Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Tatizo ni hii lugha ya malkia.

"
But Boeing executives confirmed to Business Insider on Wednesday that all of "teens" have been sold and will be delivered over the next two years.

Boeing declined to reveal who picked up the last of them.
"

Hiyo sentensi inajibu mengi kuhusu wanaopiga makelele kuwa
1. kwa kuwa zitachukua miaka miwili basi sio terrible teen.
2. Zilishauzwa kwa kuwa boeing hadi hiyo siku habari inaandikqa hakukuwa na official confirmation nani mnunuzi.,which ofcourse came in december once talks were finalized and our mighty jpm kuingia mlango wa kutokea na kujizolea li-terrible teen moja matata

Business insider wanasema baada ya kukutana na mabosi WA boeing wameambiwa terrible teens zote zimeshauzwa tangu julai 2016, hivyo kuwapelekea wateja ingechukua hadi miaka miwili kwa sababu mbalimbali ikiwemo pengine wateja wengi waliamua kulipa kwa awamu kadhaa kabla ya kuchukua ndege.
Boeing wamesema wameuzia Tanzania dreamliner 787 kwa dola mil.224 haitawezekana wauze ndege ya dola mil.99 kwa bei ya juu tofauti na uhalisia itawaletea matatizo. Hivyo nawapinga wote wanaosema boeing wametudanganya .
 
Kimweri nina hakika hatujauziwa ndege ya aina hiyo. Sijafanya kwa ushabiki bali kwa kuangalia facts. Na ndio maana nikasema sioni any convincing fact ya kitu hiki. Nalokubaliana na wee ni kuhakikisha adhabu kali kama hii rumous ni ya kweli. Sitaogopa kutumia ufahamu wangu kusema hili ni kweli au si kweli eti kwa kuogopa kuhusishwa na upuuzi ambao naamini haupo.

Unakataa kuwa hatujauziwa ndege yenye hiyo serial number wakati wewe hutoi uthibitisho wa serial number ya nyengine.,

Kama ulihusika kwenye manunuzi jiandae kuwa responsible.

Ndege kuwa na features za zamani na ufanisi kidogo ndio sababu ya jina la terrible teens, has nothing to do with them being used.

Its about time hii mikata ya kitapeli muwe mnaiweka waI ili mnapoingizwa mjini ijulikane mapema, before its too late.
 
The Tomorrow People, nimeisoma kwa makini sana posting yako na ina ukweli kadhaa ndani yake. Hata hivyo kwa faida ya wasomaji na wachangiaji wenzetu ni vizuri nikaweka sawa baadhi ya mambo ili kuutenda haki mjadala huu. Maelezo na ufafanuzi wako wa maana ya serial number, line number, na hata terrible teen kama ulivyoyajengea kwa kutumia taarifa kutoka mitandao mbalimbali ni sahihi kabisa.

Tatizo langu, kwa kutumia elimu yangu ndogo katika mambo ya ndege, linakuja kwenye conclusion yako na kutumia hizo website kuthibitish hoja yako bila kujua au kusema nani wamilki wa hizo website. Kampuni ya Boeing ndio iliyoiuzia ndege Tanzania hivyo kwa hali ya kawaida lazima kungekuwa na uthibitisho wa ununuzi wa ndege hii kutoka kampuni hiyo. Uthibitisho wa Boeing unaoutumia katika posting yako ni wa bei ($224.6M) na siyo kuwa Tanzania imeuziwa mojawapo ya Terrible teens. Ni vizuri pia tukaelewa maana ya list prices ambayo ndio imeonyeshwa katika website ya Boeing ili kujua kuwa hii siyo bei waliyouziwa Tanzania. Uthibitisho uliotumia kuonyesha kuwa Tanzania imeuziwa mojawapo yaTerrible teens ni kutoka tovuti zifuatazo:

