Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Mkuu uko sawa na hii Serikali ya kifisadi imeshaanza kuweweseka eti itatatuma wataalamu wakachunguze ubora wa ndege miezi chungu nzima baada ya kulipa cash! Kwanza tangu lini tuna "wataalamu" wa kukagua ubora wa ndege!? Na kwanini hawakuzikagua hizo ndege kabla ya kulipa cash!? Mpiga madili maarufu nchini kishafanya yake kwa mara nyingine tena.
BAK una mahaba na kueneza uzushi tu kila mara! Umekusaidia nini tangu ujikite na kubandika uzushi tu. Naamini akili yako imekuwa mgando kiasi unafikiri ndani ya sanduku.

Kwa taarifa yako, taarifa za aina ya ndege inayosemekana imeagizwa na Tanzania yenye kumbukumbu na. 35508 Boeing 787-8 LN19 siyo sahihi. Ndege hiyo imeagizwa na Rwandair na siyo ATC. Link za mitandao zinazowekwa humu jamvini zinakinzana kabisa. Fanya juhudi kidogo kupata ukweli.
 
...
... Uthibitisho uliotumia kuonyesha kuwa Tanzania imeuziwa mojawapo yaTerrible teens ni kutoka tovuti zifuatazo:

Boeing 787 Register - Welcome

... Hii ni website ya amatures hivyo kutumia habari zao kama uthibitisho wa Tanzania kununua mojawapo ya Terrible teens hazina mashiko. Uangalifu wa hali ya juu na kutafuta habari katika vyanzo vilivyo karibu au kutoka ndani ya Boeing yenyewe ni muhimu katika kuthibitisha jambo hili badala ya kuamini habari kutoka website au blog ya mtu mmoja tena amature. Sioni kwa nini Tanzania wangeamua kusubiri karibu miaka miwili kupata ndege hii wakati iko tayari ikisubiri mnunuzi. Muda mrefu kiasi hiki ni kwa ajiri ya kutengeneza ndege mpya. Kama ndege tayari ina serial number na line number, lazima ingekuw katika website ya Boeing au website za makampuni credible hasa yanayotoa habari za kibiashara. Ajabu sijaona reference ya website yoyote inayoaminika kimataifa kwa habari za kibiashara iliyobeba habari hii pamoja na kuwa na mvuto kutokana na hizo terrible teens. Kwa kifupi hii ni habari ya kutunga na ndio maana website zinazoaminika kimataifa haziwezi kuitumia habari hii kwa kujua kuwa ni uongo na uzushi kwa kuogopa matatizo ya kisheria.

www.airliners.net/forum/viewtopic.php?t=1335649
Websita hii haina sehemu yeyote inayosema Tanzania imenunua mojawapo ya Terrible teens kama inavyodaiwa kwenye website ya huyu jamaa hapo juu. Website hii ambayo ina forum kama ya jukwaa la siasa kwa maswala ya ndege inazungumzia kuwapo Terrible teens na kuishia hapo. Sasa sijui ni kwanini imetumika kama kithibitisho kuwa Tanzania imenunua mojawapo ya Terrible teens. Inajaribu kuelezea failure ya uongozi wa Boeing mwanzoni mwa projekti ya 787.

www.airportspotting.com/boeing-finding-homes-terrible-teen-787s/

Website hii inazungumzia habari ya Ethiopia kununua Terrible teens kwa matumizi yao na siyo Tanzania kununua mojawapo ya Terrible teens. Wanatoa pia historia ya manunuzi yanayotazamiwa. Inaonekana habari hii ni ya zamani kidogo. Haijatoa uthibitisho kuwa Tanzania imenunua mojawapo ya Terrible teens hivyo haina uhusiano na habari za Tanzania kununua mojawapo ya Terrible teens.

www.boeing.com/commercial/customers/air-tanzania/air-tanzania-787-order.page

Hii ni website rasmi ya Kampuni ya boeing na inatoa habari za tanzania kununua ndege ya Boeing 787-8 na kujiunga na familia ya Boeing. inathibitisha bei kuwa ni list price. Mara nyingi list price siyo lazima iwe ni contarct price (bei iliyoko kwenye mkata) baada ya punguzo. Bei hii ni kwa ndege mpya na siyo mojawapo ya Terrible Teens kama inavyokuwa speculated kwa kutumia habari za mtandao wa amature mmoja. huyu ni mtu ambaye alikuwa anatoa habari za formula one na kuamua kuiuza website hiyo na kuanzisha hii ya B787.

