiwezekani ukiniambia kwa miaka labda 8 sawa
 
Boeing hawajatupiga. Inawezekana wametuuzia kwa $80. Wabongo in power wameinflate wapige cha juu...boeing hawawezi kuwa waovu kiasi hicho....tunanyongana sisi mwenyewe kama ile radar

Sent from my Y4 using JamiiForums mobile app
 
Wapigwe Tu Hakuna Namna
Wanajifanya Serikali Hainunui Mitumba Acha Ije Tu Maana Kazi Kubwa Sifa
Hii ndege sio Mtumba. Ni brand new ila wateja hawaitaki mana inadefect itokanayo na overweight. Argument sio upya wake.

Ishu ni kwann tuuziwe ndege yenye defect kwa bei ya ndege isiyo na defect??
Shalom watanzania wenzangu!

Disemba 12, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa baadhi yetu tuliomchagua JPM na Tutamchagu tena 2020 Mungu akitujaalia na wengine mlinuna baada ya taarifa kutoka serikali imeweka oda Boeing, ili kununua ndege ya kisasa kabisa 787-8.

Na yakwamba serikali itatoa $224.6Millioni ili kupata ndege hiyo.

Kumekuwa na taarifa mbali mbali, kwamba manunuzi haya yana chembe chembe za ufisadi. Na kwakuwa sipendi kuamini vitu bila kufanya utafiti nami nimeona nizame kwenye websites mbali mbali kutafuta ukweli.

Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua.

1. SERIAL NUMBER(SN) NA LINE NUMBER.
-Kila ndege huwa na serial number yake kama yalivyo magari. Ndege tulioagiza serial number yake ni 35508
-Line number ni ndege ya ngapi kutengenezwa. Kwa mfano kama zimetengenezwa ndege 10. Ndege ya kwanza itakuwa LN1, ya pili LN2 nakuendelea.

2. TERRIBLE TEENS NI NINI?
Terrible teens ni zile ndege za mwanzo kutengenezwa za Boeing 787-8. Hizi ndege zilikuwa 20. Kwahiyo hiyo ni Line number 1-20 (Kuwa makini hapa). Na hizi ndege zilifanyiwa majaribio mengi na matengenezo mengi mapya ili kupata ndege bora zaidi.

Kwa kifupi tunaweza sema zilikuwa sample ya kutengenezea ndege zingine. Kutokana na kufanyiwa modification za mara kwa mara hizi ndege zilipitiliza uzito uliotakiwa. Kutokana na kuongezeka uzito ndege hizi hata uwezo wake wa Masafa ukawa Umepungua kwa Maili 1000 au KM 1609.344

Kutokana na hili makampuni yaliotaka order za mwanzo kama All Nippon, Maroc etc. yaligoma kuchukua hizi ndege bali yalichukua ndege zilizotengenezwa baada ya zile 20 za mwanzo yaani Line number 21 na kuendelea.

Terrible teens zingine ziliwekwa kwenye majumba ya kumbukumbu na baadhi ya kampuni walizichukua. Zikabaki 12 uwanjani miaka mitano bila mnunuzi toka 2009 zilipoanza tengenezwa.

Kutokana na aibu iliyokuwa inaipata Boeing ya kukaa na mindege isiyo uzika. Ikaamua yafuatayo

(a) Kutafuta Wateja ambao hawatajali issues ya kikomo cha masafa ya ndege

(b) Kuziuza hizi ndege kwa bei rahisi ( karibu nusu bei kutoka $224M hadi $99M)

CONCLUSION
Kutoka katika websites ya Boeing na na web zingine za usafiri wa anga zimeweka wazi Ndege tulio iwekea order ni Boeing 787-8, serial number 35508, Line number 19.

Sasa kwa maelezo niliyotoa Line number 19 IPO ndani ya Line number 1-20. Kwa kifupi ndege tuliogiza ndio zile ndege za mwanzo 20 zilizopachikwa jina la Terrible Teens.

Swali lingine la kujiuliza kwanini tumeuziwa ndege iliyo doda ,iliyoshushwa bei hadi kufikia $99M kwa bei ya ndege mpya yaani $224.6M?

Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.

Kama nilivyokwisha sema Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini anayeipenda Tanzania. Na imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa kazi.

Nimewawekea link na picha mbali mbali kusappoti uzi.

66cbe3973d2476f0afd0ef4b23f5d581.jpg


5ffe88270490cadedd65af84f1f2a940.jpg
32a59f2db3a1932ae85e9b8bfd8d26fd.jpg


Boeing 787 Register - Welcome

www.airliners.net/forum/viewtopic.php?t=1335649

www.airportspotting.com/boeing-finding-homes-terrible-teen-787s/

www.boeing.com/commercial/customers/air-tanzania/air-tanzania-787-order.page
 
Back
Top Bottom