Boeing 787 Register - Welcome

Hii ni tovuti ambayo haimilikiwi wala kuwa na uhusiano wowote na kampuni ya Boeing. Kwa mtazamo wangu na jinsi nilivyoangalia habari zilizomo, sio rahisi kuzichukulia habari zao kwa uhakika hata wa asilimia moja. Hii ni website ya amatures hivyo kutumia habari zao kama uthibitisho wa Tanzania kununua mojawapo ya Terrible teens hazina mashiko. Uangalifu wa hali ya juu na kutafuta habari katika vyanzo vilivyo karibu au kutoka ndani ya Boeing yenyewe ni muhimu katika kuthibitisha jambo hili badala ya kuamini habari kutoka website au blog ya mtu mmoja tena amature. Sioni kwa nini Tanzania wangeamua kusubiri karibu miaka miwili kupata ndege hii wakati iko tayari ikisubiri mnunuzi. Muda mrefu kiasi hiki ni kwa ajiri ya kutengeneza ndege mpya. Kama ndege tayari ina serial number na line number, lazima ingekuw katika website ya Boeing au website za makampuni credible hasa yanayotoa habari za kibiashara. Ajabu sijaona reference ya website yoyote inayoaminika kimataifa kwa habari za kibiashara iliyobeba habari hii pamoja na kuwa na mvuto kutokana na hizo terrible teens. Kwa kifupi hii ni habari ya kutunga na ndio maana website zinazoaminika kimataifa haziwezi kuitumia habari hii kwa kujua kuwa ni uongo na uzushi kwa kuogopa matatizo ya kisheria.


www.airliners.net/forum/viewtopic.php?t=1335649
Websita hii haina sehemu yeyote inayosema Tanzania imenunua mojawapo ya Terrible teens kama inavyodaiwa kwenye website ya huyu jamaa hapo juu. Website hii ambayo ina forum kama ya jukwaa la siasa kwa maswala ya ndege inazungumzia kuwapo Terrible teens na kuishia hapo. Sasa sijui ni kwanini imetumika kama kithibitisho kuwa Tanzania imenunua mojawapo ya Terrible teens. Inajaribu kuelezea failure ya uongozi wa Boeing mwanzoni mwa projekti ya 787.

www.airportspotting.com/boeing-finding-homes-terrible-teen-787s/

Website hii inazungumzia habari ya Ethiopia kununua Terrible teens kwa matumizi yao na siyo Tanzania kununua mojawapo ya Terrible teens. Wanatoa pia historia ya manunuzi yanayotazamiwa. Inaonekana habari hii ni ya zamani kidogo. Haijatoa uthibitisho kuwa Tanzania imenunua mojawapo ya Terrible teens hivyo haina uhusiano na habari za Tanzania kununua mojawapo ya Terrible teens.

www.boeing.com/commercial/customers/air-tanzania/air-tanzania-787-order.page

Hii ni website rasmi ya Kampuni ya boeing na inatoa habari za tanzania kununua ndege ya Boeing 787-8 na kujiunga na familia ya Boeing. inathibitisha bei kuwa ni list price. Mara nyingi list price siyo lazima iwe ni contarct price (bei iliyoko kwenye mkata) baada ya punguzo. Bei hii ni kwa ndege mpya na siyo mojawapo ya Terrible Teens kama inavyokuwa speculated kwa kutumia habari za mtandao wa amature mmoja. huyu ni mtu ambaye alikuwa anatoa habari za formula one na kuamua kuiuza website hiyo na kuanzisha hii ya B787.

Ninahkika 100% kuwa Boeing hatajaribu kujiingiza katika aibu kama hii kwa kuiuzia Tanzania ndege ya Terrible Teens huku akijuwa kuwa makabidhiano ya ndege huhusisha uhakiki wa uzito. Sijui atahonga wangapi iliwakubali kuchukua ndege yenye uzito tofauti na ule Tanzania wanataka. Ninaona mambo mengi sana kwa kutumia ufahamu wangu mdogo wa mambo ya ndege yanayonifanya nisiamini hata chembe habari ya Tanzania kuingizwa mkenge. Rbu tufuatie na baadae mje mnisute kwa kusema uongo wakati mojawapo ya Terrible Teens itakapo kuja Tanzania. Nilisema wakati wa bombardier kuwa sio kweli kuwa zimetumika bali ni mpya. nikamaliza kwa kusema I stand to be hanged kama itathibitishwa kuwa nilichosema ni uongo. I stand to be hanged kama itathibitishwa kuwa Tanzania imenunua mojawapo ya terrible teens au ndege hiyo sio mpya au haijatengenezwa kwa order ya Tanzania.
Mkuu, umeeleza vzr kwa kuwa umejitahidi kutoka nje ya box, ninachoweza kusema kama itathibitika kuwa kuna watu wamemzunguka presidor asee nahic data be hanged....

