The Tomorrow People
JF-Expert Member
- Jul 11, 2013
- 2,674
- 2,801
Shalom watanzania wenzangu!
Disemba 12, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa baadhi yetu tuliomchagua JPM na Tutamchagu tena 2020 Mungu akitujaalia na wengine mlinuna baada ya taarifa kutoka serikali imeweka oda Boeing, ili kununua ndege ya kisasa kabisa 787-8.
Na yakwamba serikali itatoa $224.6Millioni ili kupata ndege hiyo.
Kumekuwa na taarifa mbali mbali, kwamba manunuzi haya yana chembe chembe za ufisadi. Na kwakuwa sipendi kuamini vitu bila kufanya utafiti nami nimeona nizame kwenye websites mbali mbali kutafuta ukweli.
Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua.
1. SERIAL NUMBER(SN) NA LINE NUMBER.
-Kila ndege huwa na serial number yake kama yalivyo magari. Ndege tulioagiza serial number yake ni 35508
-Line number ni ndege ya ngapi kutengenezwa. Kwa mfano kama zimetengenezwa ndege 10. Ndege ya kwanza itakuwa LN1, ya pili LN2 nakuendelea.
2. TERRIBLE TEENS NI NINI?
Terrible teens ni zile ndege za mwanzo kutengenezwa za Boeing 787-8. Hizi ndege zilikuwa 20. Kwahiyo hiyo ni Line number 1-20 (Kuwa makini hapa). Na hizi ndege zilifanyiwa majaribio mengi na matengenezo mengi mapya ili kupata ndege bora zaidi.
Kwa kifupi tunaweza sema zilikuwa sample ya kutengenezea ndege zingine. Kutokana na kufanyiwa modification za mara kwa mara hizi ndege zilipitiliza uzito uliotakiwa. Kutokana na kuongezeka uzito ndege hizi hata uwezo wake wa Masafa ukawa Umepungua kwa Maili 1000 au KM 1609.344
Kutokana na hili makampuni yaliotaka order za mwanzo kama All Nippon, Maroc etc. yaligoma kuchukua hizi ndege bali yalichukua ndege zilizotengenezwa baada ya zile 20 za mwanzo yaani Line number 21 na kuendelea.
Terrible teens zingine ziliwekwa kwenye majumba ya kumbukumbu na baadhi ya kampuni walizichukua. Zikabaki 12 uwanjani miaka mitano bila mnunuzi toka 2009 zilipoanza tengenezwa.
Kutokana na aibu iliyokuwa inaipata Boeing ya kukaa na mindege isiyo uzika. Ikaamua yafuatayo
(a) Kutafuta Wateja ambao hawatajali issues ya kikomo cha masafa ya ndege
(b) Kuziuza hizi ndege kwa bei rahisi ( karibu nusu bei kutoka $224M hadi $99M)
CONCLUSION
Kutoka katika websites ya Boeing na na web zingine za usafiri wa anga zimeweka wazi Ndege tulio iwekea order ni Boeing 787-8, serial number 35508, Line number 19.
Sasa kwa maelezo niliyotoa Line number 19 IPO ndani ya Line number 1-20. Kwa kifupi ndege tuliogiza ndio zile ndege za mwanzo 20 zilizopachikwa jina la Terrible Teens.
Swali lingine la kujiuliza kwanini tumeuziwa ndege iliyo doda ,iliyoshushwa bei hadi kufikia $99M kwa bei ya ndege mpya yaani $224.6M?
Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.
Kama nilivyokwisha sema Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini anayeipenda Tanzania. Na imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa kazi.
Nimewawekea link na picha mbali mbali kusappoti uzi.
Boeing 787 Register - Welcome
www.airliners.net/forum/viewtopic.php?t=1335649
www.airportspotting.com/boeing-finding-homes-terrible-teen-787s/
www.boeing.com/commercial/customers/air-tanzania/air-tanzania-787-order.page
Updates:
Serikali kupitia waziri wa uchukuzi imesema imenunua LN719 na si LN19.
Pia baadhi ya mitandao ya wanahabari inayo ripoti taarifa za ndege, ambayo mwanzo iliripoti kuwa tumenunua LN 19 nayo sasa inasema tumenunua LN 719.
Pamoja na taarifa hizi, lakini ukakasi bado uko pale pale, kwa sababu zifuatazo.
1. LN 719 ambayo serikali sasa inadai imenunua ni Boeing 787-9 na si 787-8
2. Mkataba wetu wa mwanzo na Boeing ilikuwa kununua 787-8. Na 787-9 ambayo tunadai tumenunua ni ndege kubwa zaidi na bei yake ni zaidi ya $224.6M
***Kutokana na huu ukakasi, mi nimeamua kusubiri hiyo ndege ije. Tutajua tu kama ni 787-8 au 787-9, maana haya madege yanatofautiana urefu. Na njia rahisi kutofautisha hii midege ni kuhesabu idadi ya madirisha. Siku ya uzinduzi pale air port nitakuja Bongo Dar kushuhudia.