Ukisoma taarifa mbalimbali ikiwemo Boeing wenyewe ndege hizi zimewekewa price listing ya $224 , lakini bei zake halisi zimepunguzwa ili kuvutia wateja. Katika msingi kama huu kuna uwezekano kuwa Boeing na serikali ya Tanzania walikubaliana bei ya chini tofauti na bei ya Tangazo lakini pia wakaamua wasipublish bei hiyo ya makubaliano ili kulinda heshima ya ndege kibiashara.
Sina hakika sana na hili ila ni mawazo na mtazamo wangu binafsi kuwa kama ukiuza au ukanunua bidhaa kwa nusu bei ya thamani yake kuna uwezekano mkubwa ukashusha heshima ya bidhaa hiyo na pengine kuwapa watu walakini wa usalama wa matumizi yake na hivyo kushindwa kupata abiria, na pengine hata kwa kampuni nzima na hivyo kuathiri hata ndege nyingine za brand nyingine ulizonazo katika fleet.
Katika mtazamo huo hiki kinachotokea sasa hakikutarajiwa na pengine damage yake huenda ikawa sawasawa au zaidi ya kile kampuni/serikali ilichojaribu kukilinda...
Haya ni mawazo na mtazamo wangu tu binafsi, sio facts!