Natunza huu Uzi kwa ajr ya reference..
 
Areafiftyone, ninajaribu tu kukieleza kile ninachokiamini kwa uelewa wangu na sijawa mtetezi wa wezi hata siku moja. Kama ningejilidhisha kuwa kuna ufisadi, ningesema pia. Sijaliangalia hili swala kwa mihenuko ya kisiasa bali kwa kitaaluma. Sina upande wa sasa tumewapata na kuishi kwa kuviziana ili upate mtaji wa kisiasa badala ya kutetea maslahi ya nchi yangu bila kuangalia au kuongozwa na itikadi. nafikiri ni vizuri mikataba ikawa wazi huenda hili ninalolitetea lingeeleweka kwa urahisi hata kama huna uelewa wa maswala ya ndege.

NOD kwa jinsi ulivyotetea swala hili, inaelekea umehusika kwa njia moja au nyingine katika sakata hili .Mkuu kuna shida, na inaelekea mmepiga. Ngoja tusubiri tuone kama mtapona, lakini kwa jinsi mambo yalivyo kuna haja ya Bunge na CAG kuhusishwa ili mbivu na mbichi zifahamike . Kama tuhuma hizi ni kweli, dah,kweli Tanzania in shamba la bibi. Ingekuwa China watu wangekula shaba mkuu.
 
Ufupishiwe ili iweje!? Kwani nawe ni Bashite wa Kolomije huelewi kilichoandikwa kwa kuwa umezoea mstari mmoja mmoja!? Tulizana soma kwa kina ili uelewe huwezi tafuta zile za mstari mmoja mmoja hii waachie wenye uwezo wa kuelewa hata kama ni page 100.

Kama umeendelea kusoma utakuwa unajutia hata kuniquote, kwa sababu haukuangalia nje ya box. Nyie msioipenda awamu hii mkiniona tu nimeandika mnajua kumwaga lolote, nimewazoea ila na kuwajibu lazima niwajibu nikiamua. Ha ha ha haaaa
 
Tatizo umekuwa mshabiki wa Bashite mpaka umekuwa mjinga kama yy. Usichoelewa kitu gani hapa?

Nimeandika sijaelewa au?

Unaona sasa wewe na mimi nani mdaku? Nani hatumii fikra hata kidunchu.

Ha ha haaaaa

Jisikitikie, na mjue kuwa uandishi sio kimoja tu kama vile mlivyokuwa mnanyonyeshwa.
 
Upende awamu hii kwa lipi? Nchi ina utajiri wa kutisha lakini bado imegubikwa na umaskini uliokithiri. Inabidi kujitoa ufahamu ili kukipenda na kukitetea chama cha wahuni, mafisadi na mabashite wa Kolomije.

Kama umeendelea kusoma utakuwa unajutia hata kuniquote, kwa sababu haukuangalia nje ya box. Nyie msioipenda awamu hii mkiniona tu nimeandika mnajua kumwaga lolote, nimewazoea ila na kuwajibu lazima niwajibu nikiamua. Ha ha ha haaaa
 
Upende awamu hii kwa lipi? Nchi ina utajiri wa kutisha lakini bado imegubikwa na umaskini uliokithiri. Inabidi kujitoa ufahamu ili kukipenda na kukitetea chama cha wahuni, mafisadi na mabashite wa Kolomije.

Wape muda ndipo Raisi wetu ambaye hana hata miaka miwili anajaribu kufanay hivyo, nasi wananchi ni wajibu wetu kufanya yetu pia tuendeleze na kitajirisha nchi yetu kwa unayoyasema.
 