Ninahkika 100% kuwa Boeing hatajaribu kujiingiza katika aibu kama hii kwa kuiuzia Tanzania ndege ya Terrible Teens huku akijuwa kuwa makabidhiano ya ndege huhusisha uhakiki wa uzito. Sijui atahonga wangapi iliwakubali kuchukua ndege yenye uzito tofauti na ule Tanzania wanataka. Ninaona mambo mengi sana kwa kutumia ufahamu wangu mdogo wa mambo ya ndege yanayonifanya nisiamini hata chembe habari ya Tanzania kuingizwa mkenge. Rbu tufuatie na baadae mje mnisute kwa kusema uongo wakati mojawapo ya Terrible Teens itakapo kuja Tanzania. Nilisema wakati wa bombardier kuwa sio kweli kuwa zimetumika bali ni mpya. nikamaliza kwa kusema I stand to be hanged kama itathibitishwa kuwa nilichosema ni uongo. I stand to be hanged kama itathibitishwa kuwa Tanzania imenunua mojawapo ya terrible teens au ndege hiyo sio mpya au haijatengenezwa kwa order ya Tanzania.
NOD: bandiko lako litakuwa limewajibu wazushi na wanaotegemea mitandao isiyoaminika.

Mwenye nia ya dhati kujua ukweli kuhusu mauzo ya ndege apitie website: ch-aviation.com, ambayo unalazimika kuilipia ili kupata taarifa za uhakika
 
Wape muda ndipo Raisi wetu ambaye hana hata miaka miwili anajaribu kufanay hivyo, nasi wananchi ni wajibu wetu kufanya yetu pia tuendeleze na kitajirisha nchi yetu kwa unayoyasema.
bc9ce3b3a86000616cbed8fb61a46c77.jpg

Huo ni ujumbe mahsusi kwa wanaojadiliana na kiumbe hiki [B]cocochanel[/B]...!
Kwa ufahamisho tu...Magufuli amekuwa serikalini kwa zaidi ya miaka 20 kama Waziri!
[B]cocochanel[/B] hana tofauti na huyo/hiyo ndege...!​
 
Ok well said.
Unaponishangaza ni hapo unaposema una imani na JPM.. Utakuwa vipi na imani nae wakati yeye ndie ameshugulikia deal yote ya hii ndege. Kama tumepigwa yeye ndie Mhusika no 1 and not otherwise.
Kumbuka hata negotiations na Boing kafanya yeye maana yule President wa Boing alivyokuja straight alienda kukutana nae Ikulu.
Kama kuna any ufisadi kwenye hili, JPM yumo.
Mkuu elewa jamaa kazuga tu hapo.
 
Ninachojua Siyo rahisi kivile kwa Boeing kufanya huu uhuni, hii itawaletea shida hata wao wenyewe kama itagundulika...

+ 971 564 015 692 hii ndio namba ya mwakilishi wa Boeing afrika aliekutana na Rais ikulu
 
bc9ce3b3a86000616cbed8fb61a46c77.jpg

Huo ni ujumbe mahsusi kwa wanaojadiliana na kiumbe hiki [B]cocochanel[/B]...!
Kwa ufahamisho tu...Magufuli amekuwa serikalini kwa zaidi ya miaka 20 kama Waziri!
[B]cocochanel[/B] hana tofauti na huyo/hiyo ndege...!​

Ha ha ha haaaaaa

I am Cocochanel

Hadi upost hivyo umenipa nguvu zaidi za kuwapa ukweli, wadakuzi msio na sera.

Embu niambie mnapangaje kuvutia wananchi siku hizi? Au kuendelea kumsubiri Raisi wenu mpendwa aongee ndio mmwage porojo!?

Ha ha haaaaaa

Magufuli 2020

Nyuma yake

Makonda kupaa juu katika vyeo

Makonda oyeeeeeeeee
 
wanasema hiyo ndege kama vile iko ghalani. kinachoshangaza kama ndege ipo kwa nini delivery iwe 2018 na sio sasa wakati serikali imesema hela zipo? nadhani serikali inafuatilia hizi taarifa za mitandaoni. tumeona hila za kila aina mitandaoni kuichafua awamu ya 5.
hizi taarifa kama zina ukweli serikali kuingizwa mjini bado ipo nafasi kurekebisha makosa ila natia shaka kwani wanaoshikia bango ndio wale walisema bombadier ni mitumba.

unarekebisha vipi na mkataba umeshasainiwa na advance payment kufanyika
 
Wafikishie wanaokutuma ujumbe huu ;

goodfoolishman-jpg.503495

Sasa kama wewe unatumwa ndio unafikiri na mimi

Ooooo na kapicha kako kamebuma

Ha ha ha haaaaaaaaaaa

Endelea na kazi uliyotumwa humu na kwenye SN zileeee
 
Jamani kwani sumsung note 7 hamkuona janga lake? wale walio kimbilia mwanzo nn kiliwapata? iyo ni simu kwa ndege ikizingua unaimbiwa mbinguni kuna makao mazuri. sa cjui tulienda tukaona ayo makao
Mkuu mbona unapoteza muda na mtu aliyeambukizwa ujinga na Bashite? Hili choko ukilielewesha utalisikia linasema makonda oyeeee!
 
BAK una mahaba na kueneza uzushi tu kila mara! Umekusaidia nini tangu ujikite na kubandika uzushi tu. Naamini akili yako imekuwa mgando kiasi unafikiri ndani ya sanduku.

Kwa taarifa yako, taarifa za aina ya ndege inayosemekana imeagizwa na Tanzania yenye kumbukumbu na. 35508 Boeing 787-8 LN19 siyo sahihi. Ndege hiyo imeagizwa na Rwandair na siyo ATC. Link za mitandao zinazowekwa humu jamvini zinakinzana kabisa. Fanya juhudi kidogo kupata ukweli.

Ni kweli huyu anadanganya link hii inaonyesha ukweli lakini naona wanaipita kama hawaoni chochote.
Link : https://www.planespotters.net/production-list/Boeing/787
 
Route ya kwanza watapanda wabunge na mawaziri mpaka marekani na kurudi. Wakifika salama tutapanda tu
 
Rais mstaafu JMK alikuwa na msemo wake pendwa: "Akili za kuambiwa changanya na za kwako". Mtu aliyezoea kupata vitu kiujanja ujanja au kuwaibia wengine kwa zile staili za "Kanyabwoya" siku zote huwaza kuibiwa tu. Itoshe tu kujua kuwa kuna ushindani mkali sana kati ya Boeing na Airbus, kuchafuana kupo lakini kupitia kwa mawakala,kwa hilo la "Terrible teens'' huenda wengine wanaimba wimbo wasioujua. Ndege mwenyewe huyu hapa.
 
Attachments

  • C-ttBUSXYAAQP8c.jpg large.jpg
    C-ttBUSXYAAQP8c.jpg large.jpg
    17.6 KB · Views: 59
Bashite wa Kolomije ndio Hirizi na Password ya Mzee Magufuli, SO Lazima Wapige Mifyeza ya kuishi mtu na sio kufa mtu!
Mpaka watz wenzangu mpate kuzidika Wameshakula sana hawa akina Mwanambati.

Msisahau Kwenye suala la MADAWA YA KULEVYA mwana wa Kolomije amelitumia sana kujinufaisha badala ya KUKOMESHA au KUDHIBITI BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA HAPA NCHINI.
 
Watanzania hatuna hata cha angalau ni bora tungepata uongozi wa kuendelea kutumaliza kuuza mashirika ya umma,wanyama,madini,usafiri tukose hata bajaj ya serikali wabaki kutesa wanasiasa na mashangingi yao.Mwisho tuuzwe na sisi ndio watu tungefurahi.Mtu huna hata nguo unatembea matako nje,unapewa suruali unaanza kuitoa kasoro hata hujaivaa.Wachawi sio mpaka wakutwe uchi usiku wa manane wengine mnapatikana hata mitandaoni mchana kweupe.
 
Shalom watanzania wenzangu!

Disemba 12, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa baadhi yetu tuliomchagua JPM na Tutamchagu tena 2020 Mungu akitujaalia na wengine mlinuna baada ya taarifa kutoka serikali imeweka oda Boeing, ili kununua ndege ya kisasa kabisa 787-8.

Na yakwamba serikali itatoa $224.6Millioni ili kupata ndege hiyo.

Kumekuwa na taarifa mbali mbali, kwamba manunuzi haya yana chembe chembe za ufisadi. Na kwakuwa sipendi kuamini vitu bila kufanya utafiti nami nimeona nizame kwenye websites mbali mbali kutafuta ukweli.

Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua.

1. SERIAL NUMBER(SN) NA LINE NUMBER.
-Kila ndege huwa na serial number yake kama yalivyo magari. Ndege tulioagiza serial number yake ni 35508
-Line number ni ndege ya ngapi kutengenezwa. Kwa mfano kama zimetengenezwa ndege 10. Ndege ya kwanza itakuwa LN1, ya pili LN2 nakuendelea.

2. TERRIBLE TEENS NI NINI?
Terrible teens ni zile ndege za mwanzo kutengenezwa za Boeing 787-8. Hizi ndege zilikuwa 20. Kwahiyo hiyo ni Line number 1-20 (Kuwa makini hapa). Na hizi ndege zilifanyiwa majaribio mengi na matengenezo mengi mapya ili kupata ndege bora zaidi.

Kwa kifupi tunaweza sema zilikuwa sample ya kutengenezea ndege zingine. Kutokana na kufanyiwa modification za mara kwa mara hizi ndege zilipitiliza uzito uliotakiwa. Kutokana na kuongezeka uzito ndege hizi hata uwezo wake wa Masafa ukawa Umepungua kwa Maili 1000 au KM 1609.344

Kutokana na hili makampuni yaliotaka order za mwanzo kama All Nippon, Maroc etc. yaligoma kuchukua hizi ndege bali yalichukua ndege zilizotengenezwa baada ya zile 20 za mwanzo yaani Line number 21 na kuendelea.

Terrible teens zingine ziliwekwa kwenye majumba ya kumbukumbu na baadhi ya kampuni walizichukua. Zikabaki 12 uwanjani miaka mitano bila mnunuzi toka 2009 zilipoanza tengenezwa.

Kutokana na aibu iliyokuwa inaipata Boeing ya kukaa na mindege isiyo uzika. Ikaamua yafuatayo

(a) Kutafuta Wateja ambao hawatajali issues ya kikomo cha masafa ya ndege

(b) Kuziuza hizi ndege kwa bei rahisi ( karibu nusu bei kutoka $224M hadi $99M)

CONCLUSION
Kutoka katika websites ya Boeing na na web zingine za usafiri wa anga zimeweka wazi Ndege tulio iwekea order ni Boeing 787-8, serial number 35508, Line number 19.

Sasa kwa maelezo niliyotoa Line number 19 IPO ndani ya Line number 1-20. Kwa kifupi ndege tuliogiza ndio zile ndege za mwanzo 20 zilizopachikwa jina la Terrible Teens.

Swali lingine la kujiuliza kwanini tumeuziwa ndege iliyo doda ,iliyoshushwa bei hadi kufikia $99M kwa bei ya ndege mpya yaani $224.6M?

Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.

Kama nilivyokwisha sema Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini anayeipenda Tanzania. Na imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa kazi.

Nimewawekea link na picha mbali mbali kusappoti uzi.

66cbe3973d2476f0afd0ef4b23f5d581.jpg

5ffe88270490cadedd65af84f1f2a940.jpg
32a59f2db3a1932ae85e9b8bfd8d26fd.jpg

  • 6 are in various stages of rework (lines 10, 15, 16, 17, 18, and 19)
 
Back
Top Bottom