Shalom watanzania wenzangu!

Disemba 12, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa baadhi yetu tuliomchagua JPM na Tutamchagu tena 2020 Mungu akitujaalia na wengine mlinuna baada ya taarifa kutoka serikali imeweka oda Boeing, ili kununua ndege ya kisasa kabisa 787-8.

Na yakwamba serikali itatoa $224.6Millioni ili kupata ndege hiyo.

Kumekuwa na taarifa mbali mbali, kwamba manunuzi haya yana chembe chembe za ufisadi. Na kwakuwa sipendi kuamini vitu bila kufanya utafiti nami nimeona nizame kwenye websites mbali mbali kutafuta ukweli.

Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua.

1. SERIAL NUMBER(SN) NA LINE NUMBER.
-Kila ndege huwa na serial number yake kama yalivyo magari. Ndege tulioagiza serial number yake ni 35508
-Line number ni ndege ya ngapi kutengenezwa. Kwa mfano kama zimetengenezwa ndege 10. Ndege ya kwanza itakuwa LN1, ya pili LN2 nakuendelea.

2. TERRIBLE TEENS NI NINI?
Terrible teens ni zile ndege za mwanzo kutengenezwa za Boeing 787-8. Hizi ndege zilikuwa 20. Kwahiyo hiyo ni Line number 1-20 (Kuwa makini hapa). Na hizi ndege zilifanyiwa majaribio mengi na matengenezo mengi mapya ili kupata ndege bora zaidi.

Kwa kifupi tunaweza sema zilikuwa sample ya kutengenezea ndege zingine. Kutokana na kufanyiwa modification za mara kwa mara hizi ndege zilipitiliza uzito uliotakiwa. Kutokana na kuongezeka uzito ndege hizi hata uwezo wake wa Masafa ukawa Umepungua kwa Maili 1000 au KM 1609.344

Kutokana na hili makampuni yaliotaka order za mwanzo kama All Nippon, Maroc etc. yaligoma kuchukua hizi ndege bali yalichukua ndege zilizotengenezwa baada ya zile 20 za mwanzo yaani Line number 21 na kuendelea.

Terrible teens zingine ziliwekwa kwenye majumba ya kumbukumbu na baadhi ya kampuni walizichukua. Zikabaki 12 uwanjani miaka mitano bila mnunuzi toka 2009 zilipoanza tengenezwa.

Kutokana na aibu iliyokuwa inaipata Boeing ya kukaa na mindege isiyo uzika. Ikaamua yafuatayo

(a) Kutafuta Wateja ambao hawatajali issues ya kikomo cha masafa ya ndege

(b) Kuziuza hizi ndege kwa bei rahisi ( karibu nusu bei kutoka $224M hadi $99M)

CONCLUSION
Kutoka katika websites ya Boeing na na web zingine za usafiri wa anga zimeweka wazi Ndege tulio iwekea order ni Boeing 787-8, serial number 35508, Line number 19.

Sasa kwa maelezo niliyotoa Line number 19 IPO ndani ya Line number 1-20. Kwa kifupi ndege tuliogiza ndio zile ndege za mwanzo 20 zilizopachikwa jina la Terrible Teens.

Swali lingine la kujiuliza kwanini tumeuziwa ndege iliyo doda ,iliyoshushwa bei hadi kufikia $99M kwa bei ya ndege mpya yaani $224.6M?

Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.

Kama nilivyokwisha sema Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini anayeipenda Tanzania. Na imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa kazi.

Nimewawekea link na picha mbali mbali kusappoti uzi.

66cbe3973d2476f0afd0ef4b23f5d581.jpg


5ffe88270490cadedd65af84f1f2a940.jpg
32a59f2db3a1932ae85e9b8bfd8d26fd.jpg


Boeing 787 Register - Welcome

www.airliners.net/forum/viewtopic.php?t=1335649

www.airportspotting.com/boeing-finding-homes-terrible-teen-787s/

www.boeing.com/commercial/customers/air-tanzania/air-tanzania-787-order.page
Mlitegemea mihela waliyomwaga 2015 oktoba wangelipaje haraka bila kutumia mbinu ya manunuzi ya kirwandarwanda???
 
Jamani kwani sumsung note 7 hamkuona janga lake? wale walio kimbilia mwanzo nn kiliwapata? iyo ni simu kwa ndege ikizingua unaimbiwa mbinguni kuna makao mazuri. sa cjui tulienda tukaona ayo makao

Kama hukuelewa nilichoandika pita huko.
 
This whole thing regarding those planes is so terribly convoluted...

So much information...you don't know for sure who's telling the truth and who's not!

But oh well...nowadays anybody can be an expert on anything and everything.
sure bro.
 
Jiulize ni kwanini serikali iko kimya kuhusu tuhuma hizi ndio utapata jibu.
serikari sio genge la wacheza bao wabishane kwa kila jamboa,yani sio genge la wahuni pia.Si tunataka ndege huo utaalamu hautowqsaidia mimilioni ya watu wasio na smart phone.Zito aliasema bombadier tumepigwa lakini asa ivi kila akipanda anapiga selfie
 
Mkuu uko sawa na hii Serikali ya kifisadi imeshaanza kuweweseka eti itatatuma wataalamu wakachunguze ubora wa ndege miezi chungu nzima baada ya kulipa cash! Kwanza tangu lini tuna "wataalamu" wa kukagua ubora wa ndege!? Na kwanini hawakuzikagua hizo ndege kabla ya kulipa cash!? Mpiga madili maarufu nchini kishafanya yake kwa mara nyingine tena.

Unakataa kuwa hatujauziwa ndege yenye hiyo serial number wakati wewe hutoi uthibitisho wa serial number ya nyengine.,

Kama ulihusika kwenye manunuzi jiandae kuwa responsible.

Ndege kuwa na features za zamani na ufanisi kidogo ndio sababu ya jina la terrible teens, has nothing to do with them being used.

Its about time hii mikata ya kitapeli muwe mnaiweka waI ili mnapoingizwa mjini ijulikane mapema, before its too late.
 
Business insider wanasema baada ya kukutana na mabosi WA boeing wameambiwa terrible teens zote zimeshauzwa tangu julai 2016, hivyo kuwapelekea wateja ingechukua hadi miaka miwili kwa sababu mbalimbali ikiwemo pengine wateja wengi waliamua kulipa kwa awamu kadhaa kabla ya kuchukua ndege.
Boeing wamesema wameuzia Tanzania dreamliner 787 kwa dola mil.224 haitawezekana wauze ndege ya dola mil.99 kwa bei ya juu tofauti na uhalisia itawaletea matatizo. Hivyo nawapinga wote wanaosema boeing wametudanganya .
Tatizo lako kama la bosi wako ni lugha tu!
 
Kuboresha utalii ni pamoja na kufufua Airline,
Sio kwa strategy hiyo ndugu. Biashara ya ndege sasa hivi imekuwa ngumu na yenye ushindani mkubwa sana. Watu wanaangalia mashirika yenye akili zao, tena kupeleka Boeing 787 au Airbus 380 yataka uwe na hub iliyoeleweka. Tutakuja kukutana humu baada ya miaka 10 ijayo uhai ukiwepo.
 
Mkuu uko sawa na hii Serikali ya kifisadi imeshaanza kuweweseka eti itatatuma wataalamu wakachunguze ubora wa ndege miezi chungu nzima baada ya kulipa cash! Kwanza tangu lini tuna "wataalamu" wa kukagua ubora wa ndege!? Na kwanini hawakuzikagua hizo ndege kabla ya kulipa cash!? Mpiga madili maarufu nchini kishafanya yake kwa mara nyingine tena.
Hawawajui wazungu hawa. Nafuu iwe wajanja wamekula chenji ikuwa ni kuingizwa mjini hiyo timu ndio itaingizwa mjini mara dufu. Natamani niwe kwenye timu ya uchunguzi, ubilionea uleeeeee
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom